Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu
Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu
Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu
Ebook85 pages51 minutes

Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu

Rating: 3 out of 5 stars

3/5

()

Read preview

About this ebook

Mwongozo wa Kigogo ni kitabu ambacho kimetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi, mwalimu na msomi wa fasihi katika kuelewa na kuchambua kwa kina tamthlia ya Kigogo. Mwongozo huu una sehemu tatu kuu. Kwanza, ni sehemu inayoshughulikia mtitiriko wa matukio katika kila onyesho na tendo. Sehemu ya pili inazamia uchambuzi wa fani na maudhui nayo ile ya tatu ni sehemu ya kujitathmini. Sehemu hii ya tatu inajumuisha maswali kadha pamoja na majibu yake. Vipengelele vyote vikuu vya uchambuzi wa tamthlia vimeshughulikiwa kwa mapana. Vipengele hivi ni pamoja na: dhamira, maudhui mbalimbali, mbinu za kisanaa pamoja na tamathali za usemi, mandhari, sifa za wahusika na uhusika wao. Ili kumpa msomaji uhondo kamili, maswali kielelezo yametolewa. Haya ni maswali pamoja na majibu yanayolenga kutoa dira ya namna maswali yanavyofaa kujibiwa na uhakiki kutekelezwa. Kila jibu limetolewa hoja za kuridhisha kuambatana na mitindo mipya ya utahini pamoja na matarajio ya watahini. Ni maswali ya kumfikirisha msomaji na wakati huo huo kumpa nyenzo za kukabiliana na maswali mengine. Kuna maswali chungu nzima yakiwa ni pamoja na yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli na madai yaliyotolewa katika tamthlia. Ni mwongozo ambao umesukwa ukasukika; ukapikwa ukaiva.

LanguageKiswahili
Release dateMar 31, 2021
ISBN9781393401247
Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu
Author

SHADRACK KIRIMI

Shadrack Kirimi ni msomi, mwandishi na mtafiti wa Kiswahili. Ameandika makala na vitabu vya marudio kwa wanafunzi wa shule za upili vikiwa ni pamoja na Hadubini ya Lugha, Hadubini ya Fasihi, Uchambuzi wa Fasihi, Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu, na Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine: Maswali na Majibu. Pia, ana tajriba pana katika utahini na kufundisha katika shule za sekondari.

Read more from Shadrack Kirimi

Related to Mwongozo wa Kigogo

Related ebooks

Reviews for Mwongozo wa Kigogo

Rating: 3 out of 5 stars
3/5

2 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mwongozo wa Kigogo - SHADRACK KIRIMI

    Utangulizi

    Mwongozo wa Kigogo ni kitabu ambacho kimetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi, mwalimu na msomi wa fasihi katika kuelewa na kuchambua kwa kina tamthlia ya Kigogo. Mwongozo huu una sehemu tatu kuu. Kwanza, ni sehemu inayoshughulikia mtitiriko wa matukio katika kila onyesho na tendo. Sehemu ya pili inazamia uchambuzi wa fani na maudhui nayo ile ya tatu ni sehemu ya kujitathmini. Sehemu hii ya tatu inajumuisha maswali kadha pamoja na majibu yake. Vipengelele vyote vikuu vya uchambuzi wa tamthlia vimeshughulikiwa kwa mapana. Vipengele hivi ni pamoja na: dhamira, maudhui mbalimbali, mbinu za kisanaa pamoja na tamathali za usemi, mandhari, sifa za wahusika na uhusika wao. Ili kumpa msomaji uhondo kamili, maswali kielelezo yametolewa. Haya ni maswali pamoja na majibu yanayolenga kutoa dira ya namna maswali yanavyofaa kujibiwa na uhakiki kutekelezwa. Kila jibu limetolewa hoja za kuridhisha kuambatana na mitindo mipya ya utahini pamoja na matarajio ya watahini. Ni maswali ya kumfikirisha msomaji na wakati huo huo kumpa nyenzo za kukabiliana na maswali mengine. Kuna maswali chungu nzima yakiwa ni pamoja na yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli na madai yaliyotolewa katika tamthlia. Ni mwongozo ambao umesukwa ukasukika; ukapikwa ukaiva.

