Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Tarishi
Tarishi
Tarishi
Ebook193 pages2 hours

Tarishi

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook


    Kwa mujibu wa  taarifa zilizonaswa na majasusi, ni kwamba balozi za Marekani na Uingereza zipo hatarini kushambuliwa miaka kadhaa baadaye. Siku ambayo ilipangwa kwa muda mrefu, kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani angetembelea ubalozi wa nchi yake jijini Dar es salaam.

    Mashirika ya kijasusi ya nchi hizo yanaingiwa na mashaka makubwa, kutokana na habari walizopata bomu ambalo lingetumika kulipua lingetikisa jiji zima. Ndiyo hapo sasa inabidi EASA waingilie kati suala, na inakuja kubainika chimbuko la lote ni nchini Somalia.

    Majasusi watatu wanatumwa huko, akiwemo Norbert Kaila wanafanya kazi yao vyema. Shida inakuja ni pale wakitaka kuondoka, na hapo mmojawapo alishagunduliwa kuwahi kufika nchini humo hasa jimbo la Juba akafanya maafa ambayo yalipelekea awekewe kisasi.


    Inageuka kuwa operesheni ambayo ilikaribia kugharimu maisha yake, ili kufanikisha wenzake wengine watoroke na mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka hasa. 

LanguageKiswahili
PublisherMambosasa
Release dateFeb 23, 2024
ISBN9798224820740
Tarishi
Author

Hassan Mambosasa

  Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.     Elimu ya juu aliipata  chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.     Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika  hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni. 

Read more from Hassan Mambosasa

Related to Tarishi

Related ebooks

Related categories

Reviews for Tarishi

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Tarishi - Hassan Mambosasa

    DIBAJI

    Dar es salaam ndiyo mji mkubwa kuliko yote Tanzania, licha ya kutokuwa mji mkuu wa nchi ila ulizidi kwa kila kitu majiji yote. Ndiyo sehemu ambayo ni kitovu cha biashara haswa bidhaa zinazotoka nje ya nchi. Bandari yake ni kubwa sana, inayohudumia sehemu mbalimbali nchi nzima na mataifa ya jirani.

    Jiji hili ndiyo limebeba balozi nyingi za mataifa mbalimbali, kwakuwa mwanzo liliwahi kuwa mji mkuu wa nchi nzima. Kabla makao makuu hayajaja kuhamishiwa Dodoma, ila bado shughuli za serikali zilianzia huko.

    Ndiyo hapo sasa kwenye mji huu mkubwa kuliko yote, sehemu ambayo kunaongoza kwa idadi kubwa ya watu kuliko majiji yote. Kunatokea tishio kubwa, la shambulio la kigaidi, likilenga balozi mbili tofauti. Jambo ambalo linafanya majasusi wa nchi husika kutaka kubisha hodi.

    Iliwabidi wawasiliane na shirika la ujasusi Afrika ya mashariki (EASA), kabla ya kuchukua uamuzi huo. Ndiyo hapo walipewa agizo la kukaa kando, shirika la ukanda husika lingeifanya kazi hiyo.

    Ndiyo hapo waliteuliwa majasusi watatu, waliyokuwa na uzoefu mkubwa na mazingira ya Somalia kwenda kuifanya kazi hiyo. Zikipikwa data mbalimbali, kuficha utambulisho. Nao waliifanya kazi vyema, iliyowachukua muda mrefu kiasi kwamba majasusi wa kigeni wakaanza kuingiwa na mashaka.

    Shida inakuja kutokea ni baada ya mmoja wa majasusi hao watatu, kutambulika nchini Somalia kupitia operesheni aliyowahi kuifanya iliyojulikana kama UA AMA UFE . Hakujua kama mmoja wa familia ya adui aliyemmaliza, alishuhudia kila kitu na huyo ndiye akaja kuwapa habari wengine.

    Tarishi ni mtu ambaye anahusika kusambaza barua kutoka eneo moja kwenda jingine. Jasusi huyu alipachikwa kwenye taasisi isiyo ya kisheria ambayo ilihusika usambazaji jumbe za siri sehemu moja kwenda nyingine. Kuwawezesha wana mgambo kuwasiliana, pasipo mambo yao kuingiliwa na serikali.

    Shida ikaja baada ya operesheni kuisha, walishamjua ni mpelelezi na hata kundi jingine lililowahi kufanya naye kazi, liliyataka maisha yake kwa namna zote. Akaanza kuwinda na makundi zaidi ya mawili kila mmoja akitaka kumwangamiza.

    Suala hilo lilimbidi kwa wepesi wa hali ya juu ajitoe sadaka, wanamgambo wamkimbize yeye. Huku wenzake waliyokuwa na mtuhumiwa muhimu kwenye operesheni watoke salama mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Yalikuwa maamuzi ambayo yalipelekea akione kifo, mpaka ilifika wakati alikaribia kukata tamaa na kufahamu siku yake ilifika. Ni Tarishi huyo.

