Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Pili, #2
Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Pili, #2
Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Pili, #2
Ebook1,339 pages18 hours

Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Pili, #2

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kitabu hiki MNNNMA ni kiberiti kinacho washa moto wa mabadaliko makubwa, na kama siyo mapinduzi ndani ya kanisa lote linalo zungumza Kiswahili. Katika hiki tunaona mtizamo mpya wa theolojia, changamoto katika tafsiri za biblia ndani ya lugha ya Kiswahili, na jipya zaidi ni uhamisho wa waumini toka udini kuelekea mahusiano na Mungu YHWH.

Kitabu kinachukulia biblia yote kuwa fumbo la picha, na hivyo kutumia mstari wa wakati uendao mbele katika mduara, kuonyesha mwanzo hadi mwisho wa kila kitu. Na kama hili halitoshi, kinaweka dai tatanishi kwamba, biblia yote iliandikwa kwa ajili ya ukombozi wa Adonai Yeshua Kristo, na kwamba yote humo pamoja na maisha yako yote, ni kwa ajili ya Mungu YHWH kuwa na familia yake tu.

Kitabu kinacho dai tete la kuifunua kweli iliyo moja na ya pekee mahali pote, wakati wote, na kwa vizazi vyote. Na katika kunogesha uelewa; kinapinga mafundisho yaliyo zoeleka kwamba, mtu ataishi Mbinguni na Mungu milele, kwa kudai maandiko yote yanasema, ni Mungu YHWH anaye hamia katika Dunia mpya ndani ya Yerushalem Mpya kuishi humo milele na watoto wake watakatifu.

Kitabu kinajikita katika malumbano ya kidini na sayansi, na kuitumia teknolojia ya sasa kuelezea dhana nyingi za kiimani. Na kwa kila funzo la kinadharia unalo pewa, pia huonyeshwa jinsi ya kutenda hilo uhesabiwe mstahiki wa ahadi hiyo ya Mungu. Na katika ujasiri mkuu kinaweka dai ya kuwa, hicho ni ujumbe halisi wa Mungu YHWH kwa kanisa lake tukufu linalo zungumza Kiswahili.

Ni kitabu ambacho kila anayefunza dini hawezi kukikosa, na kwa kila mtu anaye taka kujua kweli ya mambo ya kiungu, hiki ni kitabu muhimu zaidi sokoni kwa sasa. Tunakiona kutawala malumbano katika kumbi za mihadhara, mimbari za masinagogi, na hata madarasani kufunzwapo dini. Ni kitabu ambacho kitafungua jicho la kila muumini, kwani katika lugha ya Kiswahili hakipo kinacho zama katika kina chake hiki. Kwa kweli uhamsho wa kanisa linalo zungumza Kiswahili sasa umefika wakati wake!

LanguageEnglish
Release dateJan 29, 2023
ISBN9798215047187
Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Pili, #2
Author

Shannel S Silwimba

Ana elimu ya chuo kikuu, na amehudumu kwa miaka 25 katika makampuni 3 ya kimataifa akiwa mkuu wa idara. Anao uzoefu katika sekta ya kilimo biashara, usindikaji, uzalishaji viwandani, na usambazaji wa bidha za chakula na mafuta.

Related to Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe

Titles in the series (1)

View More

Related ebooks

Religion & Spirituality For You

View More

Related articles

Related categories

Reviews for Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe - Shannel S Silwimba

    Tahariri

    Yeshayah 50:4

    Adonai YEHWIH amenipa mimi uwezo wa kuzungumza kama mtu msomi, ili kwamba mimi, kwa maneno yangu, nijue jinsi ya kumkidhi aliye choshwa. Kila asubuhi yeye huyahamsha masikio yangu kusikia kama yale ya msomi. [Tafsiri ya Complete Jewish Bible].

    Wagalatia 1:12,16,20

    Kwani mimi sikupokea hili toka kwa mtu, wala mimi sikufundishwa [hili], bali ni kwa ufunuo wa Yeshua Kristo ... Kumfunua Mwana wake ndani yangu, hata niweze mfundisha yeye kati ya Mataifa; saa hilo sikushauriana na wenye mwili na damu: ... Na sasa haya mimi ninayo andika kwenu, tazama, mbele za Mungu, mimi sisemi uongo.

    Matendo 5:38-39

    Na sasa mimi nasema kwenu, jizuieni toka watu hawa, na waacheni wenyewe: kwani kama huu ushauri au kazi hii ikiwa ni ya watu, haitaishia kuwa lolote lile: lakini kama ikiwa ni ya Mungu, nyie hamwezi ipindua; tena isije kutikana nyie mwapigana na Mungu.

