Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri
Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri
Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri
Ebook421 pages4 hours

Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

James Kemoli Amata ni mwalimu mstaafu. Alifunza Kiswahili kwa miezi 376 katika Shule Kuu Sekondari ya Wasichana ya Moi, Eldoret (Septemba 1976 – 1986 na Julai 1990 – Februari 2000); Shule ya Sekondari ya Wangulu, Wodanga (1987 – Julai 1990) na Shule ya Sekondari ya ST John The Baptist, Likuyani (Februari 2000 – 2007) akastaafu.
Hivi sasa ni mwandishi asiye na mipaka huku akiwa mtekelezi wa tiba mbadala katika Kampuni ya Bidhaa za Afya ya Tiens na wakati uo huo akiwa mjasiriamali katika kampuni kuu ya Fountain Enterprises Progaramme (FEP).

LanguageKiswahili
Release dateOct 30, 2013
ISBN9781311362728
Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri
Author

James Kemoli Amata

I am a retired secondary school teacher of Kiswahili (and Christian Religious Education) and an excited preventive healthcare marketer with Green World Health Products Company.I am a 1976 University of Nairobi Bachelor of Education [Arts (Hons)] graduate and a freelance content writer with a passion for writing and indeed I am a farmer-like author with many titles.I published my first book in 1985, by traditional publishing. I have tried self-publishing and now I am in great heat to explore E-publishing.However, I will never forget my Taaluma ya Ushairi (with Kitula King’ei) from which the publisher ate fat alone, and happens to be an E-book without my knowledge.As I do my business, I worship God in African Kenya Sabcrynnsk of Soi (Prayer and Healing) Church.

Read more from James Kemoli Amata

Related to Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri

Related ebooks

Reviews for Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri - James Kemoli Amata

    Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri

    James Kemoli Amata

    Tufanye mambo yasiyo ya kawaida,

    Ingawa kamwe si jambo la kawaida,

    Kufanya jambo lisilo la kawaida,

    Ulaghai ndiwo mambo ya kawaida.

    Zingatia haki, Mungu Akubariki,

    Puuza haki, yakupate ya kukupata.

    © James Kemoli Amata, 1987

    Anwani ya Mahali:

    Tiens Specialty Shop

    KVDA Plaza, Mezzanine Floor

    Eldoret

    Kenya

    Anwani ya Posta:

    PO Box 2-30105

    Soy

    Kenya

    Rununu: +254 721 720 699/+254 734 720 699

    B-Pepe: kemoli2003@yahoo.com

    Uandishi wa Insha na Tungo Nzuri

    Ni jambo la aibu na kinyume cha sheria mtu mwenye mizani kujigeuza kupe na kula jasho la mtu mwingine.

    Kimetangazwa

    Na James Kemoli Amata katika Smashwords,Oktoba30, 2013

    Maelezo ya Idhini ya Toleo la Smashwords

    Kitabu hiki cha kielektroniki kimeidhinishwa kwa raha na furaha yako peke yako ya kibinafsi. Usikiuze tena wala usiwape watu wengine. Ukitaka kutumia pamoja na mtu mwingine, tafadhali nunua nakala ya ziada kwa kila mtumizi. Iwapo unakisoma kitabu hiki lakini hukukinunua au hakikununuliwa kwa matumizi yako wewe peke yako, hivyo basi kirudishe kwa Smashwords.com na ununue nakala yako mwenyewe. Asante kwa kuiheshimu kazi ngumu ya mtunzi huyu.

    Usanii wa jalada na Edward Odoyo

    Picha ya jalada ni kwa hisani ya Yvette Rose Ng’onyere na Briana Rachami

    Toleo la Smashwords

    Nina wingi wa shukurani kwa Smashwords. Imekubali kukitoa kitabu hiki - Insha na Tungo Nzuri - ambacho kwa miaka mingi, tangu 1987, kilikuwa mimba isiyotoa mtoto. Mwanzoni mswada ulikuwa Uandishi wa Insha. Tangu mwaka huo imekuwa safari ndefu yenye mabonde na milima, miiba na mawe, ukame na magharika, majangwa na mabahari, majitu na mazimwi na wapekuzi na majizi.

    Watu wengi wamedokoadokoa mpaka shishangai mhadhiri mzima wa chuo kikuu akiiba kazi ya mawazo ya mwalimu tu wa shule ya sekondari.

