Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu
sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu
sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu
Ebook165 pages1 hour

sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kim Ung-yong alizaliwa nchini Korea ya Kusini katika jiji la Seoul. Alipokuwa na umri wa mwaka mmoja tu, tayari alikuwa amejifunza alphabeti za Kikorea na maumbo (characters) 1,000 ya lugha ya Kichina. Alipofikisha umri wa miaka mitatu alikuwa anaweza kufanya hisabati ngumu za mada ya 'calculus'. Kim alipofikisha umri wa miaka mitano, tayari alikuwa ametunga, kuchapisha na kuuza kitabu chake cha kwanza. Ni katika umri huo wa miaka mitano Kim alikuwa akiongea vizuri lugha za Kikorea, Kijapani, kingereza, Kifaransa na Kijerumani! Kitabu hiki kimesheheni mifano ya watoto waliozaliwa na akili za juu kama Kim. Hawa ni watoto ambao kila mzazi angetamani kuwanao. Ni kweli kwamba, sababu za vinasaba 'genetic' zaweza kuwa moja ya vyanzo vya mtoto kuzaliwa na akili za juu kuliko kawaida (more than 100% of IQ), lakini tafiti za kisayansi zinamletea mzazi kanuni nyepesi za kumwezesha kumzaa mtoto mwerevu.

Ni dhahiri kwamba, haiwezekani kubadilisha vinasaba vilivyomo katika seli za baba au mama ili apatikane mtoto mwenye akili za juu za kipekee, lakini, wenza wawili wanayo nafasi ya kuchaguana kwa kujali ubora wa mbegu za kiume na ubora wa mayai kwa jinsia ya kike: Hapo swala la umri wa wenza; uwiano wa umri baina yao; na katika umri upi wapate mtoto na umri upi wasizae kabisa ni mambo ya msingi. Hilo limeongelewa kwa mapana. kitabu pia kinamuongoza mzazi katika kanuni za kuboresha homoni 'hormones' zinazohusiana na ujenzi wa ubongo na akili kwa ujumla. Kitabu kinaaza na homoni za mama na kisha homoni za mtoto mwenyewe. Aidha, kitabu kinaelezea namna ya kutengeneza mazingira ya mtoto kuanzia mazingira ya tumboni mwa mama na mazingira ya baada ya kuzaliwa. Kanuni hizo na zingine kadhaa ndizo mada zilizomo katika kitabu hiki. Ni bayana kwamba kwa kiwango kikubwa, ukosefu wa maarifa, uzembe na umaskini ndivyo vimewasababishia watoto wengi udumavu wa akili.

SAYANSI YA KUMZAA MTOTO MWEREVU  ni kitabu kinachomfundisha mzazi namna ya kumzaa (kumpata) mtoto ambaye kama hatafikia kiwango cha kuitwa "prodigy" au "genius", basi ataitwa mwerevu; yaani binadamu mwenye uwezo mzuri katika kuyamudu masomo yake na kutatua changamoto za maisha. Elimu hii, inamuandaa mtoto kuanzia mazingira ya kabla ya kutungwa kwa mimba yake; kichanga tumboni; kuzaliwa na kufikisha umri wa miaka minne.

Mtoto aliyeandaliwa kwa sayansi hii, daima atakuwa ni mshindi masomoni na maishani. Kitabu hiki, ni mkusanyiko wa tafiti zilizofanywa na wataalamu mahiri wa mambo ya afya, saikolojia, elimu, sanaa na wengineo katika mabara ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Ulaya, Asia na Australia. Baadhi ya tafiti hizi zimechukua takriban muda wa miaka 40 ili kukamilika!

Msomaji atagundua kwamba, kabla hajafanya uamuzi wa kuzaa na mwenza wa namna gani, alipaswa kwanza kupata maarifa yaliyoko humu. Lakini pia, kama tayari uchaguzi wake haukuwa wa kisayansi katika kumchagua mwenza, basi bado yapo maarifa ya kurekebisha dosari za kumzuia kumpata mtoto mwerevu. Kitabu chafaa kabla ya ujauzito, na kama mzazi amechelewa kupata maarifa haya, basi elimu hii bado itafaa endapo mtoto hajafikisha umri wa miaka minne. Hilo ni angalizo muhimu lenye sababu za kibaiolojia.

