Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu
Ebook57 pages41 minutes

Roho Mtakatifu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

 

Kwa mtu anayesoma ujumbe huu, wewe ni muhimu sana kwa Mungu na ulimwengu mzima. Je, inaonekana kana kwamba chochote unachofanya maishani, huwezi kupata matokeo unayotaka? Je, unatafuta majibu katika sehemu mbalimbali za maisha yako? Inaweza kuwa ya kiroho, kihisia, kisaikolojia, kijamii, kiuchumi, kitaaluma au afya.

 

Unaposoma kitabu hiki, amini kwamba utatambua suluhu la kudumu kwa(za) changamoto zako kwa usaidizi wa nguvu kuu zaidi, nguvu za Roho Mtakatifu. Kitabu hiki kitakuwezesha kupata furaha, amani, na uwezo wa kushawishi na kubadilisha mapenzi yako, kukidhi hitaji lako kuu na kuanza kuishi maisha yenye mafanikio.

 

Unaposoma kitabu hiki, Roho Mtakatifu na awe halisi kwako kama ambavyo amekuwa kwangu kwa miaka mingi hadi sasa. Kuanzia sasa, tembea katika ushirika wa ndani zaidi na Roho Mtakatifu. Shalom.

LanguageKiswahili
PublisherNinah Shali
Release dateFeb 5, 2024
ISBN9798224807512
Roho Mtakatifu

Related to Roho Mtakatifu

Related ebooks

Reviews for Roho Mtakatifu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Roho Mtakatifu - Ninah Shali

    JEDWALI YA YALIYOMO  UKURASA

    VICHWA 

    KUWAPA 

    SHUKRANI 

    DIBAJI 

    UTANGULIZI 

    SURA YA KWANZA 

    Roho Mtakatifu ni nani?

    Nyakati  tatu

    SURA YA PILI 

    Kwa nini Roho Mtakatifu?

    SURA YA TATU 

    Jinsi ya kujazwa na nguvu ya Roho Mtakatifu.

    Jinsi ya kutembea na Roho Mtakatifu

    SURA YA NNE 

    Hitimisho.

    Vidokezo Vya maombi

    KUWAPA

    Kitabu hiki kimetolewa kwa Roho Mtakatifu na kwa kila mtu aliye na kiu ya Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wake na Roho wa Mungu kama msaidizi. Utukufu na heshima yote kwa Mungu Baba.

    Aya za Biblia zimechukuliwa kutoka New King James Version {NKJV} Isipokuwa imeonyeshwa vingine.

    Tolea la kwanza Hakimiliki © 2020 na Ninah Shali.

    Roho Mtakatifu.

    Kitabu hiki hakiwezi kutolewa tena kamili au sehemu kwa njia nyingine yoyote bila idhini ya kuandikwa kutoka kwa mwandishi.Haki zote zimehifadhiwa chini ya sheria ya hakimiliki ya kimataifa.Kwa habari zaidi tafadhali wasiliana na:

    Ninah Shali kwa facebook

    SHUKRANI

    Kwanza  kabisa, ningependa  kutoa  shukrani  zangu  za  dhati  kwa  mwenyezi Mungu ambaye ameniruhusu kuinjilisha juu ya Roho wake kupitia maandishi haya.

    Pili, nawashukuru wazazi wangu wazuri sana, Bwana na Bibi Agripina Majala na familia yangu yote kwa kuwa nami nyakati na misimu yote.Halafu, nawashukuru washauri wangu wote wa kiroho.  Sina uwezo wa kuongeza au kupunguza neno ni Mungu tu anayeweza kuwazawadia.Nawashukuru washirika wangu wote katika mwili wa Kristo na kwa watumishi wa Mungu ambao wanainjilisha injili ya kweli ya Yesu Kristo kupitia jumbe zao za  maandishi  au  za  sauti  ambazo  zinanihimiza  kiroho  kila  ninapozisoma  au kuzisikiliza.

    Shukrani  zangu  za  mwisho  ziende  kwa  kampuni  ya  uchapishaji  na  kila atakayesoma kitabu hiki.

    Mungi awabariki nyote.

    DIBAJI

    Tangu utotoni mwangu nilijua (kupitia ndoto, maono, ufunuo) kwamba nina wito wa  kumtumikia  Mungu  lakini  sikujua  kwa  jinsi  gani.  Wakati  fulani  maishani mwangu nilijiunga na kusanyiko fulani la kidini {Nyumba ya Watawa} nikitamani kuwa  mtawa  katika  kutafuta  wito  wangu. Walakini  hata  huko  sikuupata  na ikanilazimu kujiondoa. Mnamo Julai, 2009 nilipata maono ambapo nilielekezwa na kuamriwa  kuhudhuria  ibada  ya  Kanisa  la  ukombozi  wa  mlima  Sayuni  huko Mombasa Kenya. Siku ya kwanza katika ibada ya kanisa hilo, na kwa muda wote wa ibada siku hiyo, Roho Mtakatifu alinihudumia {machozi yalinitiririka mashavuni mwangu} na kunihukumu kumkubali Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wangu. Papo hapo, amini usiamini, nikakutana na Roho wa Mungu.  Sitasahau kamwe jinsi macho  na  masikio  yangu  ya  kiroho  yalivyofunguliwa  na  kuangazwa  kwa mwangaza  mkubwa  sana  ambao  uliweka  bayana  jukumu  langu  la  mbinguni: kuinjilisha injili ya kweli ya Yesu Kristo kwa wanadamu wote ili kuokoa roho kutoka  vifungo  na  kutoka  kuzimu.  Kuanzia  mudo  huo, nilianza  kuhudhuria mafundisho ya Biblia,  kuisoma  kwa kina, na kutafakari juu  ya  neno  la Mungu. Nimehudhuria mikutano tofauti ya injili, huduma na ufufuo sio tu kama mshiriki lakini pia kama mtumishi katika mwili wa Kristo. Nimekuwa kwenye mafunzo ya Mungu miaka yote hii. Mwishowe, nimeandika yale ambayo Bwana wangu Yesu Kristo aliniuliza kwa madhumuni ya kushiriki yote ambayo ameweka ndani yangu, kama shoka lake la kiinjili, kueneza injili ya kweli ya Mungu kwa mataifa yote kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, unaposoma kitabu hiki, ni ombi langu upate suluhisho za kudumu katika changamoto zako, upate furaha, amani, mwangaza wa kiroho, pia upate  maarifa,  hekima na ufahamu wa nguvu  za  Roho  Mtakatifu ili kuendeleza ufalme wa Mungu (urithi uzima wa milele), ushawishi na ubadilishe mapenzi yako ili uanze kuishi maisha mazuri.  Roho Mtakatifu awe wa kweli kwako kama vile alivyokuwa kwangu katika miaka iliyopita hadi sasa. Naomba utembea katika ushirika wa kina na Roho Mtakatifu, akupe ushindi katika maeneo yote

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1