Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu
Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu
Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu
Ebook60 pages35 minutes

Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu

Rating: 4.5 out of 5 stars

4.5/5

()

Read preview

About this ebook

Mwongozo huu umetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kuwafaa wanafunzi na walimu katika uchambuzi wa vipengele mbalimbali riwaya ya Chozi la Heri. Vipengele hivi ni pamoja na ploti, dhamira, maudhui, mbinu za lugha, wahusika na uhusika wao. Ni mwongozo ambao unarahisisha uelewaji wa masuala yanayoonekana changamano na tata kwa kutoan msuko ulio sahili. Mwongozo huu ni wa kipekee kwa maana una maswali kadha ya kumchokonoa mwanafunzi. Isitoshe, maswali haya yametolewa majibu yenye hoja za kuridhisha. Majibu haya yanalenga hasa matarajio ya watahini na mitindo mipya ya kutahini ambapo unapata mwanafunzi anahitajika kuandika hoja kumi na nne kujibu swali moja. Kuna aina mbalimbali za maswali. Kuna yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli ama usemi fulani kutoka kwenye riwaya. Kwa kifupi, huu ni mwongozo wa aina yake ambao haumwonjeshi tu msomaji asali bali unampa fursa ya kuchovya moja  kwa  moja  ndani ya buyu lenyewe.

LanguageKiswahili
Release dateMar 28, 2021
ISBN9781393487746
Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu
Author

SHADRACK KIRIMI

Shadrack Kirimi ni msomi, mwandishi na mtafiti wa Kiswahili. Ameandika makala na vitabu vya marudio kwa wanafunzi wa shule za upili vikiwa ni pamoja na Hadubini ya Lugha, Hadubini ya Fasihi, Uchambuzi wa Fasihi, Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu, na Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine: Maswali na Majibu. Pia, ana tajriba pana katika utahini na kufundisha katika shule za sekondari.

Read more from Shadrack Kirimi

Related to Mwongozo wa Chozi la Heri

Related ebooks

Reviews for Mwongozo wa Chozi la Heri

Rating: 4.5 out of 5 stars
4.5/5

4 ratings1 review

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

  • Rating: 5 out of 5 stars
    5/5
    It has all the content and answers .. Easy to understand

Book preview

Mwongozo wa Chozi la Heri - SHADRACK KIRIMI

Na

Shadrack Kirimi

UTANGULIZI

Mwongozo huu umetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kumwelekeza mwanafunzi katika uchambuzi wa vipengele mbalimbali vya fasihi katika riwaya ya Chozi la Heri. Vipengele hivi ni pamoja na ploti, dhamira, maudhui, mbinu za lugha, wahusika na uhusika wao. Uchambuzi huu umefanywa kwa namna inayooanisha dhamira ya mwandishi na hali halisi katika jamii. Isitoshe, mchakato mzima wa kuwasuka wahusika na kuyajenga maudhui umeweza kuelezwa kwa njia sahili inayomwezesha msomaji kuielewa zaidi kazi husika. Ni mwongozo ambao unarahisisha uelewaji wa masuala yanayoonekana changamano na tata kwa kutoan msuko ulio sahili. Mwongozo huu ni wa kipekee kwa maana una maswali kadha ya kumchokonoa mwanafunzi, Isitoshe, maswali haya yametolewa majibu yenye hoja za kuridhisha. Majibu haya yanalenga hasa matarajio ya watahini na mitindo mipya ya kutahini ambapo unapata mwanafunzi anahitajika kuandika hoja kumi na nne kujibu swali moja. Kuna aina mbalimbali za maswali. Kuna yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli ama usemi fulani kutoka kwenye riwaya. Kwa kifupi, huu ni mwongozo wa aina yake ambao haumwonjeshi tu msomaji asali bali unampa fursa ya kuchovya moja  kwa  moja  ndani ya buyu lenyewe.

1.0 Riwaya: Chozi la Heri (Assumpta K. Matei)

1.1 Msuko/Ploti

1.1.1 Sura ya Kwanza

Ridhaa anatazama jumba lake la kifahari linaloteketea. Ndani ya jumba hili ameteketea Terry mkewe, watoto wake wawili: Annatila (Tila) na  Mukeli pamoja na Lily Nyamvua (mkaza mwana) na Becky (mjukuu wake). Nyamvula ni mke wa Mwangeka (Kitinda mimba wa Ridhaa). Mwangeka hakuwepo wakati wa mkasa huu kwa maana alikuwa amesafiri kudumisha amani. Ridhaa anakumbuka mjadala aliokuwa nao na mkewe usiku wa kuamkia msiba. Anakumbuka akisikia mlipuko mkubwa uliomtia uziwi. Anazimia. Anaelekea shambani, mimea yake imeteketezwa pia. Anarudi katikakati ya chumba. Humu ndimo alimozaliwa Mwangeka. Ridhaa anakumbuka dayalojia yake na binti yake Tila kuhusiana na nchi ya Wahafidhina kutokua kidemokrasia licha ya kujipatia uhuru miaka hamsini iliyopita.

Ridhaa anakumbuka walivyojipata katika Msitu wa Heri. Walihamishiwa huku na babake Mzee Msubili kwani ardhi yake haingewatosha wanawake kumi na wawili na watoto kadha. Ridhaa alikuwa na umri wa miaka kumi. Anapoanza masomo anasutwa na watoto wenyeji kwa kuitwa Mfuata Mvua. Ridhaa anajitahidi masomoni na kuhitimu udaktari.

Uharibifu huu wote wa kuchomewa mali na familia ulikuwa umesababishwa na Mzee Kedi pamoja na majirani wake wa miongo mitano kwa kumuona kama mgeni baada ya Mwekevu kutawazwa kama kiongozi wa Wahafidhina. Majirani hawa wanamtenda Ridhaa licha ya ukarimu na mchango wake kwa sehemu hii.

1.1.2 Sura ya Pili

Sura hii inamulika ghasia zilizotukia baada ya uchaguzi na maisha ya wakimbizi katika Mlima wa Mamba. Kaizari ndiye msimulizi. Baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya wa kike, Mwekevu, ghasia zilishamiri kwa maana kulingana na baadhi ya Wahafidhina mwanamke hakufaa kuongoza. Vurumai hii inasababishwa na wafuasi wa mpinzani wa kiume wa Mwekevu. Mali iliteketezwa, nao biadamu wakapoteza uhai. Vijana waliokuwa wakiandamana nao wakaishia kupigwa risasi. Baadhi ya Wahafidhina, wakiwemo Kaizari, Ridhaa, Selume na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bwana Kute, Bwana Kangata na wengine wanakimbilia katika Msitu

Enjoying the preview?
Page 1 of 1