Bi. Janeth Kalinga ambaye ni mhadhiri Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (DUCE) pamoja na mwandishi mahiri wa vitabu Mwl. Samson Manyala, wamekuandalia kitabu hiki katika lugha rahisi kueleweka. Aidha, japo mtoto na mzazi aliyeongelewa ni wakitanzania, lakini kitabu bado kinabakia kuwa ufumbuzi kwa wazazi wote wanaoelewa au kutumia lugha ya Kiswahili kokote ulimwenguni. Kama ilivyo kwa Tanzania, kitabu hiki ni muhafaka vilevile kwa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, na Malawi. Nchi hizi licha ya kuwa watumiaji au waelewa wa Kiswahili, lakini mazingira yao na changamoto zao kijamii (kielimu) na kiuchumi hazitofautiani sana na za Tanzania.

 
LanguageEnglish
Release dateFeb 11, 2020
ISBN9788835372110
sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu

Related to sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu

Related ebooks

YA Health & Daily Living For You

View More

Related articles

Reviews for sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu - JANETH KALINGA

    SAMSON MANYALA NA JANETH MKINI

    SAYANSI YA KUMZAA MTOTO MWEREVU

    UUID:

    This ebook was created with StreetLib Write

    http://write.streetlib.com

    Table of contents

    SHUKRANI

    IKISIRI

    YALIYOMO

    SURA YA 1: JINSI MTOTO ANAVYOATHIRIWA NA UMRI WA WAZAZI WAKE

    SURA YA 2: KUUJENGA UBONGO WA MTOTO ANGALI TUMBONI

    KUUJENGA UBONGO WA MTOTO

    SURA YA 3: MANUFAA YA MUZIKI KWA MTOTO

    SURA YA 4: MAPUMZIKO YA MAMA MJAMZITO

    SURA YA 5: NAMNA YA KUMLAZA MTOTO KICHANGA

    SURA YA 6: RATIBA YA USINGIZI KWA KICHANGA

    SURA YA 7: RATIBA YA USINGIZI KWA MTOTO CHINI YA MIAKA MINNE

    SURA YA 8: KUMLAZA MTOTO SAMBAMBA NA MAMA

    SURA YA 9: MAZIWA ANAYOPASWA KUNYONYA MTOTO KUKUZA UBONGO

    SURA YA 10: HISIA ZINAVYOTAWALA UKUAJI WA AKILI

    SURA YA 11: MAZOEA HUUMBA UBONGO

    SURA YA 12: VIFAA VYA MICHEZO VYENYE KUKUZA UBONGO

    SURA YA 13: UHURU NA UKOMO WA AKILI

    SURA YA 14: KUSIFU KUZURI NA KUSIFU KUBAYA

    SURA YA 15: VYAKULA MUHIMU KWA UKUAJI WA AKILI

    SURA YA 16: MAMBO MENGINE MUHIMU KWA MASOMO YA MTOTO MDOGO

    SURA YA 17: HITIMISHO

    TAFITI ZILIZOHUSISHWA

    SHUKRANI

    Waandishi wa kitabu cha SAYANSI YA KUMZAA MTOTO MWEREVU, Bi Janeth Kalinga na Bw. Samson Manyala, Wanatoa shukrani kwa wote waliochangia na kuwezesha utayarishwaji na ukamilishaji wa kitabu hiki. Hakika ni kundi kubwa la watu wenye taaluma mbalimbali katika sayansi ya afya ya binadamu; malezi, elimu; michezo na sanaa kutoka katika mabara ya Amerika ya Kusini, Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Asia na Australia waliotoa mchango mkubwa kufanikisha kazi hii. Kwa wote tunasema: ASANTENI. Aidha, shukrani za pekee zimuendee mhariri, Adonis Byemelwa, ambaye alitumia muda wake kupitia na kurekebisha muswada wa kitabu hiki. Tunasema ASANTE SANA!

