Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Nsungi 2: NSUNGI, #2.2
Nsungi 2: NSUNGI, #2.2
Nsungi 2: NSUNGI, #2.2
Ebook285 pages3 hours

Nsungi 2: NSUNGI, #2.2

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

   Inaendelea ilipoishia kitabu cha kwanza, Hawa anawasili chuoni akiwa kama mwanafunzi mpya. Dhumuni kuu linakuwa ni kuendeleza harakati zao zilezile, bado hajataka tamaa kama alivyo Mkuu wake. Mbinu mpya wamekuja nayo hapo chuoni.


    Lucy naye ananogewa na penzi la Miko, asijue hana weka mwake. Anafikia kugombanishwa na marafiki zake baada ya kuambiwa uongo. Mzozo huo unapelekea binti ajitenge na wenzake, akiwatuhumu ni wanafiki. Asijue kama alifanyiwa vile baada ya kundi la kijana yule kubaini uwezo wa Maria.


    Hawa anatumwa na Lifa kwenda kumshawishi Lucy aje upande wao baada ya kuona hali ni hiyo ameshagombana na wenzake. Waliona ni wasa mzuri sana wa kukamilisha harakati zao. Binti naye anakubaliana na hila zao, na kuishia kuwapa masharti kutimiza suala hilo.


    Mwishowe Lucy anakuja kuijua rangi halisi ya Miko, wakati huo ameshachelewa sana.

LanguageKiswahili
PublisherMambosasa
Release dateFeb 16, 2024
ISBN9798224855483
Nsungi 2: NSUNGI, #2.2
Author

Hassan Mambosasa

  Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.     Elimu ya juu aliipata  chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.     Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika  hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni. 

Read more from Hassan Mambosasa

Related to Nsungi 2

Titles in the series (4)

View More

Related ebooks

Reviews for Nsungi 2

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Nsungi 2 - Hassan Mambosasa

    DIBAJI

    Ujio wa Hawa chuoni hauna kama ilivyo kawaida, kafika kwa ajili ya kutimiza kazi ya kiongozi wake. Napo anaungana na kundi la Lifa na Remse, wakiwa na maadui wa pande mbili zingine tofauti.

    Harakati zao wanazianza kwa kutafuta mwenye picha upande mwingine wa nchi, sambamba na kutaka kuharibu muunganiko wa Maria na marafiki zake, kusudi aje kuwa upande wao.

    Atlaf na wenzake nao hawapo nyuma wanaendeleza harakati chafu. Kundi la vijana wake wanakuja kuingia mikono mibaya ya Maria, wanaishia kupigwa vibaya. Hadi wakatambua ukiachana na watu wa Remse bado walikuwa na adui wengine, na hawakufahamu walitokea upande gani.

    Lucy naye anachanganywa na penzi la kijana Miko, anajikuta akigombana na marafiki zake pasipo kujijua.  Hakujua kijana aliyekuwa naye hakuwa na wema kwake, na si sehemu ya kundi salama. Mapenzi yamemvika upofu akichanganywa na namna kijana alivyomjali. Kiasi cha kufikia kuamini kila alichoelezwa. Mpaka anakuja kufanya mauaji, yanayopelekea kuibua kwa kiumbe mpya anayekuwa mfuasi wake.

    Bado napo Hawa anatumia wasaa huo kumshawishi kuungana nao, kusudi wapindue harakati zote za kina Salmin. Lucy anawapa masharti magumu akiwa na mashaka nao, ila bado hana wasiwasi na mpenzi wake. Anapokuja kushikwa na kundi la kina Miko ndiyo hapo alijua hakuwa mwema muda huo ameshachelewa.

    1

    Kukurubiwa huko, kulipokewa na bashasha pana toka kwa binti shombe. Ambaye pia alitazamana mwanaume aliyefika naye, aliyejulikana kama mzazi katika mchakato mzima wa kumpokea  mwanamke huyo.

