Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Siri Kali
Siri Kali
Siri Kali
Ebook159 pages2 hours

Siri Kali

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Shida Kwisha ana kisa, “Mrembo alinijulisha kuhusu mradi wa kuwekeza. Bila kuuliza maswali mengi niliingia. Nami niliwaambia watu wengi lakini ni wachache sana walionisikiliza. ‘Mtu hana kitu, ni uwekezaji gani atakwambia na umsikilize?’ watu walinichekelea.”
Wale watu wa zamani walikuwa watu wa kawaida. Walikuwa maskini wakabadilika kiasi cha kuwa matajiri si wa kutajika tu bali wa kutisha. Walipataje utajiri? Swali hilo lilikuwa kero kwao kwa kuwa walitaka wao wawe matajiri peke yao. Kiini cha utajiri kilikuwa siri kali. Siri kali hiyo ndiyo aliyoipata mtu aliyetambua umaskini si kizalia. Akaitoa hiyo siri kali ya siri kali tano kwa watu ili kila mtu aweze kuwa tajiri. Siri kali ilikuwa, ni na itakuwa dawa ya mabadiliko. Ukiipata na uitumie utatajirika. Ukiipata lakini usiitumie utabaki maskini vivyo hivyo.

LanguageKiswahili
Release dateJun 3, 2013
ISBN9781301591107
Siri Kali
Author

James Kemoli Amata

I am a retired secondary school teacher of Kiswahili (and Christian Religious Education) and an excited preventive healthcare marketer with Green World Health Products Company.I am a 1976 University of Nairobi Bachelor of Education [Arts (Hons)] graduate and a freelance content writer with a passion for writing and indeed I am a farmer-like author with many titles.I published my first book in 1985, by traditional publishing. I have tried self-publishing and now I am in great heat to explore E-publishing.However, I will never forget my Taaluma ya Ushairi (with Kitula King’ei) from which the publisher ate fat alone, and happens to be an E-book without my knowledge.As I do my business, I worship God in African Kenya Sabcrynnsk of Soi (Prayer and Healing) Church.

Read more from James Kemoli Amata

Related to Siri Kali

Related ebooks

Reviews for Siri Kali

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Siri Kali - James Kemoli Amata

    Siri Kali

    Iwapo bado unaabudu uajiriwaji kazi na mtindo wa zamani wa kufanya biashara, USIKISOME KITABU HIKI.

    James Kemoli Amata

    Vitabu vingine vya mwandishi huyu

    Mwongozo wa Kipekee wa Mwisho wa Kosa, Africawide Network

    Mwongozo wa Kipekee wa Kifo Kisimani, Africawide Network

    Mwongozo wa Kipekee wa Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine,

    Africawide Network

    Mwongozo wa Kipekee wa Utengano, Africawide Network

    Mtaala wa Fasihi Kwa Shule Za Sekondari, Igudwa Publishers

    Highly Regretted: An autobiography of a bad teacher, AuthorHouse, 2010

    Kisa cha Zahara Mage, Mvule Africa, 2008

    A Villa For Zahara

    An Introduction to the Theory and Practice of Network Marketing

    Bahati Alikata Kiu

    Before and After Your Wedding

    Don’t Wait for the Government

    Dunia Ina Mema Mengi

    How I Became God’s Enemy

    How To Fail Any Examination

    Keep on scratching! Or change by choice

    Kijana Aliyetaka Kufa Vizuri

    Life is Health and Wealth

    Mashairi Rahisi: Mazoezi na Majibu

    Mitihani Kielelezo ya Kiswahili KCSE

    Nelson Mandela Madiba

    Obesity and Poor Health

    Relax, Doctor

    Satan In An Angel’s Robe Hid in Sabcrynnsk

    Ushairi na Aina na Bahari za Mashairi

    You Can Be There Before You Reach There

    Beauty Face

    Let Us Heed Good Advice

    Tuchambue Tamthilia: Mstahiki Meya ya Timothy M. Arege

    Sweet Beauty Face

    Siri Kali

    James Kemoli Amata

    Anwani ya Mahali:

    Tiens Specialty Shop

    KVDA Plaza, Mezzanine Floor

    Eldoret

    Kenya

    Anwani ya Posta:

    PO Box 2-30105

    Soy

    Kenya

    Rununu: +254 721 720 699/+254 734 720 699

    B-Pepe: kemoli2003@yahoo.com

    Siri Kali

    Hakimiliki© James Kemoli Amata, Jumamosi, Septemba 08, 2012

    Ni jambo la aibu na kinyume cha sheria mtu mwenye mizani kujigeuza kupe na kula jasho la mtu mwingine.