    Unabii – 30 Mei 2007

    N ajimimina nafsi yangu ndani ya kitabu. Watu hawatasoma kitabu, watakuwa wakinila MIMI (kwani MIMI ndiyo kitabu). Watu watakula kitabu na hawata-kisoma (na watakihisi kile walacho ndani ya tumbo lao). Utukufu wangu utakuwa bayana ndani yao, watajua kuwa ni MIMI. MIMI, MIMI naongea kwao na wao watakubali na kukombolewa...

    Hili Tunasema Sisi

    Pale Jenerali anapo mpa askari wa daraja la chini kabisa ujumbe kufikisha kwa makamanda vitani, amri hiyo hutangulia zote, na kwayo askari huyo hubadilika daraja mpaka aufikishe ujumbe. Na kwa ujumbe huo, mpangilio mzima, na mwenendo mzima wa jeshi vitani hubadilika.

    Dibaji

    Mpendwa, jina la kitabu chako hiki ni MWANA-ADAM NI NANI NAYE NI NINI MUNGU AMKOMBOE (MNNNMA). Kwa minajili ya kuufikia umma wote wa wanao zungumza Kiswahili tulio tumwa kwao, tuli-kichapisha pia katika vijitabu vidogo tokea baadhi ya masomo yake. Kwa uelewa huu basi, kama mpendwa unacho kimoja wapo ya hivi, tambua kwamba huo siyo ujumbe wote unao kustahili kuupokea.

    Tunasema hivi sababu kitabu MNNNMA kimegawanyika katika vyuo vitatu vikupasavyo mpendwa kuhitimu: CHUO CHA KWANZA hufunza kuhusu Mwanzo Mtakatifu & Kuingia Dhambi. CHUO CHA PILI hufunza kuhusu Fumbo La Ukombozi & Ufunuo wa Ukombozi. CHUO CHA TATU hufunza kuhusu Mwisho Mtakatifu & Kuondoka Dhambi. Hivyo ni ushauri wetu umiliki kitabu chote cha (1) MWANA-ADAM NI NANI NAYE NI NINI MUNGU AMKOMBOE.

    Lakini kama hivyo sivyo kwako, basi uanze na (2) CHUO CHA KWANZA, ndipo kifuatie (3) CHUO CHA PILI, na ndipo umalizie na (4) CHUO CHA TATU. Na kama hata hivi sivyo ilivyo kwako, basi acha tukuvutie kwa baadhi ya masomo ndani ya MNNNMA tuliyo yatoa kama vitabu huria ifuatavyo: -

    5)  Historia na Maisha ya Yeshua Kristo

    6)  Jinsi ya Kusali & Kuongea na YAHWEH

    7)  Utatu Mtakatifu

    8)  Mafundisho ya Utajiri

    9)  Mafundisho ya Ndoa

    10) Ufufuo na Uchukuo

    11) Yisrael

    12) Ujio wa Pili wa Yeshua Kristo

    Pamoja na hivi ni kile tunacho kisambaza bure katika masoko ya vitabu mitandaoni, kinachoitwa Milenia ya Kristo. Lengo la hiki ni kuwatambulisha kazi ya MNNNMA wale wote wanaoishi ughaibuni, lakini wanaongea Kiswahili. Kwa jinsi hii, hawa pia wapokee ujumbe wao, kupitia umiliki wa kitabu MNNNMA.

    Kitabu hiki MNNNMA kinaleta habari njema kwa kanisa zima linalo zungumza Kiswahili. Kitabu chako hiki kinaifumbua hadithi ya fumbo la nyakati, na pamoja nalo hilo, kinategua kile kitendawili cha kale, pale malaika walipo muuliza Mungu: ... Je mtu (anaye kufa) ni nini, ambaye wewe unamjali hivi? Na mwana wa adam, ambaye wewe humtembele? Kwani wewe umemfanya yeye chini kidogo ya elohim (malaika), na {bado} umemzinga na taji la utukufu na heshima. Wewe umemfanya yeye kutawala juu ya kazi za mikono yako; wewe umeweka vyote chini ya miguu yake: ... [Zaburi 8:4-6].

