Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hanjamu Ya Msaliti
Hanjamu Ya Msaliti
Hanjamu Ya Msaliti
Ebook140 pages1 hour

Hanjamu Ya Msaliti

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

   Siku zote msaliti hakubali kuona akisalitiwa, hata kama kukiwa hakuna dalili ya kufanyiwa hivyo. Hawezi kuwa na  amani asilani, daima huhisi atageukwa kama alivyogeuka mwingine. Hawezi kustahimili kufanyiwa jambo alilomfanyia mwingine, maumivu yake huyajua.
   Ndiyo hapo Saibah binti wa Sultan Zuad aliyemsaliti mumewe, mpaka akaja kufumwa na kijakazi kitandani. Bado alifikia kumwonesha jeuri ya waziwazi na si kukubali alikosea, kisa nyumba waliyoishi ni kwao. Mpaka bwana yule aliamua kuondoka na kumwachia nyumba, na akabaki akikaa nje akiendelea na majukumu yake kama Mkuu wa majeshi wa himaya.
   Aliachwa solemba na kijakazi yule, akaja kujua mume ni wa muhimu. Wakati ambao yupo vitani. Alipokuja kurudi ni majeruhi na hana fahamu, muda huo napo mwanamke aliyependwa na mumewe anarejea kumjulia hali. Ndiyo hapo sasa wasiwasi wa penzi wa msaliti unapoibuka
    

LanguageKiswahili
PublisherMambosasa
Release dateFeb 13, 2024
ISBN9798224164462
Hanjamu Ya Msaliti
Author

Mambosasa

  Hassan  Mambosasa born in Tanga region in Tanzania. He  won Nyabola kiswahili for short stories in 2022. Currently he live in Tanga city.

Read more from Mambosasa

Related to Hanjamu Ya Msaliti

Related ebooks

Related categories

Reviews for Hanjamu Ya Msaliti

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hanjamu Ya Msaliti - Mambosasa

    DIBAJI

    Sultan Zuad, mtawala wa himaya anaumizwa kichwa na kuhusiana na binti yake. Ameshafikisha umri ambao anauona unatosha kuolewa, ila bado binti hana uelekeo wa kutaka kuolewa. Wachilia mbali kumpata huyo mchumba wa kumchumbia, suala ambalo si kawaida kwenye himaya hiyo.

    Kawaida ya tawala za enzi, binti wa kufikia umri huo alitakiwa kuwa kaolewa au tayari kachumbiwa. Ndiyo hapo sasa Sultana anafikia kumweleza mkewe kuhusiana na suala hilo. Naye anaenda kumfikishia binti yao, ambaye aliishia kusema waitwe vijana wa mji mzima atachagua yupi ambaye angemfaa kuwa mumewe. Suala hilo linatimizwa.

    Fuad kijana wa kuzaliwa baba mwarabu, na mama mweusi anafanikiwa kumwokoa waziri wa serikali ya Sultan, aliyekuwa akizama baharini. Jambo ambalo linalazimu kufanyika kwa karamu, na kupongezwa kwa jambo hilo. Kwa kijana wa kimasikini kujipa ushujaa huo ambao hata magadi wa waziri yule hawakuweza kuufanya..

    Upande wa binti Sultan kweli alifanikiwa kuendesha shindano hilo la kumsaka mume. Ila hadi linamalizika hakumpata aliyemtaka. Aliishia kutoa sababu ambayo hadi kwa mzazi wake ilikubaliwa na siku hiyo ikapita nayo.

    Siku inayofuata binti anaenda sokoni kununua  vitu muhimu, kwa ajili ya maandalizi ya siku ya tafrija ya kupongezwa kijana aliyemwokoa waziri. Huko napo anakutana na Fuad dukani, ambaye alikuwa akilalamika apewe pesa yake na muuzaji, ndiyo hapo aje kupisha binti wa sultan aingie kununua.

    Binti anaishia kumwamuru mtumishi wake amuumiza, na anaondolewa dukani hapo akiwa na jeraha mguuni. Mchana nao unapita na hadi unakuja kufika wakati maalum wa kupongezwa kijana kwa kumwokoa waziri.

    Binti Sultan anakutana na kijana tena kwa mwonekano mwingine. Anaonekana kuvutiwa naye ila napo anajikuta na wakati mgumu, baada ya kuambiwa waziwazi aliyemdharau mchana wa siku hiyo ndiye huyohuyo.

    Inakuwa zamu yake kuanza  kuhangaika, hasa baada ya kuona mambo kadhaa yaliyomvutia mno kwa kijana huyo. Ila napo Fuad hana shida naye, wala mali za nyumbani kwao. Inamuwia vigumu sana kumpata.

    Fuad ana mpenzi anayeitwa Semeni, ambaye anampenda hasa. Ila napo binti anaingiwa na wakatii mgumu. Ikiwemo kupokea vitisho yeye na familia yake, inambidi kuondoka mbali hasa wakati huo kijana ni mwenye maisha mazuri sana kutokana na zawadi nzuri alizopewa ikiwemo nyumba na eneo.

