Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Robo Mwezi: Watumishi Wa Campoverde
Robo Mwezi: Watumishi Wa Campoverde
Robo Mwezi: Watumishi Wa Campoverde
Ebook253 pages2 hours

Robo Mwezi: Watumishi Wa Campoverde

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

ROBO MWEZI: Dunia ambayo Elio anatorokea huenda isiwe kipande cha mawazo yake, lakini utando uliofumwa kwake. Wakati wa likizo kijijini atapata fursa ya kukutana na mlinzi atakayemfichulia ukweli. Kando na kundi la kuchekesha, wa ukweli na wa kimawazo, atapambana ili kujipatia tena uhuru wake. Vituko vya mtoto huyo vitakufanya ufahamiane na mapepo, mlinzi, kifuli, vidonda, tulivu za miujiza, na utasafiri kote duniani ukitumia taa za trafiki,ukizunguka mbuyu au kupaa ndani ya mpira wa barafu
LanguageKiswahili
PublisherTektime
Release dateJun 4, 2021
ISBN9788835422280
Robo Mwezi: Watumishi Wa Campoverde

Related to Robo Mwezi

Related ebooks

Reviews for Robo Mwezi

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Robo Mwezi - Massimo Longo E Maria Grazia Gullo

    Table of Contents

    Cover

    Title

    Copyright

    Indice

    Prologo

    Sura ya kwanza

    Sura ya pili

    Sura ya tatu

    Sura ya nne

    Sura ya tano

    Sura ya Sita

    Sura ya Saba

    Sura ya nane

    Sura ya Tisa

    Sura ya Kumi

    Sura ya kumi na moja

    Sura ya kumi na mbili

    Sura ya kumi na tatu

    Sura ya kumi na nne

    Sura ya kumi na tano

    Sura ya kumi na sita

    Sura ya kumi na saba

    Sura ya kumi na nane

    Sura ya kumi na tisa

    Sura ya ishirini

    Robo Mwezi

    Watumishi wa Campoverde

    Imetafsiriwa na Kennedy Langat

    Hakimiliki © 2019 M.G. Gullo – M. Longo

    Picha ya jalada na michoro iliundwa na kuahiririwa na Massimo Longo

    Haki zote zimehifadhiwa

    ISBN

    ISBN-13:

    JEDWALI YA YALIYOMO

    Dibaji

    "Kila kitu kitakuwa sawa, wewe ni mvulana mkubwa sasa....Rudi na ucheze na Watoto wengine. Tutakutana tena, ninakuahidi''

    Mtoto alimtazama akitiririkwa na machozi alipoondoka mtu ambaye amekuwa akicheza naye tangu mwanzoni.

    Mtoto alikimbia kurejea kwenye vijigari kwenye bustani iliyojuani, ambako alikwenda kucheza na watoto wengine jirani, huku fikra za rafiki ya kimawazo zikififia polepole.

    Baada ya kujipenyeza kwenye mahali watoto wengine walikuwa, hatimaye angeweza kupanda kwa kitelezo. Hakupoteza hata muda na alianza kuteleza kwenda chini ya kitelezo, akisukuma kwa bidii kadri awezavyo. Hakuteleza hata hadi mwisho, wakati alipoona msichana mwenye nywele nyeupe akikimbia kutoka kwa mama yake na kuelekea kwenye miguu yake. Hakuweza kupunguza mwendo na alimgonga kwa nguvu.

    Msichana huyo mdogo alipoteza mwelekeo na kugonga kichwa chake kwenye ukingo wa kitelezo.

    Alijaribu kumfikia mtoto huyo msichana ili kuhakikisha kuwa alikuwa sawa, lakini akasukumwa kando bila huruma na mamaye, ambaye alikuja kumwokoa. Ghafula, kundi la babu na akina mama walikusanyika karibu na msichana huyo maskini.

    Alipokuwa akijaribu kutambaa mbali na miguu ya watu wazima, alihisi kwamba alikuwa amezimia. Mtu mmoja aliita ambulensi! Huku sauti hiyo ikijitokeza kwa nguvu kwenye maskio yake, alianza kuingiwa na hofu. Alikimbia kuelekea msituni nyuma ya bustani.

