Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Siri Ya Ajabu
Siri Ya Ajabu
Siri Ya Ajabu
Ebook177 pages6 hours

Siri Ya Ajabu

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Watu wengi wanaishi maisha ambayo hawakutamani kabisa kuyaishi, wengine wamekata tamaa na kukosa matumaini, wengi wanatamani kufanikiwa lakini hakuna njia inayojitokeza kuwaletea mafanikio, wengi wameshindwa kufikia malengo na ndoto zao na hivyo kufa na kuzikwa na ndoto ambazo zingeweza kuibadilisha historia ya dunia.

Hii ni kwa sababu wengi wamekosa kuifahamu siri ya ajabu ambayo kila aliyewahi kuijua ilibadilisha maisha yake na inaendelea kubadilisha maisha ya watu wengi kwa kila anayeweza kuitambua.

Siri hii yenye nguvu imekuwa ikifichwa na haitambuliki kirahisi japo matokeo yake ni ya moja kwa moja katika maisha ya kila mtu, lakini leo Siri hii ipo mikononi mwako. Kila unalolitaka katika maisha yako haijalishi ni kubwa kiasi gani unaweza kulipata kupitia siri hii.

Utakapomaliza kukisoma kitabu hiki Maisha yako yatachukua sura mpya na utaanza kuona mabadiliko makubwa katika Maisha yako. Utagundua kwamba hukutakiwa kuishi maisha unayoishi kwa sasa.

Utapata majibu ya kila swali na chanzo cha kila jambo na kila tatizo ulilonalo katika maisha yako.

FRANK CHRISTIAN ni mwalimu, mwandishi na mhamasishaji wa maendeleo kwa watu wa rika mbalimbali, Pia amewahi kuwa mwanachama wa Umoja wa Vijana wa Umoja wa Mataifa Vyuoni (UNCHAPTERS), Pia ni mwanzilishi wa shirika la Frontline Aid.

LanguageEnglish
Release dateAug 10, 2017
ISBN9781370676613
Siri Ya Ajabu
Author

Frank Christian

Whatever reason you have been thinking is holding you back is a lie that has manifested into reality, but you just have to believe that everything can be changed.

Related to Siri Ya Ajabu

Related ebooks

Personal Growth For You

View More

Related articles

Reviews for Siri Ya Ajabu

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

3 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Siri Ya Ajabu - Frank Christian

    Siri Ya

    Ajabu

    Siri Ya

    Ajabu

    Frank Christian

    Copyright © 2017 Frank Christian

    Published by Frank Christian Publishing at Smashwords

    First edition 2017

    All rights reserved. No part of this book may be reproduced or transmitted in any form or by any means, electronic or mechanical, including photocopying, recording or any information storage or retrieval system without permission from the copyright holder.

    The Author has made every effort to trace and acknowledge sources/resources/individuals. In the event that any images/information have been incorrectly attributed or credited, the Author will be pleased to rectify these omissions at the earliest opportunity.

    Printed and bound by Novus Print Solutions

    Mwandishi:

    Frank Christian

    E-mail: chrissalbert90@gmail.com

    Haki zote zimehifadhiwa, hairuhusiwi kunakili, kuzalisha, kuhifadhi au kuhamisha kwa namna yoyote labda kidijitali au kianalojia taarifa zilizopo katika kitabu hiki bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mwandishi na mpiga chapa.

    Taarifa zote zilizopo katika kitabu hiki ni kwa ajili ya kutoa elimu na sio tiba mbadala au matibabu ya aina yoyote ya mapungufu ya kiafya hivyo maelezo ya kitabu hiki sio mbadala wa matibabu na ushauri kutoka kwa madaktari na wataalamu bali ni elimu inayokusaidia kubadili mtazamo na kufikia namna sahihi itakayokusaidia kufanya mambo kwa usahihi.

