Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki
Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki
Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki
Ebook177 pages1 hour

Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Juma Ramadhan Magola Kilaza (Magola wa Chumbi), ambaye alijulikana zaidi kwa jina Kilaza ambalo ni jina la ukoo, ni mmoja kati ya wanamuziki bora kuwahi kutokea Tanzania. Mwanamuziki huyu, alianza kupiga muziki kwenye miaka ya 1960. Katika Maisha yake, alishiriki katika bendi za Morogoro jazz, Cuban Marimba, TK Lumpopo, Magola International na Les Cuban, zote za Morogoro akishiriki kupiga muziki unaojulikana zaidi kama muziki wa dansi ama rumba. Kitabu hiki, kinasimulia maisha yake kimuziki, mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili, kuelimisha, kuburudisha, kuliwaza na kukuza sifa ya Morogoro. Kitabu pia, kinasimulia changamoto alizopitia, na visa vilivyovuma sana kati yake na mwanamuziki mwingine maarufu wa Morogoro Mbaraka Mwinshehe Mwaruka.

LanguageKiswahili
PublisherMarwa
Release dateDec 19, 2023
ISBN9798215951231
Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki
Author

Anthony Marwa

KUHUSU MWANDISHI  Anthony Marwa Mwita (PhD) pia ni mwandishi wa kitabu Mbaraka Mwinshehe Mwaruka soloist national na rumba la Kitanzania. Kutokana na mapenzi yake ya muziki amefungua studio za kurekodi muziki KC Records mjini Dar es salaam na kutumia fursa hiyo kuzirekodi tena baadhi ya nyimbo za nguli Juma Kilaza na Mbaraka Mwinshehe. Tayari nyimbo kadhaa za nguli hawa Semeni, Asha, Zena na Morogoro hoyee za Juma Kilaza na Shida, Morogoro yapendeza, Esta na Soniasa za Mbaraka Mwinshehe zimekwisha rekodiwa. Baadhi ya wanamuziki walioshiriki kurekodi nyimbo hizo ni wanamuziki wa zamani wa bendi hizo na watoto wa nguli hao Maneno Juma Kilaza na Muhtaji Mbaraka Mwinshehe.

Related to Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki

Related ebooks

Reviews for Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki - Anthony Marwa

    TABARUKU

    Natabaruku kitabu hiki kwa wazazi wangu Marwa Mwita Taragwa na Chausiku Werema walionilea kwa mapenzi makubwa. Pia kwa mke wangu mpendwa Mbilijao Philipo na wanangu Wilbrod Anthony, Taragwa Anthony, Sophia Anthony na Mossi Ramadhan

    .

    YALIYOMO

    SHUKRANI

    Kwanza kabisa napenda kumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa ulinzi na Baraka zake, ulioniwezesha kukamilisha kazi hii ya tunu. Ninamshukuru kwa kunijalia afya njema kipindi chote nilipokuwa naandika kitabu hiki.  Wapo watu ambao lazima niwataje, kutokana na msaada walionipatia. Napenda kutoa shukrani za pekee, kwa Saidi Makelele, aliyekuwa mwanamuziki wa bendi za Super Volcano, Magola International, Les Wanyika, Les Cuban na bendi zingine akipiga chombo cha tarumbeta pia David Senyagwa aliyekuwa mwanamuziki wa Cuban Marimba akipiga gitaa la kati (rhythm) na Ramadhan Juma Kilaza mtoto wa Juma Kilaza. Utayari wao katika kushirikiana nami katika kutoa taarifa muhimu, umechangia kwa kiasi kikubwa kukamilisha kitabu hiki. Bila ushirikiano huo taarifa juu ya harakati za nguli wa muziki Juma Kilaza na mchango wake katika kuelimisha na kuburudisha jamii kwa njia ya muziki nisingeweza kuzipata kikamilifu.

    1 UTANGULIZI

    Juma Ramadhan Magola Kilaza, ambaye alijulikana zaidi kwa jina Kilaza ambalo ni jina la ukoo, ni mmoja kati ya wanamuziki bora kuwahi kutokea Tanzania. Mwanamuziki huyu, alianza kupiga muziki kwenye miaka ya 1960. Katika Maisha yake, alishiriki katika bendi za Morogoro jazz, Cuban Marimba, TK Lumpopo, Magola International na Les Cuban, zote za Morogoro akishiriki kupiga muziki unaojulikana zaidi kama muziki wa dansi. Kitabu hiki, kinasimulia maisha yake kimuziki, mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili, kuelimisha, kuburudisha, kuliwaza na kukuza sifa ya Morogoro. Kitabu pia, kinasimulia changamoto alizopitia, na visa vilivyovuma sana kati yake na mwanamuziki mwingine maarufu wa Morogoro Mbaraka Mwinshehe Mwaruka.