    Ni ndani ya fumbo hilo la nyakati, na uteguzi wa kitendawili hicho, ndimo historia yote ya mtu na ukombozi wake vilihifadhiwa kwa umahiri na umakini usio pimika. Kwayo haya mguso wake ulifika mapema, lakini ni uandishi kadri tunavyo pokea (Uandishi Kimapokezi - Inspiration) ulio anza rasmi katika mwezi wa Mei 2007 mpaka Oktoba 2007. Uandishi huo ulifanyikia katika meza ya chakula, tena ulikuwa wa tokea mwanzo wa kitabu mpaka mwisho wake, kwa kadri ya uono wetu hafifu wakati huo. Ujalizi wa Mapokezi (Authorship) ulianza Oktoba 2007 mpaka Augusti 2011, na ndiyo ulio tupatia mgawanyiko wa vyuo, masomo, na mada ambazo mpaka leo bado ziko ndani humu.

    Uhakiki wa Kitabu (Review) ulianza tokea Agusti 2011 mpaka Oktoba 2014. Lengo lake hili lilikuwa kuhakikisha uchambuzi wa ndani kabisa wa yaliyo pokelewa, unalandana na maaandiko. Hakika hiyo kwisha kupatikana, ndipo tuliingia katika hatua ya Uhariri Fasihi (Editorial – Literature) kusahihisha majalizi yaendane na mapokezi, pamoja na maandiko. Hili lilifanyika tokea Oktoba 2014 mpaka Desemba 2016. Tukiwa sasa tunacho kitabu makini mbele zetu, ndipo Uhariri Fasaha (Editorial – Fluent) wa usomekaji ulifanyika tokea Desemba 2016 mpaka Septemba 2021. Kama biblia ilivyo, kitabu hiki nacho kimeandikwa ili kisomwe mbele za watu.

    Katika juhudi za umakini wa kufikisha mapokezi, ilituwia vema kwamba, sasa wakati umefika wa uwepo wa Biblia Fasaha, na hivyo misingi yake ilianza kusimikwa kwa sisi kufanyia Tafsiri Maandiko (Translation) yote ambayo tayari yameshaingia kitabuni. Na hili lilituchukua sisi kipindi cha tokea Septemba 2021 mpaka Aprili 2022. Na kwisha hilo, ndipo hitimisho la kazi hii lilifika kwa Usanifu na Kibali (Ratification), ulio anza mara moja Aprili 2022 na kukamilika Novemba 2022. Ndipo sasa kikawa tayari kupigwa chapa, hata leo hii kiwe mkononi mwako mpendwa.

    Juhudi zote hizi katika uandishi wake kitabu chako hiki, zilikuwa ujenzi juu ya msingi ule-ule wa awali, kwani yote yale ambayo tulipokea, yalibakia kama yalivyo na pale-pale yalipo wekwa kwa upokeo wa awali. Katika miaka yote hii 15 na miezi 6 tuliyo kuwa katika uandishi wa kitabu chako hiki, sisi kwa binafsi yetu tulipokea makuzi makubwa sana, ili kuinuka hadi kufikia upeo wa uelewa ambao YAHWEH anautaka katika Kanisa lake tukufu linalo zungumza Kiswahili. Hivyo tulijifunga kwa uadilifu kwayo mafunzo hayo, na kwa miaka 12 ya awali tulitumia takribani masaa 3 kila siku (part-time), na takribani masaa 10 (fulltime) kwa kipindi kilicho bakia mwishoni.

    Sisi tunaamini: kipindi chote hiki tulicho chukua, ni kwa ajili ya sisi kuinuka katika uelewa uhitajikao kupokea kitabu kile kilichopo katika masijala za Mbinguni, hata kiwe pacha na hiki kilichopo mkononi mwako leo hii. Katika vyote na yote ndani humu, tafadhali sana mpe sifa na utukufu Mungu YAHWEH pekee.

    Utangulizi

    Watangulizi wetu wameshafanya kazi itakiwayo, kwamba sasa majani ni makavu, na kinacho hitajika ni kiberiti tu. Hiki kitabu cha MNNNMA ndicho kiberiti kwa ajili ya mapinduzi ya upendo, na uamsho mkuu ujao. Hivyo kwako wewe usiye mtu kati ya watu, YAHWEH ameiinua sauti yako isikike ndani ya Kanisa lake duniani. Tazama, mboni ya jicho lake amegeuka kukutizama akishang’aa, ni nini hicho Elohim wake afanyacho nyumbani mwako.