    Nimeandika kitabu hiki kwa ajili ya Taifa langu la Tanzania, watanzania na

    Watu wa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati na nchi zote za kusini mwa

    Jangwa la Sahara,

    Ili kiwasaidie kufahamu siri yenye nguvu

    Inayomsaidia kila mtu

    Ulimwenguni

    Kuwa chochote anachokitaka.

    YALIYOMO

    Shukurani

    Utangulizi

    Sura ya kwanza

    Sura ya pili

    Sura ya tatu

    Sura ya nne

    Sura ya tano

    Sura ya sita

    Sura ya saba

    Sura ya nane

    Sura ya tisa

    Sura ya kumi

    Sura ya kumi na moja

    Sura ya kumi na mbili

    Sura ya kumi na tatu

    Sura ya kumi na nne

    Sura ya kumi na tano

    Mwisho

    Zawadi ya siri kwa watoto

    Shukurani

    Namshukuru Mungu kunipa ujasiri, afya, pumzi na maarifa ya kuweza kukiandaa kitabu hiki ambacho naamnini kitakuwa msaada kwa watu wa mataifa mengi ya Afrika katika kujikwamua kutoka katika wimbi la matatizo mbalimbali.

    Natoa shukrani za kipekee kwa wazazi wangu walezi Bw. Na Bi. Elisaa J. Mbise na mama yangu mpendwa Elimbora E. Sumari kwa kunitia moyo kila wakati nilipokuwa nikiandika kitabu hiki.

    Napenda kuwashukuru marafiki zangu na wale wote waliohusika na kujitoa kwa namna moja au nyingine bila kuchoka ili kuileta ndoto hii ya kitabu hiki katika uhalisia.

    Mwisho napenda kuwashukuru Reach Publishers hususan Kitengo cha usanifu (Design department) kwa kazi kubwa waliyoifanya kunishauri, kuhariri na kusanifu kitabu hiki.

    Utangulizi

    Wakati fulani katika maisha yangu niliwahi kuona kuwa mambo yote ni mabaya na mimi ni fukara na masikini. Nilipata uchungu sana na kuwaza sana na wakati mwingine nilisali lakini mambo hayakuwa mazuri kama nilivyokuwa nikiyatarajia. Nilihudhuria semina mbalimbali za ujasiriamali na mafundisho ya kufanikiwa kifedha lakini bado mambo hayakubadilika.

    Niliamua kuanza kuchunguza na kutafakari ni kwanini baadhi ya watu wana uchumi mkubwa na maisha mazuri na kila walichohitaji wanakipata na wengine wamebaki kuwa maskini na watu wenye matatizo mengi katika maisha.

    Siku moja niliamua kukaa na kutafakari kwa kina kwa muda mrefu na ndipo NIKAHISI kama vile kuna kitu fulani ambacho SIKIJUI na ili nifanikiwe ni lazima nikijue. Nikajiuliza sasa nitawezaje kukijua ili hali tayari sina hata fununu ya kitu au jambo hilo? Kitu hicho ndiyo siri ninayokueleza leo ambayo itakua mwanzo mpya wa maisha yako.

    Hakuna utakalolitaka likashindikana na wala hakuna fursa utakayoitaka ushindwe kuipata. Kitabu hiki kitakua ni msaada mkubwa sana kwako, uchumi wako na wa nchi, afya yako, furaha na utakua huru kuwa chochote unachotaka.

    Naamini siri hii itakua msaada kwa nchi nyingi za Africa pia ambazo zimekuwa katika umasikini na matatizo mbalimbali kwa muda mrefu. Utakapoanza kusoma kitabu hiki, utapata majibu ya kila swali katika maisha yako na chanzo cha kila jambo linalotokea katika maisha yako.

    Nimeeleza kwa mifano namna siri hii ilivyoweza kubadilisha nchi nyingi za magharibi pamoja na mataifa mengine makubwa kama marekani kuanzia karne zilizopita na namna kugundulika kwa siri hii kulivyoleta gunduzi mbalimbali za kisayansi katika mataifa hayo na nina uhakika kama sio kuifahamu siri hii basi huenda hata kimaendeleo tungeweza kuwa sawa na mataifa haya makubwa.