    Ndiyo kwa wakati huo binti Sultan anapohimiza sana kwa baba yake amsaidie aolewe na Fuad. Sultan kwa kumpenda bintiye anaenda kumshawishi, mwishowe anakubali kwa heshima ya kiongozi huyo na si kwamba alimpenda mtoto wake. Anaozwa na kutokana na uwezo wake kivita aliyobainika nao anaingizwa na jeshi na kufanywa mkuu wa majeshi.

    Furaha ya ndoa yao napo haidumu, binti anamchoka mumewe mapema. Anakuja kurudisha penzi la siri sana, alilokuwa akilifanya na mtumwa wake. Kumbe hata usichana wenyewe haukuwa nao hadi muda wa kuozwa. Ila mumewe aliamua kumhifadhi hakusema kitu. Mwishowe anakuja kumrudisha aliyemwanza kwa usiri.

    Mwishowe wanakuja kufumaniwa ila bado binti anajawa na kiburi, akamtakia maneno mabaya ikiwemo kuishi kwenye nyumba ambayo ni mali yao. Ndiyo hapo Fuad alichukua hatua ya kuondoka zake, ila napo binti anakuja kuachwa ghafla na yule kijakazi. Kumbukumbu za mume zinamjia, anajijua anamhitaji hasa. Alipomwita anabaini ameshaondoka vitani, hayupo mjini.

    Fuad anakuja kurudishwa mgonjwa kutokana na kujeruhiwa na upanga wenye sumu. Semeni naye ambaye ana maisha mazuri, alirejea upesi sana baada ya kuipokea habari hiyo. Hapo ndiyo mtihani unatokea, msaliti alipohisi atasalitiwa na hataki hilo litokee.

    1

    Mvumo wa kutoka mashariki kuelekea magharibi ulirindima, minazi  pamoja na miti mingine iliyopo  ndani ya mandhari hiyo. Ilipepesuka vibaya kwa mkumbo huo, hali hiyo ilidumu ikiwa na karaha kubwa kwa miti ambayo haikuisha kulalama ikitoa mivumo ya aina yake pale matawi au makuti yalipovamiwa. Karaha kwa viumbe hai waliyojichimbia ardhini, ikawa ni  burudani kwa viumbe hai watembeao juu ya mgongo wa ardhi. Mgeuko wa hali ya hewa kutoka ile ya joto  liletwalo na jua hadi kuwa mpulizo,  ndiyo ikawa hivyo kwa upande wao.

    Wakati huu eneo la kiwambaza  cha juu kabisa la kasri la kifahari, alionekana Mtu mzima mwenye kilemba chenye taji kichwani mwake. Kanzu matata ya rangi ya kahawia ikiwa imemkaa mwilini mwake, miguuni akiwa amevaa kiatu kilichoinuka mbele mithili ya pembe la Ng'ombe. Huyu alisimama akiwa  ameweka mikono kwenye ruva za sehemu hiyo ya juu,  kando yake kukiwa na vijana wawili waliyoshikilia  magobori. Macho yake aliyaelekeza mbele hatua  takribani mia moja ambapo kuna ufukwe wa bahari ukiwa na bandari iliyoegeshwa Majahazi kadhaa.

    Alijidhihirisha ni namna gani alivyozama ndani ya dimbwi la fikra,  hata pale kiumbe mwingine alipofika hapo na kumwita. Hakuweza kung'amua hilo, kama vile ni mwenye kutosikia. Kumbe wala haikuwa hivyo, isipokuwa kuwa mbali kinafisi ikapelekea hayo.  Aling'amua kuwa anahitajika na yule aliyepo nyuma yake, hadi pale alipoguswa  begani na kiganja ndiyo akageuka  nyuma kutazama.

    Muhibu lipi likusibulo maana wananitia shaka  kupitiliza Aliambiwa na Mwanamke mwenye mavazi ya gharama mwenye taji kichwani mwake, hapo akajikuta mwenyewe akiinama chini kwa sekunde kadhaa  baada ya kuulizwa hivyo.

    Mahbuba, hababi wa fuadi wangu. Mwenye kuisuuza roho yangu, unayependezwa na  mtima wangu. Kipi kikusibucho?, Aliulizwa kwa mara ya pili.