    Ghafula, kila kitu karibu naye kikawa giza. Upepo baridi ulikuwa umesheheni sauti za kutisha. Mistari asiyoijua ilianza kuchanganyika na mazungumzo ya wazazi kwenye bustani. Zilikuwa zikitoka nyuma ya kundi la miti, ambayo vivuli vyao virefu vilikuwa vinajidhihirisha. Kisha, sauti hiyo ambayo ilikuwa ikijitokeza kutoka pande tofauti ilizidi kuendelea kusikika. Alikuwa akimfikia zaidi na zaidi, hadi alipohisi kuwa ilikuwa ikinong'oneza maskioni mwake:

    Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom…

    Aliweka kichwa chake kwenye mikono yake ili kutuliza sauti hiyo, lakini haikusaidia. Alipiga magoti na akafunga macho yake...

    Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom…

    Sura ya kwanza

    Anaepuka nikijaribu kumkumbatia……….

    Elio, Elio, njoo hapa! Nisaidie kuanua mboga kabla ya dharuba kuja, tafadhali.

    Elio alikuwa amesimama wima akiwa amevalia viatu vyake vipya na alikuwa akimtazama mamaye, ambaye alikuwa akihangaika katika shughuli zake.

    Elio! Usisimame tu hapo! Chukua hii! Alimtikisa na kuweka begi iliyojaa mboga kwenye mikono yake. Elio hakuwa na nia ya kufanya kitu kingine. Alipanda ngazi zilizoko nje ya jengo, akageuka na kufungua mlango. Alianza kutazama taa nyekundu ya lifti ambayo mwangaza wake haivumiliki. Kisha, akaacha kusubiri na kupanda ngazi kwenda kwenye nyumba yake gorofani. Aliweka mboga kwenye meza ya jikoni na kwenda moja kwa moja hadi chumba chake cha kulala kusikiza muziki kitandani.

    Mara tu alipopanda gorofani mamake akaenda kumtafuta. Alisimama mlangoni akipiga kelele: Unafanya nini? Hatujamaliza bado, njoo unisaidie!.

    Sawa, nko njiani... akajibu Elio bila kusonga. Kwa kweli alitaka tu kumwepuka. Giulia akatoka, akitarajia kwamba mara hii itakuwa tofauti. Hakuwa na matumaini. Alikuwa akihangaika kumtia moyo mwanawe, ambaye alikuwa akizidi kuwa mwenye kutojali. Kutoka Mlangoni, aliweza kusikia wazi hatua za dadaye huku akimwita kwa sauti ya furaha. Elio! Elio! Ondoa makalio kitandani na uje usaidie mama. Anakusubiri huko chini. Alimfokea huku akifahamu kwamba itakuwa bure tu. Elio hakusonga hata inchi moja. Badala yake, aliongeza sauti ya muziki na kuendelea kutazama dari, kana kwamba hakuna kinachotendeka. Giulia, ambaye alikuwa amechoka kutokana na mabishano na mwanawe kuliko kutokana na uchovu, mwishowe alilazimika kupandisha mboga akisaidiana na bintiye, Gaia. Huku akipanda ngazi ya jengo hilo lililo na orofa tano, ambako lifti yaonekana kutofanya kazi kila siku (na kwa kejeli, siku sote haifanyi kazi wakati anapotaka kubeba mboga kupanda ngazi kwenda juu), aliendelea kufikiria kuhusu Elio. Jengo hilo lilipakwa rangi nyeupe na ya machungwa, kama majengo mengine ya baraza la Gialingua, mtaa ambao walikuwa wanaishi. Familia ishirini ziliishi katika mtaa huo, na zilikuwa zimegawanywa katika gorofa ishirini zilizoangalia pande tofauti ya jengo lenyewe.

    Hii ni mara ya mwisho unafanya hivi! akamfokea akiwa jikoni. Tutatatua hii punde to baba yako atakaporejea nyumbani!

    Elio hakuwa hata anamsikiliza kwa kuwa alikuwa amezama katika muziki huo wa kuchukiza. Hakuna na hakuna anayeweza kutikisa hisia za uchoshi na ubishi aliousheheni. Dunia yake isiyopendeza ilikuwa kama makazi kwake. Huo ndio ulikuwa utu wake na dunia ililazimika kumzoea. Gaia alikuwa tofauti kabisa: alikuwa na umri wa miaka kumi na mitano, ana macho angavu na nywele fupi nyeusi. Saa ishirini na nne hazikotosha kwake kushughulikia maslahi yake yote.