    Nimejaribu kufuatilia sana kwa undani tafiti za kisayansi zinazoelezea uwepo wa siri hii na namna ilivyoweza kuyabadili maisha ya watu wengi ulimwenguni. Pia nimejaribu kusoma na kuchimbua kwa undani makala na vyanzo vingi vinavyofafanua juu ya siri hii na cha ajabu ni kwamba kila mtu mkubwa kuwahi kutokea ulimwenguni na aliyefanikiwa sana mfano Plato, Shakespeare, Newton, Hugo, Beethoven, Lincoln, Emerson, Edison, Einstein, washington, woodrow wilson, henry ford, andrew carnegie na wengine niliowafuatilia kwa ukaribu niligundua kila mmoja alikuwa anaielewa siri hii, hivyo na mimi nimeamua nikufunulie siri hii iweze kuleta mwanzo mpya kwako na kwa familia yako.

    Niliendelea kuchunguza kwa undani na ni kama vile kila niliyemchunguza alikuwa ananiongoza na kunipeleka kwa mtu mwingine mwenye kuijua siri hii ya ajabu, mmoja baada ya mwingine na wote ni watu waliofanikiwa mno.

    Nimejaribu kuliongezea neno WEWE mkazo katika kitabu hiki kwani nitazungumzia zaidi mambo yanayokuhusu wewe binafsi unayekisoma kitabu hiki na hivyo unapokisoma tambua kwamba ninazungumza na wewe moja kwa moja unaekisoma kitabu hiki sasa hivi. Kitabu hiki ni kwa ajili yako wewe na kitaendelea kuwa mwongozo wa kiwango cha juu katika kufikia malengo mengi na ndoto ulizo nazo katika maisha yako na kuweza kuyabadili maisha yako ndani ya muda mfupi tu.

    Kitabu hiki kitakufunulia siri ya ajabu ambayo watu wengi huzaliwa na kufa bila kuitambua jambo ambalo linawapelekea kuishi maisha ambayo siyo ya ndoto zao.

    Utakapomaliza kukisoma kitabu hiki utakua umegundua siri halisi ya nguvu na chanzo cha kila tokeo katika maisha yako.

    Labda mtu mmoja kati ya laki moja wanaijua SIRI ya mafanikio ya Henry Ford, na hao wanaojua hawataki kuizungumza kwa sababu ya URAHISI wake, sentensi moja tu inaweza kuielezea SIRI hiyo kwa ufasaha

    NAPOLEON HILL.

    Sura ya kwanza

    Siri hii ni nini?

    Wanafalsafa na watu waliolianzisha Taifa la Marekani waliijua siri hii, Wachina pia waliigundua siri hii kutoka katika vitabu vya dini yao ya Kibudha, imekuwa ikirithishwa kutoka kwa wanafalsafa wakubwa hadi kwa waandishi wakubwa kuwahi kutokea duniani, Siri hii alirithishwa Napoleon Hill ambaye alikuwa mwandishi mkubwa huko marekani kutoka kwa Andrew carnegie ambaye alimwambia aifanyie uchunguzi kwa miaka 25 kwa mamilionea 500 na baadae akaandika kitabu kilichouzwa sana kiitwacho THINK AND GROW RICH, Baadaye Napoleon nae aliirithisha kwa Earl Nightingale ambaye nae aliirithisha kwa mwandishi Bob Proctor.

    Siri hii itakupa chochote unachotaka kama furaha, afya na mafanikio. Unaweza kufanya au kuwa chochote unachotaka, haijalishi ni kikubwa kiasi gani.

    Je wewe msomaji unataka kuwa nini? Je ni ndoto gani ambayo ukiipata maishani mwako utakuwa na furaha? Je unahitaji kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa? Je unahitaji maisha yako yaweje? Hii ni siri kubwa katika maisha yako.