    Hata hivyo, hilo si jambo la kujalisha. Kilicho kikuu ni kwamba nina watu ambao watanufaika kwa kazi hii kwa njia halali. Walioiba, wabarikiwe kadiri ya wizi wao. Waliowasaidia wezi kuiba, vilevile wabarikiwe kwa kiwango cha usaidizi wao katika kazi haramu ya wizi.

    Ukweli ni kwamba, wezi walioiba mawazo yangu katika mswada wa kitabu hiki, mahabithi wakiwa si haba katika tasnia ya uandishi, katika hii dunia iliyojaa matapeli, hunifanya nijihisi ni tayari kuwasomea halbadria au kumba Roho Mtakatifu wa Mtume Petro awashukie, au Yule wa Elia awateremshie moto. Hata hivyo, naomba hilo lisitokee, lakini la kuwafika liwafikie kwingineko katika Jina Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

    Jambo la kweli ni kwamba upanga ni uleule. Wewe uliyetumia asali ya nyuki bila hiari yake utakapodungwa usilie. Bora tu yatakayokupata yakupatie kwingine.

    Mambo mengi yamefanyika tangu 1987 hadi leo, 2013. La kawaida ni kwamba mimi si mwalimu wa darasani tena; mimi ni mwalimu mstaafu, aliyekuwa mwalimu. Namshukuru sana Mwenyezi-Mungu kwa hili, kwani Amenibariki kupindukia na Angali Ananibariki. Si wote wafauluo kustaafu. Wengine hufutwa.

    Linalonihuzunisha wakati mwingine ni kuwa wengi wa marafiki zangu tayari wameenda na hawatawahi kuona matokeo ya mchango wao katika uandishi na utolewaji wa kitabu hiki. Daima nitawakumbuka Shadrack Agufa Endusa, Dani Kemoli, Morris Etsula, Dkt. Dave Wando, Kasisi C.B. Peter na Profesa Naomi Luchera Shitemi. Hata hivyo, watabaki hai katika nafsi yangu.

    Daima sitaisahau historia ya kitabu hiki iliyoanza karibu miongo mitatu iliyopita nikiomba mawazo, mtazamo na hisia hasi viniondokee niendelee kufurika mawazo, mtazamo na hisia chanya.

    Naam, kitu kikubwa ni kwamba mipango yote imo katika mokono ya Mungu naye mwanadamu ni mnyoo tu.

    Leo hii kinitiacho furaha kubwa ni kule kuendelea kuwasiliana na baadhi ya wanafunzi wangu wa zamani huku wengine wakinifurahikia ingawa walisomea katika shule zingine. Wote hao ninawakaribisha katika shughuli zangu za sasa.

    Namkumbuka vizuri sana Catherine Mutakale wa Likuyani kwa kazi ngumu aliyonifanyia wakati wa kuuanda mswada wa kitabu hiki katika awamu yake ya mwisho.

    Napenda niwashukuru sana Rose Mudora Adagala wa Shield Exalted Printers, Skymark, Eldoret, kwa usaidizi wake mkuu; Betty Amwayi na Agnes Kanus wa Japtech IT Solutions, Kogo Plaza, kwa kusimama name katika shughuli nyingi za uandishi; Muthoni Karega kwa moyo alionipa ingawa sasa ni karibu miaka ishirini iliyopita; Job Were wa Tiens Healthcare Products Company kwa kunionyesha njia ya kurejesha na kuimarisha afya; na Sylvia Waseme Wandere wa Fountain Enerprises Programme, kwa kuwa mama yangu mkuu, kuniweka katika ulimwengu wa wajasiriamali.

    Tena napenda sana nikariri sana kuishukuru sana SMASHWORDS kwa kukubali kukitoa kitabu hiki.

    James Kemoli Amata,

    Modern Professional Worldwide, Soy,

    September, 2013.

    Nukuu

    24. Je, mwenye hekima alima daima ili apande?

    Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja?

    25. Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake,

    je, hamwagi huko na huko kunde, na kutupatupa jira,

    na kuitia ngano safusafu,

    na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemathi karibu na mipaka yake?

    26. Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha. – Isaya 28, BIBLIA TAKATIFU, Jimbo la Bologna, kwa niaba ya Baraza la Maaskofu, Tanzania, 2004.