    "Ewe Malkia wangu, mtawala wa moyo wangu. Sina kingine ila isipokuwa ni hili la Saibah. Wajua umri  unakwenda na sasa umri wake kafikisha eshwiriin, wala haoneshi dhumuni la kutaka Shababi. Yaa Habib ninaihofu fedheha kuliko kitu kingine chochote juu ya Binti yangu, kukaa bila ya mume mtoto  wa Sultan Zuad", Alieleza

    Ni haki yako kuwa namna hiyo ya Habib, ila binti mwenyewe nadhani wamwona.  Hasikii wala haeleweki  ni kipi akifiriacho juu ya hilo, hata mimi naapa kwa jina la Allah  sipo tayari kuona ninapatwa na fedheha kisa yeye

    Hakika wewe ni mama mwema kwa binti yako,  basi ni wajibu wako kuongea naye juu ya suala hili. Kama ni kitabu basi wanazuoni kadhaa amepitia na amehitimu mapema kuliko wenzake, je  lipi hilo alisubirilo. Laiti kama ingelikuwa  Makuhani si haramu kisharia, basi ningaliwafuata na kuhitaji jua tatizo la  binti yangu

    "Afuan yaa Muhibu, madhali limefika kwangu nitakaa niongee naye juu ya hili. Na imani katu hawezi kuniangusha mimi mamaye"

    Haswaaa! Mama bora haangushwi na bintiye

    Huu ni mguu niuinuao hivi sasa ni wa kwake, nikatete naye juu ya suala hili

    Malkia aliposema hivyo, alimwacha Sultan Zuad akiwa yu pekee  yake mahali hapo. Ahueni ilianza kuonekana  usoni mwake, baada ya kuhakikishiwa hilo suala  na mkewe. Alianza kujihisi ni mwenye aibu kuu kwa kukaa na binti muda mrefu ambaye hakuozwa, fedheha alihisi angeweza kuiepuka majira yeyote yale baada ya kupokelewa vyema na mkewe kwa taarifa hiyo.

    Aliendelea kuwepo eneo hilo akibarizi upepo mwanana wa bahari, alikaa hapo kupunguza joto lakini kipunguzo kilipozidi kiwango. Aliamua kugeuka nyuma na kurejea  ndani, majira hayo ni ambayo hali ya hewa ya baharini ilibadilika ghafla na wingu likatanda kila pande. Kuhofia kushuka kwa  mvua  akiwa ambapo huweza kumpata ikiwa  itanyesha ile ya kiupande, ambayo huweza kumpata ingawa sehemu ya juu imeezekwa.

    Kuingia kwake ndani hakukuonekana  mabadiliko yeyote ya hali hiyo ya mawingu mazito, isipokuwa ni upepo  mkali ukiendelea kuvuma.

    JUA KUONDOKA GHAFLA na ujio wa upepo mkali pamoja na mawingu mazito, ulipelekea hata mawimbi ya bahari nayo yabadilike ukubwa na kuwa ya kutisha. Yalifika umbali mkubwa tofauti na pale ambapo hufikia nchi kavu. Hakika watu walielewa wazi chanzo hicho kikubwa cha maji kuliko vyote  duniani, kimetibuka na wale waliyokuwa wana vyombo vidogo vya uvuvi. Hawakuthubutu kuingia huko, kuhofia kukumbwa na dhoruba kali zaidi wakiwa wapo majini.

    Upande wa katikati, eneo la mbali kutoka ilipo fukwe. Vijana wenye rika tofauti walionekana wakishindana nguvu na mawimbi makubwa. Mashua yao  yalipelekwa kutoka upande mmoja kwenda mwingine, huku maji yakiingia ndani na kuzidi kuleta athari kubwa kwao. Iliwabidi wafanye kazi ya ziada kuweza kujinasua ndani ya kibweka hicho. Vyombo vya kuchota maji pamoja na ulindwaji wa mizigo yao, waliufanya majira yote wakiwa wanaelekea ufukweni.

    Kakweree! Shikilia kamba hiyo ya Tanga!, Kijana mmojawapo aliyekaa  nyuma akiwa amejishikilia mkono wake kwenye ukingo wa Mashua alipaza sauti.

    Kabwariii! Endelea kuchota maji hivyohivyo jamani, huu mzigo wa leo ni mkubwa kupitiliza. Tuhakikishe wafika ufukweni, Alimhimiza mwingine huku yeye akiiinama chini kwa haraka baada ya tanga kuzunguka kwa ghafla na kufanya mashua yao yabadili mwelekeo.

    Turudishe tanga mahali pake, hakuna kukata tamaa,  Aliwahimiza na safari hii akiwa wa kwanza kulishika, wenzake nao walifuatia na kulirejesha lilivyokuwa hapo awali.

    Kutoa maji chomboni na kumwaga nje, kulidumu na hakuna aliyeonesha dalili ya kuchoka.  Daima hiyo ni moja ya changamoto ya kufanya kazi baharini, kukabiliana nayo ni wajibu na si kuikimbia. Ndiyo maana hawa hawakutaka kurudi nyuma kwenye suala hilo, waliendelea kugangamala nayo

    Wakiendelea hivyo, hatimaye waliweza kufika mahala ufukwe wanauona kwa mbali. Hapo ndipo walizidisha juhudi zaidi hadi wakafanikiwa kufika ufukweni salama, Mashua yao waliyafunga kwa kamba ngumu kisha wakaanza mara  moja kazi ya kutoa mzigo pasipo kujali ukubwa  wa  mawimbi yanayojiri. Kwa uwezo wake Jalali, aliyowajalia

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1