Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mnadhifishaji
Mnadhifishaji
Mnadhifishaji
Ebook217 pages2 hours

Mnadhifishaji

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Bertram na marafiki zake watatu wameanzisha genge ndogo la majambazi linaloitwa The Hawks. Anaishi peke yake na mama yake, anayefanya kazi kama mhudumu hotelini. Hamkumbuki baba yake sana, kwa kuwa alikamatwa kwa makosa ya mauaji na kufungwa kifungo cha maisha Bertram akiwa umri wa miaka misaba pekee. Siku moja, Bertram aliiba jaketi ya ngozi ya bei ghali yenye chapa ya "Schott Made in USA" kutoka kwa mkahawa, ambayo ilimletea matokeo mabaya sana, na si kwa Bertram pekee. Rolando Benito, mpelelezi katika Mamlaka ya Malalamiko ya Polisi, na wenzi wake walitumwa ili kuwauliza maswali maafisa wawili wa polisi. Mlinzi wa gereza alikuwa ameruka nje ya dirisha lake katika ghorofa ya nne, huku maafisa hao wawili wakimvuta, baada ya malalamiko ya kelele nyingi iliokuwa ukitoka kwenye nyumba yake. Kwa kuwa mlinzi huyo wa gereza alikuwa baba ya rafiki wa shule wa mjukuu wa Rolando, yeye husikia uvumi kwamba mfungwa alikufa ndani ya gereza ambalo mtu huyo alikuwa akifanya kazi, na kwamba mlinzi wa gereza alihisi ametishwa na kuteswa. Kwa hivyo mwishowe hii si kesi ya kujitoa uhai? Anne Larsen, mwanahabari wa TV2 East Jutland, ako pia katika kesi hii. Kila mtu anaonekana kuwa na uhusiano na mfungwa mmoja, muuaji Patrick Asp, aliyeua mtoto wake mwenyewe mchanga na ni mfungwa katika gereza ambalo mlinzi huyu wa gereza alikuwa akifanya kazi. Vifo hivi vya kutatanisha vikiendelea kuongezeka, na hakimu wa Mahakama Makuu akipotea bila kugunduliwa, Rolando Benito na Anne Larsen wanaunganika wakitafuta uhusiano. Uhusiano huo unapatikana kuwa ni Bertram na wizi wa jaketi, na sasa Anne ako hatarini pia.
LanguageKiswahili
PublisherSAGA Egmont
Release dateSep 11, 2019
ISBN9788726270778

Read more from Inger Gammelgaard Madsen

Related to Mnadhifishaji

Related ebooks

Related categories

Reviews for Mnadhifishaji

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mnadhifishaji - Inger Gammelgaard Madsen

    Mnadhifishaji

    Inger Gammelgaard Madsen

    Mnadhifishaji

    SAGA

    Mnadhifishaji

    Original title:

    Sanitøren

    Copyright © 2017, 2019 Inger Gammelgaard Madsen and SAGA Egmont, Copenhagen

    All rights reserved

    ISBN: 9788726270778

    1. E-book edition, 2019

    Format: EPUB 2.0

    All rights reserved. No part of this publication may be reproduced, stored in a retrieval system, or transmitted, in any form or by any means without the prior written permission of the publisher, nor, be otherwise circulated in any form of binding or cover other than in which it is published and without a similar condition being imposed on the subsequent purchaser.

    Mnadhifishaji

    Tukio la 1:6

    Orodha

    Lilikuwa lenye upana zaidi kati ya mabega, na lenye harufu ya ngozi mpya na tumbaku. Lilikuwa la rangi ya brandi, na kutoa sauti ndogo ya mkwaruzo alipoinamisha mkono wake kuwasalimu wengine, kwa kile walichokiita ishara ya genge lao.

    Ilijumuisha kila mmoja kugonga kifua chake kwa gundi, kisha kuleta kidole cha shahada na cha kati kwenye panja la kulia, na kisha kugongana gundi kila mmoja kivyake.

