Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Popote Ulipo
Popote Ulipo
Popote Ulipo
Ebook193 pages12 hours

Popote Ulipo

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

    Ajali mbili zinatokea kwenye majira tofauti, zote zikiondoka na maisha ya watumishi wa umma kutoka taasisi ambazo zina ukaribu kwenye ufanyaji kazi. Baada ya tukio hilo kunafuatia kutangazwa ufisadi uliyowahusu watumishi wao. Ikielezwa walipanga uhaini mkubwa, na walichota kiasi kikubwa cha pesa za serikali.

    Mmoja ilielezwa alifikwa na ajali akiwa  mafichoni mbugani alipofika kama mtalii. Mwingine ikitajwa alikuwa akikimbia kuelekea kujificha, ndiyo hapo alifikwa na mauti akiwa njiani. Ikawa habari iliyoshika hisia za wengi, kiasi cha kuibua wanaharakati na watu wa mitandaoni baada ya kuachiwa makala toka kwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi.

    Suala hilo lilimvutia Norbert Kaila baada ya kuona lilikuwa likihusu ubadhirifu, alitaka kufanya utafiti na kuweka kila kitu wazi. Alipoingia kwenye kazi hiyo, ndiyo hapo alikuja kukutana na mengine ambayo hakuyajua. Mchezo mchafu ukihusisha mfanyabiashara na watumishi wa taasisi zile za wafanyakazi wale.

LanguageKiswahili
PublisherMambosasa
Release dateMar 10, 2024
ISBN9798224449101
Popote Ulipo
Author

Hassan Mambosasa

  Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.     Elimu ya juu aliipata  chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.     Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika  hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni. 

Read more from Hassan Mambosasa

Related to Popote Ulipo

Related ebooks

Related categories

Reviews for Popote Ulipo

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Popote Ulipo - Hassan Mambosasa

    DIBAJI

    Watumishi wawili wanapokea ujumbe usiyoeleweka kwenye simu zao, kwa nyakati tofauti. Hao walikuwa ni wazalendo ambao waliondolewa makazini kwa namna isiyoeleweka. Mmoja akiwa likizo ya lazima, mwingine akisimamishwa.

    Pindi waupokeapo ujumbe huo wenye kuwaambia siku yao ya kifo imekaribia. Hawakuchukua muda mrefu walikumbana na mauti. Ndiyo hapo mengine mapya yalifikia kuibuka.

    Tuhuma mpya kusambazwa dhidi yao na watu waliyotaka kupata umaarufu na pesa kwa kutumia mtandao. Si hilo tu familia nazo zikaja kuingia misukosuko. Baada ya kufikwa na mauti tangu waliposoma ujumbe unawaambia Popote walipo.

    Mlolongo wa matukio unamvuta Norbert Kaila kuingia kazini kuchunguza. Ndiyo hapo anakuja kujua makubwa sana yaliyojificha. Yasiyofahamika na wengi. Siri za serikali zipo matatani, zikiwa mikononi mwa watu wasiyo stahiki. Pia kuna dhuluma kubwa ilifanyika, kufikia kufuta rekodi za ulipaji za wafanyabiashara halali waonekane wakwepaji uchangiaji wa maendeleo ya kiserikali.

    Popote Ulipo, ni riwaya ya kijasusi iliyobeba jina la ujumbe ule. Uliyopelekea maisha ya wazalendo kukatisha kinamna yake, baadaye ikaja kujulikana ni hujuma mbaya iliundwa dhidi yao.

    1

    Ilikuwa ni siku ambayo alijawa shauku kupitiliza, kiasi cha kufikia kutamani majira ya kupumzika yasifike. Kusudi aanza kufaidi na macho, wachilia mbali kujongea na miguu yake kutoka eneo moja kwenda jingine. Ilimradi nyakati hizo ziwe bora zaidi maishani mwake, ambazo zilimfanya asijutie kukubali jambo aliloelezwa na wakubwa.