    WASIFU WA WAANDISHI

    Samsoni J. manyala ni mwalimu, mchunguzi wa maswala ya elimu na muandishi wa vitabu. Katika kitabu hiki akishirikiana na Bi. Janeth E. Kalinga, amedadisi kwa kina tafiti za watu mbalimbali katika somo la ukuzaji akili ya mtoto na hatimaye kuwapa wazazi njia na misingi ya malezi bora. Mwalimu Manyala ni mwandishi wa vitabu (Amazon) hususani mashairi katika lugha ya kingereza, mwandishi ni baba wafamilia.

    Bi Janeth kalinga ni mwalimu kindakindaki na mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika elimu, katika chuo kikuu cha dar es salaam. Janeth alimaliza elimu ya msingi mikocheni mwaka 1991, baadaye akajiunga na shule ya sekondari ya wasichana Kisutu na kumaliza mwaka 1995. Mwaka 1988 alihitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari Mkwawa na kujiunga Chuo cha ualimu Marangu, na kuhitimu mwaka 2001. Janeth alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam na kumaliza shahada ya elimu mwaka 2006, na kisha akaendelea na shahada ya uzalimili chuoni hapo na kufuzu mwaka 2008. Mwandishi ni mke wa mchungaji, Helerd Mkini, na wamebarikiwa watoto watatu (3).

    IKISIRI

    Wazazi wengi wanajiuliza maswali kadhaa kuhusu tabia na uwezo wa kiakili wa watoto wao, baadhi ya maswali ni kama haya:

    Kwanini mwanangu hana akili darasani?

    Kwanini mwanangu hupendelea michezo zaidi ya masomo?

    Mtoto wangu alianza masomo kwa ufaulu mzuri, mbona sasa huvurunda tu?

    Kwanini mwanangu ni msahaulifu sana?

    Endapo mtoto atayamudu masomo yake kuanzia ngazi za awali hata kupata shahada ya chuo kikuu na ikiwa atafanikiwa kupata ajira au kutopata, mzazi uanza tena kujiuliza:

    Pamoja na gharama zote nilizozitumia kumuelimisha mwanangu, mbona ameshindwa kuyamudu maisha?

    Mbona mtoto wangu hafanani na mtoto wa fulani ilihali wamesoma pamoja?

    Mbona ajira yake haina mafanikio?

    Mbona ameshindwa kujiajiri?

    Ndugu mzazi au mzazi mtarajiwa, katika kitabu hiki utapata ufumbuzi wa maswali kama hayo na mengine mengi. Binafsi nilivutiwa sana kumfahamu mtoto kinadharia, na kwa msingi huo niliazimia na kisha kuchukua hatua mahususi katika somo hilo. Nimepata fursa ya kuwa mwalimu katika shule za sekondari za serikali na binafsi kwa miaka kadhaa. Nimepata pia fursa ya kufundisha watoto wadogo katika shule za awali na msingi. Fursa ya kufundisha shule za awali na msingi, ilinipa mwanya mkubwa wa kuelewa mahitaji ya wazazi pamoja na watoto kwa mapana zaidi kuliko ilivyokuwa katika shule za sekondari ambako nilikuwa nikijishughulisha na vijana. Katika kuwafundisha watoto wadogo, ndipo nilipong’amua janga la UWEPO WA WATOTO WENGI WENYE MATATIZO YA UWEZO WA KIAKILI. Nimetafiti mambo mengi kinadharia, na kupitia tafiti za wataalamu mahiri duniani ili niweze kuwasaidia wazazi.

    Kuna mzazi ambaye alilalamika sana juu ya utendaji wa waalimu hasa wanavyomlea na kumfundisha binti yake darasani. Alidhania kwamba, labda madhaifu ya waalimu ndiyo yalisababisha matokeo ya mwanaye kuwa mabaya. Hayo yalitokea baada mzazi huyo kushuhudia (mimi) mwandishi wa kitabu hiki akigawa matokeo ya wanafunzi kwa baadhi ya wazazi. Matokeo hayo kwa bahati nzuri, yalikuwa ni ya wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza, ya tatu na ya nne. Watoto hao walikuwa darasa moja na binti yake ambaye hakufanya vizuri kimasomo. Baada ya kuona hayo matokeo hakulalamika tena bali aliniomba faragha. Mwalimu, nitakuona baadae watu wakishapungua. Aliporudi kwa mara ya pili, aliketi kwa unyenyekevu akiwa ameshika tama na kuniuliza taratibu, Mbona mtoto wangu nafasi yake darasani haipandi? Mzazi mwenzangu, maswali kama haya na mengine mengi, tumekuwa tukijiuliza na hata kufikia hatua ya kupachika majibu kadhaa yenye kuonesha kukata tamaa kama vile:

    Labda mtoto amerithi ujinga wa ukoo.

