Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Ninang'atuka 2014
Ninang'atuka 2014
Ninang'atuka 2014
Ebook96 pages35 minutes

Ninang'atuka 2014

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Ni kitabu chanye hazina ya mashairi yaliyotungwa na mtunzi
aliyebobea katika fani ya utunzi wa nyimbo, tenzi na mashairi.
Mtunzi wa kitabu ametunga tungo za kitabu hiki akifuata na kulinda
maadili ya lugha ya Kiswahili kwa malengo ya kuelimisha, kuburudisha na
kufundisha jamii zote. Usomapo kitabu hiki utapata uhondo kamili wa
lugha ya Kiswahili kwani mtunzi wa kitabu ametumia maneno ya Kiswahili
sanifu, Kiswahili cha mitaani na maneno aliyoyatohoa kutoka lugha mbali
mbali ambayo hutumiwa kwa wingi mitaani.
Katika kurasa za mwisho za kitabu hiki, mtunzi ameweka kamusi ya
Kiswahili cha mitaani ili wale wasioelewa Kiswahili cha mitaani waweze
kupata burudani kamili wanaposoma ama wanapoimba mashairi yake.
LanguageEnglish
PublisherXlibris US
Release dateDec 26, 2013
ISBN9781483689647
Ninang'atuka 2014
Author

Dardanus Mfalme

Dardanus Mfalme, popularly known as Dardan King, is a Tanzanian-American multi-talented writer, producer, composer, poet, musician, and multi-instrumentalist who is one of the best-selling artists and writers of Swahili music and Swahili poetry books worldwide. For a complete biography, visit www.mfalme.com.

Related to Ninang'atuka 2014

Related ebooks

Poetry For You

View More

Related articles

Related categories

Reviews for Ninang'atuka 2014

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Ninang'atuka 2014 - Dardanus Mfalme

    NINANG’ATUKA 2014

    Dardanus Mfalme

    Copyright © 2013 by Dardanus Mfalme.

    All rights reserved. No part of this book may be reproduced or transmitted

    in any form or by any means, electronic or mechanical, including photocopying, recording, or by any information storage and retrieval system,

    without permission in writing from the copyright owner.

    Rev. date: 10/30/2013

    Xlibris

    1-888-795-4274

    www.Xlibris.com

    140826

    Yaliyomo

    Utangulizi

    1. Nang’atuka

    2. Kanyaboya

    3. Mishumaa

    4. Jalamba

    5. Jeuri

    6. Msosi

    7. Skuna

    8. Umaarufu

    9. Suti

    10. Mafisadi

    11. Usinipite

    12. Hujaumbika

    13. Mgomo

    14. Nashukuru

    15. Fukara

    16. Miujiza

    17. Manabii

    18. Chuki

    19. Jembe

    20. Mbio

    21. Nyoka

    22. Haki

    23. Amani

    24. Punda

    25. Kijiti

    26. Suka

    27. Wazazi

    28. Umbu

    29. Maendeleo

    30. Nyakati

    31. Uchi

    32. Mzalendo

    33. Bangi

    34. Kitimoto

    35. Mfalme

    Kamusi ya Kiswahili cha mitaani

    Utangulizi

    Wasalaam,

    Ninapenda kuwakaribisha wapenzi wa mashairi, nyimbo na tenzi katika kitabu cha Ninang’atuka 2014. Kitabu hiki kina utajiri wa mashairi niliyoyabuni kutumia mbinu tofauti hivyo kufanya tungo hizi kuwa na ladha tofauti. Kama ilivyo ada yangu, nimechanganya tungo nilizozitunga miaka ya nyuma na tungo nilizozitunga hivi karibuni. Mchanganyiko huo unafanya tungo hizi kuwa zenye hisia tofauti hivyo kumgusa kila msomaji kwa namna ya kipekee.

    Sababu hasa ya kukiita kitabu hiki ninang’atuka 2014, ni kutokana na uamuzi nilioufanya wa kung’atuka katika fani ya muziki wa kizazi kipya ujulikanao kama ‘Bongoflava’.

    Uhondo kamili utaupata mara usomapo shairi la kwanza la kitabu hiki ambalo limebeba jina la kitabu.

    Katika kurasa za mwisho wa kitabu hiki, nimeweka kamusi ndogo ya Kiswahili cha mitaani ili wale wasioelewa Kiswahili cha mitaani nilichokitumia humu kitabuni na katika nyimbo nilizotunga waweze kunielewa barabara.

    Karibuni.

    1. Nang’atuka

    La hasha katu bwatuka, kinywani pumba kutoka,

    Mwiko kwangu kuropoka, ulimbukeni epuka,

    Kujikweza nimechoka, kama zoba kazibuka,

    Nang’atuka Bongoflava, ni mchezo wa kijinga.

    Mchezo hauna refa, wala wa kando mwamuzi,

    Mchezo kushiba sifa, nahau za kipuuzi,

    Wale wasoziba ufa, watajenga kwa machozi,

    Nang’atuka Bongoflava, ni mchezo wa kijinga.

    Kama ni umaarufu, utapata kwa mafungu,

    Ukiuliza sarafu, unazungushwa kizungu,

    Utashiba kwa harufu, ukoko wa kuu jungu,

    Nang’atuka Bongoflava, ni mchezo wa kijinga.

    Wanaita rapu gemu, mchezo pasi kanuni,

    Kujinadi na mademu, shobozi za luningani,

    Robo na nusu nidhamu, maadili jalalani,

    Nang’atuka Bongoflava, ni mchezo wa kijinga.

    Walioasisi fani, wameshachomoa timu,

    Mifukoni taabani, gemu limewadhulumu,

    Kujirudi ukubwani, hazitorudi timamu,

    Nang’atuka Bongoflava, ni mchezo wa kijinga.

    Si neno la mkosaji, sizitaki mbichi hizi,

    Nguli alovikwa taji, mwenye shahada ya kazi,

    Kama vile mahujaji, kila mwaka mwaga dozi,

    Nang’atuka Bongoflava, ni mchezo wa kijinga.

    Haina msisimko, hii fani matangazo,

    Ngoma pasi mdundiko, kuchezeka maigizo,

    Hasi ni mpangiliko, hata bubu ana tuzo,

    Nang’atuka Bongoflava, ni mchezo wa kijinga.

    Maisha ya maigizo, hata mlo danadana,

    Suruali mlegezo, mfukoni senti huna,

    Kuleteana mizozo, promota shavu kanona,

    Nang’atuka Bongoflava,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1