    Kimetangazwa

    Na James Kemoli Amata katika Smashwords, Jumatatu, Juni 03, 2013

    Maelezo ya Idhini ya Toleo la Smashwords

    Kitabu hiki cha kielektroniki kimeidhinishwa kwa raha na furaha yako peke yako ya kibinafsi. Usikiuze tena wala usiwape watu wengine. Ukitaka kutumia pamoja na mtu mwingine, tafadhali nunua nakala ya ziada kwa kila mtumizi. Iwapo unakisoma kitabu hiki lakini hukukinunua au hakikununuliwa kwa matumizi yako wewe peke yako, hivyo basi kirudishe kwa Smashwords.com na ununue nakala yako mwenyewe. Asante kwa kuiheshimu kazi ngumu ya mtunzi huyu.

    Nawatabaruku

    Rose M. Adagala, Esther Sumukwo na Jemimah Kang’alika Mwangi

    Kimekokotolewa na Lilian Mumbua Odoyo

    Usanii wa jalada na Edward Odoyo

    Picha ya jalada ni kwa hisani ya Judy Jebichii Ng’etich

    Ukiri

    Bila Jeniffer Chepkirui Lihasi, wa Modern Professional Centre, Soy, singeweza kuisarifu kazi hii. Daima amekuwa msaada kwangu kila niwapo na haja ya huduma za tarakilishi.

    Beatrice Amwayi wa Kogo Plaza, Eldoret, ametekeleza wajibu muhimu sana katika kuiwezesha kazi hii kuwa jinsi ilivyo.

    Katika uandishi wa kitabu hiki nimewafurahikia Catherine Sarbabi, Eveleen Pwokah, C.B. Peter, Isaac Kimaiyo Chebii, Richard Wekesa na James Shimanyula.

    Mkono wa Wilson Maiyo u katika kazi hii.

    Nukuu

    Ugali usio na kitoweo usinichome bure, hayati Babu Mzee Musa Idah alisema.

    Nitayakumbuka daima maneno hayo, hasa tangu alasiri ya Mei 25, 1999.

    Siri Kali

    James Kemoli Amata

    * * *

    Hints

    Kitangulizi

    1

    Watu Waliokuwa Si Watu

    2

    Mbegu Mbaya

    3

    Elimu Ya Mabadiliko

    4

    Enzi Mpya

    5

    Ukweli Mchungu

    6

    Umaskini Si Kizalia

    7

    Watu Na Ndoto Zao

    8

    Nafasi Ya Mwisho

    9

    Jahazi Limeng’oa Nanga

    10

    Maisha Ya Kuyagura

    11

    Ruwaza Ya Mrembo

    12

    Kizazi Kipya

    13

    Kumbukumbu

    14

    Shukrani

    Faharasa

    Mwandishi

    Kitangulizi

    USIKISOME KITABU HIKI, iwapo unachukia upuuzi

    Iwapo kweli unachukia upuuzi, HIKI KITABU USIKISOME!

    Naomba nianze kwa shajara, hasa sehemu tu ya shajara. Jumanne, Septemba 15, 2012 tulimzika Amu Abinayo Majanga Idah.

    Jumanne, Machi 19, 2013 tukamzika Shangazi Deborah Lunyagi.

    Hapa ndipo sehemu tu ya shajara yangu inaanzia na hata tena si mwanzo bali ni kama kichocheo cha hadithi hii ya kubuni huku ikitishia kuwa kisa cha kweli kilichosheheni UKWELI.

    Kabla ya hii siku niliota ndoto mbili na si ndoto mbili bali ni ndoto mbili tu ambazo nimechagua kwa uamuzi wa kibinafsi kuziandika katika hii sehemu tu ya shajara.

    Kumbe ndoto niliyoiota haikuwa ndoto tu, ilikuwa UKWELI, ukweli mtupu.

    Nilikuwa nyumbani, kijijini. Nikakuwa nimeliegesha gari langu si gari la PRADO Land Cruiser jeusi. Akaja Meya (ambaye kwa heshima zote sitamtaja jina) akashangaa na kutokwa, "Kali Mr Kemoli yagula ku umudoga kuli yigu mba (Hata Bw Kemoli hajawahi kununua gari (kubwa) kama hili), Mudanyaatulizi hayi izisendi zyagulii umudogigu (Mudanya ametoa wapi pesa ambazo amenunulia gari hili)?"

    Hiyo ndoto si ndoto tu iliyopita hivyo lakini sijawahi kuisahau. Hata niliiandika pahali.

    Ndoto ya pili na si hiyo tu bali ni ndoto nyingine lakini ya pili mimi kuiandika katika sehemu hii tu ya shajara.