    Jambo ambalo aliliona kama si kuzuiwa asiendelee kufanya kazi kwa manufaa ya wengine. Ila napo aliishia kuona ni sahihi kuelekea huko alipotakiwa, kwa kutakiwa mapumziko kusudi aje kurejea na nguvu zaidi ya kufanya kazi zake kama kawaida. Furaha ilimtawala hasa, pindi alipowasili tu kwenye geti kuu, la hoteli ya kitalii maarufu duniani ambayo iliwahi kuchukua tuzo ya hoteli bora huko Marekani.

    Nani asiyeijua Singita? Miongoni mwa watu wanaofuatilia mambo mjini, habari zake ziliwakaa vinywani hasa kutokana na umaarufu wake na pia gharama kubwa za huduma zinazotolewa hapo. Eneo hilo ndiyo mahala ambapo watu maarufu sana duniani hufika kwa siri, huishia kukaa na kufurahia na kisha kurejea kwenye nchi zao.

    Hiyo ni hoteli ya kifahari iliyopo ndani ya mbuga ya wanyama ya Serengeti. Mahali kuliposheheni vituo lukuki vya utalii, wanyama wa aina mbalimbali ambao waliwavuta watu kuja huko kuwaangalia. Ndiyo hapo kukafikia kujengwa mradi huo wa gharama kwa wenyeji wengi, ila haukuwa hivyo kwa wageni ambao waliyofika hapo. Kiasi cha kufikia kutoa pesa wakae kwa siku kadhaa, mpaka walipokinai haja zao na kuondoka.

    Ndiyo mahala hapo alipofikia Kinangi Joel, kijana wa kisasa na mchapakazi hasa, mwenye elimu kubwa ambayo ilipelekea kuajiriwa na kutegemewa kwenye ufanyaji kazi wake, kiasi kwamba alikuwa mwiba hasa kwa wavivu wawapo kazini. Kiasi kwamba alipandishwa madaraja kwa miaka aliyofanya kazi, mpaka kuja kufikia kupewa likizo hiyo ya ghafla, huku gharama zote za kwenda kujiliwaza angelipiwa.

    Likizo ambayo aliona kama ni kaba koo baada ya kutoka katikati ya jukumu kubwa alilokuwa akilifanya, lililomfanya akaingiwa na migogoro kadhaa na mkubwa wake. Ila bado akiendelea na utendaji wake, ndiyo hapo sasa ikafika habari ya kupewa likizo hiyo na wakubwa zake ambayo aliamua kuipokea vyema.

    Ndiyo hapo bwana huyu kapera, aliyejitika zaidi kwenye ufanyaji kazi akiwa si mwingi wa starehe. Alipoamua kupanda ndege iliyomtoa mjini, mpaka kumfikisha kwenye uwanja wa ndege mdogo uliyopo mbugani. Mahali ambapo alijikuta na faraja kubwa baada ya kufika na kupokewa kwa bashasha, kisha akaja kupelekwa kwenye chumba cha hoteli kilichojengwa kinamna yake kikiwa na kila kitu ndani.

    Mpaka alifikia kujuta kuchelewa kufika hapo mbugani, majira ambayo giza lilikuwa likinyemelea mpaka alifikia kukaa chumbani pekee. Baadaye akaja kutoka tena na kuelekea kupata chakula, sehemu ambayo alikutana na watu wa mataifa mbalimbali kwenye mgahawa wa hapo.

    Kinangi alipiga picha za kutosha kwenye eneo alilokaa, asijali kama ni mpweke sana. pia alikuja mwenyewe kwenye hoteli, aliishia kufurahi tu na mazingira, kumwondolea uchovu mwingi ambao ulimkumba kutokana na kutumikia mwajiri wake. Aliona ana haki ya kufurahia kwa ofa hizo alizoandaliwa, akijuta sana alikuwa akipitwa na mengi sana kwa kujituma kwake kupitiliza na hata kutozitumia likizo vizuri, mpaka ilipokuja kutokea hiyo.

