Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mnadhifishaji Tukio la 3: Jaketi
Mnadhifishaji Tukio la 3: Jaketi
Mnadhifishaji Tukio la 3: Jaketi
Ebook39 pages28 minutes

Mnadhifishaji Tukio la 3: Jaketi

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Bertram anaogopa kuenda kwa polisi kuwaambia kuhusu kile alichokipata kwenye jaketi aliyoiba kwani yeye ni mhalifu anayesakwa na hataki jambo lolote linalihusiana na utekelezaji wa sheria. Jioni moja anajaribu kupiga simu bila kujitambulisha huku akiwa amelewa na baada ya kuvuta sigara kadhaa, ila polisi wanakataa kumuamini. Baadaye wakati Bertram anagundua kuwa maisha ya mama yake yamo hatarini, anajaribu kumuonya ila pia mama yake hamuamini. Bertram anaanza kumfuata mama yake na kutambua kuwa anakutana na mwanamume ambaye Bertram hamfahamu.

Wakati Bertram anamuuliza mwanamume yule ni nani, mama yake hatimaye anakubali kuwa yule ni mpenzi wake na kuwa wanapanga kuondoka katika eneo lile na kuanza maisha mapya pamoja. Bertram anaamua kupekua ili kujua anapoishi mwanamume huyu, na kuvunja nyumba na kuingia ili kugundua yale atakayoweza kuhusu mwanamume huyu. Anapoangalia vitu vya mwanamume huyu, anapata mkusanyiko wa pasipoti ghushi, na picha ya mwanamume yule akiwa amevalia jaketi ile ambayo Bertram alikuwa ameiba.



The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.
LanguageKiswahili
PublisherSAGA Egmont
Release dateSep 11, 2019
ISBN9788726270808

Read more from Inger Gammelgaard Madsen

Related to Mnadhifishaji Tukio la 3

Related ebooks

Related categories

Reviews for Mnadhifishaji Tukio la 3

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mnadhifishaji Tukio la 3 - Inger Gammelgaard Madsen

    purchaser.

    Mnadifishaji

    Tukio la 3:6

    Jaketi

    Bertram akashtuka wakati kengele ya mlango iliita. Akazima sigara lake kwa haraka kabla ya kuufungua mlango.

    Felix akaingia ndani na wote wakaelekea katika chumba cha Bertram wakiwa kimya.

    Je, uliona video zile? Bertram akauliza kwa sauti iliyokwaruzika. Hakuwa ameweza kumfikia Felix wikendi nzima kupitia simu. Felix na wazazi wake walikuwa wamekwenda nchini Sweden kusherehekea siku yake ya kuzaliwa baada ya kufikisha miaka 16 pamoja na babu na nyanya yake, walioishi kule, na simu yake ya rununu haikuwa imetengenezwa kupokea simu za kimataifa.

    Una uhakika video zile ni za kweli? Felix akauliza, huku akionekana kumeza kitu mara kadhaa.

    Matukio ya mauaji pamoja na ajali ile ya barabarani yametajwa katika gazeti na kwenye runinga.

    Na inadhihirika kuwa hayakufanyika kwa jinsi yalivyoelezwa.

    Tutafanya nini, Felix?

    Bertram akaketi kitandani mwake huku akimwangalia Felix kwa huzuni. Felix ndiye alikuwa mwerevu katika kikundi chao, na walipoongea kwa simu walikuwa wamekubaliana kuwa hawangeenda kwa polisi kwa vyovyote vile na kuhatarisha wao wenyewe kuanza kuchunguzwa.

    Itatubidi kuchunguza mmiliki wa jaketi ile. Ikiwa tutaweza, huenda tutapata njia ya kumuripoti kwa polisi.

    Ila, hatujui iwapo mmiliki huyu ndiye anayewaua watu hawa…

    "Felix akaketi katika kiti cha dawati yake Bertram na kukuna nywele zake zenye rangi ya shaba. Siku ya leo hakuwa amezifunga juu ya kichwa chake bali aliziacha kuninginia hadi kwenye mabega yake.

    Diski ile ya hifadhi ilikuwa katika jaketi yake. Hivyo ni kwa nini awe anatembea nayo?

    Bertram akakubali.

    Ilikuwa vyema kuwa na mtu ambaye angeweza kuzungumza naye kuhusu yaliyokuwa yametendeka. Yeye na mama yake walikuwa wamekasirikiana kwa siku kadhaa sasa. Wakati hili lilitendeka, hawakuwa wakizungumziana na kila mmoja alijaribu kumkwepa mwenzake jinsi awezavyo, jambo ambalo lilikuwa gumu kufanyika katika nyumba yao yenye vyumba viwili. Ila haikuwa kwamba mama yake Bertram aliamini kile Bertram alikuwa amesema.

    Wakati alikuwa ameweza kumridhisha mama yake kuangalia ukurasa ule wa siri kwenye kipakatalishi chake, muunganisho kwenye mtandao haukuwa dhabiti kutokana na kosa la seva kutoka kwa mgavi wao, na Eva Maja alikuwa ametikisa kichwa na kumuita mwongo aliye na ubunifu usio dhahiri kwa mara nyingine. Eva Maja alimshutumu Bertram kuwa yeye ndiye alikuwa ametengeneza ukurasa ule huku akijaribu kuwaogofya wengine.

    Mambo haya yote sio kuwa yanakuhusu kwa njia yoyote, Bertram: mlinzi wa jela na wakili, na hakuna unayemfahamu kati yao. Inawezekana kuwa wao walistahili kufa, sawia tu na mwanamume ambaye baba yako alimuua.

    Bertram akashtuka kwa kumbukumbu ya baba yake na kutikisa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1