Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mnadhifishaji Tukio la 2: Ruko
Mnadhifishaji Tukio la 2: Ruko
Mnadhifishaji Tukio la 2: Ruko
Ebook40 pages28 minutes

Mnadhifishaji Tukio la 2: Ruko

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Roland Benito, ambaye anakifanyia kazi Kitengo Huru cha Malalamiko kuhusu Polisi, ametumwa pamoja na mfanya kazi mwenza kwenda kuwahoji maafisa wawili wa polisi ambao wameitika mwito wa hali ya dharura. Mlinzi mmoja wa jela amejirusha kutoka kwa dirisha ya chumba chake kilicho katika orofa ya nne, punde tu maafisa hawa wawili wanapowasili baada ya kupata malalamishi kuhusu muziki wa sauti ya juu kutoka kwa chumba hicho. Kwa mtazamo wa juu, hakuonekani kuwa na jambo lolote la kukisiwa kuhusu hali hii ila pale inapotambulika kuwa mlinzi huyu wa jela ni baba ya rafiki wa dhati wa mjukuu wake Roland wanaosoma pamoja, Roland anasikia kuwa mfungwa mmoja amefariki kwenye jela pale alipokuwa akifanya kazi na kuwa mlinzi huyu wa jela amekuwa akihisi kutishiwa na anayefuatwa. Je, inawezekana kuwa haya hayakuwa mauaji ya binafsi hatimaye? Anne Larsen, mwandishi wa habari kutoka TV2 East Jutland, pia ananukuu hadithi ya vifo hivi. Wakati wa utafiti wake, anatambua kifo kingine, wakili wa utetezi aliyefariki katika ajali ya barabarani. Anatambua kuwa vifo hivi vyote vinahusishwa na mfungwa mmoja, Patrick Asp muuaji wa mtoto, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumuua mtoto wake mdogo wa kike, na ambaye ni mfungwa katika jela ambayo mlinzi yule wa jela alikuwa akifanya kazi.



The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.
LanguageKiswahili
PublisherSAGA Egmont
Release dateSep 11, 2019
ISBN9788726270792

Read more from Inger Gammelgaard Madsen

Related to Mnadhifishaji Tukio la 2

Related ebooks

Related categories

Reviews for Mnadhifishaji Tukio la 2

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mnadhifishaji Tukio la 2 - Inger Gammelgaard Madsen

    purchaser.

    Mnadhifishaji

    Tukio la 2:6

    Ruko

    Jua lilikuwa limeshachomoza wakati Roland Benito na Mark Haldbjerg walisafiri kutoka Horsens na kurejea katika makao makuu ya Kitengo Huru cha Malalamiko kuhusu Polisi katika eneo mraba, karibu na kituo kikuu cha gari moshi katika mtaa wa Aarhus.

    Inaonekana kuwa huenda hii itakuwa ni mojawapo ya hali za dharura iliyo nyepesi . Kufikia umbali huu, hakuna ishara yoyote ya kuwepo kwa njama yoyote. Maafisa hao wawili wanaonekana kuwa hawakuhusika katika kutekeleza kifo cha mlinzi huyo wa jela. Mark akasema, huku akivunja kimya kilichokuwepo toka walipoondoka katika jengo ambalo mlinzi wa jela aliyeitwa Julius Habekost alikuwa amejiua kwa kuruka kupitia dirisha la chumba chake kilicho katika orofa ya nne.

    Huenda tunaweza kukosoa kidogo jinsi George Marsh alimuacha Leif Skovby akaingia kwenye chumba peke yake huku yeye akibaki kuongea na jirani aliyekuwa kwenye ngazi – mwanamke aliyekuwa amepiga simu ili kulalamika kuhusu kelele iliyokuwa katika chumba hicho.

    Mark akatabasamu akiwa na uchovu.

    Haikuwa rahisi vile kumuondokea mwanamke yule punde anapoanza kuongea. Tumetambua hilo sisi wenyewe.

    Roland akatabasamu pia. Alikuwa wa ajabu kweli, mjane yule aliye na takriban umri wa miaka 80, Asta Bernt. Alionekana kama ambaye alikuwa ametoroka kutoka kwa mfululizo maarufu wa runinga uitwao Matador, hata ingawaje hakuweza kuamua ni muigizaji yupi wa kike aliyekomaa alifanana na mwanamke huyu. Huenda ni kwa vile ilimjia kuwa mwanamke yule alikuwa amepamba nyumba yake kama vile mandhari ya kipindi hicho kwa kutumia karatasi za rangi za kupamba ukuta na mapazia mazito ambayo yalipendwa katika miaka ya 1930 wakati kipindi kile kilirekodiwa.

    Mwanamke yule alikuwa ameashiria mara kadhaa kuwa kwa hakika yeye hakuwa mtu wa kuathirika na kuwepo kwa kelele, kwa kawaida hili halikumfanya kuwaita polisi, ila kulisikika ni kama kwamba kulikuwa na jambo baya lilikuwa linatendeka. Kuna kitu kilichokuwa kimeanguka kwenye sakafu na kuvunjika ila hakuna aliyefungua mlango wa Julius Habekost wakati mwanamke yule alienda kubisha ila hakuwa amemsikia yeyote akiwasili au kuondoka kutoka kwa chumba kile. Maafisa wale wawili wa polisi walikuwa wamemuambia kuwa jirani yake alikuwa ameruka kupitia dirisha lake na kufariki papo hapo. Mwanamke huyu ndiye alikuwa shahidi bora zaidi kwani alikuwa amewazamisha na mazungumzo wakati huo wote. Isipokuwa wakati ambao Leif Skovby aliweza kuingia kwenye chumba kile kwa kuugonga mlango, na alifanya hivi yeye mwenyewe.

    "Nashangaa ikiwa mwanamke yule anadanganya kuhusu kelele iliyokuwepo. Hakukuwa na chochote kilichoonekana kuanguka au kuvunjika. Hakukuonekana ni kama kulikuwepo na vurugu kama alivyoelezea. Maafisa wote

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1