    Jack ndiye aliyeibuni. Yeye hakupendezwa na jambo lolote lenye utaratibu; jambo lolote lile la kulazimishwa. Hii ilimfanya kupata utambuzi, na kwa wakati huo haikumlazimu kufanya kazi yoyote. Yeye ndiye alikuwa mkubwa kabisa kwa umri katika kundi lao na alipaswa kuwa mwanafunzi wa useremala katika msimu wa kupukutika kwa majani ila mama yake ndiye alimlazimisha kumuona mwanasaikolojia kwa sababu ya azma yake isiyo ya kawaida ya kuhesabu kila kitu na kurudia jambo hili tena na tena.

    Huku akiwa na kiburi katika sauti yake, Jack akawaambia kuwa mwanasaikolojia aliita hali yake Tatizo la Azma isiyo ya kawaida na Kufanya jambo na Kulirudia tena na tena. Kwa sasa, alikuwa na kitu ambacho wenzake hawakuwa nacho.

    Bertram alitamani kupata utambuzi pia. Alikuwa akitafuta kazi tangia alipokamilisha Mitihani yake ya Mwaka wa Tisa, baada ya kuamua muda mrefu hapo awali kuwa hataenda katika sekondari ya juu baadaye; ila kazi nyingi hazikupatikana.

    Huu ndio wakati alipokutana na Jack na wengine: The Hawks, ndivyo walivyojiita. Hii ilikuwa dhihaka ambayo haikufanywa kwa njia ya werevu kwa wale walioitwa "Nighthawks," kikundi cha raia binafsi nchini kote walioshika doria kwenye mitaa wakati wa usiku ili kudumisha amani.

    Hawks walikuwa werevu na katili, waliwawinda ndege wengine, na kubeba silaha tofauti tofauti zenye ncha kali zilizoongezwa; TheNighthawks lilikuwa tu kundi la watu waliokuwa wakikaa muda mrefu bila ya kulala wakati wa usiku.

     Alaaaaa, una jaketi ya kupendeza! Felix akasema, akionekana amependezwa sana; na kwa mara ya kwanza kuonekana akiondoa macho yake kutoka kwenye skrini iliyowaka ya kompyuta bapa, jambo lililofanya uso wake kuonekana umekwajuka zaidi na wenye kijivu kuliko ulivyoonekana mahali kwingine.

     Hivi uliitoa wapi wewe? Jack akaachilia moshi wa sigara kupitia mwisho wa mdomo wake huku akimtazama Bertram kwa kumshuku.

     Ehe, uliiba wapi? Kasper akauliza, huku akigonga ndipo.

    Kwenye mkahawa, Bertram akakubali, huku akiingiza mikono yake kwenye mifuko ya jaketi na kujaribu kujionyesha kuwa mjeuri. "Hii ni jaketi ya bei ghali: Schott, Made in USA."

    Sikufahamu Mrembo Eva alihudumia wateja bainifu vile," Jack akasema na tabasamu lililopindika, huku akidondosha jivu kutoka kwa sigara lake.

    Bertram alikasirika kila mara Jack alipomuita Eva Maja vile. Hakumuita ‘mama,’ alihisi jina hilo lilisikika kuwa la kitoto. Pia hakupendezwa na jinsi Jack alimtazama Eva kana kwamba yeye alikuwa mwanamume aliyekomaa na kuwa na uzoefu mkuu kwa mambo yanayohusisha wanawake. Alikuwa amepata rafiki mmoja tu msichana na ilichukua msichana huyo muda wa juma moja tu kuchoshwa naye.

    Kile Bertram alihisi kufanya kwa wakati huu ni kumpiga ngumi Jack kwenye uso ila alijua kwa hakika kuwa hili lilikuwa wazo mbaya. Azma yake ya kurudia jambo hili tena na tena ilikuwa ya kusababisha mauti pindi alipopata jinsi ya kutumia ngumi zake. Isitoshe alikuwa amejifunza mchezo wa kupigana ndondi. Alidai kuwa kufanya hivyo kulikuwa njia moja ya matibabu.