    Walitoka jengo hilo na kujongea kwa miguu yao, wakielekea upande wa kulia ambapo walifika jirani na tawi la benki ya CRDB wakaingia kulia kwake na kwenda hadi zilipo ngazi  ambazo ziliwafikisha ilipo  ghorofa ya kwanza. Huko walikabidhi fomu zingine pamoja na kivuli cha kadi ya bima kisha wakasonga wakaondoka na kurejea hadi garini kwa mara nyingine. Ambapo dereva aliwafungulia, wakaingia na kuketi kiti cha nyuma.

    Nadhani kazi yangu imekwisha ewe Mniru wangu, Mwanaume yule alisema kwa utiifu mkubwa mbele ya binti huyo ambaye alionekana wazi ni mdogo kwake.

    Kutoka kwa kauli yake hiyo, ghafla mrembo yule alipungua ukubwa wa mwili, akaja kuonekana ni mtoto mdogo mno ambaye hata  elimu ya msingi hajafika katikati. Huyo alidhihirika akiwa amevaa nguo za kiasili  ambapo uso wake ulionekana ni  wenye umakini mno.

    Pamoja na kutokea hayo  hakuna aliyeshtuka miongoni mwa waliopo humo, si dereva wala huyo  mtu mwenye asili ya ushombe ambaye kampeleka hadi  kule kufanya usajili hapo chuoni hapo.

    Yule bwana ndio kabisa aliendelea  kuwa utulivu mkubwa, akidhihirisha heshima kwa  mtoto mdogo.

    Vyema kwa kazi yako  nzuri, sasa hivi sasa nahitaji kuelekea  moja kwa moja hadi kule chuoni ninapotakiwa kusoma. Nadhani tunaelewana nikisema hilo, ni moja kwa moja  Mazimbu. Bado kuna kazi  hujaimaliza. Ongea na Mtwavi hakikisha awe na kila kitu changu muhimu muda ambao tutafika kule, Mtoto alisema.

    Pasi na shaka Mniru, Aliitikia kwa utiifu wa hali ya juu, huku akimwacha Mtoto huyo akitazama mbele ambapo dereva wa gari aligeka pao hapo.

    nikifumba macho na kufumbua tuwe tayari tushafika mazimbu Agizo jipya lilitolewa na  kweli papo wakawa wapo kwenye kona ya kuelekea  mwisho wa daladala za Mazimbu. Ambapo motokaa hiyo ilionekana kushika njia huku jamaa akiongoza usukani.

    Hata  haikueleweka walifika vipi na kwa kasi gani umbali huo wa zaidi ya kilomita tatu kutoka yalipo makao  makuu ya chuo hadi kampasi nyingine. Hakika ni ajabu mno, ingawa haikuwa  la kutisha miongoni mwa watu waliyopo hapo  na hao ndio kwanza walitulia vilevile kudhihirisha  ni namna  gani mambo hayo wameyazoea.

    Basi  motokaa  ile ikaangia eneo la chuoni baada ya kufika mwisho wa stendi ya  daladala, ambapo  alipitia upande ambao kuna maktaba ya zamani ya  chuoni hapo. Walipofikia usawa wa jengo la awali la vitabu, waliingia kushoto  na  kufuata uelekeo ambao kuna tawi la benki ya CRBD humo ndani ya kampasi ya Solomon Mahlangu.

    Walipofika usawa wa  njia ya kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe wa chuo, dereva alikanyaga breki na kupelekea motokaa hiyo isimame pao hapo. Punde mlango wa kushoto mwa dereva ukafunguliwa ambapo aliingia  mtu wa makamo  ambaye alidhihirisha ni mwenye kuwa nazo za kiasi mifukoni mwake.

    Kazi uliyopewa na mwenzako umeitimiza, Mniru aliuliza.

    Hakika imemalizika  muda huu,  na vitu vyako tayari vimeshawekwa  chumbani  unapofikia hivi sasa. Si mulemule kwa yule binti, Mtu huyo alisema.