    Mtabaruku

    Kwa heshima ya Dkt. James Serumaga aliyenitia uchu wa kukiandika kitabu hiki kwa maneno yake, Mwalimu, mngali mnawafundisha watoto wetu jinsi ya kuandika vizuri? Kweli mnawafunza hati sahihi na nadhifu za kusomeka kwa urahisi?

    Na wazazi wangu, Gerishom Amata na Rosebetter Muhonja ambao bila wao ningekuwa wapi, ati niandike?

    Yaliyomo

    Shukrani

    Utangulizi

    Sehemu ya kwanza

    Msingi wa insha bora

    1.1 Urefu wa insha

    1.2 Hatua muhimu

    1.3 Vidokezo

    1.4 Mpangilio

    1.5 Kichwa

    1.6 Utangulizi

    1.7 Maendelezo

    1.8 Kiini

    1.9 Msamiati

    1.10 Tahajia

    1.11 Sarufi

    1. 12 Herufi sahihi

    1.13 Kukamilishia neno katika mstari mwingine

    1.14 Uakifishaji

    I. Alama za uakifishaji (viakifishi)

    II. Herufi kubwa na ndogo

    1.15 Usafi

    1.16 Tahadhari

    1.17 Kujiandaa

    Sehemu ya pili

    Mifano ya insha na tungo zingine

    2.1 Maelezo (ufafanuzi)

    2.2 Mazungumzo (dayolojia)

    2.3 Mahojiano

    2.4 Hotuba

    2.5 Barua

    2.6 Tungo za risala

    2.7 Ripoti

    2.8 Kumbukumbu

    2.9 Dibaji (utangulizi)

    2.10 Mapitio (Tahakiki)

    2.11 Ardhilhali

    2.12 Tangazo

    2.13 Mapendekezo

    2.14 Wasifukazi

    2.15 Hojaji

    2.16 Shajara

    2.17 Ratiba

    2.18 Resipe

    2.19 Insha na tungo za kiteknolojia

    2.20 Maagizo

    2.21 Insha za mjadala

    2.22 Insha za wasifu

    2.23 Insha za methali

    2.24 Hadithi za kubuni

    2.25 Mdokezo

    2.26 Tungo za kitaaluma

    Sehemu ya tatu

    Tungo za kisanii

    3.1 Fasihi kwa jumla

    3.2 Hadithi fupi

    3.3 Fasihi-simulizi (hadithi)

    (a) Hadithi (simulizi)

    (b) Ngano za hekaya (kiayari)

    (c) Ngano za kishujaa

    (d) Ngano za usuli (visasili)

    (e) Ngano za mtanziko

    (f) Ngano za kimafumbo

    (i) Ngano za istiara au jazanda

    (ii) Ngano za mbazi (vigano)

    (iii) Ngano za mchapo (au mchapo)

    (g) Ngano za kichimbakazi

    (h) Ngano za soga

    (i) Simulizi za kihistoria

    (i) Tarihi

    (ii) Ngano za migani (visakale)

    (iii) Ngano za usuli (visasili)

    (iv) Ngano za shajara

    (v) Ngano za kumbukumbu

    (j) Hurafa (halafa, khalafa)

    2. Maigizo

    (a) Tamthilia (michezo ya jukwaani, mchezo ya kuigiza)

    (b) Mazungumzo

    (c) Majigambo (vivugo)

    (d) Vichekesho

    3. Ushairi

    (a) Ngonjera (ushairi wa kisemezano, ushairi wa kijibizana)

    (b) Malumbano (ushairi wa kihotuba, maoni)

    4. Nyimbo

    (a) Nyimbo za mapenzi

    (b) Nyimbo za historia

    (c) Nyimbo za wasifu (tondozi)

    (d) Nyimbo za maonyo

    (e) Nyimbo za mahubiri (ibada, dini, tambiko)

    (f) Nyimbo za mitakasohisia

    (g) Hodiya (wimbo wa kazi, kihimizo, kihamasishaji)

    (i) Wawe (vave)

    (ii) Kimai (kimaji)

    (h) Bembezi (bembelezi, pembejezi)

    (i) Mbolezi (tahalili, nyimbo za maafa, nyimbo za maombolezi, nyimbo za kilio)

    (j) Tendi

    (k) Nyiso (nyimbo za tohara)

    (l) Nyimbo za kisiasa

    (m) Nyimbo za arusi

    (n) Tumbuizo

    (o) Tenzi (tendi)

