Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mwanga Wa Usiku: Mfululizo Wa Vitabu Vya Kuunganishwa Kwa Damu Kitabu Cha Pili
Mwanga Wa Usiku: Mfululizo Wa Vitabu Vya Kuunganishwa Kwa Damu Kitabu Cha Pili
Mwanga Wa Usiku: Mfululizo Wa Vitabu Vya Kuunganishwa Kwa Damu Kitabu Cha Pili
Ebook281 pages3 hours

Mwanga Wa Usiku: Mfululizo Wa Vitabu Vya Kuunganishwa Kwa Damu Kitabu Cha Pili

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kat Santos alikuwa hajamuona mwenye kilabu cha Mwanga wa Usiku kwa miaka. Hiyo ilikuwa hadi Quinn alipoamua kumteka nyara ghafla na kumshitaki kuwa alimtega kwa mauaji yaliyo timizwa na wafyonza damu. Walipogundua kuwa adui alikuwa akiwachezea, familia zote mbili zinaunganisha nguvu zao kuwazuia wafyonza damu kuutisha mji wao.

Quinn Wilder alimuangalia kwa macho ya njaa ya simba tangu siku aliyozaliwa. Alipofikia ujana, hamu ya kumdai kuwa mwenzake kuligeuka kuwa mgawanyiko mkubwa kati yake na kaka zake waliyokuwa walinzi wake. Wakati baba zao walipouana vitani, mahusiano kati ya familia hizo mbili zili katika na aliwekwa mbali naye. Akimchungulia kutoka mbali, Quinn anaviona vita vya wafyonza damu kuwa na uzuri wake wakati Kat anasahau kukaa mbali naye. Kat Santos alikuwa hajamuona mwenye kilabu cha Mwanga wa Usiku kwa miaka. Hiyo ilikuwa hadi Quinn alipoamua kumteka nyara ghafla na kumshitaki kuwa alimtega kwa mauaji yaliyo timizwa na wafyonza damu. Walipogundua kuwa adui alikuwa akiwachezea, familia zote mbili zinaunganisha nguvu zao kuwazuia wafyonza damu kuutisha mji wao. Wakati vita vya chini kwa chini vikishika kasi, pia miale ya tamaa kwa kile kilichoanza kama kuteka nyara inageuka haraka kuwa mchezo hatari wa utongozaji
LanguageKiswahili
PublisherTektime
Release dateAug 28, 2023
ISBN9788835455608
Mwanga Wa Usiku: Mfululizo Wa Vitabu Vya Kuunganishwa Kwa Damu Kitabu Cha Pili

Related to Mwanga Wa Usiku

Related ebooks

Related categories

Reviews for Mwanga Wa Usiku

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mwanga Wa Usiku - Amy Blankenship

    Sura ya 1

    Quinn Wilder aliangalia kote kwenye ofisi ya Warren asijue ikiwa kumpata mmuaji lilikuwa ni jambo zuri au baya. Kulikupiga kelele kwingi kulikuwa kumeisha… au alitarajia kumeisha. Alimuangalia Kane wakati huu ambao mfyonza damu huyo alikuwa amekigeuzia chumba mgongo. Kane hakujali kujitetea… Michael alimfanyia kazi hiyo vizuri.

    Angemkasirikia yule mfyonza damu mwenye nywele nyeupe na pia angeomba msamaha wakati huo huo, lakini kwa wakati huu alicho kihisi kumhusu Kane ulikuwa uoga wa ajabu na, kama mnyama wa kuwinda, hakupenda hisia hiyo.

    Kane alitabasamu akiangalia nje ya dirisha. Alihitaji kuipunguza sauti ya kuweza kusikiza mawazo ya watu wengine. Kwa hiyo, wale chui na simba walikuwa pamoja tena...kwa hiyo? Walimtaka afanye nini, acheze densi kwa furaha? Hakuwa na muda huo.

    Wafyonza damu wasiokuwa na nafsi walikuwa wengi zaidi yetu kwa angalau kumi kwa mmoja. Ikiwa nitakumbuka kwa sahihi, Devon alikuwa mpiganaji mkali. Pengine tunaweza kumuita arudi kutusaidia. Stefano alitoa wazo lake, Kwa jinsi kikosi cha wafyonza damu kinavyo kuwa, inaonekana kuwa tutapoteza vita hivi. Ikiwa hatuta unda kikosi chetu wenyewe, basi itabidi tufunge virago na kutoroka.

