Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mauzauza Ya Raha: Kuchagua Upendo Badala Ya Hofu
Mauzauza Ya Raha: Kuchagua Upendo Badala Ya Hofu
Mauzauza Ya Raha: Kuchagua Upendo Badala Ya Hofu
Ebook172 pages1 hour

Mauzauza Ya Raha: Kuchagua Upendo Badala Ya Hofu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

”Atazamaye nje huota ndoto. Atazamaye ndani, Huamka”-Carl Jung
Mauzauza Ya Raha; Kuchagua Upendo badala ya Hofu ni kitabu cha 4 katika ”Tetralojia ya Kuamka”. Kitabu hiki kinafunua njia nyingi za uwongo kupitia maisha ambazo tunaweza kuchukua na jinsi tunaweza kupata amani ya kweli ya ndani na kusudi maishani mwetu.
Wakati uhusiano wetu na ulimwengu unaotuzunguka unapoundwa kupitia lenzi zinazotawala za hofu, Safari yetu ya Maisha mara nyingi inaweza kuwa ya upweke na udhalimu. Shida zetu hazikomi, mizigo yetu ni nzito, mara nyingi hutuongoza kujijengea vizuizi vya ndani, vya kutulinda kutokana na kiwewe cha kihemko. Bado vizuizi vile vile vinatumika kututenga na kila kitu kinachotuzunguka, pamoja na uhalisia wetu.
Mauzauza Ya Raha ni kitabu cha kiroho kinachofunua jinsi ya kukumbatia upendo badala ya hofu, Acha kutafuta maana na furaha ya ndani kupitia shughuli za nje na mahusiano katika ulimwengu; badala yake, kutafuta kutoka ndani.
LanguageKiswahili
PublisherTektime
Release dateAug 17, 2022
ISBN9788835442240
Mauzauza Ya Raha: Kuchagua Upendo Badala Ya Hofu

Related to Mauzauza Ya Raha

Related ebooks

Reviews for Mauzauza Ya Raha

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mauzauza Ya Raha - Ken Luball

    Mauzauza Ya Raha :

    ––––––––

    KUCHAGUA UPENDO BADALA HOFU

    ––––––––

    Riwaya ya Kiroho na Ken Luball

    & Bodhi ( Mwongozo wa  Kiroho )

    Translator: Samwel Lubisia

    Copyright Claimant: Ken Luball

    Ujumbe wa mwandishi:

    Nini Maana ya  Uzima?

    Maana ya uzima,

    Sababu tupo hai,

    Ni kuisikiliza kwa makini Roho  aliye ndani yetu ,

    Na kuifuata katika njia atakayotuongoza.

    Vipo vitabu vinne  katika Tetralojia ya Kuamka :

    Leo Naenda Kufa: Uchaguzi Maishani

    Mwongozo wa  Roho: Safari Maishani

    Utulivu: Kijiji Cha Matumaini

    Mauzauza ya Raha: Kuchagua Upendo badala ya Hofu

    Maisha ya kiroho  hali ya ni kuamini  yuko Mungu (Roho au Nafsi) katika kila maisha,  na kwa sababu hii maisha ya kila mmoja ni muhimu , ni sawa na  yameunganishwa.

    Lengo langu la  kukiandika kitabu hiki  ni Kuwaamsha  na kuwasaidia wengine, Walioamka, huelewa kikamilifu maana  ya  Kuiona Nuru, na kwa hivyo,  Safari yao katika Maisha yaweza kutambulika kikamilifu.

    Hadithi tatu zimeandikwa katika nafsi ya  kwanza, kufuatilia  safari ya Kiroho Maishani mwa mtoto. Wanapopata  mafunzo ya jinsi ya  kuyajibu maswali  hayo [niliyouliza mwanzo] kwa njia ya  kueleweka, kuvutia, na ya kipekee, ambayo  sio tu ya kufikirisha bali pia  kusisimua.

    Bodhi ni Mwongozo wangu wa Kiroho ; ananizungumzia kwa urahisi huku nikiandika mawazo yake. Japo safari yangu ya   Kuiona Nuru, haijakamilika, Bodhi, akiwa Mwongozo wa Roho, Bila Shaka  Amelimika. Tulikiandika kitabu hiki kwa ajili ya  wote wanaotaka kuianza safari ya Kuamka  au Wameamka na wanatafuta njia ya  Kuiona Nuru

    Ni kwa upendo tu na msaada wa Bodhi

    tuliweza kuviandika vitabu hivi kwa pamoja

    Ili kufahamu  mengi kuhusu vitabu vyote vinne vya Kiroho katika tovuti yangu http://kenluball.com