    (p) Nyimbo-jadi (nyimbo-jadiiya)

    5. Maghani

    (a) Majigambo (kivugo)

    (b) Tondozi

    (c) Pembezi

    (d) Rara

    Sehemu ya nne

    Maelezo ya ziada

    Sehemu ya tano

    Usahihishaji wa insha

    Jedwali la Kukadiria Kiwango cha Insha na Tungo

    Sehemu ya sita

    Maswali ya mazoezi

    Marejeleo

    Baadhi ya vitabu vingine vya mwandishi huyu

    Ripoti ya Utathmini wa Uandishi wa Insha

    Shukrani

    Sina njia ya kuwashukuru watu wote walionifaa hata wakaniwezesha kukiandika na kukiandaa kitabu hiki hadi kikawa jinsi kilivyo sasa. Kusema kweli kitabu hiki ni kazi ya wengi. Kwa sasa ninaweza kuwataja tu:

    Mwenyezi-Mungu kwanza;

    Halafu, Margaret M’mbone, mke wangu;

    Na wana wangu Tabuley Musungu, Jemimah Kang’alika, Annette Kalenya, Juliet Minage, Felix Amata na William-Collins Idah;

    Na wajukuu wangu Aurelia M’mbone, Rose Walegwa, Carmila Muhonja, Yvette, Rose Ng’onyele, Alison Raheli Savane, Denzel Kemoli, Briana Rachami;

    Mashemeji zangu Hesbon Mwendwa Aligula wa Mbale, Maragoli, na Abwaoo Ndayara wa Kahoya Estate, Eldoret;

    Rafiki na somo yangu Dan Kemoli wa KEBAMU Associates, Cerified Public Accounts (K) Nairobi;

    Rafiki mkubwa na mwalimu wenzangu Morris Etsula alipokuwa na hata baada ya kutoka Shule Kuu ya Sekondari ya Wasichana ya Moi, Eldoret na kuuhama ualimu;

    Rafiki mkubwa na mwalimu wenzangu Dave Wando wa Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret;

    Ndugu yangu Eshmael Endusa wa Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret;

    Ndugu yangu Shadrack Agufa Endusa, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mseto ya Wangulu, Wodanga.

    Washirika wangu katika tasnia ya uandishi:

    Dkt. A.G. Gibbe aliyekuwa wa Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret;

    Prof. Naomi Luchera Shitemi wa Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret;

    Bi. Priscah Silavula wa Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret;

    Kasisi C.B. Peter na Isaac Chebii wa Zapf Chancery Research Consultants and Publishers, Eldoret;

    Mwalimu Tasman Imbisi Chogo wa Shule ya Sekondari ya St. John the Baptist Likuyani, Soy;

    Na Bernard Lihasi Omega na Jeniffer Chepkirui Lihasi wa Modern Professional Centre, Soy.

    Pia, ninajisikia mwenye fahari na furaha kuwashukuru sana wanafunzi wangu wa Kiswahili wa Shule ya Sekondari ya St. John the Baptist Likuyani, Soy (Februari, 2000 - ); Shule Kuu ya Sekondari ya Wasichana ya Moi, Eldoret (Septemba 1976 - 1986 na Julai 1990 - Februari, 2000); Shule ya Sekondari ya Mseto ya Wangulu, Wodanga (1987 - Julai, 1990).

    Ninawashukuru mno walimu wote ambao walinifunza, akiwemo Trizah Onzere wa Shule ya Msingi ya Wangulu, kwani bila wao nisingekuwa kitu.

    Kati ya Walimu Wakuu siwezi kuwasahau Jane Kidiga, hayati Ank de Vlas, Avedi Buliva, Benson Mudangale Onzere na Seth Ambale.

    Siwezi kusahau Chuo Kikuu cha Nairobi kwa kunituza Shahada ya Shani ya Ukufunzi (B.Ed. Arts (Hon));

    Na Baraza la Mitihani ya Kitaifa la Kenya (Kenya National Examinations Council) kwani bila hilo nisingepata chemchemi ya mafunzo ya uandishi yaliyo katika kitabu hiki. Kwa kweli yaliyomo yalitokana na mzinga wa KNEC. Hasa shukrani zangu maalumu chakari ziwafikie B.M. Makau, Peter Itebete na Alice Kasibwa.