    Pengine mwanamuziki aliyechangia sana katika kumkuza na kumuimarisha kimuziki ni Salum Abdalah Yazide, aliyekuwa kiongozi, muasisi, mtunzi mkuu na muimbaji wa bendi ya Cuban Marimba. Uzoefu ama kuimarika huku, kulitokana na ushirikiano uliokuwepo kati yao toka mwaka 1963 hadi 1965 ambapo Salum alikuwa akimruhusu Juma Kilaza kushiriki katika bendi kama mwanamuziki wa Cuban Marimba, japo wakati mwingine alikuwa anaishi mbali na Morogoro. Matokeo ya ushirikiano huo mzuri, ulifanya utunzi na uimbaji wa Juma Kilaza kufanana sana na ule wa Salum Abdalah.

    Lakini ili kufahamu vyema harakati za kimuziki za mwanamuziki, huyu ni vyema kujua asili ya muziki huu wa dansi ama rumba ili kujua jinsi ulivyoingia na kuenea nchini.

    Muziki huu wa dansi, kama unavyojulikana nchini Tanzania, asili yake ni muziki wa mitindo ya Rumba, Samba na Bolero kutoka Cuba na sehemu zingine za Marekani ya kusini. Uliingia na kuenea eneo zima la Afrika Mashariki na ya kati, kwenye miaka ya 1930.

    Muziki huu ulienea zaidi nchini Tanzania, wakati huo Tanganyika, baada ya kwisha kwa kilichoitwa vita vya pili vya dunia mwaka 1945. Nyakati hizo, ndipo chombo cha kupiga muziki wa santuri (Gramafoni) kilipoingizwa nchini. Chombo hiki hakikuhitaji betri, ama umeme hivyo ilikuwa rahisi kukitumia. Ili kufanya Sahani iliyobeba santuri kuzunguka na kutoa muziki, mtumiaji alipaswa kunyonga mkono uliokuwa umepachikwa sehemu ya pembeni ya gramafoni hiyo.

    Huenda gharama kubwa pekee, ilikuwa kununua sindano mara kwa mara zilizokuwa zikipachikwa kwenye ncha ya kichwa kinachowekwa juu ya santuri. Sindano hii iliyopachikwa, ilikuwa ikipita kwenye mikwaruzo iliyotengenezwa kwenye Sahani hizo za santuri, wakati ikizunguka hutafsiri mikwaruzo hiyo kuwa sauti. Sauti hiyo ama muziki, ulitoka katika spika ndogo ambayo nayo pia ilikuwa imepachikwa kwenye kichwa hicho. Sindano hizi zilikuwa zikiisha baada ya kutumika kwa muda mfupi, na zilikuwa hazifai tena hivyo kutupwa.

    Gramafoni - chombo cha kupiga muziki 

    SAHANI ZA SANTURI ZILIZOAMBATANA na chombo hicho, zilikuwa na chapa ya  GV (Gramaphone Victor) na namba. Jambo lililofanya wapenzi wengi wa muziki kuzitambua santuri hizo kwa namba, hasa kwa kuwa lugha iliyotumika katika uimbaji ilikuwa ngeni kwao.

    Santuri hii ilitambulika kama GV1

    Kwa maana hiyo, pia kulikuwa na GV2, GV3 nakuendelea.

    Wakazi wa mjini ndio wa kwanza kuvutika na muziki huu na kuamua kuanzisha vikundi vya kucheza dansi (ball room dancing) na baadhi viliunda vikundi maalum vya kupiga muziki. Wanachama wa vikundi hivyo walilipa kiingilio cha uanachama na kushiriki katika kuchangia ununuzi wa ala za muziki, pale ilipohitajika. Kikundi cha kwanza ni kile cha Dar es salaam jazz, kilichoanzishwa mwaka 1938. Azma na furaha kuu ya wanachama ni kukutana na  kucheza muziki. Hivyo wapiga muziki walikuwa wakipiga muziki kwa mapenzi yao na wala sio kama njia ya kujiingizia kipato. Vikundi vingine vya namna hii vilivyoanzishwa ni pamoja na Cuban Marimba iliyoanzishwa mwaka 1948 chini ya Salum Abdalah Yazide (SAY) mjini Morogoro (Mukabarah: 1972) bendi hii ilifanikiwa kupata wanachama zaidi ya miambili.