    Vizuri Profesa kwa kufanya kazi yako kwa ufanisi mkubwa, sasa muda huu ni wa mimi kuja kutimiza kazi  iliyonileta hapa, Mniru alisema na kisha akabadilika na kuwa na umbile  lile la urembo la hapo awali, kutoka  utoto hadi kuwa msichana mwenye kuvutia.

    Muda huohuo gari liliondolewa mahala hapo na kuelekea upande yalipo mabweni ya chuo hiko, ambapo lilikuja kusimamishwa  njia panda ya kuelekea mabweni ya 'unit 4'. Hapo ndipo Mniru  alishuka sambamba na wanaume wawili wanaomtumikia. Akiwa na nguo zake aliongoza moja kwa  moja hadi eneo ambalo alitakiwa kuishi.

    Mizigo muhimu yote ilikabidhiwa kwa  wasichana wawili wa chumba hicho ambao aliwakuta wakiwa wanaanika nguo hapo nje. Ukawa ndiyo  mwanzo wa  mwanadamu huyo mwenye uwezo wa ajabu kufika hapo bwenini, akionekana ni mrembo ambapo baadhi ya wavulana walishaanza kumuwekea hesabu pindi alipokatisha mbele yao.

    YAKIJIRI HAYO UPANDE wa tarafa ya Mbagala, kwenye kata ya Mbagala kuu mtaa kibondemaji B. Mita chache tu kutoka ilipo shule ya msingi kizuiani, na mashariki ya msikiti wa mtaa huo. Watoto  kadhaa wa shule ya msingi wakiwa na fulana za rangi ya bluu, walifika kwenye nyumba mojawapo ya kupanga kwenye eneo hilo. Ambapo walikutana na mwanamke akiwa anafua nguo, huku akiimba nyimbo ilimradi kazi iweze kwenda vyema.

    Shikamoo  mama Hawa, Walimsalimia mkubwa huyo kwa pamoja ambapo aliwaitikia kwa bashasha kuu.

    Mama Hawa, mwalimu Eliza kasema Hawa akachukue ripoti yake, jana alitakiwa kuichukua ila hakuwepo, Mtoto mmojawapo alisema.

    Haya nitamwambia wanangu, mwenzenu kaenda kwa babu yake kumwona anaumwa kesho ataingia darasani kama kawaida. Tena  huyo hapo anarudi kaletwa na mjomba wake, Mama  huyo alisema na kweli walipoangalia upande wa kulia wa eneo alilopo walimwona binti mdogo mwenye kufanana kila kitu na yule wa kule chuoni, akiwa ameongozana na kijana ambaye alionekana  wa kipato cha chini.

    Watoto hao walimkimbilia na kuanza kuongea naye, ambapo hawakukaa sana walimwacha na kuondoka eneo hilo  kuwahi majumbani mwao.

    Mama yule alipomwona mtoto kafika aliacha kufua kabisa akabaki ni mwenye kumtazama, ambapo  alisogea hadi jirani naye na akionesha ni mwenye kuhakiki kitu. Kitendo hiko kilimfanya mtoto yule aachie tabasamu  pana  halafu macho yake yakatoa mwangaza  wa ajabu mno.

    Labat!, Mwanamama alisema kwa mshangao.

    Kwa mara nyingine tena tupo pamoja baada ya kuishi vile miaka miwili  iliyopita. Mniru yupo kazini nimeletwa kuja  kuchukua nafasi yake hapa nyumbani kwa usalama wako, Mtoto  huyo alisema  na kisha akamtazama  kijana aliyemleta halafu akasema, unaweza kwenda hivi sasa ewe mtumishi.

    Kauli hiyo ilipotoka, kijana akapotea  kimazingara na kubaki Mama Hawa pamoja na Hawa bandia. Ambapo hata kufua yenye hakuendelea zaidi ya kuingia naye ndani  pamoja,  walifikia kwenye kitanda wakaketi kwa pamoja.

    Nafikiri umesikia  kile kilichosemwa na  hao watoto hapo nje, Mama Hawa alisema.