    Na Tume ya Kuwaajiri Walimu, Nairobi, ambayo bila hiyo nisingewapata wanafunzi nijivuniao, na ambao ni kwa ajili yao na kutokana nao nilikiandika kitabu hiki.

    Bila shaka wapo wengine chungu nzima ambao siwezi kuwataja moja kwa moja. Ninawasihi wanisamehe.

    Utangulizi

    Kitabu hiki kinahusu uandishi wa insha na tungo zingine. Insha ni mtungo wa maneno kwa uandishi wa nathari juu ya jambo fulani. Nathari ni maandishi ya moja kwa moja, yaani, maandishi ya kawaida ya kufululiza.

    Insha hutoa habari juu ya jambo kwa madhumuni maalumu. Madhumuni muhimu katika insha ni kueleweka, na kueleweka huko hutegemea jinsi insha ilivyoandikwa. Insha iliyoandikwa vizuri hueleweka kwa urahisi.

    Lengo kubwa la mtihani ni kuupima uwezo wa mtahiniwa. Lengo la mtahiniwa ni kupata maki nyingi iwezekanavyo katika mtihani. Ni matumaini yangu, inshallah, watakaokitumia kitabu hiki kwa makini watapata haja yao katika uandishi wa insha na tungo bora.

    Kitabu hiki kitawafaa waalimu na wanafunzi wa shule za upili. Kitawawezesha kuzingatia mitindo mbalimbali ya uandishi wa insha na tungo nzuri.

    Vipengele muhimu vimezingatiwa kwa lengo la kuimarisha uandishi wa kila aina ya insha na tungo. Mambo ambayo hupuuzwa na wanafunzi kuwa ni vikorokoro lakini yaziathirizo insha na tungo vibaya yameelezwa katika kitabu hiki. Iwapo watahiniwa watayajali na kuyazingatia, bila shaka uandishi wao utakuwa bora.

    Faida kubwa itapatikana iwapo wanafunzi watafanya mazoezi ya mara kwa mara na kusahihishiwa kazi zao. Hata hivyo, si vyema na hata haiwezekani wanadamu kuzitegemea nguvu zao tu. Bibilia, katika Methali 16:3 inasema, "Mkabidhi Bwana kazi zako, na mawazo yako yatathibitika."

    Kitabu hiki kimekusudiwa kuwasaidia watu wote wenye lengo la kuandika insha na tungo nzuri za kuvutia. Ni matumaini yangu kuwa kitawasaidia wale wote ambao wanajiandaa kufanya mtihani na waandishi wengine ambao wana haja ya kuandika vizuri.

    Pia, ni yakini sitakuwa mwalimu milele na milele. Kuna kustaafu ambako ni lazima kwa maisha ya mwajiriwa yeyote yule. Mtu asihadaike ati umeajiriwa kwa masharti ya kudumu - kudumu kitu gani?

    Siku moja itakuja, ualimu nitawacha,

    I njiani inakuja, siku hiyo sitaicha,

    Na ambayo sitaitaja, Jalali ameificha,

    Siku hiyo yaja kasi, siku ya kuwacha kazi.

    Mzigo nimeubeba, ambavyo sinayo pupa,

    Japo uzito si haba, miye sijatapatapa,

    Hata zizidi dharuba, moyo huatanipapa,

    Siku hiyo yaja kasi, siku ya kuwacha kazi.

    Siku hiyo itafika, kwa kalamu kunipiga,

    Ama pengine kuchoka, au dunia kuaga,

    Takapostaafika, hili si jambo la soga,

    Siku hiyo yaja kasi, siku ya kuwacha kazi.

    Wanaokula fahali, kwao vyeo ni fahari,

    Hawaoni la kujali, kukalia majabari,

    Walimu yao mithili, wananipa kufikiri,

    Siku hiyo yaja kasi, siku ya kuwacha kazi.

    Nimepata maumivu, kufundisha madhaifu,

    Pamoja nao werevu, wasiojua upungufu,

    Maadui wa uvivu, ambao ni maarufu,

    Siku hiyo yaja kasi, siku ya kuwacha kazi.

    Siku yangu ya kwaheri, siku ya kuwacha kazi,

    Nawatakieni heri, msilale usingizi,

    Msome mkifikiri, mjaze wenu ujuzi,

    Siku hiyo yaja kasi, siku ya kuwacha kazi.