    Kama kawaida, Bertram alizamisha hasira yake.

    "Je, unafikiri TheHandler atataka kuichukua lakini?" Kasper akauliza, ambaye ndiye alikuwa sababu ya The Handler kuwawinda kila mara. Ilikuwa ni vyema kuwa aliweza kuuza vitu walivyoiba ila jamaa huyu mnene anayezeeka alikuwa akimkera Bertram. Alikuwa akiingilia shughuli zao sana ni kana kwamba alikuwa anawachunguza kila mara. Ni kwa nini tu hangetekeleza wizi wake kibinafsi?

    Bertram hakumuamini The Handler, na The Handler pia hakuwaamini The Hawks. Mara ya kwanza ilionekana kuwa raha wakati walikuwa peke yao na wakati wizi wa madukani ulikuwa ni mchezo tu. Kwa hakika walipata pesa kutokana na wizi wao wa sasa ila pesa hizo zilikuwa na gharama.

    "Sitaki TheHandler afahamu lolote kuhusiana na hili."

    Hivyo unataka kujiwekea mwenyewe? Kasper akaonekana ameshangazwa.

    Bertram akaketi chini kando ya Jack kwenye sitaha la mbao lililotazama mto.

    Jua lilikuwa limeamua kuipa siku hii ya mwezi wa Aprili mwanga na kuifanya kuhisi ni kama yalikuwa ni majira ya kuchipua. Bado alipendezwa na jaketi. Upepo bado ulikuwa na ubaridi

    Alitazama juu na kuangalia upinde wa mvua uliobandikwa juu ya Makavazi ya Aros, pale ambapo wageni walikuwa  kama madoa tu nyuma ya glasi iliyotiwa rangi. Upinde huu wa mvua ulionekana ni kama ni Kitu Kinachopepea ambacho Hakijabainiwa kimetua juu ya jengo kubwa la mraba lililokuwa na makavazi hayo. Ilionekana ni kana kwamba viumbe vigeni vya angani walikuwa wakipanga muda wao nyuma ya glasi ya jinsi ya kuvamia mji.

    Wakati wa usiku hakuweza kulala kwa sababu kwa kawaida yeye hulala hadi kufikia saa sita za mchana, aliketi kwenye kipakatalishi chake akiandika kuhusu mambo ya aina hiyo: Madubwana, wanyonya damu na pepo chafu; damu na hadithi za kuogofya. Angeweza kupata utambuzi kwa hakika ikiwa mwanasaikiatria angesoma mambo ambayo alikuwa ameandika. Akatema mate kwenye maji yaliyokuwa ya rangi ya kijani kibichi na hudhurungi kwenye mto na kisha kutikisa kichwa.

    "TheHandler hatakosa kuichukua akifahamu hili. Huenda akapata pesa kidogo kwa kuiuza na sisi…"

    "Nyamaza, Felix! Tulikubaliana kwamba tutakuwa tukijiwekea baadhi ya vitu. Sio lazima TheHandler ajue kila jambo," Jack akanguruma kwa hasira, na Felix akabadilisha mtazamo wake na kuuelekeza kwenye skrini ya kompyuta bapa na kujizamisha ndani kwa mara nyingine tena.

    Je, ulitoa kila kitu kwenye kipochi? Afadhali ungegawa, Jack akazidi kusema kwa hasira. Akarusha shina la sigara kwenye maji. Shina hilo lilianguka kando na pale ambapo Bertram alikuwa ametema mate.

    Hakukuwa na chochote kwenye mifuko.

    Hivyo, hauna ufahamu ni nani anayeimiliki? Na ikiwa ni ya polisi ama kitu kama hicho? Huenda hata ikawa ni yule aliyekushika jana usiku.