    Lau kama ningelikuwa umbali wa kilomita kumi kutoka hapa ningeweza kuyapata yote. Mwalimu  Eliza Benson ndiyo  yule msichana aliyemaliza chuoni na kupangiwa kazi hapo ndiyo anamhitaji Mniru kufika shuleni

    Basi kazi kwako wacha nikamalize kufua hapo, nafikiri una mengi sana ya kunieleza huko utakapo

    Ukafue! Mbona mimi nimeshazimaliza zile nguo kwa macho tu pale  nilipozitazama, hivi sasa nimezianika chungulia hapo dirishani utaona,

    Kweli Mama Hawa aliangalia nje, aliona nguo zikiwa zimeanikwa na kubanwa na vibanio kabisa. Hapo alijikuta akitabasamu kwa kuweza kujiwa na kiumbe huyo, ambaye ni jini  wa kike na mwenye umri mrefu ndani ya himaya ya kijini ya Mazimifu.

    HABARI YA  KUJA MWANAFUNZI mpya hapo chuoni, tena akiwa ni mrembo kupitiliza mwenye asili ya uchotara. Ilizagaa chuoni hapo mithili ya moto  wa nyikani, ambapo ndani ya muda mfupi tu wavulana waliyopo hosteli walikaa macho tenge  kuweza kumwona mrembo huyo akitoka nje ya chumba alichofikia.

    Si hao tu hata baadhi ya wafanyakazi na wauza biashara wa hapo chuoni, walibaki  kimkao wa tayari kujionea uumbaji uliyotukuka ambao anao  mnyange aliyefika chuoni.

    Yaani hata mabinti waliyoanza kusikia  sifa zake, walishaanza kuingiwa na wivu wakataka kujua ni kipi haswa alichonacho, ambacho wao hawana hadi apewe pongezi zisizomfikia. Ndipo wakafika chumba anachoishi mara wamsalimie, au wajifanye wanahitaji kuongea na wengine waliyopo chumba hiko  hata kumweleza juu ya  mwenzao mmoja wa humo ndani hayupo majira hayo. Ilimradi tu kuweza kumtia machoni mwenye kuvutia namna hiyo.

    HATIMAYE HABARI ZIKAWAFIKIA kina Maria, ambao kwa pamoja walitumia maono  yao na kuweza kumwona jinsi alivyo msichana yule. Tena akiwa ni bashasha kwa kila mtu ambaye alifika  chumbani na kumsalimia, maono yao yaliwasaidia kubaini hilo lakini kila walipomwangalia usoni muda ambao wakitumia macho ya ajabu kumwangalia. Basi walihisi machozi yakiwalenga kama vile wamemulikwa na kitu chenye mwanga mkali.

    Hivi ni mimi tu au ni nyinyi?, Moza aliuliza huku akiwa ameketi kwenye kochi sebule ya kifahari, muda huo ambao walishapokea maelezo kutoka kwa Salmin. Ambaye alimchukua mpenzi wake na kuwaacha hapo wakiwasubiri.

    Mwenzenu yule mdada kila nikimtazama usoni nahisi machozi kunilenga. Si kawaida hii, Lucy alisema.

    Au ni lile bweni maana ndimo alipokuwa akilala Happy mule, isije ikawa kuna nguvu iliachwa  baada ya mauzauza yale, Mariam alisema.

    Labda, Moza akaitikia

    Haikuchukua muda mrefu, ambapo Salmin na Maria wakarejea kutoka chumbani walipokuwa. Walifikia kwenye kochi na kuketi, hapo  mabinti hawa wakawaeleza kila kitu juu ya walichokiona kule chuoni wakiwa hapo  kochini.

    Salmin na Maria nao waliona vilevile, ambao kile kilichowakuta wao walipoangalia na mwenzao kilimpata hikohiko. Salmin tu ndiye aliyeweza kuona vyema kilichojiri kule hadi kukawa ni hivyo, ambapo akili yake iligutuka na kubaini kuja  jambo baya ambalo linanyemelea.