    Labda mtoto amelogwa (dhana potofu).

    Labda ni madhara ya midomo ya watu kwa kuwa alisifiwa mno.

    Labda shule aliyosoma ni mbaya.

    Labda mwalimu wa somo fulani anazembea.

    Labda amejiingiza katika anasa za makundi rika, (Peer Influence).

    Ndugu mzazi, majibu haya yasiyo ya kitafiti siyo ya kweli au yanaweza yakawa na asilimia ndogo sana katika ukweli wa jambo linalomsibu mwanao.

    Katika nchi zilizoendelea kama vile Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na hata China, wazazi wamevutiwa sana na namna sahihi ya kuwawezesha watoto kiakili na kifikra ili waweze kumudu masomo yao na hata katika maisha ya kila siku katika jamii. Jamii hizo zilihamasika tangu miaka ya nyuma na imekuwa katika mitaala yao ya kitaaluma na katika maisha ya mtu mmoja mmoja. Hiyo ndiyo tofauti kubwa inayosababisha wao kuendelea zaidi yetu katika nyanja za kiuchumi na sayansi. Uvumbuzi mwingi na ubunifu mwingi upo huko kuliko barani Afrika ambapo hata kwa waliosoma sana wanabakia kuwa ni wasomi kwa vyeti tu; kwa maana ya wenye kutegemea kuajiriwa tu.

    Profesa Ross A. Thompson, mhadhiri wa saikolojia katika chuo kikuu cha Califonia, Marekani anasema: Hili ndilo suala muhimu linaloshughulikiwa na wazazi wa kizazi hiki nchini Marekani. Kuongezeka kwa wanafunzi wasiojiweza na hata kutokuwa na ubunifu mkubwa ni sugu katika familia zetu, taasisi za mafunzo na taifa kwa jumla. Watunga sera na wadau wa elimu ndio walewale wasomi wa vyeti ambao wameathirika na mazingira kimalezi katika historia zao za nyuma. Lakini tatizo hilohilo, ndilo linaloshughulikiwa kwa nguvu zote katika nchi zilizoendelea na kusababisha watafiti wa masuala ya saikolojia, afya na elimu kufanya tafiti za kina za muda mrefu ili kunusuru watoto ambao wazazi na walezi wao watavutiwa na ufahamu huo.

    Kitabu hiki siyo elimu yetu pekee sisi waandishi kama ambavyo nilidokeza awali, bali ni utafiti wa kitaaluma ambao mwingine umetafitiwa kwa zaidi ya miaka hamsini. Huu ni utafiti wa wasomi mabingwa kuanzia miaka ya nyuma hadi sasa. Kitabu kimehusisha kazi nyingi muhimu kutoka mabara ya Amerika ya kusini, Amerika kaskazini, Ulaya, Asia na Australia. Kama mwalimu wa mwanao, nimechambua tafiti mbalimbali kisha kuzielezea katika lugha nyepesi inayoeleweka hata kwa mtu mwenye kiwango kidogo cha elimu.

    Mtoto ninayemzungumzia hapa ni yule mdogo, kuanzia aliyeko tumboni, kichanga aliyezaliwa hadi yule mwenye umri wa miaka minne. Umri wa miaka sifuri hadi minne (0-4) yaani kabla ya masomo ya awali, ni muhimu kuliko wowote kwa ujenzi wa akili ya mwanadamu. Kutokana na tafiti za kisayansi (kibaolojia), ubongo wa binadamu hukua kwa haraka sana tangu akiwa tumboni mwa mama yake hadi pale atakapotimiza miaka minne. Katika umri huo, ubongo wa mtoto huwa umefikia asilimia tisini (90%) ya ukuaji wa ubongo wa mtu

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1