    Walikaribia kukamatwa wakati karani aliyekuwa kwenye duka la vitu vya kielektroniki alipogundua kile walichokuwa wakifanya. Ilikuwa ni sadfa kuwa kulikuwa na gari la kushika doria lililokuwa karibu kwani kwa kawaida huwa hawafiki kwa haraka vile. Konstebo mmoja alikuwa ameruka kutoka kwenya gari na kumshika Bertram kwenye kola ila Bertram aliweza kujiondoa pale na kukimbia.

    Ila polisi yule alikuwa ameona uso wake na angeweza kumtambua kwa haraka kwa alama ya kuzaliwa ya hudhurungi, yenye ukubwa wa sarafu ya Korona 10 kando ya jicho lake la kulia. Konstebo yule alimakinika sana na alama ile.

    Bertram akapandisha mabega kuonyesha kutojali.

    Na angewezaje kuhakikisha kuwa alama hiyo ilikuwa ni yake?

    Hiyo alama iliyoko nyuma ya bega. Ni alama ya kuchomeka?

    Bertram hakuwa ameitambua alama hiyo nyeusi, ilionekana kama mguso wa karibu wa sigara iliyowashwa.

    Ahaaaa , akasema kwa sauti ndogo.

    Jack akatabasamu tabasamu lake lililopindika mara nyingine. Akawaambia kuwa tabasamu lake lilipindika vile kwa vile alifanyiwa upasuaji wa kurekebisha dosari la mdomo- sungura alipokuwa mtoto. Wengine walidai kuwa ilitokana na vita ambavyo ndivyo pekee alivyoshindwa pale ambapo mpinzani wake alimgonga kwenye mdomo wa juu na hili likamfanya kuanza kufanya mazoezi katika kupigana ndondi. Kisha akatazama kitu kilichokuwa nyuma ya Bertram kwa macho ya kusinzia.

    "Shindwe! Tunapozidi kuzungumza kuhusu TheHandler, tazama ni nani aliyekuja kutuona."

    Bertram akageuza kichwa chake na kuona mwanamume yule mfupi mnene akitembea huku akivuka nyasi pale ambapo wanafunzi kadhaa walijishughulisha na kusoma wakiwa chini ya miti. Hata ikiwa hali ya hewa haikuwa kama ile ya majira ya kuchipua, kulikuwa na watu wengi katika Bustani la Mill.

    TheHandler akasita mbele yao na kujaribu kupumua. Maeneo ya makwapa katika shati lake yalijaa jasho.

    Niliwaza kuwa huenda mko hapa, kama kawaida. Nina kazi yenu ya usiku wa leo.

    Kazi yenye malipo? Jack akauliza, huku akitaka kusikika kama asiyejali.

    Kazi yenye malipo mazuri kwa hakika. Mtapata kiasi cha kawaida. The Handler akapanguza pua lake kwa kutumia sehemu ya nyuma ya mikono yake. Ila ninahitaji watu wawili tu kati yenu. Kazi hii inapaswa kufanyika kwa werevu zaidi, mwaona. Jack, itabidi uwe mmoja wao.

    Mbona mimi? Jack akateta.

    Ni wewe tu uliye na miaka 18 na una leseni ya kuendesha gari. Nina gari tayari. Kasper, unaweza kuenda naye. Ninafikiri wewe ndiye mwenye nguvu zaidi kuliko wote.

    TheHandler akawakazia macho wote wanne akiwa na nia ni kama kwamba hakuwahi kugundua jinsi walivyo hadi wakati huu. Hakuonekana kutambua mtazamo wa kuudhika alioupata kutoka kwa Jack ambaye kwa hakika alijifikiria kuwa mwenye nguvu zaidi. Hakika kuwa yeye ndiye alikuwa mjeuri kwa wote halikuwa jambo la kutatiza.