    Mnamjua yule ni nani? Salmin aliuliza.

    Hatujui ndiyo maana tukawa  tunashangaa jinsi alivyo mrembo vile, Moza akasema.

    Mmoja wa binadamu mwenye nguvu za kichawi toka anazaliwa, mmoja wa  kati  ya wenye kusoma  mawazo ya ubongoni mwa watu. Mchawi  mkubwa kutoka Mazimifu, ambaye ni mtoto mdogo aliyemsumbua sana Maria akiwa ndotoni. Msaidizi mkubwa wa Nsungi aliyeandaliwa kama wakitwaa madaraka ya duniani., Salmin alisema na kuweka kituo kisha akaendelea, Yule  ndiye alifika kipindi mkiwa shuleni kama dada yake Lifa, ambaye baadaye alikuja kuwaingiza kwenye pori lile kubwa kabla  ya kuja kuwaokoeni na kukimbia nanyi eneo la mbali sana

    Mama yangu si bure Lifa atakuja sasa hivi huko chuoni, inabidi tumuwahi, Maria akasema

    nyinyi kuweni watulivu tu, kila kitu mfanye kama vile tulivyoongea na kuwapa maagizo. Sijaja peke yangu huku, nina jemedari hatari wa Majichungu ameshafika muda mrefu naye mtamwona tu. Jueni huyo mpo naye kundi moja. Lengo ni kuzuia dunia isitawaliwe na shetani au damu isimwagike. Diplomasia au  nguvu pasipo maafa ndiyo kitu pekee kinachohitajika kutumika. Mtakaoweza kumbana na Mutwe au Buzebdi ni nyinyi tu na siyo wengine ndani ya dunia hii

    Hapo sawa  kabisa, maana yule mshenzi bado sijamsahau balaa alilofanya kule shuleni. Ndiyo chanzo cha sisi kutumbukia porini hadi tukaja kuwa  hivi tulivyo hivi leo, Lucy alisema.

    Hakuna atakayeweza kutimiza ujinga wao, ikiwa tutazuia  Remse  wa kwanza asiamke wala Mutwe wasifike kule. Nitazama ndani kuepuka zaidi nijue chanzo cha ugomvi wao hawa  viumbe  wa jamii zinahusiana, nikijua nadhani pia nitawajuza ili mjue ni namna tunaweza kulikabili hili suala

    MAJIRA HAYO UPANDE mwingine wa nchini Tanzania, kwenye mkoa wa Iringa kandokando ya mto Ruaha kulionekana magari ya kifahari yakiwa yameegeshwa pembezoni mwa njia ipitayo porini kwenye msitu wa hifadhi hiyo. Huku kukiwa na watu watatu  ambapo wawili walivaa suti nyeusi huku mmoja akiwa amevaa shati jeupe na suruali sawa na wenziye. Tena iliyochomekewa  vyema kiunoni mwake.

    Wawili walibaki wakiwa wamesimama wima  huku mmoja akiwa amechutama ukingoni kabisa  mwa  maji, wala hajali ngwena wakali waliyopo humo ndani. Tena ndiyo kwanza aliyashika maji ila  hakuna kiumbe  mlafi wa nyama aliyeweza kumsogelea na kumvuta kwenye uwanja wao wa  fujo.

    Bwana yule akiwa amechutama namna hiyo, maji yalianza kutokota kama vile ni yenye kuchemka. Hali hiyo ilimfanya  arudi juu haraka sana, papo hapo aliibuka mtu kwenye maji akiwa ni mwenye  macho ya rangi ya njano. Huku mwilini amevaa nguo za magome ya miti, ambapo alipiga goti la kiheshima mbele yake.

    Nasikiliza amri yako ewe Atlaf Sabai, kiongozi wangu, Mtu huyo alisema.