    Giulia alikuwa mwanamke mwenye nguvu pia. Lakini, kinyume cha bintiye, alikuwa na nywele nyeupe zilizopindika, alikuwa mnene kiasi lakini mwepesi na aliyejitolea. Alikuwa mama wa kawaida mwenye umri wa miaka 42: kila wakati alikuwa na ratiba ngumu akijaribu kudumisha usawa kati ya kazi na familia.

    Ilikuwa chakula cha jioni. Hata hivyo, hakuna kelele zilizosikika kutoka chumba cha kulala cha Elio. Kwa kweli, hajasonga tangu alipokimbia kujitosa kitandani na kuvaa vipokea sauti vinavyobanwa kichwani.

    Alisikia sauti ya ufunguo katika kufuli wa mlango wa mbele. Wakati uo huo, huku mlango ukiwa bado haujafungwa vizuri, sauti ya hamaki ya Giulia tayari ilikuwa imemkera mumewe:

    Hatuwezi kuendelea kufanya hivi!

    Mpenzi, wacha niingie chumbani kwanza...

    Giulia alimbusu mumewe na kurudi kulalamika.

    Ni kumhusu Elio, sivyo? alisikika kama aliyekata tamaa wakati alipouliza.

    Ndio, ni yeye. akajibu Giulia.

    Wakati uo huo, Carlo akatoa mkebe wa chakula ndani ya begi lake ambalo alikuwa akienda kuacha jikoni. Kisha, alikuwa akienda kuweka mkoba wake kwenye kabati la nguo. Ndani ya mkoba huo, kila wakati angeweka jezi ya ziada kwa kwa sababu ya mawimbi ya joto ambayo yalikuwa yakipiga eneo hilo mwezi huo wa Mei.

    Alikuwa mwema, mwenye umri wa miaka arobaini na mbili, mrefu na mwembamba. Nywele zake zilikuwa zimegeuka kijivu, lakini wakati mmoja zilikuwa zinafanana na za bintiye. Uso wake uliochongoka ulikuwa wazi: kwenye pua lake lililofanana na mdomo wa ndege alikuwa akivalia miwani duara ya chuma.

    Tuizungumzie kumhusu baadaye? kwa upole alimmwuliza bibiye, akitarajia kwamba atasononeka.

    Ndio, uko sahihi mpenzi. alijubu, lakini aliendelea kulalamika hadi wakati chakula cha jioni kilipoandaliwa.

    Kwa bahati, Gaia hakuacha kuongea kuhusu siku yake, akichukulia machungu yake madogo kwa njia ya kutia moyo.

    Giulia alikuwa amemaliza kuandaa mezani wakati aliposema:

    Umwite Elio.

    Haina maana na unaifahamu. alijibu. Unajua hatasonga hata inchi moja, isipokuwa aitwe na baba...

    Giulia, kisha akamgeukia mumewe:

    Ameshinda katika chumba hicho tangu nilipomrudisha nyumbani kutoka shule. Anazidi kuwa mbaya.

    Si tulisema atakuwa akirudi nyumbani mwenyewe kuanzia sasa na kuendelea?

    "Nilikuwa katika eneo hilo...

    Nilikuwa nikinunua mboga..."

    Kila siku unatoa vizingizio ili kumlinda, lakini tena unalalamika kuhusu tabia yake!

    Carlo alikuwa akitikisa kichwa chake kama ishara ya kutokubali. Kisha, akaamka kwenye kochi na kwenda kwenye chumba cha watoto.

    Aliingia kwenye chumba hicho cha kulala bila kubisha hodi na kumpata Elio katika mahali papo hapo ambako Giulia alikuwa amemwacha. Alikuwa akitazama dari kwa macho yaliyofunikwa, na alikuwa bado amevalia vipokea sauti vya maskio vyeupe vya Wi-Fi, na hata alikuwa hajavua viatu vyake.

    Carlo hakuamini kwamba alikuwa mvulana yule yule ambaye angeandamana naye kila wakati kwa safari ya kuendesha basikeli. Sasa alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, alikuwa mrefu kama yeye, na macho yake ya kijani kibichi bado yalikuwa mazuri, lakini yalionekana yaliyokufa. Katika miaka michache iliyopita, amekuwa akiugua unyongovu. Carlo alikuwa hajasikia kicheko chake kwa muda mrefu, hivi kwamba alikuwa amesahau jinsi inavyosikika. Alikuwa akijuta kwamba hangeweza kukaa naye kwa muda mrefu kama awali. Hata hivyo, alikuwa na shaka kwamba, kufikia sasa, umakinifu wake utathaminiwa.

