Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hatima ya Vibwengo 1: Wanajeshi Shupavu
Hatima ya Vibwengo 1: Wanajeshi Shupavu
Hatima ya Vibwengo 1: Wanajeshi Shupavu
Ebook32 pages20 minutes

Hatima ya Vibwengo 1: Wanajeshi Shupavu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Adui mwenye nguvu aliwasili kwenye nchi ya Vibwengo. Alitaka kumfanya mtumwa kila mtu anayeishi pale. Ikiwa Vibwengo wataokoka, watahitaji vyote ujasiri na matumaini.
Vibwengo walilikimbia jeshi la adui, na walilazimishwa kujificha msituni. Deizi akawa rafiki wa Kibwengo mdogo anayeitwa Humulus. Kwa pamoja, wakafanya ugunduzi ambao uliwawezesha Vibwengo kujibu mashambulizi dhidi ya adui. Je, watakuwa na nguvu ya kutosha?

Hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vinne vya "Hatima ya Vibwengo." Visome vitabu vyote katika mfululizo:
Wanajeshi Shupavu
Moyo wa Jabali
Makaburi Yaliyosahaulika
Filimbi ya Kichawi
LanguageKiswahili
PublisherSAGA Egmont
Release dateAug 27, 2019
ISBN9788726254594
Hatima ya Vibwengo 1: Wanajeshi Shupavu

Related to Hatima ya Vibwengo 1

Titles in the series (38)

View More

Related ebooks

Related categories

Reviews for Hatima ya Vibwengo 1

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hatima ya Vibwengo 1 - Peter Gotthardt

    purchaser.

    Hatima ya Vibwengo 1

    Wanajeshi Shupavu

    Hii ni hadithi ya moja ya enzi mbaya sana katika historia ndefu ya Vibwengo. Ilitokea wakati adui mkubwa pamoja na jeshi lake walipoingia kwenye nchi ya Vibwengo. Lengo lake lilikuwa ni kuwafanya vibwengo wote watumwa. Vibwengo walijawa huzuni na hasira. Adui aliiteketeza nchi yao nzuri na uhuru wao ulikuwa hatarini. Bila kusita, walijibu mapambano. Walijua kwamba walikuwa wanapigana kwa ajili ya hatima ya Vibwengo.

    Mti wa mwarobaini ulio kwenye ua la kasri ulizaa majani magumu, ya kijani. Kundi dogo la Vibwengo lilikaa chini ya mti. Mmoja wao alikuwa Malkia Veronika. Aliishi kwenye kasri pamoja na walinzi ambao waliapa kuilinda nchi ya Vibwengo dhidi ya tishio lolote.

    Leo, malkia aliwakusanya marafiki zake ili kusherehekea ujio wa masika. Kwenye meza mbele yao kulikuwa na mikate iliyookwa vema, mkate-tangawizi, matunda makavu na mayai mabichi.

    Haya ni majira yanayopendwa sana katika mwaka, alisema malkia. Pindi kila kitu kinapokuwa cha kijani moyo wangu hujawa furaha. Na mwaka huu, nina sababu nyingine ya kuwa na furaha. Nilikuwa na hofu kwamba watoto wangu wametoweka milele. Na sasa wamerudi kwangu.

    Alitabasamu na kumtazama binti yake, Daisy, na kijana wake, Bramble. Wamerejea hivi karibuni kwenye nchi ya Vibwengo baada ya safari ya hatari kupitia ufalme wa kigeni.

    Na wote mmekuwa wakubwa sana, Karafuu aliwaambia. Alikuwa mlezi wao walipokuwa wadogo.

    Daisy alikuwa mrefu karibia kama mama yake sasa. Kaka yake mdogo, Bramble, pia alianza kukuwa haraka.

    Nasikia umekuwa mjuzi sana wa kujilinda, Bwana Hazel, ambaye ameoa kwa Karafuu alisema. Alikuwa akimfundisha Daisy jinsi ya kujilinda miaka kadhaa iliyopita.

    Daisy ni bingwa! alisema Bramble.

    Daisy aliona aibu.

    Bramble yuko sahihi, alisema Bwana Blackthorn, ambaye ni mlinzi kijana. Alikuwa amewasindikiza

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1