Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5
Ebook34 pages23 minutes

Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Liv Løkke ana majinamizi, baada ya moto ule na maisha ya awali kuletwa kwa ulimwengu wake wa sasa. Anne Larsen anawasiliana naye. Mwanahabari huyo amemtembelea kakake, na ana hamu kubwa ya kutaka kujua kile alichotaka kutoka kwake, hata anakubali shingo upande kukutana naye kwenye hoteli moja mjini Rhanders. Lakini madai ya mwanahabari huyo yanamkasirisha sana; anaondoka hotelini humo akiwa na ghadhabu. Anapoona tangazo kwenye gazeti kuwa mwanawe Johan Boje alimuona muuaji, anaenda nyumbani mwake Johan Boje kukutana na mwanawe mbele ya mahali alipozikwa babake.
LanguageKiswahili
PublisherSAGA Egmont
Release dateOct 8, 2019
ISBN9788726283587
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5

Read more from Inger Gammelgaard Madsen

Related to Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5

Related ebooks

Reviews for Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 5 - Inger Gammelgaard Madsen

    purchaser.

    Hisia ya Hatia Ichomayo

    Sura ya 5

    Moto ulichoma kwa ukali usiostahimilika. Ulibadilisha ngozi kuwa malengelenge ambayo yaliumiza yalipopasuka. Alitazama mikono yake kwa macho yaliyokuwa yakiteketea na kuona kano na mifupa zikitokeza, huku ngozi pembezoni ikiyeyuka polepole. Alimsikia mamaye akipiga nduru; nduru iliyofika kwa mpigo kwenye ubongo wake uliokuwa ukichemka. Miguu yake ilikuwa imelemazwa, kama aliyekwama ardhini. Kisha akamwona.

    Villads. Aliingia kwenye moto, polepole na kwa ukakamavu, kana kwamba haukumdhuru. Alitaka kupiga nduru ili kujaribu kumzuia, arudi Copenhagen akaishi huko, lakini koo lake lilikuwa likiteketea pia, na tumbo yake pia. Kilichotoka kinywani mwake ni ndimi za moto pekee, kana kwamba alikuwa zimwi. Ghafla, alivutwa ndani ya moto. Alipigana, akatapatapa kote, lakini hakukuwa na kitu chochote cha kushikilia. Alijaribu kumwita Villads, akajaribu kumwita mamaye, lakini alikuwa peke ndani ya moto uliokuwa umegeuka kuwa jinamizi kubwa jekundu lenye macho ya uovu na ulimi unaoyumba wa moto. Ulimfikia kwa urahisi na kuanza kumchoma, sehemu baada ya sehemu. Alipiga nduru.

    Liv aliketi kitandani mwake kwa mshtuko. Nduru hiyo ilikuwa imemwamsha. Jasho liliteremka kwenye paji la uso wake na mikono yake yalikuwa na majimaji alipojaribu kuifuta ndoto hiyo usoni mwake.

    Kulikuwa giza nje ya dirisha, na nambari nyekundu, ya kidijitali kwenye saa yake ya kengele zilisoma saa 7:35 usiku. Polepole, alituliza pumzi yake. Ilikuwa ni ndoto tu, hata kama ilionekana kuwa kweli.

    Ndoto za kutisha zilikuwa zimeanza tena. Ilikuwa ni kosa lake: John Boje. Alijilaza kwenye shuka lililoloa jasho. Blanketi lake lilikuwa kwenye sakafu, lakini  alihisi joto, kwa hivyo akaliacha huko. Aliangalia juu kwenye dari, akiwa na hofu kuwa jinamizi hilo litarudi akifumba macho yake tena.

    Saa ya kengele ilipoanza kulia, aligundua lazima alikuwa amelala tena, kwa sababu ilimshtua na kumwamsha. Alijitahidi kuketi na alikuwa karibu kuangukia blanketi iliyokuwa sakafuni, ndipo akasimama. Saa ya kengele ilikuwa daima juu ya rafu katika chumba, hivyo ilimlazimu kusimama ili kuizima. Vinginevyo, angelipuuza tu na kuendelea kulala.

    Kwa nini alikuwa ameiweka ilie mapema hivyo? Alikuwa na likizo siku hiyo,  aligundua ghafla. Alitakiwa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1