    James Kemoli Amata

    Shule ya Sekondari ya Wangulu, Wodanga, 1987

    Sehemu ya kwanza

    Msingi wa insha bora

    1.1 Urefu wa insha

    Ni muhimu ifahamike kuwa urefu wa insha hutegemea kiwango cha mwandishi, masharti na muda. Kuna insha za namna nyingi: fupi na ndefu; za mitihani na za mashindano; na zingine za watungaji kujiamulia wenyewe kuziandika.

    Wanafunzi na watu wengine ambao wanajiandaa kufanya mtihani wa kidato cha nne, Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE) wanahitaji wajizoeze kuandika insha fupi. Kila insha iwe ikiandikwa katika dakika arobaini na tano hivi. Muda huo uwe ni ule unaotumiwa katika kufikiri, kupanga, kuandika na kuipitia insha kwa ajili ya kuyasahihisha makosa watakayoyaona waandishi.

    Insha ambazo si za mitihani zaweza kuandikwa katika muda wowote ikitegemea jambo ambalo mwandishi ameamua kuandika juu yake.

    Wanafunzi wale waandikao maneno matano sita hivi katika mstari wajizoeze kuandika insha za urefu wa kurasa mbili hadi mbili na robo za karatasi ndefu (A4) za mitihani. Kwa jumla insha ziwe za urefu wa maneno 390 hadi 400.

    Kumbuka: Wale waandikao maneno matano sita hivi katika mistari ya karatasi ndefu wazikadirie tungo zenye maumbo maalumu, kama vile, mazungumzo (dayolojia), mahojiano, ripoti, mapendekezo, aridhilihali na kumbukumbu za mkutano, kwa kipimo cha urefu wa kurasa mbili na robo hadi mbili u nusu.

    Tungo za aina hii kwa kawaida ni za maandishi ya mipangilio maalumu. Baadhi yazo huwa katika vichwa mbalimbali. Zikiwa zenye vichwa mbalimbali ni sharti kila kichwa kiandikwe baada ya mstari mmoja kuachwa.

    1.2 Hatua muhimu

    Kabla ya kuanza kuandika insha, ni muhimu sana uamue unataka kuandika juu ya nini. Inafaa uchague ile mada iliyo rahisi kwako kuweza kujieleza kikamilifu na kwa urahisi.

    Ikiwa umeamua uandike insha yako mwenyewe ni vizuri uchague kuandika juu ya mambo ya maana. Hakuna haja kuandika mambo yasiyo muhimu ama mambo machafu yasiyofaidi. Ni jambo zuri uache muda wa saa ishirini na nne au zaidi tangu kuitafiti mada hadi uanzapo uandishi wa insha yenyewe.

    Kama unaandika insha za kufanyia mazoezi ni heri uchague mada zenye habari ambazo unazielewa. Iwapo hulijui au hulielewi jambo, ufanye uchunguzi kwanza. Ukisha kupata habari muhimu ndipo baadaye uandike insha yako kulingana na jinsi unavyoijua na jinsi unavyoikumbuka habari inayohusika.

    Katika mtihani ni muhimu uyasome maagizo kwa makini. Kwa mfano, maagizo yanaweza kuwa:

    Chagua mojawapo ya habari zifuatazo kisha uandike insha isiyopungua kurasa mbili za karatasi za majibu.

    Au:

    Chagua mojawapo ya habari hizi kisha uandike insha ya maneno yasiyopungua 400.

    Mwandishi aliye na mwandiko mkubwa anafaa ajaze kurasa mbili u nusu. Naye mwenye mwandiko mdogo ajaze kurasa mbili. Ni heri uandike insha nzuri ya kiwango kinachotakikana kuliko ndefu (zaidi ya maneno 400) ambayo haitakuwa na mambo muhimu hadi mwisho, na pengine yenye makosa na uchafu mwingi kupindukia.

    Kuna watahiniwa au waandishi ambao wana kipawa cha kujieleza kikamilifu katika maneno machache sana. Watu kama hao wanaweza kuandika insha bora zaidi katika kurasa mbili tu zenye hoja nyingi zaidi. Ni heri uwe na insha fupi nzuri badala ya insha ndefu ya kuchukiza na kuchosha.

    Katika insha zihitajizo idadi fulani ya maneno, hasa katika mitihani, mwandishi anasamehewa maneno machache katika viwango vyote. Kwa mfano, akitakiwa aandike insha ya urefu wa maneno 400, anaweza kuandika insha yenye maneno 390.