    Nilikuwa katika nyumba ya baba yangu. Nje ya nyumba yangu nilikuwa nimeegesha magari mawili mapya. Tukiwa amu yangu mmoja (ambaye kwa heshima zote sitamtaja jina), baba yangu na mimi, amu alifadhaika, "Onyoo hai izisendi zyugulii imidoga jivili (Umepata wapi pesa ambazo umenunulia magari mawili)?"

    "Mbuguu ku zizyo (Nilitoa katika zako), katika hasira iliyojificha katika unyenyekevu, nilimpa jibu. Henza mwa kaunti yoyo olole (Angalia katika akaunti yako uone)."

    Basi hizo ni ndoto tu na ndoto ni ndoto tu kwa watu wengi. Sikwambii mimi ni mmoja wao au la. Wasomi husema ndoto ni mawazo aliyokuwa nayo mtu, kwa ufahamu au la si hoja. Kwamba ndoto ni matokeo ya ubongo kushughulika ama pengine kuhangaika kwa sababu ya mawazo ndio ujuba wa watu waliovila vitabu vihusuvyo utendakazi wa ubongo.

    Liwalo na liwe.

    Siku nyingi tangu tujuane

    Marehemu Victor Malova alikuwa mtu mwema sana sana. Akiwa katika gari yao au ya rafiki yake, akiendesha au kama amebebwa, alikuwa hamwachi mtu yeyote aliyekuwa anaelekea alikokuwa anaelekea.

    Noah ni mtu wa watu katika barabara hiyo.

    Mwalimu Juvenalis Skipper Nyongesa amekuwa akinibeba katika gari lake. Siku moja nilimtaka msaada anipelekee watoto na wajukuu wangu hadi Soy waabiri gari kwenda Voi. Siku hiyo walikuwa wasafiri kwa Simba Coach ambayo haimgoji abiria nayo mvua ikawa inanyesha kunyesha.

    Nilifunza na Grace Luvonga. Mume wake amekuwa akinibeba kutoka Soy na badala ya abetee mahali pake amekuwa akipapita anifikishe nyumbani ndipo ageuze gari kwenda kwake.

    Barabara ya Likuyani-Kogo ina watu wengi wazuri sana wenye magari ya kibinafsi. Daktari Oyugi na Mzee Arthur Gitonga daima hawaniachi wanaponipata barabarani nikienda au nikitoka Soy. Pamoja na hao yupo Daktari Munala wa Seregeya ambaye siwezi kumsahau kati ya watu ambao kuwemo kwangu katika magari yao si kero. Wangekuwa wananipita kama kwamba hawajaniona. Barabara iyo hiyo ina mtumishi mmoja wa Mungu. Haikosi aliamriwa, Usiwahi kumbebea mwanadamu awaye yeyote yule katika hili gari. Utakapofanya hivyo hakika utakufa. Kumbuka hapo atakaye kufa.

    Siku moja

    Nilikuwa Soy nikitaka kwenda Eldoret kwa bahati tu nikamwona David Alela. Nilimsalimia na kumwambia nilikokuwa ninaenda. Alikuwa na furaha sana kunipeleka. Sikuwa nimejua alikuwa amechomoa chuma.

    Ijumaa, Machi 15, 2013

    Shangazi yangu Deborah Lunyagi aliaga dunia baada ya muda mrefu wa kuugua ugonjwa wa shinikizo la damu na ndugu yawo kisukari.

    Maziko yalikuwa Jumanne, Machi 19. Baba alitoka nyumbani, akiandamana na mzee wa kijiji Mugera, mbele yangu. Punde tu nikawa nimekaribia kufika katika njia ya kwenda Mwilongo, hadi Bendera. Akatokea Kidaha katika gari lake. Aliangalia nilikokuwa. Punde tu nilifika barabarani nikawa ninakimbia niwafikie baba na mzee wa kijiji. Nikaona wanaabiri gari la Kidaha. Nilijongea katikati ya barabara ikawa hawangeniona katika kioo cha kando. Wakaondoka wakaenda. Punde bodaboda wa pikipiki alifika nikamwuliza anipeleke hadi makutano ya Chavakali.

    Kufika Chavakali wazee waliokuwa mbele yangu walikuwa wameshuka na wanataka kuabiri gari la kutupeleka Bunyore, Ivunangwe.

    Ulikuwa wapi? baba alishangaa.

    "Nilikuwa tu katika gari mlimokuwa lakini hamngeniona.

    Kilikuwa kicheko. Mzee wa kijiji aliponiuliza niseme ukweli nilimpa jibu fupi, "Amadiku gaa gukugingwa gafa (Siku zangu za kubebwa ziliisha), ndukanaa mbe ning’ingaa avandi (nastahili niwe nikiwabeba wengine).