    Kasper akasimama akiwa tayari na kupanguza uchafu kidogo kutoka kwenye suruali yake. Kila mara alionekana mwenye wasiwasi wakati TheHandler alikuwa karibu. Bertram hakufahamu jinsi hawa wawili walijuana ila bila shaka mwanamume huyu alimuogofya Kasper  na kumfanya achanganyikiwe.

    "Hivyo tunapaswa kufanya nini basi?" Bertram akauliza, akiashiria Felix kwa kidole cha gumba.

    TheHandler akamtazama kwa muda kwa macho yake kengeza yaliyo mekundu kwa damu. Fununu zilikuwa kwamba alizamisha pesa zote alizozipata kutoka kwa wizi wao kwenye pombe. Hata hivyo, jambo la muhimu lilikuwa kuwa walipata mgawo wao, haikumjalisha Bertram kile TheHandler alifanya na mgawo wake.

    Unaweza kusaidia baadaye wakati bidhaa zitakapofikishwa kwa mnunuzi. Tuna maagizo ya kidogo ya fanicha bunifu zilizoko katika kituo cha hifadhi katika mtaa wa Hasselager.

    TheHandler akampa Jack kipande cha karatasi chenye anwani ya eneo moja viungani, na picha ya kiti cheusi. Walikuwa wameiba moja iliyofanana na hii hapo awali. TheHandler alikiashiria kama The Egg.

    Bertram hakuona lolote la kumpendeza kuhusu hili na aliona hasara kwani alielewa hakuna jinsi gharama yake ingekuwa Korona 70,000. TheHandler alikuwa bado anamtazama kwa shauku.

    Una jaketi nzuri sana, kijana. Ulipata pesa, sio? akauliza.

    Upepo baridi wa ghafla ulivuma kwenye bustani ni kama kwamba ilikuwa ishara na kuchakarisha matawi. Bertram akatetemeka.

    Ni…aa, nilihifadhi kiasi kidogo kila wakati ulipotulipa, akasema kwa sauti ya kichinichini.

    TheHandler akatikisa kichwa mara kadhaa huku ameinua nyusi zake ni kama kwamba hakuamini.

    Inaonekana ninawalipa pesa nyingi mno basi! Jaketi hiyo inaonekana kuwa ya bei ghali.

    Eva Maja alinipa kiasi kidogo cha pesa pia, akadanganya.

    Eva Maja? Mama yako? Hivi aliwezaje kupata pesa zozote akiwa anafanya kazi katika jalalani hilo?

    Hilo sio jalalani. Ni mkahawa mzuri.

    Mzuri! TheHandler akakoroma. Hakuna jambo zuri aidha katika eneo hilo wala mama yako.

    Akatikisa sigara kutoka kwa kifurushi chake na kujaribu kuwasha huku mkono wake ukikinga tishali kutoka kwa upepo. Kasper mara moja akaenda kumsaidia.

    TheHandler alikuwa bado anamwangalia Bertram, moshi uliokuwa ukipulizwa kutoka kwa mapua yake ukimfanya kuonekana kama zimwi lililokasirika.

    Na, mzee wako amekusalimu. Anasema amekukosa kukuona.

    Bertram hangeweza kusema jambo lolote. Akameza mara kadhaa na mpigo wake wa moyo ukawa wa kasi.

    Nasikitishwa sana nawe, kijana. Nilipokuwa katika jela, singeweza ikiwa mke wangu na watoto hawakuja kunitembelea. Mama yako pia haendi kumuona.

    Bertram bado hakusema lolote, na TheHandler akatikisa kichwa chake na kumuacha. Jack na Kasper walimfuata alipoondoka. Alikuwa anaenda kuwaelezea jinsi watakavyoingia ndani ya kituo cha hifadhi. Bertram alijua utaratibu huu.

    Felix hakuwa ameondoa macho yake kwenye skrini, hata wakati TheHandler alikuwa hapo. Alikuwa katika dunia yake yeye mwenyewe.