    Mwandishi anatakiwa ajipime mwenyewe ili ajue kiasi cha maneno ambayo yeye huyaandika katika mstari mmoja au ukurasa mzima kwa jumla. Iwapo atakuwa amefanya hivyo, hatapoteza wakati wa mtihani wake akijisumbua kuhesabu idadi ya maneno katika insha yake.

    Mwandishi asipojua kimbele kiasi cha maneno ayaandikayo katika ukurasa mmoja basi ahesabu maneno katika mistari michache mizima kisha apige mara idadi ya maneno katika mstari mmoja na idadi ya mistari katika ukurasa. Hivyo, atakisia ukurasa una maneno mangapi na atumie kiasi hicho kuamua ataandika insha ya urefu gani.

    Ni muhimu ikumbukwe jinsi insha ilivyo ndefu, hasa katika mtihani, ndivyo idadi ya makosa inavyozidi kuongezeka.

    1.3 Vidokezo

    Baada ya kujua mada ya insha, urefu unaohitajika, muda alio nao - kidato cha nne ni saa moja na robo tatu ya kutumiwa kuandika insha mbili, moja ya lazima na moja ya kuchagua - mwandishi afikirie juu ya vidokezo na uzito atakaokipa kila kidokezo.

    Vidokezo ni fununu; mambo muhimu; hoja katika insha na uandishi wowote ule. Katika uandishi wa insha, vidokezo ni muhimu sana, kwani humsaidia mwandishi katika kujieleza kwake. Vidokezo mwafaka huwa maneno au vifungu vya maneno ambavyo hutoa fununu kwa mwandishi kuhusu mambo atakayojihusisha nayo katika uandishi wake. Kwa hivyo, vidokezo humwongoza mwandishi katika uzingatiaji wa kiini cha habari.

    Vidokezo ni matokeo ya kuwaza kabla ya kuanza kuandika. Mtu hukumbuka mambo tofauti katika wakati tofauti. Huenda alikumbuke jambo lililo muhimu sana baadaye. Katika mtihani na wakati mwingine wowote ule wa kuandika insha, vidokezo viandikwe jinsi vinavyokumbukwa. Wakati huo mwandishi ajiondoe katika hali ya wasiwasi. Awe mtulivu na kila akumbukapo jambo aliandike. Kama ni mtihani anaweza kutumia mistari ya kwanza michache ya karatasi ya majibu. Katika nafasi hiyo aandike mambo muhimu yasiyopungua sita saba hivi, ya kutumia katika insha ya kurasa mbili.

    Baada ya kupata vidokezo vyake, mwandishi ajisitishe. Avichunguze vidokez kwa lengo la kukipa kila kimoja uzito mwafaka: kipi akipe uzito zaidi; kipi akipe uzito wa kadiri; kipi akieleze kidogo tu na kipi akitaje tu.

    Aidha, aamue ni vidokezo vipi vinavyofaa kuelezwa pamoja, yaani, katika aya moja na vipi vifuatane, na kadhalika. Uzito wa hoja utategemea umuhimu wa jambo lenyewe. Tena utategemea muda alio nao mwandishi na nafasi, yaani, urefu wa insha inayohitajika.

    Jambo muhimu lielezwe kikamilifu bali yasiyo muhimu sana yapunguziwe maelezo. Hata hivyo, mambo yote yanaweza kuwa muhimu. Katika hali kama hiyo ni sharti uzito utofautiane kwa sababu kadha wa kadha. Yale anayoyaelewa vyema kabisa ayape uzito zaidi ya ule atakaoupa yale asiyoyaelewa sana. Pia, muda na nafasi haviwezi kumruhusu mwandishi alieleze kila jambo kwa urefu ambao angetaka.

    Katika mfano ufuatao: mwandishi tayari amejiuliza: Swali hili linataka nini? Amefikiri na ameendelea kufanya hivyo. Ameandika vidokezo jinsi alivyovikumbuka (katika haraka yake ya kutaka kulijibu swali hilo katika dakika arobaini na tano hivi).

    Katika mtungo usiopungua maneno 400 eleza hatua zinazostahili kuchukuliwa kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula.

    -kutodharau vyakula fulani 8, - amani 4, - punguza tamaa ya pesa 2, - unyunyiziaji 3, - elimu 4, - siasa safi 5, - punguza ulafi 2, - kilimo bora 3, - badili tabia ya ulaji 7, - maghala ya kuhifadhia 7, - badili desturi 6, - kabili idadi ya watu1.

