Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Simu Ya Kuzimuni
Simu Ya Kuzimuni
Simu Ya Kuzimuni
Ebook46 pages29 minutes

Simu Ya Kuzimuni

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Mengi yamasemwa na nyingi zikatolewa ahadi kwa vijana kuhusiana na mustakabali wao. Vijana wakasoma na kuhitimu, 'Someni vijana mtapata kazi nzuri sana!' Wakapiga kura kuwachagua viongozi watakaozitimiza ndoto zao, ila 'zao' zikawa ndoto zao viongozi! Wazazi, walimu na waelekezi wa vijana wayajua waingoja siku watakapoona kutimia kwa mazao ya bidii ya kuwaelimisha vijana wasomi. Nani atakayewanasua vijana kutokana na vyeti visivyozaa kazi kwenye utandu wa ufisadi, ujomba, uraibu wa mihadarati, ukabila, usorajua na maovu mengineyo?Viongozi? Labda jumuiya nyingine ya viongozi wenye azma na ari ya kuijali kesho ya vijana.

LanguageKiswahili
PublisherWadi Kyhia
Release dateDec 14, 2020
ISBN9781005946890
Simu Ya Kuzimuni
Author

Wadi Kyhia

A trained journalist and author.I love good books.

Read more from Wadi Kyhia

Related to Simu Ya Kuzimuni

Related ebooks

Reviews for Simu Ya Kuzimuni

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Simu Ya Kuzimuni - Wadi Kyhia

    Simu Ya Kuzimuni

    Wadi Kyhia

    Copyright 2020, Wadi Kyhia

    Smashwords Edition

    No part of this work may be reproduced or transmitted in any form or by any means, electronic or mechanical, including photocopying and recording, or by any information storage or retrieval system without the prior written permission of the author.

    Tamthilia hii ni masimulizi ya kubuni. Majina, hulka, biashara, mashirika, mahali, matukio na visa ni mazao ya jazanda ya mwandishi au yametumika kwa kubuni. Ufanano wowote kuwaelekea watu halisi, wanaoishi au waliofariki, matukio au mahali ni tukizi tu.

    Kimeandikwa na kuhaririwa

    Katika Kiwara cha Utunzi

    Chapisho la Fanya Mwenyewe

    (F. M Publications)

    mailto:wadikyhia@gmail.com

    This ebook is licensed for your personal enjoyment only. This ebook may not be re-sold or given away to other people. If you would like to share this book with another person, please purchase an additional copy for each recipient. If you’re reading this book and did not purchase it, or it was not purchased for your use only, then please return to your favorite ebook retailer and purchase your own copy. Thank you for respecting the hardwork of this author.

    TABARUKU

    Mpendwa ninangu,

    Ukarimu wa maskini hupotelea moyoni mithili ya umande jua liwakapo.Tutampaa samaki siku moja, hata kama atakuwa kambare na uvundo wake.

    SHUKRANI

    Ningependa kuzitoa shukrani zangu za dhati kwa Mola, mpaji wa vipaji, msanii mkuu wa vionekanavyo na visivyoonekana.

    Pili, nawashukuru wahadhiri wangu katika Taasisi ya Mafunzo ya Mawasiliano nchini Kenya (KIMC) -Mlinipa mtego wenye chambo nijinasie samaki.Inshallah! Sitoula wali mkavu.

    WAHUSIKA

    Mwalimu Panda

    Waridi

    Mtama

    Limau

    Mtindi

    Mumunye

    Hindi

    Mnazi

    ONYESHO LA KWANZA

    (Chumbani mwa mabati makuukuu katika mtaa wa mabanda wa Usorajua. Chumba hiki kilichogawanywa kwa msutu, kina uhaba wa vyombo; ila tu mikeka ya kulalia, vyombo vya kupikia na simu juu ya mkweche wa meza.Ni saa moja usiku.Kibahaluli kinawaka kwa uzembe.Waliokuwa kwa wakati mmoja wanafunzi wa Mwalimu Panda Zikua wanakutana kwenye makazi ya mmoja wao, Mashuke Mtama, kama ilivyo desturi yao. Hii ni baada ya siku kutwa ya kugaagaa huku na kule ili kutafuta riziki ya siku yenyewe ila pasi bahati.Gumzo lao linageuka na kuwa msutano)

    TUMBA WARIDI: (Akiutoa ukoko wa usiku uliopita kwenye sufuria ndogo ya kusongea ugali. Ni zamu yake kukiandaa kilalio – ugali wa unga wa mtama kwa kisamvu) Mtama?!

    MASHUKE MTAMA: (Kwa beuo) Naam Daktari Waridi!

    WARIDI: Po! Nemsi za nini! Nakuulizaje, yaani ina

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1