    Yaliyomo

    Utangulizi................................................................................................................................. uk 1

    Yaliyomo.................................................................................................................................. uk 2

    Msuko...................................................................................................................................uk 3-10

    Fasili ya anwani Kigogo....................................................................................................uk 10-11

    Dhamira.............................................................................................................................uk 11-12

    Maudhui.............................................................................................................................uk 12-17

    Wahusika na uhusika......................................................................................................uk 17-25

    Mbinu za kisanaa.............................................................................................................uk 25-31

    Tamathali za usemi............................................................................................................uk 31-35

    Maswali na majibu............................................................................................................ uk 36-41

    Maswali ya ziada....................................................................................................................uk 41

    Marejeleo...............................................................................................................................uk 42

    Onyesho la Kwanza

    Tendo la kwanza

    Tendo hili linatokea katika karakana ya kina Sudi, Kombe na Boza ambao wanaendelea na kazi yao ya uchongaji. Karakana hii imo katika soko la Chapakazi. Mazingira ya soko yamechafuliwa kama inavyodhihirishwa na maji machafu machafu yanayopita mitaroni. Taka na kemekali zinatupwa humo jambo ambalo linachangia uzukaji wa maradhi hatari. Ashua, mke wa Sudi anawaletea chai na mahamri wachongaji hawa. Anaeleza jinsi wanavyoangaishwa na wenye nguvu kwa kutozwa kodi zaidi ilhali kodi hiyo haitumiki kuboresha mazingira ya soko.

    Tangazo la Majoka kuhusiana na kuadhimisha miaka sitini ya uhuru linapeperushwa kupitia redio. Sherehe hizi zingefanyika kwa muda wa mwezi mzima halafu kilele cha sherehe hii kingesadifiana na hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Majoka. Muda uliotengewa sherehe hii unaibua mjadala mkali baina ya Sudi na Boza.

    Katika sehemu hii, Soko la Chapakazi linaibuka kuwa mandhari makuu ambamo matendo ya tamthilia yangetekelezewa. Bidii za Sudi, Kombe na Boza zinadhihika. Aidha kuna uchafuzi wa mazingira, unyanyasaji kutokana na utozwaji kodi, udiketa wa Majoka wa kufanya maamuzi bila kushauri watawaliwa na sababu za kuzuka mapambano kudhihirishwa.

    Tendo la pili

    Mshauri mkuu wa Majoka, Kenga anawasili kwenye karakana. Lengo lake ni kumrai Sudi kumchongea Majoka sanamu ya hayati babake, Marara bin Ngao. Sudi anaukataa mradi huu. Kenga anaudharau mchongo wa Boza ambaye anadai kuwa alikuwa akichonga sananu ya Marara bin Ngao. Kenga anavutiwa na mchongo wa kike wa Sudi. Sudi anawaarifu kuwa ni mchongo wa shujaa halisi wa Sagamoyo. Kauli hii inamshtua Kenga kwani haonekani kufahamu shujaa yeyote wa kike Sagamoyo. Ubarakala wa Boza unajidhihirisha nao mtazamo tofauti wa Sudi kuhusu utawala wa Majoka unabainika; haupendi. Kenga analaumu Tunu kwa kumlisha Sudi kiapo aukatae mpango wa Majoka. Kenga anajaribu kutumia vishawishi zaidi ili kujaribu kumvutia Sudi. Kenga anamwarifu kwamba akikubali mradi huo, Majoka angemzawadi na maisha yake pamoja na familia yake kubadilika. Sudi anatofautiana na wazo hili la ufadhili wa mradi kutoka nje. Kwa sudi mikopo hii ni mzigo mkubwa kwa vizazi vijavyo. Kenga anamwamrisha Chopi kuwaletea Keki wachongaji hawa. Boza anaichangamkia. Sudi anaikataa kwa madai kuwa kuwa haya ni makombo tu. Kenga anakasirika na kuondoka. Mgogoro unaivuka baina ya Sudi na machongaji wenzake. Sudi anajaribu kuwazindua kuhusiana na uovu wa Majoka. Kombe anaonekana kupata mwanga kidogo. Tunu na Ashua wanawasili wakihema na kuwaarifu kwamba Kenga alikuwa akipanga njama fulani alikokuwa akihutubia wahuni. Wanaamua kuelekea huko.

    Tendo la tatu

    Tendo hili linafanyika barazani mwa nyumba ya Sudi. Ni siku mbili baada ya kufungwa kwa soko la Chapakazi. Sudi, Boza na Kombe wameamua kuendelea na kazi yao ya uchongaji nyumbani kwa Sudi. Tunu na Siti wanawasili upesi. Wanaarifu kuhusiana na maadamano na athari zake. Wafanyakazi katika kiwanda cha Majoka walikuwa wameandamana na kuungwa mkono na wachuuzi waliokuwa wameenda kuona kama soko limefunguliwa. Vijana watano pamoja na wachuuzi sokoni walikuwa wameuawa. Mojawpo ya sababu za maandamano hayo ni kupanda kwa bei ya chakula mara dufu katika kioski

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1