    Kwa ghafla, akajizaba kofi kwenye paja na kuanza kucheka kwa nguvu.

    "Vizuri! Nimeweza! Hakuna mtu katika cyberspace anaweza kuficha lolote kutoka kwa Felix!"

    Ulifanya nini? Bertram akauliza, huku akitabasamu kwa ajili ya kicheko cha Felix. Haikuwa mara nyingi ambapo hisia zake zilionekana kwa uwazi vile.

    Felix akageuza skrini kumuelekezea Bertram ila Bertram hakuelewa nambari zozote na alama za ishara alizokuwa akiona.

    Nini hiyo?

    Felix akachukua kompyuta bapa tena huku akionekana amekasirika. Akaandika kidogo na kumuonyesha tena skrini.

    Vema, hii ni rahisi kuelewa?

    Um, ni tovuti ya chuo cha sekondari, nini …

    Hauelewi? Nimeweza kuingia kwenye mfumo wa teknolojia wa shule ya sekondari ya ndugu yangu. Nimebadilisha asilimia yake ya kutokuwepo shuleni na kuiweka kuwa 0%.

    Felix akacheka tena, na Bertram akatikisa kichwa chake.

    Watagundua mabadiliko hayo kwa haraka, ama? Unafahamu unaweza kufungwa jela miaka mingi kwa kufanya hivyo, sio?

    Hakuna atakayejua. Sio kwa jinsi nimeiweka. Isitoshe, ninafanya hivi ili kujifurahisha tu.

    Sina mzaha, Felix. Polisi wanazidi kujiboresha katika mambo kama haya. Ikiwa watagundua kuwa ni wewe, basi...

    "Kisha? Hautakuja kunitembelea jela ama? Sio ati nimemuua mtu yeyote kama jinsi baba yako alifanya ama…" Felix akajibu kwa ukali, ila akajuta kwa mara moja.

    Tazama, niwie radhi kwa kusema hivyo. Ninaelewa sababu za wewe kukataa kwenda kumuona baba yako, wakati yeye… na kwa nini mama yako pia haendi kumuona.

    Itoshe kuzungumza kuhusu baba yangu, sawa? Bertram akasema kwa sauti ndogo huku amekaza meno. Na kuhusu Eva Maja, pia!

    Niwie radhi.

    Felix akazubaa akiangalia maji katika mto yakipita kwa uvivu. Mashavu yake yalionekana vyema hadi pale yanapounganika na paji lake la uso lililokwajuka lililoonekana leo kwani alikuwa amekusanya nywele zake zenye urefu wa kufikia mabega na kuzifungia juu kichwani. Bertram akamuangalia akiwa upande. Alifanana msichana. Kila mara yeye huwa si mchangamfu. Wawili hawa hawakufanana kwa lolote lile, ila jambo la ajabu ni kuwa alimjua Felix kwanza wakati yeye na Eva Maja walihamia katika jengo hilo la ghorofa; ambapo Kasper na Jack waliishi pia.

    Yeye na Felix walikuwa katika darasa sawa shuleni na kwa ufasaha walikuwa wamekua kwa pamoja katika uwanja uliokuwa na eneo la sherehe ya kula ikari ya umma katika majira ya joto; pale ambapo harufu ya bangi mara nyingi iliizidi ile ya ikari, na ambapo wanaume mara nyingi walibugia pombe sana na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe. Halikuwa jambo la kutisha kuona gari la polisi likisimamishwa pale baada ya watu wengine walioishi karibu walipochoshwa na kelele na mapigano. Ila maisha yalikuwa yamekuwa bora wakati ule, wakati kwa mara moja ilikuwa ni yeye tu na Eva Maja.

    "Ninasema tu, Felix… Uwe mwangalifu. Usimfanye TheHandler atambue ujuzi wako. Kwa hakika atajaribu kuutumia ili

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1