Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Maisha mchanganyiko
Maisha mchanganyiko
Maisha mchanganyiko
Ebook71 pages1 hour

Maisha mchanganyiko

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Kila atakaye kujua siri za maisha hujua, kila azidharauliye huishi bila kujua kwa maana kila siri iko wazi kwa yeye aliyewahi kuifikiria na kuipitia lakini kama hujawahi kuifikiriana kuipitia ni vigumu sana kuelewa.
Hivyo Mungu kwa nguvu zake amenitia nguvu kuandika kitabu hiki kinachoitwa “MAISHA MCHANGANYIKO (zijue siri za maisha)” Nikiwa namatumaini kabisa kuwa utafunguka na kuzijua siri za maisha kama zilivyo na itakusaidia kutoka mahali ulipo na kuingia mahali pazuri zaidi katika maisha yako.
KARIBU TUSOME PAMOJA.
 

LanguageEnglish
PublisherTila Media
Release dateDec 12, 2017
ISBN9781540125880
Maisha mchanganyiko
Author

Joel Kiongole

Joel Kiongole, famous with name Pastor Joe is an engineering student at Univerisity of Dae es salaam, Tanzania. He is passioned to teach the word of God, he writes Christian articles that he shares through social networks and also write books

Related to Maisha mchanganyiko

Related ebooks

Christianity For You

View More

Related articles

Reviews for Maisha mchanganyiko

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Maisha mchanganyiko - Joel Kiongole

    Shukrani

    Mpaka kitabu hiki kimekmilika sio kwa nguvu zangu bali ni kwa msaada wa Mungu namrudishia sifa, utukufu na heshima.Nawashukuru sana ndugu zangu kwa kunitia moyo pale nilipotaka kukata tamaa.Na pia sio juhudi zangu pekee bali kwa juhudi za wengi marafiki zangu kwa msaada wenu wa hali na mali.msaada wenu wa mawazo na maombi umekuwa sababu kubwa sana ya kukamilika kwa kitabu hiki. Mungu awabariki sana.

    Maalumu

    Kitabu hiki nakitoa maalumu kwa baba yangu Mpendwa Frank Kiongole aliyefariki miaka kadhaa iliyopita kwa ajali ya pikipiki akiwa katika harakati za kutimiza majukumu yake ya kisiasa sumbawanga mjini. Nakumbuka upendo wake, busara, huruma na hekima zake Baba pumzika kwa amani sitakusahau.

    Utangulizi

    Maisha tunayoishi yana mambo mengi sana kiasi cha kuyajua na kuyapatia ufumbuzi wa mambo hayo ndio kiasi chako cha furaha na amani.

    Jinsi unavyotambua mambo mengi yanavyoenda katika maisha ndivyo unavyokuwa unahitajika kuwasaidia wengine ambao bado hawajafahamu sana juu ya maisha yanavyoenda.

    Maisha yetu yameficha siri nyingi sana ambazo ni vizuri kuzijua ili uishi bila woga, hofu, mashaka, kujishtukia na kutojiamini. Wale pekee wanaozijua siri za maisha ndio hao pekee wanaoishi bila woga,hofu, mashaka na kutojiamini

    Asilimia kubwa ya watu katika dunia tunashindwa kuishi na watu vizuri sio kwa sababu ni watu wenye tabia mbaya sana hapana.Wala sio kwa sababu ni watu wakaidi sana hapana bali ni kutokana na kushindwa kujua siri ndogo ndogo za maisha na namna ya kuishi na watu.

    Asilimia kubwa ya watu tumepoteza kujiamini na kukaribisha woga sio kwa sababu sisi ni watu ambao hatuna uwezo kiasi hicho hapana bali ni kutokana na kutojua siri fulani ambazo maisha yamebeba.

    Watu wengi sana wamekata tamaa na kuhairisha mambo mengi sana ambayo walipanga kufanya kutokana na matatizo ambayo yanawakuta kila siku.Wengine wamejitia tamaa hadi maisha yao sio kwa sababu  wao ndio wenye matatizo makubwa kuliko wao ila ni kutokana na kukosa  kujua siri ndogo ndogo ambazo maisha yamezificha..

    Kila atakaye kujua siri za maisha hujua, kila azidharauliye huishi bila kujua kwa maana kila siri iko wazi kwa yeye aliyewahi kuifikiria na kuipitia lakini kama hujawahi kuifikiriana kuipitia ni vigumu sana kuelewa.

    Hivyo Mungu kwa nguvu zake amenitia nguvu kuandika kitabu hiki kinachoitwa MAISHA MCHANGANYIKO (zijue siri za maisha) Nikiwa namatumaini kabisa kuwa utafunguka na kuzijua siri za maisha kama zilivyo na itakusaidia kutoka mahali ulipo na kuingia mahali pazuri zaidi katika maisha yako.

    KARIBU TUSOME PAMOJA.

    Yaliyomo

    Shukrani

    Maalumu

    Utangulizi

    Sura ya kwanza

    Anza siku yako vizuri

    Sura ya pili

    Chagua kitu sahihi cha kufanya ukiwa peke yako

    Sura ya tatu

    Ishi maisha yako halisi kila utakakoenda

    Sura ya nne

    Usilazimishe kila mtu akupende

    Sura ya tano

    Kumbuka na simulia ulikotoka

    Sura ya sita 

    Kila mtu madhaifu na matatizo yake

    Sura ya kwanza

    Anza siku yako vizuri

    Siku moja nilikuwa na wenzangu wengi tukiongea juu ya maisha ya kawaida na maisha ya kiroho. Ghafla mmoja wetu akauliza swali ambalo kwa muda kidogo lilikosa majibu katika wengi wetu.Ilibidi kila mmoja ajaribu kufikiri kidogo kitu cha kujibu ili mchango wake uwe na maana kwa wenzake.baada ya muda majibu yakaanza kupatikana kutoka kwa wenzangu mbali mbali na kuanza kuchangia.Hata mara baada ya kupata majibu hayakuwa sawa kwa kila mmoja aliyetoa.Hakuna aliyeonekana kukubaliana au kukataa majibu ya mwenzake bali kila mmoja alijaribu kuchangia anachofahamu.

    Swali lilikuwa ni Je nitaianzaje siku yangu vizuri?Binafisi nililisikia swali vizuri saana lakini nilikosa jibu kwa wakati huo kwa maana niliona ni swali lenye maana kubwa katika maisha yetu na haliitaji majibu ilimradi tu tunaweza kujibu. Asilimia kubwa ya wote waliotoa majibu walitoa kutokana na jinsi wanavyohisi ni vizuri kuianza siku vizuri.Wachache kati yao walitoa majibu kutokana na maisha yao halisi.Na wengine pia walitoa majibu kutokana na jinsi walivyo na uhakika wa namna ya kuianza siku vizuri.

    Mwanzo wa siku yako unasema juu ya mwisho wake.

    Mmoja wa rafiki zangu ninaowapenda sana alisema kitu kizuri sana juu ya mwanzo na mwisho wa jambo.AlisemaMwisho wa jambo unauona kuanzia mwanzo

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1