    Ikiwa jamii hizi hazingetenganishwa kwa muda mrefu, ungejua kuwa Devon anashughulika kumfukuza mwenziwe asiye kuwa tayari nusu ya dunia kwa wakati huu, Kat alimjibu Stefano, lakini alikuwa akimuangalia Quinn alipolisema.

    Kejeli imetamulika, Stefano alitabasamu. Kaka yake alimkasirisha Kat kwa kumteka nyara. Akimuangalia Quinn, alishangaa ni kwa nini kaka yake hakusema chochote kuhusu Dean kuwasaidia na wale wafyonza damu karibu na kilabu. Wakiwa na mmoja wa walioanguka akiwa upande wao lilikuwa jambo la kujivunia… sio jambo la kuweka siri.

    Alisikia kumhusu yule alieanguka mwengine aliyemsaidia kumtoa mwenzake Devon na rafiki yake, lakini sasa alipokuwa ametoka na Devon na wale wasichana wawili, Devon alikuwa ndiye msaidizi wao wa pekee. Ninauunga mkono hoja ya kumuia Devon arudi nyumbani kwa matumaini ya kuwa yule aliyeanguka… aliitwa nani?

    Kriss, Kat alijitolea.

    Ikiwa Kriss atarudi na Devon, basi tutakuwa tume sawazisha hesabu kwa sababu tayari tunaye mmoja wa walioanguka hapa aliyekuwa tayari kutusaidia, Stefano alimalizia.

    Na je, unadhani tutawarudisha vipi? Quinn aliuliza akiangalia upande wa Warren. Unajua jinsi wanaume wa aina yetu huwa wakati tumepata wenzi. Njia tu ambayo Devon atarudi ni ikiwa mwenzake atakuwa naye.

    Hapa kuna wazo jipya kwako… Mwambie ukweli, Kat alibweka na kumuangalia Quinn machoni wakati alipogeuka kumuangalia. Almuinulia unyusi na kisha akatabasamu kwa kutosheka wakati alipogeuza macho yake kutoka kwake.

    Quinn alikunja uso kwa maneno yake lakini hakusema chochote kwa kulipiza kisasi.

    Kane alitoa sigara kwenye kesi yake na kuiwasha. Nitasema kuwa msichana huyu aliyekati yetu ana hoja nzuri. Ukiwa taka watoto wa paka kurudi, ni lazima kuwatupia chambo.

    Kweli, Michael alisema akijaribu kuleta mzaha kwenye chumba hicho. Nitaweka tu bakuli la maziwa kwenye mlango wa nyuma na kusubiri na wavu wa kipepeo.

    Kane na Kat walitabasamu wakimuona Michael akiwa amekaa kwenye giza na wavu wa kipepeo mikononi mwake akiwasubiri wale watoto wa paka waje na kuanza kunywa maziwa kwenye bakuli.

    Kriss anahitaji kurudi, Kat alikubali. Nimewahi kumuona akipigana na ni sawa na bomu kubwa. Lakini ikiwa nitamsoma vizuri, hatarudi na Tabby.

    Je, utamfanya vipi aliyeanguka kumuacha anayemlinda na kuchagua upande kwenye vita? Stefano akauliza.

    Huwezi, Michael akasema. Walioanguka ni wachache na hawapatikani kwa karibu. Wawili tu niliokutana nao ni Dean na Kriss, na hutaki kumkasirisha mmoja wao. Alimuangalia Quinn, Je, kuna uwezekano kuwa Dean atamuuliza Kriss kuikatiza likizo yake?

    Maswali zaidi kadha yaliulizwa kutoka upande wa chui kwenye chumba kile lakini Kane alihisi baridi ikimuingia kwenye ngozi wakati alipo ya zuia. Alijua halisi ni nani walie kuwa wakiongea kumhusu. Ikiwa Kriss atarudi… basi Tabatha atafuata.

    Kila mmoja isipokuwa Michael alishtuka wakati Kane aligeuka ghafla na kuwa tazama.