    1

    __ Somalia .

    Kijana machachari aliyekata nywele zake kwa mtindo wa panki, akiwa na sharafa zilizochongwa kwa ufasaha mpaka zikaja kuunganika na ndevu za wastani zilizofugwa na kuchongwa vyema. Huyu alivaa kanzu nyekundu, ambayo kwa juu upande wa kifuani ilifunikwa na kijambakoti. Begani alizungukwa na mkanda wa mkoba, ambao ulikuja kushuka mpaka chini ya kwapa. Mguuni alivaa kiatu cha wazi maarufu kama kubadhi, kilichoundwa kwa kutumia ngozi.

    Huyu alikuwa akipiga mwendo katikati ya mtaa uliyochangamka, akipishana na watu  kadhaa waliyo kwenye hamsini zao. Wasimjali tu kwakuwa hawakufahamiana naye, na wale yeye hakuwahi kuwaona kabla. Walizingatia ile kauli kama haujuani basi ni kubishana tu.

    Ulimwengu ule wa kutoleana salamu kila tunapokutana, ulishadidimia siku nyingi. Umebaki huu wa kupishana kama mabubu, ikiwa hakuna anayejuana na mwenzake. Ule upendo uliyoundwa kulingana na jamii kushirikiana, haukuwepo tena. Nani angeanza kuchangamkia tena, ndani ya mji ambao huhesabika kama mji  hatari kwenye nchi hiyo.

    Ndiyo maana bwana huyu hakujihangaisha, wala kushangaa wengine kutojihusisha walau kumsabahi kila alipopishana nao. Ila napo matembezi yake hayo, alikuja kushangazwa hasa na jambo ambalo lilijiri ghafla. Pasipo matarajio yake mwenyewe, katika eneo hilo ambalo alikuwa na uhakika hakuna anayemjua hata mmoja.

    Akiendelea kukaza mwendo napo alifika kijana aliyekuwa akielekea umri wa kubalehe. Huyu alimziba njia ghafla, na alimtazama kwa umakini mno na kisha alimsukuma kwa nguvu mno. hadi mwanamke aliyekuwa ameongozana naye alishangazwa sana na jambo hilo. Hata kabla bwana yule hajatafakari kuhusiana na kitendo kile, kijana yule alirusha ngumi ya haraka sana kuelekea kwake ambayo aliishia kurudi nyuma upesi ikapita. Alipofanya tendo hilo aliishia kuambiwa, muuaji wewe! Sitakuwa na amani mpaka na wewe nikuue,. Alipoanza kusema hivyo yule mwanamke alimshika kwa nguvu, huku akimuusia kutulia na aache kufanya fujo.

    Bwana yule alibaki akishangaa tu, imekuwaje mpaka afikie kutamkia neno lile. Aliishia kusimama huku akimwangalia tu, muda ambao alikuwa akihangaika sana kutoka mikononi mwa mwanamke mrefu aliyevaa juba ambaye alimkamata vilivyo. Alipiga kelele aachiwe ila napo haikutimizwa hilo, mpaka baadhi ya watu walijaa na kushangaa tukio hilo.

    Ilimbidi yule mwanamke aongee, niwie radhi kaka, huyu mpwa wangu akili zake hazipo sawa. Si mara ya kwanza kumshambulia mtu kama hivi. Leo alikuwa mtulivu nikaona nije naye kutembea, kumbe bado tatizo lipo. Alipokuwa akiongea hayo napo mwanaume wa kisomali mwenye mwili mnene akiwa amevaa kanzu nyeusi na kofia nyeupe ya kufuma alifika. Huyu alisaidiana naye kumwondoa hapo, wakielekea upande ambao kulikuwa na gari.

    Bwana yule aliishia kusikitika tu, kisha alizungusha jicho lake kila pande. Aliona watu kadhaa wakimshangaa, ambao aliwapuuzia na kuendelea na safari yake. Siku hiyo ilionekana wazi hakutarajia kukutana na kijana mdogo kama yule, aliyekaribia kumharibia siku kwenye mji huo hatari. Isingelikuwa yule mwanamke kufafanua utata huo, muda huo angelikuwa na mashaka makubwa ya usalama wake.

    Nani asiyepajua Mogadishu? Miongoni mwa watu waliyoishi hapo Somalia, mji mkuu wa nchi hiyo ambao umekuwa na matukio lukuki ya kila namna. Mpaka kuja kutajwa moja ya sehemu hatari ndani ya nchi hiyo, kukiwa na watu wa aina mbalimbali wakikatiza huku na huko. Mbaya usingeweza kumjua ni nani, na wale mwema vilevile. Heri hata ungeonekana na asili yao moja kwa moja, wakati wakikuandama hivyo.