    Kutokana na vidokezo hivi insha ya urefu wa kurasa mbili hadi mbili na robo inaweza kuandikwa. Mwandishi amejiamulia mwongozo wa kufuata kujieleza. Amevipa vidokezo nambari za kumwongoza kutambua cha kuanza nacho, vya kuviweka pamoja na cha kumalizia insha.

    Kulingana na vidokezi hivi insha itakuwa na mambo kumi na mawili ila maelezo yatakuwa katika aya nane. Baadhi ya mambo yataelezwa katika aya moja kulingana na mwongozo ambao unatambuliwa kwa tarakimu zilizo mwishoni mwa kila kidokezi. Vidokezo vya mambo hayo vimeambatanishwa na tarakimu moja. Mifano nne (4) na mbili (2).

    1.4 Mpangilio

    Kutokana na vidokezo, mwandishi hupata fursa ya kukisia mpango ambao insha yake itachukua. Mpango hutegemea sana aina ya insha. Kwa mfano, insha za methali na za hotuba zinatofautiana na pia ni tofauti na zile za mazungumzo.

    Kwa jumla insha inatakiwa iwe na utangulizi, maelezo na hitimisho. Insha ya mpangilio mzuri huwa na utangulizi mfupi, kati ya mistari mitatu hivi kufikia sita. Hata hivyo, lililo la thamani si idadi ya mistari bali ni UFUPI wa utangulizi. Utangulizi uwe mfupi. Utoe maelezo kiasi tu. Umjulishe msomaji kiini cha habari lakini si kwa kutoa orodha ya mambo ambayo yanaelezwa katika insha yenyewe.

    Ni wajibu wa mwandishi kujizuia asimchoshe msomaji na kumtoa hamu ya kusoma kwa kumfahamisha kimbele mambo yaliyomo. Amwache asome na kujigundulia mwenyewe yaliyomo. Mfano wa utangulizi usiofaa ni kama huu ufuatao:

    Hatua zinazostahili kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula ni: kukabiliana na idadi ya watu, kupunguza ulafi na tamaa ya pesa, kunyunyizia mimea ya vyakula maji wakati wa kiangazi na kuanzisha kilimo bora ...

    Insha iliyopangwa vizuri huandikwa katika aya mbalimbali. Aya huanzwa kwa kuachwa nafasi ya kiasi cha nusu inchi hadi inchi moja kutoka mstari wa pambizo.

    Aya ziwe za urefu wa kadiri tu. Zisiwe ndefu kuzidi kiasi wala fupi sana. Baada ya utangulizi aya ya mwanzo wa maelezo kamili iwe ya jambo muhimu. Lipe jambo hilo uzito wa kwanza kwa kulieleza kwa urefu zaidi. Aya zinazoelekea mwisho ziwe zenye maelezo mafupi kuliko ya zile zilizotangulia lakini ziwe na maelezo kamili. Uyaeleze mambo yanayohusiana pamoja katika aya mojamoja. Kwa mfano, uzembe na uzohali uelezwe katika aya moja na wizi na unyang’anyi katika aya nyingine, na kadhalika.

    Aya za mambo ambayo umeyapa uzito mdogo ziwe fupi kuliko za mwanzoni. Mpangilio huu una maana ya kwamba insha zianze kwa mambo muhimu na ziishie katika maelezo ya yale ambayo si muhimu sana. Baada ya utangulizi mfupi, sura ya insha yaweza kuwa hivi:

    aya ya pili na ya tatu - mistari kumi kumi hivi,

    aya ya nne na ya tano - mistari chini ya kumi kila moja,

    aya ya sita na ya saba - mistari michache kila moja,

    aya ya mwisho iwe fupi zaidi.

    Mpango huu ukizingatiwa, hakutakuwepo na hali ya kuwa na aya ndefu sana zilizojaa utondoti zikifuatwa na fupi sana na kisha ndefu tena. Hali kama hiyo haimpendezi msomaji. Hebu ichunguze mifano mitatu ya mipango ifuatayo kwa minajili ya kuunda taswira ya sura ya insha kimpangilio.

    (I) UTANGULIZI: aya moja ya mistari kumi na miwili.

    MAENDELEZO: aya tano za mistari miwili, mitano, tisa,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1