    Yaliyomo

    Dibaji:   Kwa  watoto wa ulimwengu

    Chapter 1:  Kutafuta Mwanga Wako

    Chapter 2:  Utangulizi wa Uhusiano Akili, Mwili  na  Roho

    Chapter 3:  Ukuta, Barakoa na Mlango

    Chapter 4:  Uhusiano wa Akili, Mwili na Roho

    Chapter 5:  Roho Anayapa maisha yetu Maana

    Chapter 6:  Roho na Kiona Nuru

    Chapter 7:  Kuishi katika Nuru

    Chapter 8:  Kuchagua Upendo badala ya Hofu

    Chapter 9:  Kuishi na Roho

    Chapter 1:  Mauzauza  ya Raha

    Chapter 11:  Maana ya  maisha

    Hitimisho

    Nyongeza Tafakari za Kiroho

    Kuruhusu Ken

    Kwa ajili ya  Watoto wa Dunia

    Tunakitoa kitabu hiki kwa ajili ya Watoto wa Dunia. Ni matumaini yetu kwamba wazazi wako, na wote unaowapenda, watakisoma kitabu  hiki  na kwa kufanya hivyo, wataweza  kukusaidia Kuchagua  njia yako maishani kwa busara. Ni matumaini yetu kwamba  safari yako  itajazwa na upendo, furaha na ya kukushangaza.

    Dibaji:

    Kwa Ajili ya Watoto wa ulimwengu

    Unavyoendelea kuwa mkubwa,

    Utagundua maisha yana changamoto

    Ulimwengu sio mahali pazuri  sana kuishi  siku zote

    Utaona mambo mengi  na kushangaa

    Ni kwa nini mabaya  huwafanyikia wengi

    Utawaona  wasio na chakula cha kutosha

    Au mahali pa kuishi, na wengine

    Wasiopenda  mtu kwa sababu yuko tofauti.

    Tofauti na picha  ya hapo juu, bila kujali rangi yako ya ngozi ni gani,

    Nchi unayoishi, jina lako, dini,

    Au tofauti zozote zilizopo,

    Ni muhimu  kutoamini  yeyote  ni bora  zaidi

    Au wa maana  zaidi kumliko mwingine.

    Kila maisha  ni ya maana [kwa kiwango  sawa]

    Bila ya kujali  tofauti  zozote zilizopo kati yetu

    Kuishi maisha Mazuri  haihusiani lolote na kazi uliyonayo,

    Wala pesa unazopata,

    Kuwa mashuhuri au lingine  lolote unaloweza kusikia

    Unapokua mkubwa.

    Ila  la muhimu  ni kwamba wewe  ni mtu  mzuri.

    Kuwa mtu anayejali hisia za wengine

    Kuwasaidia  unapoweza,

    Kuwatendea wote  kwa wema na upendo,

    Hata kama wao hawakutendei hivyo.

    Utawapata wengi ulimwenguni  wasio  na furaha,

    Wanajijali wenyewe tu.

    Tafadhali usiwe kama wao

    Unaweza kuubadili ulimwengu kama tu utaisikiliza

    Sauti nyamavu moyoni mwako na

    Kushiriki ujumbe huo na wote.

    Kumbatia maishani  kwa heshima  na unyenyekevu.

    Kua mkarimu kwa kila  mtu

    Shirikisha  uzuri  ulio moyoni mwako  na wote  waliotofauti au

    Wanapambana

    Na muhimu  zaidi, watendee wengine

    Jinsi ungependa  utendewe

    Ukifanya hivi, utakua mwenye furaha.

    Usichague kuishi ulimwengu ambao kila mtu ana hofu,

    Kujihofia wenyewe tu.

    Ila wajali wengine, kuwa mkarimu, mwenye  huruma,  upendo,  heshima, mnyenyekevu, mwenye  subira, mwema, mwenye  shukurani na matumaini maishani.

    Kuwa mjasiri; jali hisia za wengine,

    Kuwa mtu mwenye  urafiki na uwasaidie  wakiwa tofauti au wakiwa wahitaji

    Ukifanya hivi, unaweza  kutapata maisha yako yakawa  yenye furaha na maana.

    Njia  unayoichagua maishani  itaamua

    Mustakabali  wa  Dunia.

    Kizazi cha  zamani  hakijafanya kazi nzuri sana

    Kuilinda  sayari yetu na [kuwalinda] wenzao

    Ni juu yako, kufanya mabadiliko

    Ambayo  lazima  yafanywe

    Kwa  kuchagua njia iliyo sawa  maishani .

    "Maono yako yatakuwa wazi tu

    Utakapotazama ndani ya moyo wako

    Atazamaye nje, huota ndoto.

    Atazamaye ndani, huamka"

    Carl Jung

    Sura Ya 1:

    Kupata  Mwanga Wako

    Majibu tunayoyatafuta, ili kupata mwanga wako ,

    Unaotuwezesha kukumbatia amani ya ndani,

    Upendo  na maana  maishani  mwetu,

    Huenda yasiwahi patikana kwa kutazama nje.

    Ila kwa kujitazama ndani alipo Roho,

    Kukubali na Kuruhusu Roho  kuongoza safari

    Yako maishani, hata hivyo zipo changamoto.

    Hii ni kwa sababu ya kutawaliwa na hali ya [1]Ego.

    Ego ambayo tumefunzwa na kuamini tangia kuzaliwa kwetu.

    Kuamka huanza pindi tunapoanza kudadisi kuhusu kila ambacho tulijifunza.

    Nuru huja baada ya kukubali ukweli kwamba

    Yote tuliyojifunza hayakuwa sawa.

