Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kioo Chenye Kiwi
Kioo Chenye Kiwi
Kioo Chenye Kiwi
Ebook42 pages24 minutes

Kioo Chenye Kiwi

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Utandawazi umeipanua mipaka ya kidini na ile ya sekta ya habari na mawasiliano.Washindani katika nyanja mbili hizi wako mbioni kiuchumi na kijamii kila mmoja akitaka kuwa msaliaji,ima fa ima. Mapera Kipanga anatumia kila senti kushiriki shindano la 'Peperuka na Ndege Dola' linalotangazwa kwenye Idhaa ya Sauti Yetu,stesheni ya redio afanyapo kazi Njozi,mwanawe.Shindano lamwehuza Kipanga huku Njozi akiujua ujanja ulioko kwenye shindano hilo.Ukabila, ujomba, unyanyasaji kingono na kasumba potovu ya bahatinasibu ni maovu yanayomkatisha Njozi subira kazini.Anaamua kuoa machweoni ila Kipepeo, mkewe mtarajiwa, ashapachikwa ujauzito na Kasisi Mtakakitu.Je, kioo hiki - dini na sekta ya habari na mawasiliano - kitaeuliwa na nani?

LanguageKiswahili
PublisherWadi Kyhia
Release dateDec 29, 2020
ISBN9781005321833
Kioo Chenye Kiwi
Author

Wadi Kyhia

A trained journalist and author.I love good books.

Read more from Wadi Kyhia

Related to Kioo Chenye Kiwi

Related ebooks

Reviews for Kioo Chenye Kiwi

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kioo Chenye Kiwi - Wadi Kyhia

    Kioo Chenye Kiwi

    Wadi Kyhia

    Copyright 2019, Wadi Kyhia

    Smashwords Edition

    No part of this work may be reproduced or transmitted in any form or by any means, electronic or mechanical, including photocopying and recording, or by any information storage or retrieval system without the prior written permission of the author.

    Tamthilia hii ni masimulizi ya kubuni. Majina, hulka, biashara, mashirika, mahali, matukio na visa ni mazao ya jazanda ya mwandishi au yametumika kwa kubuni. Ufanano wowote kuwaelekea watu halisi, wanaoishi au waliofariki, matukio au mahali ni tukizi tu.

    Kimeandikwa na kuhaririwa

    Katika Kiwara cha Utunzi

    Chapisho la Fanya Mwenyewe

    (F. M Publications)

    mailto:wadikyhia@gmail.com

    This ebook is licensed for your personal enjoyment only. This ebook may not be re-sold or given away to other people. If you would like to share this book with another person, please purchase an additional copy for each recipient. If you’re reading this book and did not purchase it, or it was not purchased for your use only, then please return to your favorite ebook retailer and purchase your own copy. Thank you for respecting the hardwork of this author.

    TABARUKU

    Mke wangu mpendwa Maria; wanetu Joy na Maggie.Msaada wenu ni wa kipekee.

    SHUKRANI

    Ee, Mungu nisemeje? Nakiinua kikombe cha shukrani kwa wema wako.

    WALIOMO

    Kipanga

    Njozi (Bw.Harusi)

    Kipepeo (Bi. Harusi)

    Kundi la wanawake waimbaji

    Mama Kipepeo

    Rita

    Kasisi Kufuru Mtakakitu

    Kundi la waumini

    Wanahabari wenye kamera

    Onyesho la kwanza

    [Alfajiri na makungu yake.Siku ni Jumamosi.Kijiji cha Bahatinasibu.Wanawake wanakijiji wako kwenye michakamichaka ya lele za nyimbo za harusi.Wanasikika wakiimba kwa mahadhi na furaha ugani pa mastakimu ya Kipanga Mapera mwenye umri wa miaka 75 na Njozi Mchana, mwanawe, mwenye umri wa miaka 45.Ni siku ya Njozi kufunga pingu za maisha]

    KIPANGA: (Anazinduka kutoka usingizini na kuuzibua msutu. Ajinyosha na kutazama kwenye paa la nyumba. Anayaona masalio ya nyota za alfajiri) Uuuu!...aaaah!Weee!Njozi!Bado walivuta blanketi ilhali... Umesahau? (Anakitingiza kibahaluli kuhakiki uwepo wa mafuta taa, kisha

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1