    Napo akijipiga picha, alipokuja kushusha simu chini. Alimwona binti mrembo akiwa amekaa kwenye kiti kilichopo mkabala naye. asielewe alifika muda gani, mpaka alimfanya aduwae akimtazama mnyange huyo aliyependeza hasa, ambaye aliishia kutabasamu tu baada ya kukutanisha macho yao.

    "Are you Tanzanian or foreigner?", Binti aliuliza swali pasipo salamu walipokutanisha macho yao, akiongeza kingereza kwa kuweka mbwembwe akitaka kujua kama ni mtanzania au mgeni.

    "(akitabasamu) Mtanzania niliyeamua kuja kutoa ushamba", alijibu, binti aliishia kucheka kusikia hilo, alidhihirisha urembo wake uliyopo usoni mwake kiasi kwamba bwana huyu alibaki akimshangaa zaidi.

    Kwake hakuwa mgeni machoni mwake, ila hakujua aliwahi kumwona wapi na kwenye mazingira gani. Ameshakutana na wanyange wa kila namna, kutokana na mfumo wake wa kazini na hata sehemu zingine za vikao mbalimbali. Si rahisi kumkumbuka kila mmoja, ndiyo kama ilivyo kwa aliyeyavutia macho yake ambaye alifika ghafla wakati akijipiga picha.

    "(akidatisha vidole na kisha akaja kumwelekeza kidole cha shahada) Nilijua tu ni mwenzangu ila sikuwa na uhakika, nilitaka niverify kwanza"

    Kumbe sote ni washamba na tumekuja kutoa ushamba wetu hapa, tujichunge tusije kuonekana tumerukwa na akili kwa ushamba, alitumbukiza tena masihara na kumfanya binti acheke hasa.

    "Anyway Rose Basilia, sijui mwenzangu nani"

    Kinangi Joel, ukipenda unaweza kuniita Kinangi tu inatosha, alijibu muda huo aliposikia jina la mrembo, ndiyo akili yake ikaja kukaa sawa na kukumbuka kwanini alikuwa akiona sura yake si ngeni, mpaka alijilaumu kutomfahamu huyo binti.

    Jina hilo ungelitaja mjini tu, basi hata mtoto mdogo angekwambia ni nani huyo. Ndiye yeye akaja kulitoa kumbukumbuni mwake kirahisi, hata kama ni mambo mengi mengine si ya kusahaulika kabisa. Hadi alijilaumu moyoni mwake, ila uso wake ulijawa na tabasamu pana kama vile hakukuwa na kitu kimetokea. Mwishowe aliishia kusema, Safari ya mwenyewe, au ulikuja na mtu nisije kupigwa hapa.

    "No usiwe na wasiwasi, sikuja mwenyewe ila sijaongozana na mswahili hadi aje kukuletea matatizo"

    "nilitaka nishangae almasi iwe haina mwenyewe na ishachimbwa ardhini. Anyway nafurahi kukutana nawe. Nadhani upo na tutaonana zaidi"

    "si sana, nadhani Tomorrow naweza kuondoka hapa. nilikuwa kwa wiki nzima. Ndiyo hapa nikaja kukuona, nakumbuka nishawahi kukuona mahala ila sijui wapi. Kama hutajali niachie  contact yako, nitakutafuta ukitoka hapa"

    Halikuwa jambo baya kwake, aliishia kumpa mawasiliano yake. Si hayo tu hadi picha walipiga pamoja ndiyo binti huyo akaja kuinuka na kuondoka. Akimwacha akiendelea kula, asijue kuonana huko kwa bahati mbaya kunaweza kuzaa jambo jingine ambalo lingekuja kujitokeza kwa makusudi.