    Vita tayari vimeanza, kwa hiyo nyinyi mkimaliza kubusiana, pangine huenda mkaungana na mawindo. Aliusukuma dirisha wazi na kuruka nje, asijali kuwa ilikuwa ni ghorofa ya pili. Koti lake leusi refu lilipepea nje nyuma yake ikifanana na mbawa nyeusi kabla ya kupotea.

    Kane alipokuwa akipotea, Michael aliyazungusha macho yake kwa jinsi alivyotoka yule rafiki yake na kufikia dirisha na kulifunga. Kila mmoja alifikiria kuwa Kane alikuwa ametua kwenye ardhi lakini yeye alimhisi kuwa juu yao, kwenye paa. Mkutano ulienda vizuri kuliko Michael alivyodhania utakuwa.

    Michael alishangaa ikiwa Kane alijua alichokifanya wakati alipoliweka lile jiwe la damu ndani ya mwili wa Kane. Wakati alipouuma mkono wake wake mwenyewe na kumwaga damu kwenye kidonda cha Kane, ilikuwa ni kwa sababu mbili. Moja ilikuwa kulisaidia jeraha lake kupona kwa haraka, lakini sababu  ya pili ilikuwa ya kibinafsi. Damu yake ikiwa ndani ya mishipa ya Kane, angeweza kufuata kila mwendo wa rafiki yake.

    Ilimkasirisha kuwa Kane alikuwa mjini kwa muda mrefu na hakulijua. Hata hakuwa akimtafuta kwa sababu alidhani kuwa Kane alikuwa amefariki. Ikiwa angempata Kane mapema… pengine angeweza kusitisha matukio haya kabla ya kutoka kwenye uthibiti wa mkono wa Kane. Lakini sasa wakati alimpa Kane damu, itakuwa bora kuliko kifaa cha kutafuta. Ikiwa Kane ataamua kutoroka… hatafika mbali.

    Sijui ni kwanini Kane ana mtazamo mbaya kuhusu kili wakati ni yeye ndiye aliyesababisha mlipuko wa wafyonza damu, Nick alisema kutoka mahali alipokuwa ameugemea mlango. Hakujali Michael akiwa kwenye kusanyiko, lakini kumuamini Kane lilikuwa wazo baya. Mtu huyo hakuonekana kuwa na akili timamu.

    Umekasirika tu kwa sababu Kane aliamua kuwacha kuwa adui, Warren alimuelezea ingawa yeye mwenyewe hakufurahishwa na Kane. Lakini hata uleta ukweliwa kuwa Kane alimtega mdogo wake wa kike kutekwa nyara na Quinn… hadi atakuwa na wazo bora kuhusu uzima wa akili ya mfyonza damu aliye fufuka.

    Michael alianza kumtetea Kane, lakini kulikuwa na miguu mingi ya kukanyagwa na hatia kwa watu wengi. Alijua kuwa Kane bado alikuwa na jambo alilolificha na alikuwa akitamani kulijua kabla limle rafiki  yake akiwa hai. Alitamani Kana ange harakisha na kutambua kuwa hakuwa peke yake tena.

    Kwa upande mwengine, Michael alijua kuwa Kane alipitia tukio ambalo asingeweza kuelewa kikamilifu hofu yake. Akiwa angekumbana na hali kama ile, Michael hakuwa na hakika angeweza kubaki na akili timamu. Kane alisalitiwa na mmoja wa rafiki zake wa dhati na kupewa hukumu ya maisha bila tumaini ya kuepuka.

    Macho yake yalikuknjamana kuelekea dirishani akitambua kuwa hilo ni swali moja alilosahau kuuliza. Kane aliweza vipi kujifungua kutoka kaburini?

    *****

    Kane alitembea mbele na nyuma kwenye paa la Densi ya Mwezi, mikono yake ikiwa imekunja ngumi kando yake. Bado aliweza kuuona mtazamo uliokuwa kwenye uso wa Kriss alipomrusha upande wa pili wa bohari kama taka. Hangeweza kupigana na aliyeanguka… hakuna aliyeweza kupigana na nguvu zilizo milikiwa na mmoja wao.

    Hata kama wangemuita Kriss ilikuimarisha kikosi chao, na Tabatha alirudi na yeye, Kane alijua kuwa Kriss hakuwa na nia ya kumshiriki Tabatha na yeyote. Halikufanyika mara nyingi, lakini Kane angeapa kwa jiwe la damu lililozikwa mwilini mwake kuwa yule aliyeanguka alimpenda Tabatha. Ikiwa ilikuwa kweli, basi Kane hakuwa na tumaini la kumkaribia mwenzake wa roho.