    Ndani humu utakutana na tafsiri fasaha za maandiko matakatifu tulizo zifanya, tulikuwa hatuna budi, bali kufanya uchokozi huo wa hadharani kudhihirisha changamoto tulizoziona. Tunajua vema, hili limetonesha lile hitaji nyeti la sisi kuwa na tafsiri ya Kiswahili fasaha kitumikacho leo hii katika nyanja zote za maisha. Kuelewa hili, tafadhali tazama mfano kwa mstari Askofu Alpha Mohamed wa kanisa Anglikana (zamani hizo wa Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro), alio utoa kwa familia ya mmoja wetu, alipo watembelea katika udogo wake: -

    Hili andiko (na hususani kwa mapanuzi yake yote tokea tafsiri ya Amplified Bible juu), kwake lilikamilika ndani ya MNNNMA. Hili andiko siku ile lilipo somwa kwa tafsiri ya kwanza, na kutaja ‘ mambo makubwa, magumu usiyo yajua ’ lilitisha sana. Lakini ni mpaka nyakati za kazi ya MNNNMA, ndipo alipo gundua nini haswa lilikuwa likifanyia unabii maishani mwake. Hii ni zaidi ya miaka thelathini (30) kupita ndipo baadaye kabisa aligundua ni ‘ mambo makubwa na makuu, yaliyo ndani ya wigo na yamefichwa, ambayo wewe hujui.’

    Mpendwa, maandiko matakatifu siyo jiwe lilokufa, kwani yako hai kama jamii yenyewe. Tokea humu utasikia yakinguruma tena kudai vazi jipya, ili kuzigusa tena nyoyo za walio wake. Neno ni lile lile, ila lugha imekuwa na kusonga mbele zaidi. Kila kizazi huifunua historia yake, hisia zao, utamaduni wao, kwa maana nzito zibebwazo ndani ya maneno watumiayo kila siku kuwasiliana.

    Umakini wetu kwalo hili ni wa kugusa kitakatifu, hivyo juhudi za dhati zilitumika kurejelea asili ya andiko kwa Kiebrania, kukimbia itikadi na falsafa za watu, na urejesho wa majina asili ya wahusika. Katika kufanya haya, tulitumia lugha kwa sarufi fasaha kufanyia tafsiri. Kupitia unyambulisho tumebebesha nafsi halisi ihusikayo, wakati, na kwake nani hilo lasemwa. Tumetambua kijadiliwacho (contextual meaning) katika kuzingatia kwa makini maana halisi ya neno, na hivyo ujumlisho wa maneno yote yatumikayo katika mstari (sentensi) kuleta maana kamilifu ya andiko.

    Ndani humu yako maeneo ambako mguso ulikuwa mkubwa, na hivyo uandishi kufuata mtiririko kadri ujavyo pasipo kujali lolote lile. Katika kuenenda huko, yako ambayo yametushtua sisi kama ambavyo yataitikisa roho yako pia. Katika yote humu, hakuna linalo tishia kujali kwetu, kama sisi kukosea kweli yake pasipo kujua, na kwa kufanya hivyo sisi kuishia kukukosesha wewe mtoto wake mpendwa.

    Katika fikra hizi, sisi hutamani haya yote yangebaki na sisi pekee yetu, pasipo uhusisho wa kanisa lake hili lote. Kwa sababu hii, wito wa kazi hii sisi tuliuchukulia kwa kujali sana, ili baada ya yote yeye Mungu, na siyo mtu, afurahishwe sana na utendaji wetu. Milolongo ya uhakiki na uhariri ni kwa ajili ya hili zaidi, kuliko yote mengine.

    Mpendwa, kazi hii pamoja na kuwa tendo la kiimani kwao walio amini pekee, lakini bado yabaki kuwa vyuo makini sana kwa kila mkufunzi na mwanafunzi wa neno lake. Kitabu kilikuja kiwe uwanja wa wasio amini katika kumpokea Adonai (Bwana) Yeshua[1] (Yesu) kama Kristo (Mfalme) na Mkombozi wao. Pia pasipo mapungufu yeyote, hiki ni waraka wa barazani katika malumbano na wasio amini kwa nini YAHWEH ndiye Mungu pekee, hata astahili kuabudiwa. Na kana kwamba hayo hayatoshi, kitabu hiki kimeandikwa kiwe msingi wa theolojia wa kanisa linalo zungumza Kiswahili, kwani chafaa kwa marejeo (referencing), na machambuzi ya kitaaluma, ili sote tuwe na maarifa na hekima.