    Japo vikundi vingi vya muziki vilivyoanzishwa nchini na hata nchini Kongo vilijiita jazz band, ukweli ni kwamba havikuwa vikipiga muziki wa jazz (ama muziki wa jazba) kama tunavyoufahamu. Kwa kweli, ni wanamuziki wachache sana waliopiga muziki wa aina hii Afrika, Hugh Masekela wa Afrika kusini ndiye aliyekuwa mashuhuri zaidi katika upigaji wa muziki wa aina hii. Bendi zote zilizoanzishwa Tanganyika, na baadae Tanzania na hata Kongo zilikuwa zikipiga Rumba, Bolero na Samba. Ilikuwa rahisi kwa wanamuziki wa nchi hizi za kiafrika kuvutika na muziki huu, kwa kuwa ulikuwa na vionjo vingi vya muziki wa asili wa jamii za Afrika. 

    Ala za muziki zilizotumika zaidi ni magitaa, Mandolin, Violin, Saksafoni, tarumbeta, manyanga, tumba na ala za kukwaruza na za kugonga. Kwa kawaida, mpangilio wa muziki kama ulivyopokelewa na wanamuziki wa dansi eneo hili la Afrika mashariki na ya kati, ulikuwa wa vipande vitatu. Kwanza muziki huanza taratibu huku ukitawaliwa na ala za kupuliza na mara nyingi huongozwa na mwimbaji mmoja, kipande cha pili kikiwa na waitikiaji na cha tatu kikitawaliwa na ala za magitaa na za kupuliza, kipande hiki cha tatu huchangamka zaidi kuliko kile cha kwanza na cha pili. Kwa kawaida muziki unapoanza wapenzi wengi husikiliza ama kuwatazama wapigaji, wachache sana hudiriki kucheza, tena taratibu hadi pale muziki unapochangamka, ndipo wengi hujitupa katika eneo la kucheza kwa kujiachia. Cuban Marimba ni moja ya bendi iliyokuwa ikipiga muziki kwa utaratibu huo, na muziki unapofika hatua ile ya tatu ya kuchangamka ndipo Juma Kilaza hukoleza muziki zaidi, kwa vionjo vyake vya rap alivyokuwa akivitumia kama Pwaga Pwaga Pwaga Pwaga weka ngoma chini na kuwapagawisha wapenzi wa muziki.

    Muziki huu ulipata wapenzi wengi sana katika eneo hili la Afrika Mashariki na ya kati. Lakini wakati wanamuziki wa Kongo wanauendeleza muziki huu wa rumba, kwa kuupatia vionjo vya asili. Wanamuziki wengi wa  Tanzania hawakufanya hivyo. Kwa sasa muziki wa rumba wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo unatambuliwa na UNESCO kama muziki wa asili wa nchi hiyo (UNESCO:2021), wakati ule wa Tanzania kama umedumaa ama kudorora.

    Hii ni kwa kuwa wanamuziki wa Tanzania, badala ya kufanya jitihada kama zile za wenzao wa Kongo, wao ndio kwanza wakahama kutoka kuiga muziki wa santuri za GV toka Cuba na maeneo mengine ya Marekani kusini na kuanza kuiga ule wa Kongo. Hali iliyodumaza kukua kwa muziki wa rumba nchini.

    Hata hivyo, wapo wanamuziki wachache ambao hawakupenda hali hii ya kuiga muziki wa kigeni moja kwa moja na hata kuthubutu kuikemea. Kilaza ni miongoni mwa wanamuziki hao wachache ambao tangu awali hawakuwa wakiiga muziki wa Kongo, ama kutoka kwingine kokote. Mwanamuziki huyu, alijijengea sifa kubwa na hata kutambulika kama mmojawapo wa wanamuziki nguli wa muziki wa rumba, kuwahi kutokea nchini Tanzania. Kilaza alivuma sana, hasa kuanzia mwaka 1969 alipokuja na mtindo wa Ambiyansey akiwa na bendi ya Cuban Marimba na kuwa mwanamuziki wa kwanza wa rumba Tanzania kurap kwenye tungo zake. Umaarufu wake ni wa kutukuka, tarehe 26 Aprili Mwaka 2015 Cuban Marimba ilipata tuzo ya miaka 50 ya muungano kutoka kwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya nne. Tuzo hiyo ilitolewa kama alama ya kuutambua

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1