    Kuanzia hivi sasa wewe ndiyo kiongozi  wa wenzako wote wa ukanda huu, unapaswa utambue  dhumuni letu lililokuwa likipiganiwa karne hadi karne litimie. Harakati mpya zimeanza  fikisha taarifa kwa wenzako. Kikao kikubwa kwa kila kiongozi wa kanda na watu wake wasaidizi  kitafanyika  leo hii makaoni kwangu. Unaweza kwenda

    Alipomaliza kauli hiyo Atlaf Sabai aliinuka wima kisha akageuka kurejea lilipo gari lake, huko nyuma alimwacha yule kiumbe mwenzake akijirusha ndani ya maji mithili ya  samaki.

    Alirejea  garini moja kwa moja akiwa amefuatana na wale wenye suti, ambapo alifikia kuketi kiti cha nyuma sambamba na wale wenzake. Motokaa ikaondolewa eneo hilo la porini, kuelekea upande wa kaskazini  mwa eneo hilo.

    Punde tu baada ya wao kuondoka upande mwa kushoto  mwa mto huo aliibuka mtu  mwenye nguo ya kijani ambazo hutumiwa sana na maaskari wa mbugani. Huyu alijitokeza mkononi akiwa na  kamera ambayo alitazama kwa furaha kisha akaanza kuangalia picha ambazo alizipiga.

    Nadhani itakuwa ni habari ya furaha zaidi, katika ufichuzi wa mila potofu, Alijisemea huku akigeuka nyuma na kuanza kupiga hatua, kuelekea upande mwingine kabisa tofauti na ule ambao Atlaf kapita.

    Bwana huyo akiwa na umakini mkubwa, aliweza kufika eneo ambalo kuna  mwinuko ambao  aliupanda na kuja kutokea sehemu  lilipo gari la wanyamapori likiwa limeegeshwa pembezoni mwa njia ya vumbi.

    Gari ikashika njia na kuondoka mahala hapo, mtu yule haikueleweka  lipi ni lengo lake la kupiga picha akiwa  kule kando ya mto. Akionesha ni mwenye kumpeleleza haswa Atlaf  Sabai.

    SIKU ZA KUKAA NYUMBANI kwa Happy nazo ziliyoyoma, hatimaye  zikafika  kikomo ikawa ni wasaa wa yeye kurejea chuoni aweze  kusoma kama kawaida maana vitu vingi vilimpita  kipindi yupo bila kushika chochote.

    Siku ya kuondoka asubuhi na mapema alipanda gari moja na rafiki yake kipenzi ambaye ni mwenye kuanza masomo chuoni hapohapo wakiwa darasa moja. Hivyo yeye akachukua wasaa wa kuwa mwenyeji wake  awapo huko chuoni.

    Ingawa na utofauti wa jinsia  baina yao, aliahidi angeweza kumfanya ajihisi si mpweke  wawapo mahali hapo hadi pale wanahitimu pamoja.

    Ndiyo ukawa  mwanzo wa Samar, ambaye mama yake mzazi alifika  kule nyumbani kwa akina Happy pindi alipokumbwa na mauzauza na kutoa ushauri murua kabisa. Pia ndiye  rafiki yake aliyemfahamu toka utotoni ambapo walicheza pamoja, walisoma pamoja  shule za awali na msingi kabla ya kutengana kutokana na elimu ya sekondari na chuo.

    Ambapo kijana huyo alianza  elimu yake ya juu kwingine, kabla ya kuja kuhamishiwa  chuo cha Sokoine  kutokana na huko alipotoka kukumbana na rungu la taasisi ya elimu ya juu. Lililopelekea kufutwa kwa leseni ya kutolea  elimu, hivyo wanafunzi wakahamishwa kwingine.

    Basi kwa pamoja wakafika  Morogoro ambapo kijana huyo aliongoza moja kwa moja hadi makao makuu, akiwa sambamba na mwenyeji wake. Huko alipokelewa na kufanyiwa usajili na hatimaye  akarejea kwa aliyemleta ambapo safari ya kuelekea chuoni  ilianza.

    Robo saa iliwatosha kuwasili, ambapo Samar alipokelewa moja kwa moja  na wenyeji wengine waliyompeleka bwenini kutokana na kupata  chumba baada ya mwanafunzi mmojawapo  kuhama huko.