    Kitabu chako hiki hakifungamani na dhehebu lolote lile, au kuafiki uwepo wa njia nyingine ya kumfikia Mungu YAHWEH, zaidi ya Mwana wa Mungu Adonai Yeshua Kristo pekee. Tunakubali ni Wakristo na Yehudaizimu (Judaism) pekee, ndiyo wenye nafasi ya kuwa na mahusiano na Mungu YAHWEH. Adonai Yeshua Kristo hakuleta dini au dhehebu duniani, bali mahusiano kamili na Mungu YAHWEH. Na kwamba kweli iko moja, na ya pekee kwa wote ulimwenguni, wakati wote, na mahali pote, kwa vizazi vyote milele. Kitabu chako hiki, kimekuja ili kuifunua hiyo kweli moja na ya pekee.

    Sasa kwako mpendwa usiye wa imani hii, njoo uchungue uone kati ya hilo lako na hili letu, lipi waona ndiyo kweli? Njoo wewe uliye jasiri wa dini nyingine ujipimishe uelewa wako na kweli hii. Usiogope njoo, kwani Yeshua wetu alituagiza tukupende kama tunavyo jipenda wenyewe. Tazama, tutakupokea kwa heshima na taadhima pasipo kukuudhi, au kuikera roho yako. Tutakukaribisha tukae kitako kujadili kwa urahisi maswali haya sugu, tokea historia ya mtu: -

    Kwa nini wewe uliumbwa? Uliumbwa ili iwaje? Kwa nini aliumba mwanamme na mwanamke? Hivi ni kweli kwamba sisi tulikuwa manyani kabla ya kuwa watu?

    Kwa nini ukombozi? Kwa nini Mungu asimteketeze satani mara moja, na wote tukarudia kuishi watakatifu raha mustarehe milele?

    Na wapi katika dini yako pameandikwa kinaga ubaga pasipo kupinda, vipi wewe waweza kombolewa ili kwenda Mbinguni? Nisomee huo mstari ulipo kitabuni mwako nami niujue?

    Je maisha ya milele ni kweli? Je gehena (jehanamu) na Mbinguni ni mahali pa kweli? Mtu akifa ana kwenda wapi? Akiwa huko ana fanya nini? Wapendwa wangu walio tangulia katika mauti wako wapi, na wanafanya nini leo?

    Hivi ufufuo na uchukuo wa wafu ni kweli utakuwepo?

    Nani ameandika maandiko matakatifu? Kwa nini yaaminike? Je kupo ambako yanapingana?

    Je ni sahihi kuwa na wake wengi au waume wengi? Ipi ni ndoa ya kwanza? Nini maana ya tunda la mti wa kati? Na je talaka ni sahihi?

    Mpendwa, thubutu kufika mwishoni mwa kitabu chako hiki MNNNMA na uone ni finyu vipi maswali haya, kwa mlinganisho na maarifa na hekima utakayo hitimu.

    Neno ukombozi ni neno la kisiasa, na ndiyo sababu sisi tulisonga mbele na kulitumia kwa ujumla wake katika maana nyingi zaidi, na zilizo sahihi zaidi katika nyakati hizi za mwisho. Tumelitumia kutafsiri maneno ‘Salvation’ na ‘Redemption’ kumaanisha ukombozi ulio tufikia kupitia kazi aliyo ifanya Adonai Yeshua Kristo, mpaka kuikamilisha hapa duniani.

    Katika mila na desturi za Kiebrania, majina ya watu au mahali hubeba wasifu wa huyo au hapo. Hivyo jina lako hubeba asili yako (roots), tabia zako (prophetic behaviours), desturi zako (tribal, nation affiliations), visifa vyako (attributes), wasifu wako (personality) na hata imani yako (religion). Ni kwa sababu hizi, juhudi za dhati zinafanyika ndani humu kuhakikisha majina asili yote yanarudishwa mahali pake.

    Katika kufanya hivi, tutajitenga pia na wasifu za wahusika wa biblia tokea simulizi nyingine zisizo za imani hii ndani ya lugha ya Kiswahili. Hili ni jambo muhimu sana kwetu katika kuchunga usafi wa wasifu zao kwa kadri ya biblia na siyo vinginevyo. Lahaja ya Kiebrania yalandana sana na ya Kiswahili, hata majina hayo kuandikwa kama yalivyo pasipo tatizo lolote kisarufi au kiisimu.