    Kwa bahati mbaya, miaka kadhaa kabla ya hayo, Carlo alikuwa amepoteza kazi yake kufuatia shida za kifedha. Kufuatia kuongezeka kwa mapato, kampuni hiyo ilihamishwa ngambo, kama kampuni nyingine nyingi.

    Carlo alijitahidi kupata kazi. Hatimaye, akapata kazi katika mji tofauti. Kila siku alilazimika kusafiri muda mrefu na kubadilisha njia ya usafiri mara kadhaa, na kusababisha kuwa mbali na familia yake kwa saa nyingi kila siku. Hurejea nyumbani akiwa amechoka na akili yake kusubaa. Baada ya chakula cha jioni, analala kwenye kochi na bila shaka kuzama kwenye usingizi licha ya jaribio ya kutaka kuwa macho.

    Carlo alidokeza kuwa Elio anapaswa kutoa vipokea sauti vya maskioni. Elio alikubaliana naye tu ili kuepuka kukemewa.

    Ni wakati wa chakula cha jioni. Njoo ule. Aliamuru. Mamake alisema kuwa umekaa hapa tangu saa kumi jioni!

    Elio aliamka kutoka kitandani, na huku akiangalia chini alitembea kupita mbele ya babaye. Na kisha akatembea kuelekea jikoni, bila hata kujaribu kujadiliana na babaye.

    Gaia tayari alikuwa ameketi mezani ambayo alikuwa ameandaa na alikuwa akiwatumia ujumbe rafiki zake na kufanya mipango nao.

    Elio aliketi mbele ya dadaye. Walakini hakuongea neno hata moja naye wakati wote wa chakula cha jioni.

    Chakula cha jioni kilibainika kuwa kisicho cha furaha. Kila mtu alikuwa akiongea kuhusu matukio yao ya kila siku, isipokuwa Elio, ambaye alikula vipande vichache vya nyama na kurejea kwenye chumba chake haraka iwezekanavyo. Mamaye alisikitishwa na ishara hiyo, na babaye pia ambaye alionekana kukunja uso.

    Wakati Giulia na Carlo waliachwa chumbani wakati walikuwa wanaondoa sahani mezani, walianza kuzungumzia mada iyo hiyo ya awali: tabia mbaya za mwanao.

    Ni nini tunafanya vibaya? Hata siwezi kuelewa! Gaia ni mtu tendaji, mwenye furaha na mwenye hiba! alisema Giulia

    Nilimpuuza sana! Carlo alijilaumu kama kawaida.

    Wewe si baba pekee duniani ambaye analazimika kuwa mbali na nyumbani kwa saa nyingi. Mimi, kwa upande mwingine, niko nyumbani kila alasiri Alirudia tena kwa kuwa hakutaka mumewe kuhisi kuwa na mzigo begani.

    Sio swala la tabia, Giulia, kwa sababu Elio hakuwa hivi awali, na unaijua!

    Natamani pia kwamba asingekuwa hivi, Carlo, lakini watoto hubadilika wanapokua. Na kisha, wanazidi na kuzidi kuwa wabaya zaidi, sivyo? Akiwa shuleni ni balaa. Natarajia kuwa hatapinga, lasivyo hatutaweza kumpeleka kwenda kambi ya majira yajayo ya joto...hatutaweza kumruhusu kwenda shule wakati wa kiangazi...hatafurahia!

    Giulia, watoto wengine kwa kawaida huburudika shuleni wakati wa kiangazi. Watoto wa Francesca na Giuseppe wanafurahia sana. Unafahamu vyema kuwa hatafanya chochote kwenye kambi ya majira ya joto! Tunahitaji kutafuta chaguo jingine, kitu ambacho kitamfanya apambane. Hata haonekani kuwa na furaha. Je! Unakumbuka jinsi tulivyokuwa na nguvu wakati tulipokuwa na umri sawa na yake?

    Bila shaka, naikumbuka! Mamangu angefoka kwenye mlango wetu kwamba chakula cha jioni kimekuwa tayari. Lakini, mara nyingi, hata singemsikia kwa kuwa nilikuwa na shughuli nyingi kwenye bustani nikijibingirisha kwenye nyasi. Tulikuwa na furaha na huru. Kwa kweli hatuwezi kumpa maisha kama hii mjini. Walakani, hajui jinsi ya kufurahia kambi ya majira ya kiangazi.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1