    Kinangi alipopata mlo, alishika njia kurudi chumbani kwake. Hakuwa na muda wa kuendelea kuhangaika nje, alipanga kwenda kujipumzisha ajiandae kwa ajili ya siku mpya. Alipanga kukishakucha baada ya kifungua kinywa tu, basi ni kutembelea sehemu mbalimbali za hapo mbugani afurahi sana kabla siku za kukaa hapo hazijaisha akafanikiwa kurudi mjini.

    Mwendo wa taratibu akielekea huko, napo alijikuta akisimama. Ashindwe kuendelea na safari yake. Hasa baada ya kuhisi mtetemo kwenye mfuko wa kulia wa suruali yake, mahala alipoweka simu yake. Kumaanisha kuna mtu alipiga, kwani aliikata sauti baada ya kufika hapo, hakutaka itoe makelele na kuwa kero kwa wengine. Aliishia kuitoa ila jina aliloliona kwenye kioo liliishia kumtisha kidogo likiwa halina namba yeyote ile ikimaanisha mpigaji alificha taarifa zake.

    Kabla hajapokea simu nayo ilikata na papo ukaingia ujumbe. Uliyomfanya asimame na kuusoma kwa umakini, jina lile pasipo namba ilikuwaje akamtumia. Huo aliusoma, ‘Mimi ni mauti yako, popote ulipo nitakufikia. Iwe ndani ya ngome nzito, katu huwezi kuniepuka. Jiandae!’.

    Maajabu!

    Yaani umauti umtumie mtu ujumbe wa maneno ya kujiandaa, hakuwahi kuliona hili na alihisi ni mtu tu alikuwa akimchezea akili. Aliyeamua kuficha namba yake ya simu kusudi, tena akitumia simu ambayo huwa ni ya matumizi yake binafsi pekee na si ofisini. Ikimaanisha alimjua nje ya maisha ya kazi, sehemu ambayo alibeba marafiki wasiyo wengi sana.

    Aliishia kupuuzia, hakuwahi kusikia kama kifo kingekuwa kinakuja kumkuta mtu akitumiwa ujumbe hivyo. Mwishowe aliingia zake chumbani, akitaka kujipumzisha. Ila kabla hajafanya hivyo alienda kuoga na kisha kuwasiliana na rafiki yake, akimwambia alifika salama na huko alikutana na  mtu maarufu mjini. Aliishia kumtumia picha yake kumwonesha, mwishowe aliagana naye na kupanda kitandani ajipumzishe zaidi.

    WEE VIPI MBONA UNATABASAMU kama mwehu na hiyo simu yako, ujue nakusubiri wewe ila nakuona wala hujali leo siku gani, ilikua sauti ya mwanamke mweupe, mwenye mwili uliyojaa kiasi chake, ambaye alijifunga kanga iliyotoka kifuani na kuja kuishia juu ya magoti.

    Alijilaza pembeni ya mwanaume aliye kifua wazi tu, chini alijisitiri kwa bukta nyekundu ya jezi. Wote wawili walikuwepo ndani ya chumba chenye kusheheni samani za kisasa, wakiwa kitandani na ndiyo hapo bwana huyo aliishia kutabasamu akiangalia simu yake. Alipofikia kuelezwa hivyo na mwanamke, alimgeuzia kioo na kumwonesha kile kilichomfanya awe hivyo.

    Hadi bibie aliishia kusema, ni makubwa mwenzangu, si alikuwa hataki kabisa kuondoka huyo, aliamua tu kisa amri. Naona ameshakutana na kifaa huko.

    ndiyo ananieleza kamfuata mwenyewe na namba ya simu kaombwa pia, na pia wakapiga akaondoka zake

    "naye rafiki yako alivyo kiwembe huyo, basi hatomwacha salama huyo. Bora umshauri mwenzako aoe, hivi huoni tukitoka pamoja wewe upo nami mkeo. Ila yeye wanawake tofauti kama vile nguo, leo ana huyu kesho anakuja na yule. Ataacha watoto wa nje hadi lini huyo"