    Sisi hujiuliza sana hili, hivi ipo shida gani kwa kanisa unaye zungumza Kiswahili kusali kwake katika jina ambalo yeye mwenyewe, alimsikia mama yake mzazi akimwitia hilo? Kwa lafudhi ya sauti ileile malaika aliyo agiza hivyo ndivyo wamwite? Jina ambalo hata Baba humwita leo akisubiria lile jipya! Ujadilifu huu hatari haumaanishi kwamba nguvu iko katika jina gani, la hasha! Wewe mwite lolote; Yeshua, Yesu, Yehoshua, Jesus, Yesus, Mungu anaijua dhamira yako nani huyo imwitaye. Maana ya jina Yeshua (Yehoshua) la Kiebrania ni ‘Mkombozi.’

    Kwa kuwa sasa wajua jina linawakilisha nini, sasa sikia haya. Lugha ya Kiswahili inalo chimbuko lake tokea lugha ya Kiarabu. Waarabu kama walivyo Waebrania, wote ni wana wa Shem (shemitic). Ni kwa sababu hii kila unaposikia katika katika vyombo vya habari vya kimagaribi wakitaja Waarabu ni ‘anti-semitic,’ yaani ‘wanapinga uzao wa Shem,’ basi tambua huo ni ujinga wa kukosa maarifa (oxymoron). Ni tokea mahusiano haya ya Kiswahili na Kiarabu (semitic), ndiyo matamshi yako Mkristo huonyesha ijumaa kuwa siku ya saba (7) kwa kadri ya dini yao, na siku ya Shabath (iliyo siku ya 7) kuitwa siku ya kwanza ya juma (yaani jumamosi).

    Hivi kitu gani kinazuia hata kalenda za kanisa kuchapishwa zikionyesha Shabath yaani jumamosi, ndiyo siku ya mwisho ya wiki? Hauko ubishi katika Ukristo kuwa; Jumapili siyo siku ya kwanza ya wiki. Waumini wote tunajua, kuwa ni Elohim mwenyewe aliyeipa siku ya saba (7) jina la Shabath, na zote nyingine akizitaja kwa namba ya siku hiyo katika wiki ni ya ngapi. Hivyo ni siku hii pekee yenye jina!

    Sasa sikia wewe kanisa unaye zungumza Kiswahili: Tengeneza kalenda yako ionyeshayo siku za wiki kwa kadri ya maandiko kuwa: Sikumosi (jumapili) - Sikupili (jumatatu) - Sikutatu (jumanne) - Sikunne (jumatano) - Sikutano (alhamisi) - Sikusita (ijumaa) na - Shabath (jumamosi). Hivi ndivyo yeye alivyo taja ilivyo, hivyo ndivyo pia sisi watoto wake tutaziita siku. Pia hivi ni makini zaidi, sababu usemapo ‘juma’ humaanisha ‘wiki’ ambalo ni siku 7, lakini usahihi ni ‘siku’ ambayo ni masaa 24 tu. Leo wewe umesikia, hivyo anza kuongea hivi, na hata sisi tutafanya hivyo humu, kudhihirisha kwamba inawezekana kabisa.

    Tokea kina cha uelewa huu, ni ushawishi wetu kwako mpendwa kuwa, Mosheh (Moses) siyo Musa, Shelomoh (Solomon) siyo Selemani, Yosef (Joseph) siyo Yusuf, Yahkob (Jacob) siyo Yakubu, Yitzhak (Isack) siyo Isaka, David (David) siyo Daudi, Iyob (Job) siyo Ayubu, Noakh (Noah) siyo Nuhu, Yeshua (Yesu) siyo Issa, na mengi mengine. Uwepo wa simulizi mbili tofauti juu ya jina moja kwenye mihadhara mitaani, huchanganya waumini. Nenda sasa na ukajitofautishe, hata wao wajue wewe ni wa Mungu YAHWEH katika Adonai Yeshua Kristo pekee.

    Shuruti tuwafunze watoto wetu tokea udogo wao kabisa kwamba: Mungu wa Abraham, Yitzhak na Yahkob, ndiye Baba wa Yeshua Kristo. Hivyo Yeshua Kristo ni Mwana wa Mungu aitwaye YAHWEH. Yeshua Kristo pia yeye ni nafsi Mwana katika Mungu huyo YAHWEH. Na tokea yeye huyu Mungu mmoja, ziko nafsi tatu maarufu kwetu; Mungu Baba (akiwa kichwa kati yao), Mungu Mwana (Adonai Yeshua Kristo), na Mungu Ruak HaKodeshi (Roho Mtakatifu). Mungu Mwana, yaani Adonai Yeshua Kristo, ndiye aliye kuja duniani katika mwili, na kufa mauti ya aibu ya msalaba kwa ajili ya ukombozi wetu. Siku ya tatu alifufuka, na siku ya arobaini (40) baadaye alipaa kurudi Mbinguni. Na huko amekalishwa mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Baba Mungu. Kinyume na hivi ni uongo, siyo biblia, na wala siyo Ukristo.

