Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi
Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi
Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi
Ebook69 pages2 hours

Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Hatuwezi kuepuka kabisa matatizo yanayotokea kati ya mshirika na mshirika kama inavyokuwa kati ya watoto wetu katika familia. Bwana Yesu alijua ya kuwa mgongano hauna budi kutokea ndiyo maana akatoa namna ya kukabiliana nayo katika maadiko. Kwa umuhimu wa pekee kabisa katika maandiko kutoka Mathayo 18:15-17. Kifungu hiki kinatuonyesha jinsi ya kukabiliana na matatizo baina ya muumini na muumini. Vinatoa jinsi iliyosalama katika kumrejesha ndugu aliyeanguka na kuwatia moyo washirika wa kawaida, ili kutilia maanani suala la kuwarejesha na kuwasaidia ndugu walioanguka ili kuwatia moyo katika wakati wao wa udhaifu.

Kitabu hiki kinachunguza mafundisho ya Yesh katika somo hili no kutuonyesha jinsi tunavyowesa kuyatumia katika misukosuko mbalimbali tunayokutana nayo.

LanguageKiswahili
Release dateMar 17, 2015
ISBN9781311849571
Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi
Author

F. Wayne Mac Leod

F. Wayne Mac Leod was born in Sydney Mines, Nova Scotia, Canada and received his education at Ontario Bible College, University of Waterloo and Ontario Theological Seminary. He was ordained at Hespeler Baptist Church, Cambridge, Ontario in 1991. He and his wife, Diane served as missionaries with the Africa Evangelical Fellowship (now merged with SIM) on the islands of Mauritius and Reunion in the Indian Ocean from 1985-1993 where he was involved in church development and leadership training. He is presently involved in a writing ministry and is a member of Action International Ministries.

Related to Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi

Related ebooks

Reviews for Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi - F. Wayne Mac Leod

    Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi

    Uchunguzi wa kitabu cha Mathayo 18:15-17

    F. Wayne Mac Leod

    Light To My Path Book Distribution

    Smashwords Edition

    Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi

    © 2010 Na F. Wayne Mac Leod

    Smashwords Edition, License Notes

    This ebook is licences for personal enjoyment only. This ebook may not be re-sold or given away to other people. If you would like to share this book with another person, please purchase an additional copy for each recipient. If you're reading this book and did not purchase it, or it was not purchased for your use only, then please return to your favorite ebook retailer and purchase your own copy. Thanks for respecting the hard work of this author.

    Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna ruhusa ya kunakiri sehemu ya kitabu hiki kwa njia yo yote ile bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mwandishi.

    Labda ielezwe vinginevyo, mistari yote ya Biblia imetolewa katika The Holy Bible in Kiswahili Union Version Published as BIBLIA Maandiko Matakatifu pamoja Na Itifaki © Bible Society of Tanzania, 1997

    Shukrani za dhati zimwendee mfasiri Mwinjilist Silvanus Peter Cheyo, na mhariri Mch.Isaac Madeleke wa Kanisa la Baptist Nyamanoro, Mwanza-Tanzania.

    Yaliyomo

    Didiaji

    1 - Kama Ndugu Yako Akitenda Dhambi

    2 - Nenda Ukamwonyeshe Kosa Lake

    3 - Mkiwa Wawili Peke Yenu

    4 - Mashahidi Mmoja au Wawili

    5 - Liambie Kanisa

    6 - Kama Akidataa Kulisikiliza Kanisa

    7 - Mtendee Kama Mpagani au Mtoza Ushuru

    8 - Kama Hakuna Suluhu

    Light To My Path Book Distribution

    Didiaji

    Nilipokea simu na kusikia sauti ile ile niliyoizoea. Alikuwa mmoja wa waumini katika kanisa ambalo nilikuwa nikihudumu. Sauti yake ilikuwa kama ya mwenda wazimu. Unatakiwa ufike hapa mara moja, aliniomba. Kwa nini, kuna tatizo gani? Niliuliza. Nitakuambia ukifika hapa’ alijibu.