    Yaani ukimwambia hilo kama unampigia mbuzi zeze, alishatendwa vibaya zaidi tukiwa chuo, toka siku hiyo hataki kumpenda mwanamke yeyote na anaogopa hiyo ndoa. Wanawake wenyewe wanajileta wenyewe wacha awatumie tu

    Makubwa mwenzangu, haya weka simu huko kando. Si muda wa matumizi yake huu. Usinicheleweshe kuamka huko

    Naye hakutaka kuleta ubishi aliishia kuweka simu kando, kisha aligeukia upande aliyopo mkewe na kuipangusa kanga aliyovaa, sambamba na mwanamke huyo kuzima taa ndogo ya pembeni ya kitanda iliyokuwa ikiwapa mwangaza.

    MAPAMBAZUKO MAPYA YALIKUWA ya furaha zaidi kwa Kinangi, wala hakuwa na habari kuhusiana na ujumbe wa maneno aliyopokea kwenye simu yake, ambao ulikuwa ukiufunga nao haukati, huishia kupotea jumla. Yaani flash message, uliyomfanya akampuuzia aliyeutuma na kuamua kuangalia furaha yake hapo.

    Asubuhi hiyo alielekea kupata kifungua kinywa, aliwasiliana na Rose  kwa muda mfupi, kabla hajaja kupanda gari la kitalii. Huku mkononi mwake akiwa na kamera ya kisasa, aliyopanga kupiga picha kadhaa kwa ajili ya kumbukumbu. Alizunguka sehemu kadhaa, ndipo akaja kuwasili eneo moja chini ya mti majira ya jua kuanza kutoa ukali wake.

    Mahala hapo alikuta puto la kupaa angani kwa kupashwa joto likiwa limewekwa chini. Kutokana na siku hiyo alipanga kulipanda na kupaa nalo angani, huku akipiga picha mbalimbali. Hakusubiri hata, alikimbilia kuingia kwenye kasha lake maalum lililo kama kapu kubwa.

    Ndani ya puto lile alimkuta kijana wa kuliongoza ambaye alikuwa ameshajiandaa kufanya jukumu lake. aliishia kusalimiana kwa kugonganisha ngumi, akitumia kiswahili cha vijana kilichomfanya mwongozaji huyo awe na furaha zaidi kumpata mzawa mwenzake. Kiasi kwamba walianzisha soga wakati mwenzake akianza kufanya jukumu lake la kuinua  kifaa angani.

    Mwishowe napo kapu liliinuliwa baada ya puto kusimamishwa, na moto kuwashwa ambao ulilipasha joto na kupelekea lianze kupaa taratibu kuelekea juu. Ilikuwa ni zaidi ya furaha kwa Kinangi akiangalia kifaa hicho kilichokuwa kikienda juu taratibu mpaka kuja kufika umbali wa mita takribani mia tano angani. Akaishia kuanza kupiga picha wakiwa angani, akitumia lenzi maalumu kuvuta picha azipate za kutosha.

    "aisee hii ni fursa nzuri sana, kama mtu akiwekeza pesa na kamera hizi atatoa dokumentari nzuri itakayomwingizia hela nyingi sana."

    Ndiyo hivyo kaka kwenye miti hakuna wajenzi, yaani hizo kazi wanakuja wazungu tu hapa. wanazunguka na kutega picha hadi usiku wala hawaogopi chochote kile wakisaka hela

    yaani huku mbugani wanaingia usiku, je wakija kuliwa na wanyama hatari wa humu

    "Kaka wale jamaa wamejipanga kisawasawa, hawana hofu hizo wanakuja kamili na timu. Unajua ukitaka kufanya kazi hizi uwe na mfuko wa kutosha, haihitaji hela za mawazo. Yaani huku wanakuja na makamera mazito sana, hadi movie wanachukulia huku. Wabongo hapa kuja kutalii kwenyewe kitendawili, achilia mbali kuandaa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1