    Safari hii ni ndefu, ngumu na mara nyingi yenye upweke.

    Maana ya uzima ni kufunga safari hii,

    kujitolea kushiriki bila ubinafsi

    Kushiriki pamoja na wengine mwanga ulio ndani yetu.

    "Ni kwa nini tuko hai? Je Nini maana ya kua hai na uzima"? Maswali haya yameulizwa kwa miaka elfu moja, yaweza kushangaza jinsi majibu yake ni rahisi. Tunapozaliwa, majibu yake tayari yalikuwa ndani yetu. Kwa hakika, pindi tu tunapozaliwa majibu ya hayo maswali yanatokomea katika changamoto ambazo sote hupitia maishani.

    "Miaka mitano ya kwanza katika Maisha ya kila mtoto ni ya maana sana". Katika muda huu

    [mtoto] hujifunza ambayo yanatarajiwa  kutoka kwao na jinsi atakavyo chukulia hali tofauti ulimwenguni.

    Wakati huu pia wanaendeleza mtazamo wa kijumla  jinsi vile watawachukulia wenzao. Maoni yao, dhana, Imani, Pamoja na matarajio hujengwa wakati huu na kujenga msingi jinsi watakavyo watendea na kuwachukulia wengine maishani mwao.

    Katika miaka hii, ikiwa mtoto atafunzwa kuutazama ulimwengu na watu wengine kwa njia mche wa giza na uhasi, pale ambapo "Hofu hutawala Upendo ", basi watakumbana na changamoto si haba. Kwa kuutazama ulimwengu kwa jinsi hii, wanajifunza ubinafsi na kutowajali wengine. Safari yao maishani huwa yenye upweke na masumbuko pamoja na mapambano.

    Kwa upande mwingine hata hivyo, ikiwa watakumbatia na kutawaliwa na "Upendo Wala si  Hofu , basi Maisha yao huchukua mwelekeo tofauti. Kwa kukumbatia msingi wa upendo na maana yake, wanaanza kuyaelewa Maisha katika njia tofauti, njia isiyo ya ubinafsi bali  ya kuwaonea huruma watu wote".  Watoto hawa huwaelewa na kuwaheshimu wengine na pia kujenga mtazamo wa Maisha wa upendo bali sio wa hofu na chuki.

    "Anayojifunza mtoto katika miaka yake mitano ya kwanza, yaweza kuadhiri Maisha yake yote"

    Masumbuko mengi tulio nayo maishani huja kama athari za Imani tulizo jenga katika miaka hii ya utotoni. Miaka tunayo shawishika kirahisi tukiwa Watoto. Tunajifunza kuhusu mahusiano yetu na ulimwengu kisha tunaanza kujaribu kuyaondoa madhara haya Maisha yetu yote. Madhara haya husababishwa na kuzikubali jumbe za uongo na ubinafsi kama jumbe za kweli na halisi, tunapoendelea kukubali majukumu yetu ulimwenguni. Anapofika umri wa kuanza shule [mtoto], mara nyingi jumbe hizi huwa zimehifadhiwa ndani yake na huchangia katika kushawishi mawazo na matendo yake [mtoto] katika Salio la Maisha yake.

    Ningependa tuangazie mfano wa mkoba ulio funguka. Kabla hatujazaliwa mkoba huu hauna chochote. Pindi tu tunapozaliwa, Ego na kila tunayoamini kuwa kweli, yanaanza kuujaza mkoba huu. Katika kutangamana kwetu, mkoba unaendelea kua mzito tunavyo endelea kuujaza na mizigo yetu kutokana na  tunayojifunza maishani mwetu. Kadri mkoba huu unavyoendelea kua mzito, ndivyo pia Mwanga wetu unazidi Kufifia, na hivyo kuna haja ya kupunguza na kuondoa mizigo tunapoanza Kuamka na kuianza safari yetu kuelekea kwenye  Nuru.

    Katika mkoba huu umejaa ubinafsi usio wa  kweli  tuliojifunza kua kweli wakati tulipokua watoto. Ingawa mkoba huu wahitaji mda kidogo tu kujazwa, yaweza kuchukua maisha yao yote "kutafuta mwanga wao" tena, kuiondoa  mizigo na kuirejelea hali ya awali  ya  utulivu  wa ndani, na ufahamu  ambao mwanzoni waliujua kabla mkoba haujaanza  kujaa; kabla Nafsi ya mtoto kujifunza mengi  yasiyo  kweli na kukubalika  kama  kweli. Kadri wanavyoubeba mkoba mzito, ndivyo pia safari  yao maishani inakuwa ngumu na pia inakua vigumu  zaidi kutafuta mwanga wao  mara tena.

    Mikoba yetu mingi hujazwa utotoni katika miaka ya kwanza mitano. Kisha tunajaribu maishani mwetu kuiondoa mizigo hii.

    Tunapotafuta mwanga wetu na kuanza kudadisi ukweli wa yote tuliyofunzwa katika miaka hii, Basi tunaanza Kuamka na kuanza kazi ngumu ya kuondoa mizigo katika mikoba yetu.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1