    Huo  ndiyo ukawa mwanzo wa Samar kuwa muongoni mwa wanafunzi wa  SUA, hata ujio wake mahala hapo uliwaka  baadhi ya watu kwa kumwona kijana mwarabu mwenye weupe wa hali ya juu. Ambaye alianza kuvuma  kama ilivyo kwa Hawa, alipoweza kujiri hapo kwa mara ya kwanza akiwa kama mwanafunzi.

    VIBWEKA VIKAHAMIA  darasa la wanafunzi wanaosoma TEHAMA, kina Maria wakiwa wamejua tayari  wapo  darasani humo na mchawi mwenye cheo kikubwa na pia walihitajika kuchunga kila kitu juu ya agizo walilopewa. Somo  kila likiendelea ikwa ni mengine juu ya mengine humo ndani, ambapo mara kadhaa  kulitokea mpambano wa  kinafasi baina yao na Hawa baada ya kila mmoja kujijua ni adui  mkubwa wa mwingine.

    Hawa alihitaji kuwa karibu na Happy majira hayo, ambapo pamoja na kuishi naye chumba kimoja. Hakuweza kuwa na mazoea naye, kila alipojaribu kuongea ilimuwia vigumu mno maana binti alionesha kutohitaji  kuongea naye.

    Mara kadhaa akiwa darasani alijaribu kumsogelea, ila alipopiga hatua aliona eneo hilo analoelekea kunawaka moto tena ule wenye kuchoma hadi majini. Jambo ambalo humfanya hata asijaribu kumsogelea. Hakuelewa nguvu hiyo ni ya nani, maana aliamini kina Maria wasingekuwa na uwezo wa namna hiyo wa kumfanyia vibweka humo ndani.

    Jambo hilo likampeleka moja kwa moja ajaribu  kuwasiliana na mkuu wake na kumpa taarifa hiyo. Ndipo alipotoka na kuelekea chooni moja kwa moja, vyoo ambavyo havipo mbali kutoka zilizopo maabara za Tehama.

    Binti huyo aliingia ndani moja kwa moja, baada ya kubaini hakukuwa na kiumbe yeyote humo ndani ingawa kwake hilo halikuwa suala gumu kuweza kufanya maongezi hata wakiwepo mengine. Ila kutokana na namna aliyohitaji kufanya uwasilianaji. Ikambidi afanye hila, choo hiko kisiweze kuingiliwa na mtu yeyote yule mwenye uwezo wa kawaida.

    Akiona hilo limetimia na amefunga mlango wa chooni, alihisi ukifunguliwa na kisha ukabamizwa kwa nguvu hadi ukamfanya ageuka kwa haraka. Atazame ni  kiumbe gani huyo mwenye uthubutu wa kuvuka vizingiti kadha wa kadha alivyoviweka pale mlangoni. Loh! Ndiyo akakutana na  kikosi cha wasichana wanne, wakiwa wamesimama tenge huku wakimtazama yeye kwa macho  ya kebehi mabinti hao ambao ni kina Maria.

    Naona hamjaridhika hadi mmeamua kunifuata hadi huku, Hawa alisema kidharau kisha akatoa  simutamba yake mfukoni kufumba na kufumba kifaa hiko cha mawasiliano kikageuka kuwa mtaimbo mrefu.

    Akimalizia hilo hakukaa sawa, alihisi mvumo wa upepo  tu,  akasogea kando  na kuona pigo zito likimkwepa na kugonga ukutani. Ulisikika mtikisiko mkubwa wa ardhi baada ya tendo hilo, ila kwao hawakujali hata ndiyo kwanza walizidi kupambana  tu.

    Hawa huko alipohamia, alihisi upepo mwingine ukimjia usawa wa shingoni. Kwa haraka aliinama na hapo ngumi nzito kutoka kwa Lucy  ikakita kwenye mlango wa choo hadi ukavunjika vipande na

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1