    Aliipoteza nafasi yake na inauma sana. Hata kama hakuwa na malaika aliyeanguka akikaa begani mwake, Tabatha hangekubali kuwa na chochote naye sasa. Na kwa wale wengine, hakujali ikiwa wabadili viungo walimpenda au la. Haya hayakuwa mashindano ya umaarufu.

    Pengine ni bora ikiwa hawata nipenda, alinongóneza akiangalia juu ya mji.

    Kane alitikisa kichwa na kuizika mikono yake ndani ya mifuko yake. Atakaa kwa muda wa kutosha kusaidia kuwaondoa wafyonza damu waovu aliyowatengenenza bila kutarajia. Lakini hilo likiisha fanyika, ataenda kuwa peke yake tena. Hivyo, wakati atakapoamua kuondoka, hakutakuwa na yeyote atakaye jali kiasi cha kumfuata.

    Wazo hilo lilimfanya akasirike.

    *****

    Trevor aliliegemeza gari mahali pa kuegemezea magari pa Envy na kulizima gari. Alitaka sana kuongea naye na kuona jinsi alivyokuwa akiendelea. Pengine alikuwa na muda wa kufikiria kuhusu aliyomwambia… hata hivyo, yalikuwa kweli.

    Akiiangalia bidhaa iliyokuwa kwenye kiti cha abiria cha gari lake, alitabasamu kabla ya kuikamata. Kweli alikuwa ameifanyia kazi suruali ile aliyokuwa ‘ameiomba’ mapema juma lile kutoka kwa Chad, na sasa alikuwa akienda kuirudisha. Hii ilikuwa kazi yake nzuri kwa siku ile. Hakuna mtu aliyetumwa jehanamu kwa kuwa na ucheshi.

    Akiikunjua suruali ile, aliuona ule uchafu na mafuta ya gari yaliyokuwa kote kwenye suruali ile. Alicheka kwa ndani wakati alipoiona tena kazi yake kwenye sehemu ya kinena. Trevor alikuwa amefanya lisilokuwa la kawaida na kujibadili kuwa mbwa ilikuirarua sehemu ya kinena ya suruali ile kwa furaha.

    Hanna, paka mzee wa Bi. Tully aliyeamua kuanza kuishi naye, alitembea hadi alipokuwa na kuinusa suruali kabla ya kugeuka, akiinua mkia wake juu ya hewa na kuimiminia mikojo ilikutoa harufu aliyokuwa ameiwacha. Trevor hakudhani angeweza kucheka kwa nguvu kama aliyvo fanya.

    Bora kabisa, alinong’oneza.

    Alitoka nje ya gari, na akauelekea mlango wa mbele na kuirusha suruali juu yam situ, karibu acheke tena wakati zilipoanguka kutoka kwenye mmea na kuanguka kwenye nyumba kubwa ya siafu. Hii ilikuwa ya kupendeza sana.

    Akipiga kengele ya mlango, aliingiza mikono yake ndani ya mifuko yake na kusubiri mlango ufunguke. Wakati ulipofunguka, Trevor aliweka sura iliyokuwa tulivu zaidi.

    Hujambo, alisema kwa taratibu.

    Chad alipumua na kuegemea kwenye fremu ya mlango, Hujambo mwenyewe, mgeni.

    Tazama, ninajua kuwa nilikosea na nilitaka kuongea na Envy… au angalau jaribu ikiwa utakubali kukiweka kipiga shoti mbali nay eye, Trevor alieleza na tabasamu ndogo.

    Ningefanya hivyo, lakini Envy hayuko hapa, Chad alijibu akijisukuma kutoka kwenye fremu ya mlango na kusimama kwa urefu wake wote. Jason alilitaja jina la Trevor katika msitari mmoja na neno mnyemeleaji na alitumai kuwa Jason alikuwa amefanya kosa. Aliamua kuchukua muda wa kuenda likozo na Tabatha na Kriss. Sijui atarudi lini.

    Trevor alipumua kwa nguvu na kutikisa kichwa alipotambua kuwa harufu ya Envy haikuwa mpya kwenye nyumba ile. Basi ninahitaji umpe habari fulani.