    Kitabu chako hiki kinawalenga wana-adam wote, tena zaidi-zaidi wale wote walio wana wa Mungu YAHWEH, yaani wale tu walio zaliwa mara pili, hata awaite watakatifu wake (saints). Hivyo shabaha kubwa ni kwao wahudumu wake, yaani maaskofu, mapadri, wachungaji, wainjilisti, watawa, watumishi, wahubiri, wazee wa sinagogi, walimu wa dini wa shule za msingi, shule za sekondari, vyuo na seminari. Pamoja nao hawa, ni wewe mwanafunzi na mkufunzi wa neno lake, na waumini wote wanayo itafuta kweli kujilisha kwa makuzi yao. Pia ni wewe usiye wa imani hii, lakini uko hapa kujua kweli ni ipi. Karibuni sana!

    Kitabu hiki hakibaki kwenye nadharia pekee, la hasha, kwani kinaongoza na kuelekeza uponyaji kwa walio hospitalini, kinaleta faraja na uhuru kwa walio kifungoni magerezani, hupanua wigo wa uelewa na hivyo utajirisho na mafanikio kwao wakulima, wavuvi, wafanya biashara, na wafanyakazi. Pia kinasimama kama ushahidi na changamoto kwa wapinzani wa kweli hii, na wale wote wasio amini bali wapendao kujua nini sisi tunaamini. Na mwisho ni kwako msomi utafutaye maarifa bila kujali itikadi au imani, kama baadhi wafanyavyo hata sasa.

    Tazama mpendwa, tukisha maliza kulumbana, kuchekana, na kukashifiana; bado suala hubaki lile-lile moja tu: Je nikifa leo, mimi nitakuwa mgeni wa nani huko niendako? Na kikubwa zaidi hapa; ni hakika ya jibu lako hilo kuwa ndiyo sahihi, na siyo ulaghai wa ibilisi satani. Tafakari ...

    Kitabu chako hiki MNNNMA pamoja na mapokeo binafsi, ni mkusanyiko wa mafunuo waliyo pokea kaka na dada zetu wengi wengine katika Kristo Yeshua. Hao waliandika au kuzungumza, na Ruak kuleta kazi zake za awali katika usikivu wetu. Kutoa shukrani kwa kila mmoja wao humu, kunahatarisha dhana nzima ya umiliki wa kazi hii kuwa wa YAHWEH. Hayuko mshiriki pamoja naye katika hili, kwani sote tu vyombo tu alivyo tumia kukufikia wewe mpendwa wake. Pale mmoja wetu afunuliwapo kweli duniani, wote hupokea kweli hiyo moja kana kwamba sisi ni wao, na wao ni sisi.

    Tokea uelewa huu, na upendo wetu sote kwa Adonai wetu Yeshua Kristo; hapa linatolewa ombi rasmi kwa pamoja kutumia michoro, picha, majedwali, takwimu, ramani, na vyote vingine vitakavyo tumika tokea vyanzo mbalimbali duniani. Hivi vyote vimesaidia kuifikisha kweli yake kwetu sisi tulio wa mwisho kati ya kaka na dada zetu. Kama tukisema maombi na shukrani zitolewe kwao wote hawa, itachukua kitambo, na pasipo utoshelezi. Hivyo basi: Katika jina la Adonai wetu Yeshua Kristo, tunakuomba Baba Mungu, ukawajali hawa wote, na kuwajulia hali zao, kwa kadri ya kazi zao kwake Mwanao Yeshua Kristo. Amin

    Kitabu kinatumia mfumo wa nguzo za zizi katika kufikisha ujumbe wake, badala ya ujenzi wa ukuta uletao matengano kwa waumini. Mfumo huu wa zizi hakubali uwepo wa kile kinacho onekana kama mgongano wa maandiko katika biblia, tokea upungufu wa uelewa makini wa yote kanisani. Hivyo kama mjenzi wa zizi anaye pigilia nguzo huku na kule, ili kondoo wakae salama ndani mwake, ndicho sisi pia tufanyacho. Ujenzi wa ukuta katika maandiko hupelekea siasa kali, na migawanyiko kundini kama ile ya kimadhehebu.