    Siri

    Nafahamu sasa unajiuliza kuwa siri hiyo ni nini au ni ipi? Labda ni kitu cha kawaida sana au ni kitu cha kutisha sana. Fuatana nami katika kila hatua ya kitabu hiki.

    Hili Ombwe (uwazi) ambapo sayari ya dunia inapatikana na ambapo tunatembea na kuishi na kuwa na maisha yetu ni aina ya nishati (nguvu) ambayo inasafiri katika mitetemo (mitetemeko) ya hali ya juu, na ombwe hilo limejawa na nguvu fulani ya ajabu ambayo inajiunganisha yenyewe na asili ya mawazo tuliyonayo akilini mwetu na kuyabadili mawazo kuwa vitu halisi katika maisha yetu ya kawaida.

    Sote tunafanya kazi au tunashirikiana na nguvu kubwa isiyo na mipaka (infinite power). Sote tunajiongoza kwa kanuni sawa ambazo ni kanuni za ulimwengu zilizokuwepo tangu kuumbwa kwa misingi ya dunia. Kanuni hizi ni sahihi kiasi kwamba hatushindwi kutengeneza Roketi za kwenda sayari nyingine au mwezini na kujua hata muda sahihi wa kurudi kwa roketi hizo.

    Ndugu msomaji haijalishi upo eneo gani au mahali gani lakini sote tunaishi katika kanuni moja asili iitwayo "KANUNI YA UVUTANO" au kwa kiingereza (the law of attraction).

    Hivyo siri hii ni kanuni ya uvutano.

    Kila kitu kinachokuja katika maisha yako ni wewe mwenyewe unakivuta kuja katika maisha yako kwa kupitia kanuni hii kubwa, na kinakuja kupitia taswira ulizonazo akilini mwako yaani kile unachokiwaza, hii ina maana chochote kinachoendelea katika mawazo yako unakivuta kuwa kitu halisi.

    kila wazo ulilonalo ni kitu halisi Printice Mulfold (1834-1891)

    Watu wengi waliowahi kuishi ulimwenguni na kuijua siri hii walifahamu kabisa kuwa kanuni hii ya uvutano au (the law of attraction) ni moja kati ya kanuni asili yenye nguvu sana.

    Waimba mashairi kama Shakespeare, Robert browning na William Blake waliizungumzia siri hii katika mashairi yao, wachoraji kama Leonardo da vinci walieleza siri hii kupitia michoro yao pia.

    Wanafalsafa wakubwa kuwahi kutokea na wasomi wakubwa kama Socrates, Plato, Isaac Newton, Pythagoras, Francis Balcon na wengine wengi wamezungumzia kanuni hii katika mafundisho na maandiko yao. Majina yao yamekuwa maarufu toka vizazi vyao hadi leo.

    Dini mbalimbali kama Ukristo, Uislamu, Hindu, dini ya Kibudha na dini ya Kijuda zote zimezungumzia siri hii kwa undani sana toka kipindi cha zamani. Miaka 3000 Kabla ya Kristo siri hii iliandikwa katika mawe japo wengi waliificha lakini imeendelea kuwepo kwa kila mtu kuitambua.

    Kanuni hii ilianza tangu mwanzo, ipo na itaendelea kuwepo. Ni kanuni ambayo inaweka kila kitu sawia ulimwenguni, na kila hatua ya maisha yako. Haijalishi ni nini unapitia katika maisha yako, haijalishi upo wapi na unafanya nini, kanuni ya uvutano inatengeneza mambo yote unayoyaona katika maisha yako na inafanya hivyo kupitia MAWAZO YAKO.

    Mwaka 1912 Charles Haanel aliielezea kanuni hii akisema kuwa ni kanuni ambayo mfumo mzima wa uumbaji unategemea.

    Watu wenye hekima wengi wamekuwa wakiijua siri hii au kanuni hii na hata vizazi vilivyopita kama

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1