    Niliahirisha nilichokuwa nikifanya na kwenda nyumbani kwake. Hii itakuwa ni safari yangu ya mwisho kulitembelea kanisa hili. Mke wangu pamoja nami tulikuwa tunatarajia kurudi nyumbani kwa ajili ya likizo fupi baada ya kutumika kwa muda wa miaka miwili katika nchi ile. Wanawake walikuwa wakijiandaa na sherehe ya kumwaga mke wangu kama ishara ya shukrani kwa huduma aliyokuwa akiifanya katikati yao.

    Nilipowasili, niliwasalimu wanakanisa na nikakaribishwa kuketi. Kuna tatizo gani? Niliuliza. Ndivyo hivyo, jibu lilitoka (akanipa jina). Amewakaribisha akina mama kutoka kanisa lile ili kuhudhuria sherehe ambayo tumemwandalia mkeo. Hakunihusisha juu ya uamuzi huu. Aliwakaribisha tu waungane nasi. Wewe ni mchungaji; nakuomba uongee naye juu ya jambo hili. Mwambie kwamba alitakiwa aongee nami kwanza, aliongea kwa hasira.

    Je! Ulizungumza naye wewe binafsi? Niliuliza. Hapana, alijibu, Asingenisikiliza. Utajuaje bila kujaribu?, niliuliza. Kama ningeenda nyumbani kwake angeweza kunipiga, alisema. Sawa kwa nini usimpigie simu? Nitampigia kama utakuwa tayari kusikiliza mazungumzo yetu kwa simu ile pale, alijibu.

    Nikitafakari jambo hili kwa muda kitambo, nilijibu. Mungu ametueleza kwamba kama tuna tatizo na ndugu yetu ni vyema kwemwendea sisi wenyewe. Naamini kama tunataka baraka za Mungu juu ya jambo hili, tunapaswa kulifanya kwa njia ya Mungu. Mimi sitafanya kitu cho chote hadi utakapokuwa tayari kufanya kwa njia ya Mungu. Sema naye wewe mwenyewe.

    Yote sawa, alisema na kwenda kuchukua simu iliyokuwa kwenye chumba kingine. Baada ya dakika chache alirudi akiwa na uso wa tabasamu. Mungu amekuwa akisema naye (alitaja jina) kwa kile alichokifanya. Amekiri na kuniomba msamaha na tukayarekebisha mambo yote. Kwa pamoja tulimsifu Mungu kwa baraka zake za ajabu.

    Wakati nikitoka nyumbani mwa mwanamke huyu, nilijiuliza na kuwaza ni nini kingetokea kama ningekuwa nimemsikiliza na kufanyia kazi mawazo yake. Hebu waza kwamba kanisa lingekuwa limeshirikishwa jambo hili. Matokeo yake yangekuwa ni hatari sana. Makanisa mengi yamegawanyika kwa sababu ndogondogo kama hizi.

    Hatupaswi kuyatelekeza matatizo kati ya waumini kama tunavyofanya kwa watoto wetu ndani ya familia zetu. Mara kwa mara hatutakubali kuona jinsi mambo yatakavyoen-deshwa. Wakati mwingine tunatenda kwa hasira na kiburi. Haiba zetu hugongana. Watu huumizwa. Maandiko yamejaa mifano mingi ya migogoro kati ya waumini.

    Bwana Mungu alijua kwamba jambo hili litaendelea kutokea, hivyo akatoa maelekezo ya jinsi gani tunaweza kulishughulikia jambo kama hili. Kwa upendeleo wa pekee hapa Yesu anatufundisha katika Mathayo 18:15-17. Katika kifungu hiki Yesu anatufundisha jinsi ya kuyashughulikia matatizo yanapotokea.

    Mathayo 18 inatoa changamoto ya kuyashughulikia mambo kibinafsi yanapotokea katikati ya mahusiano yetu. Inaelekeza njia iliyo salama kwa ndugu walioanguka ili kupatana na kuwatia moyo waumini wachanga kiroho

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1