    Kama ipi? Chad aliuliza, akionekana kuwa makini sana.

    Anafaa kukaa mbali na Devon Santos. Yeye ni habari mbaya na ataishia kumuumiza, alisema, akitumai kumleta Chad upande wake kwa kuchezea hisia zake zaulinzi kama kaka yake.

    Chad alilikunjia uso onyo la Trevor na kuikunja mikono yake juu ya kifua chake. Kama wewe?

    Muangalio wa Trevor ulianguka, Nilichofanya ilikuwa sehemu ya kazi yangu. Ndio maana sikumwambia kazi niliyofanya.

    Aliangalia kando na kuiweka mikono yake ndani zaidi mfukoni akijua kuwa Chad hakujua chochote. Alitumaini kuwa Envy haku ya rudia yale aliyomwambia kwa Chad. Raia hawaku hitajika kujua kuhusu mambo yanayoendelea usiku… hasa polisi.

    Nilimwambia kuwa mimi ni jasusi usiku ule uliponipata kwenye kilabu na ninadhani aliniamini, Aliongezea, akitazama jinzi Chad kwa ukaribu ilikuona ikiwa alijua zaidi ya alivyopaswa kujua.

    Chad alivuta pumzi, Angalia, ninajua ulimpenda mdogo wangu wa kike lakini ameisha songa mbele. Nadhani unapaswa kufanya hivyo pia. Sikwambii tu kama mfanya kazi mwenzangu au rafiki, ninakuambia kama mtu aliye yapitia. Mwache afanye uamuzi wake mwenyewe. Hata ukiwa na nia nzuri, ninadhani kuwa anatoka nje na Devon sasa.

    Trevor aliyaiunua macho yake kumuangalia Chad usoni. Nini? aliuliza kwa hatari.

    Anatoka nje na Devon kama ninavyo jua, Chad alirudia moja kwa moja.

    Trevor alihisi barifi ikiteremka chini ya uti wa mgongo wake, akageuka na kutembea bila neno lengine.  Chad alikunja uso alipomuona paka kupitia dirisha la mbele la gari la Trevor akitegemea dashibodi. Yule mtu mwengine aliharakisha kuingia ndani ya gari lake, kuwasha injini na kuondoka kwenye eneo la kuegemea magari.

    Jason, Chad aliitangazia hewa, Natumai kuwa hukusema ukweli kumhusu yeye kuwa mnyemeleaji.

    Chad alijua kuwa Envy alitoka mjini akiwa na Devon kuungana na Kriss na Tabatha kwa muda mfupi wa mapumziko. Hakuwa tayari kumwambia Trevor habari hizo kwa sababu Envy alimfanya kuapa kuiweka siri hiyo. Hata hivyo, haikuwa na maana yoyote kwa sababu kile alicho kifanya Envy hakikumhusu Trevor kwa vyovyote vile wakati huu.

    Chad alikitikisa kichwa chake na kuanza kurudi ndani wakati alipokiona kitu cha samawati kwa jicho la upande. Uso wake ulichangamka alipoiona suruali yake ikilala kwenye ardhi na kukimbia kuichukua, akikunja uso wakati alipowaona siafu waliokuwa wakitambaa juu yake.

    Furaha yake ilipotea wakati alipoona miraruko yote na macho yake yakapanuka kiucheshi alipoona sehemu ya kinena ikiwa imeraruliwa yote.

    Chad aliiteremsha suruali na kuyakaza macho yake njiani, Mbwa, tako lako ni nyasi.

    Sura ya 2

    Kat alikuwa amesongea na kusimama kando ya dirisha. Alitaka kuwa mbali sana na Quinn kama awezavyo. Karibu ayazungushe macho yake alipogundua kuwa kusongea kwake kulimleta tu kwenye upeo wa macho yake. Alitamani kuwa Envy angekuwa hapa. Alihitaji kuongea na yule mwanamke mwengine… au mwanamke tu mwengine kwa jumla. Ingekuwa bora katika mazungumzo haya yaliyojaa hoja za wanaume.

    Akiangalia kote chumbani, alitambua kuwa sio wakuu wote wa jamii ya simba walikuwepo.

    Micah na Alicia wako wapi? Kat aliuliza akijua walipaswa kuwa sehemu ya hiki… chochote kilicho kuwa.