    Rafiki, baba na ndugu Seth Ambale alikuwepo. Sitasahau alinisisitizia, "Kilimo ni muhimu sana sana katika maendeleo. Huwezi kuendelea bila kilimo. It is very very very important." Nilichekea rohoni huku nikimjibu kimoyomoyo, ‘Mbona wakulima hawapatikani katika orodha ya Who owns Kenya au Who is who in Kenya?’

    Siku iyo hiyo nilimjulisha amu William (Listwa) Idah habari moto kuhusu Levitical Investment Company Limited (LICL). Yeye ni mkulima kwa ajili ya maisha ya humu duniani mlimo mema mengi. Nitaulizia zaidi halafu nichukue uamuzi mwafaka, alihitimisha maelezo yangu.

    Jioni, Imbuga Alex, Amosi Listwa na mimi, tukawa tunarudi. Tulipofika Chavakali, karibu na NCPB ambayo ni nadra iwe na nafaka zozote, Imbuga aliona gari la Musungu (Si Musungu wa hii hadithi), ndugu yake Kidaha. Akawa mwepesi kwenda kumwuliza iwapo angetupeleka nyumbani.

    Musungu akamjibu hakuwa akienda nyumbani. Tukaendelea kwa haraka tukiomba sana mvua ituhurumie tufike kwanza. Mvua ilitupata vizuri sana mara tu baada ya kuifikia lami katika kona kabla ya Bendera. Tulijikinga hapo ikanyesha mvua kubwa sana lakini tukashukuru sana kwa kuwa hatukunyeshewa.

    Mvua ile ilinyesha kwa muda mrefu. Ilipokatika tuliendelea na safari yetu tukawa tumepita Mwilongo tumemaliza mlima. Musungu akatufikia akitaka kutubeba pasipo haja kwani tulikuwa tumekaribia mahali pa mimi kubetea. Kama Imbuga na Amosi wangeabiri mimi singeabiri kwani nilikuwa nimebakiza masafa mafupi tu na niwe nimefika.

    Jumamosi, Aprili 13, 2013

    Nilikuwa njiani natoka Likuyani naenda Soy. Nilikuwa nimefika mahali panapoitwa Kwa Rubeni. Akanifikia Prinsipo Fredrick Mwanyumba Tweni katika gari lake zuri. Alinipungia mkono wa salamu akaendelea na safari yake. Nilizifurahia sana salamu zake ambavyo si kawaida watu wawasalimie wenzao siku hizi wazisemazo ni za shughuli nyingi na za kung’ang’ana daima dawamu. Hawana furaha ya salamu na hawana nafasi ya salamu. Nilipofika Home Cup, mahali ambapo barabara imeoza kuoza na hata haipo, paombewapo, Magari yakwame tusukume tule kitu, alinifikia Fredrick Simiyu katika pikipiki yake. Akasimamisha pikipiki yake na kunisalimia. Nikamtaka aendelee na safari yake akanijibu, Siwezi kukuacha na unatembea ukienda kule ninakokwenda. Niiifurahia lifti kwa kuwa mtu akikupa lifti anakuokolea muda fulani tukielewa muda si kama pesa ambazo ukigawana na watu unasifiwa lakini ukigawana muda wako na watu unaonekana kama mtu ambaye hana kitu muhimu cha kufanya.

    Jioni nilipokuwa nimefika Kwa Rubeni ninarudi baada ya shughuli zangu niliona mtu katika Prado yake akimrushia bodaboda wa pikipiki maji ya matope shwaaaaaa!

    Jumatano, Aprili 17, 2013

    Jioni, mke wangu akitoka kanisani alikutana na rafiki yangu Pasta John Ombodo. Akawa na jambo kwake. "Msalimie rafiki yangu. Huwa tunakutania Eldoret. Alinipeleka pahali katika kitu Levitical. Margaret, anoho kogotaa (Margaret, ama tunapotea)?"

    La hasha, m sawasawa, akampa moyo bila kusita. Hamjapotea hata kidogo, mtakuja kuhisi raha hapo baadaye.

    Maneno haya ni hisia za watu wengi. Mungu abariki.

    Alhamisi, Aprili 18, 2013

    Kuna uwezekano tunashindwa kuwavutia watu na kuwashawishi kwa namna tunavyowakabili na kuwasiliana nao. Nilikuwa njiani naenda Soy. Akanifikia mtu mmoja wa bodaboda ya pikipiki. Mzee huna hata za chai mfukoni?

    Nini?

    Huna hata pesa kidogo tu za chai yangu?

    Mtu akikuona unatembea yupo yule ambaye mara moja anajua huna pesa.

    Mtu akikuona unatembea yupo yule ambaye daima anajua unabania pesa.

    Unaweza kuwa unatembea kwa sababu unataka kuonana na kuongea na

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1