    Shida bwana huyo alibeba asili si ya jamii za kikushi, wapo ambao wangemshambulia tu kwa kusikia akiitwa muuaji pasipo kujulikana kama aliua au la. Kisa tu si mwenzao, na hata nafasi ya kujitetea asingekuja kuipata pia. Au kama angeliondoka salama basi angewezwa kuwindwa na wahuni, na wa bahati tu siku zake zingebaki salama ndani ya mji huo, uliyojaa migogoro ya mara kwa mara.

    NIMEKWAMBIA MARA NGAPI huyu Amin bado hajapona, abaki nyumbani. Ona sasa, mwanaume yule ambaye alisaidiana na mwanamke kumwondoa kijana, alilalamika wakati huo akiendesha gari.

    ana mwezi sasa hajafanya kitu kama hichi, amekuwa akikutana na watu wengi na kuongea nao kwa furaha. Sikuona ajabu kumwacha akafurahi mjini

    Wakati mwingine uache ubishi, unajua leo angemsababishia matatizo mangapi yule bwana. Asingekuwa muungwana unafikiri yangefika wapi, mwache akae nyumbani huyu

    Lawama zote alipewa mwanamke yule, kwa kumwacha kijana akiwa mwenyewe mjini. Kumbe bado hali yake kiafya haikutengemaa, alikuwa akituhumu watu mara kadhaa kwa matukio tofauti. Ndiyo hapo akaja kumbebesha lawama mgeni, ambaye hawakumjua alitoka wapi. Waliishia kuomba radhi na kuondoka mara moja, kusudi asije kufanya kituko kingine ije kuwa aibu kwao.

    siku ya Idi huyu ulimwacha hivyohivyo, ila akaja kumtuhumu mchinjaji wa mbuzi kwa ajili ya kitoweo ni muuaji, akisema kamuua mama yake. Fujo aliyofanya pale mpaka tulimfunga kamba kabisa na kumfungia ndani, ilikuwa ni aibu mbele ya wageni, aliendelea kulalamika uso wake aliukunja hasa, akionesha hakufurahishwa na jambo hilo hata kidogo. Mwanamke aliishia kunyamaza kimya, huku bado kamshikilia kijana huyo ambaye alitulizana kimya garini, hakuendelea kuleta vurugu toka walipoanza safari hiyo.

    BWANA KANZU NAYE ALIKUJA kufika hadi kwenye mlango wa ofisi moja, huo aliufungua na kuingia ndani. Alikuja kutokea kwenye chumba chenye ofisi ya wastani, mahala hapo alimkuta mwanaume aliyevaa kanzu nyeupe. Huyo alikuwa na ndevu nyingi hasa, pasipo kuwa na sharubu hata thumni juu ya mdogo wake. Huyo aliketi kwenye kiti cha kuzunguka kilicho mbele ya meza zenye mafaili kadhaa juu yake.

    Naye alifikia kuketi kwenye kiti cha wageni, huku akimpa jicho mtu yule mwenye asili ya usomali aliyeshika kiko mkononi mwake. Aliyeishia kuachia bashasha kwa kumwona kwake eneo hilo, ila hakutia neno lolote zaidi ya kuweka ukimya pekee huku akiangalia tu. Ilionekana wazi hakutaka kuongea wa kwanza, ila alihitaji kupewa neno ndiyo napo aanze kuchagua cha kusema naye kulingana atakachoelezwa.

    Bwana yule ndiyo alisema, barua za leo zimefika salama zote, kazi haikuwa ngumu kuliko siku zingine. Sikuulizwa maswali na wapokeaji wake, mpaka nikafikia kuingiwa na ugumu wa kinamna yake

    ndiyo changamoto ya hii kazi, ingawa teknolojia imeendelea sana. Sisi ndiyo salama kufikisha ujumbe popote pale. Chunga tu usije kupewa tuhuma ya kufungua bahasha yeyote, kuna watu wameshachanganyikiwa na maisha yao hawachelewi kukubatiza hukumu mbaya kama hiyo.

    ndiyo maana sijibu maswali ya hovyo nitakayoulizwa nao, maelezo yangu yakija kulingana na shaka zao basi nitakuwa nimejikangaa

    "safi sana, epuka kujieleza kupitiliza. Kazi yako ni kufikisha barua tu, na si kumpa ufafanuzi wa zaidi

    Licha ya dunia kuendelea na mifumo ya mawasiliano kuimarika, kufikia kuwepo kwa mawasiliano ya simu, baruapepe, na hata namna zingine. Bado mfumo wa barua haukuwa umepewa kisogo, uliendelea kutumika kwa watu kutuma kwa kupitia shirika la posta. Bado masanduku ya anuani hayakuwekwa kando, yalipewa matumizi pia kulingana hali ilivyo.