    Quinn alimuangalia Warren kwa muangalio ambao alidhani kuwa yule chui atauelewa na kumsaidia kwa kile alichokuwa tayari kukisema. Alicia haja rudi kutoka shule ya bweni tangu mwezi mmoja na hatumleti katika vita hivi. Ni hatari sana kwa wasichana.

    Uso wa Kat uliingia Weusi zaidi na alionekana kuwa tayari kukirarua kichwa cha jamii ya simba.

    Na Micah? Warren aliuliza kabla Kat kuwa na wakati wa kuanza vita baada ya msemo wake wa mwisho.

    Hapatikani, Hasira iliyokuwa kwenye sauti ya Quinn ilimfanya kila mmoja amuangalia kwa kutaka kujua. Tumejaribu mara kadha kumpigia simu lakini anakataa kuishika simu yake.

    Stefano alivuta pumzi kwa ule ujeuri wa Quinn na kumkatiza, Micah hajapatikana kwa zaidi ya majuma mawili.

    Nini? Warren akiwa amekasirika kwa ghafla. kwa nini hamkutuita kwa msaada?

    Kwa sababu ya jariba pumbavu, Kat alikejeli. Ni wazi kuwa aliogopa kuwa hatungeweza kukabiliana na lililosema kwa sababu ya hali zetu za hasira.

    Michael alikitikisa kichwa akijua kuwa hadi familia hizi mbili zitakapo suluhisha tofauti zao, itabidi awe muamuzi. Sawa, wakati tunafanyia kazi tatizo la wafyonza damu, pia tuta kuwa macho kutafuta miongozo ya kupotea kwa Micah.

    Mantiki inadhihirisha kuwa Micah atarudi mwenyewee, huwa anarudi kila mara, Quinn aliinua mabega.

    Kat aliangalia nje ya dirisha akiwa bado amekasiriki. Quinn alithubutu vipi kugusia kuwa wasichana wasihusike? Wanaweza kumweka Alicia kando na haya ikiwa wangetaka, na kweli wanapaswa kufanya hivyo kwa kuwa alikuwa mdogo zaidi kati yao wote. Lakini wakijaribu kumzuia, basi watapata mshtuko mkubwa. Tatizo lilikuwani kwamba, sasa hata yeye alikuwa ana wasiwasi kumhusu Micah.

    Quinn angesukuma kila kitu njiani na kuwaita. Alijua kuwa wangemsaidia licha ya tofauti zao. Kwani kuna nini ikiwa baba zao waliuana… dhambi za wazazi hazifai kuwaangukia watoto wao.

    Ingawa hakulijua, Warren alikubaliana na Kat kimya kimya. Quinn ange wasiliana nao wakati alipogundua kuwa Micah amepotea. Alikuwa anaijua vizuri jinsi ubishi kati ya ndugu hao huweza kulipuka. Tofauti zao kawaida ziliishia na Micah kutoka nje na kupotea kwa siku nyingi mara moja… lakini sio majuma.

    Stefano na Nick waliendelea kuwasiliana kwa miaka hiyo yote na Nick alimjulisha kuhusu yaliyokuwa yakiendelea katika familia ya simba. Wakati Micah na Quinn walipoligana, Micah alimwambia Stefano mahali alipokuwa akienda ikiwa ataenda kwa zaidi ya siku moja. Wakati huu Micah hakuwacha ujumbe na yeyote, kumaanisha kuwa alikuwa haendi kukaa kwa muda mrefu.

    Baada ya kiota hatari cha wafyonza damu mimi na Stefano tulichokipata kanisani, hakuna anayestahili kuenda nje peke yake usiku wa leo. Tunahitaji kuwa wawili wawili, Quinn alisema akibadilisha mada.

    Stefano alijihisi tofauti wakati picha ya yule msichana aliye mpata na kumpoteza usiku ule ilipopita kwenye akili yake. Nadhani nitarudi kule usiku wa leo na kuhakikisha kuwa lile kanisa bado ni safi. Huenda tukawa tulikosa kuona kitu.

    Nitaenda na Stefano, Nick alijitolea akitaka kuwa na muda na rafiki yake wa zamani mkorofi.

    Kat aligadhabika kwa muda wakati alipofanya hesabu kimya kimya. Bilas haka, Michael angeenda na Kane, na kwa kweli hangependa kuungana na Kane kwa sababu alikuwa mbali na kuwa kamili. Hiyo ilimuacha Warren na Quinn.