    Si tu shirika la posta bali hata upande mwingine wa pili, njia hiyo ilikuwa ni muhimu salama kabisa kwa usambazaji wa barua. Ilihusu wanaharakati wa gizani na wale wanaokinzana nao. Walitumia hasa barua kuwasiliana mmoja baada ya mwingine, kwakuwa njia za mawasiliano zingine hazikuwa salama kwenye maendeleo ya sayansi ya teknolojia.

    Ndiyo hapo jijini Mogadishu kuliundwa kikundi cha wasambazaji habari kutoka mtu mmoja hadi mwingine, hicho kilikuwa na taarifa zote za wahalifu na hata wale wa ujasusi waliyopo hapo mjini. Walihusika kuchukua ujumbe kutoka kwa mtu mmoja, kupeleka kwa mwingine. Walitumia watu wenye ujuzi wa kutumia silaha na mapigano kuifanya kazi hiyo, ili ikitokea wameingiliwa basi iwe salama.

    Barua zote zilizofikishwa kwao, ziliandikwa kwa namna maalum. Zingine hata kutumia michoro isiyoeleweka kwa umma. Kusudi hata ikija kufika mikononi mwa adui, basi asijue ilimaanisha nini. Mlengwa pekee ndiye aliyeweza kuelewa kila kitu, kuanzia mwanzo hadi mwisho.

    Zilitumika bahasha maalum zilizofungwa vizuri, na zikitakiwa kutofunguliwa abadani mpaka zije kufika huko zilipotakiwa. Endapo ingetokea mfikishaji akafungua bahasha, mlengwa alikuwa na haki ya kumuua mara moja, kikundi kinachohusika na kusambaza barua hizo kisingelaumu kwa lolote. Moja ya sheria na hukumu kwa aliyefungua mzigo wa mteja, ni kifo hapohapo hakuna mjadala.

    Ndiyo bwana huyu makanzu aliifanya kazi hiyo ya hatari, aliyotakiwa kuipa umakini hasa kama alipenda maisha yake. Alipokuwa akibeba barua toka eneo moja kwenda jingine, alitakiwa awe macho muda wote mpaka atakapokuja kufikisha ujumbe eneo husika. Napo kurejea iwe hivyohivyo, hadi alipokuja kufika ofisini kwao.

    Kikundi chao kiliwindwa kwa udi na uvumba na wanausalama mbalimbali, walitaka hasa kumkamata mmojawapo kwa gharama yeyote ile. Sababu walibeba taarifa nzito hasa na wakijua maficho mbalimbali ya majasusi hadi vikundi vya wanamgambo.

    Hawakutakiwa kutoa siri yeyote ile, kazi yao ikawa ni kusambaza ujumbe namna hiyo muda wote. Pesa waliyopata ilitosha wazi kuwafanya wasiwe na shida yeyote ile mjini na waliishi maisha waliyoyataka.

    UNA UHAKIKA UMEMWONA hapa mjini?

    macho yangu hayawezi kunidanganya Kamanda, nimepishana naye hapa ila nimeshangaa sana jinsi alivyovaa. Sura yake hata niamshwe usingizini ninaijua

    sasa umeshamjua ni yeye unatakiwa kumfuatilia hadi ufahamu ni wapi anapoishi. Hatuhitajiki kutumia nguvu tena kupata tunachokitaka, tumeshajua hatuwezi kufanya hilo

    laiti kama ungenipa amri ya kutumia mapigano tena, ningekuona wa ajabu sana. Nimepoteza wenzangu kwa mikono yake, bwana yule ana shabaha sana kama na darubini ya ulengaji machoni mwake

    nina akili timamu ndiyo maana nikakushauri tubadili, uliponieleza wazi nishajua tunapambana na mtu wa aina gani. Fikiria kama tungetumia njia zetu hizi, basi hasara ni ileile. Naona tubadili mbinu sasa, kwanza tujue anapoishi ni wapi

    Yalikuwa maongezi baina ya wanaume wawili ambao walijifunga misuli pekee,  iliyoanzia juu ya kitovu kushuka chini. Waliketi kwenye busati ndani ya chumba chenye madirisha mapana yaliyofunguliwa wazi. Eneo hilo hakukuwa na kingine chochote, zaidi ya tandiko hilo. Si samani wala vitu vingine, ndiyo wawili hao walikutanika na kuzungumza.

    Ilionekana wazi walimtafuta mtu, bahati ikawa nzuri kuja kumwona wakiwa hapo mjini. Walitaka sana kumshika na kupata taarifa muhimu, shida ikawa huyo waliyemfuata naye hajambo hasa kuliko ilivyo wao.

    Nguvu haikuwa na maana

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1