    Nitaenda na Warren, Kat alijitolea.

    Hapana, Warren alimrekebisha. Tunamhitaji mtu kukiangalia kilabu.

    Ati kwa sababu mimi ni msichana hai maanishi kuwa siwezi kujisimamia, Kat aliwaonya, kisha kwa utaratibu akatoka nje ya chumba.

    Wanaume wote chumbani walijikunja wakati alipofunga mlango taratibu nyuma yake.

    Wue, Nick alinongóneza. Natamani hata angeufunga mlango kwa nguvu.

    Steven na Quinn hawakuwa wamemuona Kat kwa miaka michache lakini wangeikumbuka hasira yake vizuri sana. Kuufunga mlango taratibu nyuma ya Kat aliyekasirika ilikuwa mbaya zaidi mara kumi kuliko Kat aliyetoka nje kwa fujo. Alikuwa amekasirikia… la, alikuwa ameipita sehemu ya hasira. Alikuwa amekasirika vibaya.

    Ninaenda kumpigia Devon simu na kumfahamisha kuhusu yanayoendelea, Warren alisema na kuivuta simu ya mkononi kutoka kwenye mfuko wa suruali yake. Hakupenda kumfanyia ndugu yake hili lakini ikiwa hangefika nyumbani hangukuwa na nyumba ya kurudia. Akiibonyeza nambari kwenye simu, alitembea kuelekea mlango tofauti ulioelekea kwenye chumba cha kulala.

    Warren alisubiri wakati simu upande ule mwengine ikiendelea kuita. Mwishowe alimsikia mtu akiishika na kulaana mara tu baadaye.

    Unataka nini? Devon aliuliza akisikika kuwa na usingizi lakini mwenye furaha.

    Warren kwa haraka alimjulisha yaliyofanyika tangu Devon na Envy kuondoka chini ya saa ishirini nan ne zilizopita.

    Devon alipumua, Jamani, nauwacha mji na kila kitu kinaharibika.

    Nitakupa siku chache kisha unahitaji kuwa nyumbani. Warren alisema. Pia ninakuhitaji unifanyie kitu kimoja katika muda huo wa siku chache.

    Ni nini hilo? Devon aliuliza akisikika kuwa macho zaidi.

    Ninahitaji umuulize Kriss ikiwa atatusaidia. Mwambie Dean tayari amekubali lakini kwa hakika tutamuhitaji, pia. Ikiwa itabidi, mwambie Envy amshawishi Tabatha kuwa tunamhitaji Kriss hapa kwa sababu ulingana na ninayo yasikia, ikiwa atarudi basi yule aliyeanguka atamfuata.

    Nitaona nitakalo weza kulifanya, Devon alisema. Kriss ni mtu wa ajabu. Unajua, yeye hutembea kwa mdundo wake mwenyewe.

    Warren alitikisa kichwa, Ananikumbusha mtu mwengine ninaye mjua.

    Devon alicheka, Sawa kaka, lakini si ahidi chochote.

    Nitakuona siku chache zijazo. Warren alisema na kuikata simu.

    *****

    Quinn alimtambua Kat kwenye viwambo vilivokuwa kwenye ukuta. Kwa kuwa kila mmoja alikuwa akimsubiri Warren amalize kwenye simu yake, alisongea karibu na kiwambo kana kwamba alikuwa amesinywa. Kusinywa siyo hali aliyoihisi wakati alipokuwa akimuangalia Kat.

    Alifikiria kuwa alikuwa mrembo miaka kadha iliyopita, lakini alikuwa hakukisia kwa ukamili kile angegeuka kuwa. Miaka iliyoendea alikuwa akimuangalia Kat kwa mbali. Hata alikuwa ameajiri wapelelezi kufanya kazi hapa kwenye Densi ya Mwezi na kumpa ripoti… ingawa yule wa mwisho aliye mtuma aligeuka kuwa mmoja wa waathiriwa wa mauaji.

    Alijikunja wakati mtu mmoja alitembea hadi mahali alipokuwa Kat amesimama na kuufikia mkono wake. Kulingana na vile kamera ilifyokuwa imewekwa, Quinn alihisi kuwa yule mtu hakuwa katika hali

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1