    Mpendwa, vidole vyako vitaendelea kufungua kurasa za kitabu ambacho sicho cha kizazi hiki, bali cha kile kijacho. Kila ufunguapo ndivyo ulavyo akili, nia, na hisia za Elohim wako. Kama waridi lijifunguavyo alfajiri na mapema, ndivyo kweli na utukufu utakavyo mwagwa na Ruak HaKodeshi ndani mwako kadri ulavyo. Hata sasa Ruak HaKodeshi anao moto uwakao ndani yako pasipo uteketezi.

    Mungu Baba, katika jina la Adonai Yeshua Kristo, nakuomba, hekima, maarifa, uelewa na imani tokea haya uliyo yafikisha leo mbele za macho yangu mimi kusoma. Naomba unifungue macho yangu ya kiroho nione, na masikio yangu ya kiroho nisikie, na niamini kweli yako. Amin

    Faharisi

    [I dadi ya kurasa hizi ni kwa kadri ya fonti ya Calibri 11, kwa ukubwa (size) wa A4, na kwa upana-urefu (margin) wa kawaida (moderate), zilivyo tumika katika uandishi. Mabadiliko yanatokana na chaguzi za Wachapishaji].

    Chuo cha Kwanza

    Mwanzo Mtakatifu & Kuingia Dhambi

    1.  Mwanzo wa Yote

    1.1  Yahweh Katika Milele [14-36]

    1.2  Kuumbwa kwa Roho na Nafsi Mtu [36-39]

    1.3  Kufanywa kwa Mwili Mme na Mke [39-52]

    2.  Mpango wa Ukombozi

    3.  Uasi na Kuingia Dhambi Duniani

    3.1  Tafsiri ya Uasi na Dhambi [59-60]

    3.2  Asili ya Uasi na Dhambi [60-65]

    3.3  Kudanganywa kwa Havaa na Uafiki wa Adam [65-70]

    3.4  Dhana ya Dhambi ya Asili [71-74]

    4.  Agano la Ukombozi

    4.1 Agano la Yahweh na Abraham [78-87]

    4.2 Kafara ya Yitzhak Ndiyo Kafara ya Yeshua [88-98]

    Chuo cha Pili

    Fumbo la Ukombozi & Ufunuo wa Ukombozi

    5.  Toraha ya Yahweh na Ufunuo wa Dhambi

    5.1.  Toraha ya Mosheh [107-111]

    5.2.  Amri ya Upendo [111-115]

    5.3.  Malaika Kazini [115-129]

    6.  Umfano na Mlinganisho wa Yisrael na Kanisa

    6.1.  Utumwa wa Yisrael Misri – Utumwa wa Dhambi Leo [143-146]

    6.2.  Kuinuliwa kwa Nyoka Jangwani – Kuinuliwa kwa Yeshua Msalabani [146-148]

    6.3.  Tabanako la Mungu Jangwani – Yerushalem Mpya [148-154]

    6.4.  Kuhani Mkuu Mlawi - Yeshua Kuhani Mkuu wa Milele [154-159]

    6.5.  Kafara za Wanyama – Kafara ya Mwanakondoo wa Mungu [159-164]

    6.6.  Mizoga ya Kafara Nje ya Kambi – Mauti ya Yeshua Nje ya Yerushalem [164-170]

    6.7.  Pazia la Hekalu – Kanisa Lisilo Pazia [170-174]

    6.8.  Miaka 40 ya Yisrael Jangwani - Siku 40 za Yeshua Jangwani [174-177]

    6.9.  Ufufuo na Uchukuo Agano la Awali – Ufufuo na Uchukuo Agano Jipya la Mwisho [177-186]

    6.10.  Mitzvot za Mosheh – Mitzvah ya Yeshua [187-191]

    6.11.  Kuhesabiwa Haki kwa Matendo - Kuhesabiwa Haki kwa Imani [191-200]

    6.12.  Historia na Maisha ya Yeshua Kristo [200-259].

    7.  Jinsi ya Kupokea Ukombozi

    7.1.  Sala ya Ukombozi [262-273]

    7.2.  Kubatizwa kwa Maji na kwa Ruak Hakodeshi [273-292]

    7.3.  Kujiunga na Sinagogi [292-303]

    7.4.  Jinsi ya Kujifunza Maandiko Matakatifu [304-315]

    7.5.  Jinsi ya Kusali kwa Usahihi [315-343]

    7.6.  Kuongea na YAHWEH [343-379]

    7.7.  Utatu Mtakatifu [379-440]

    7.8.  Meza ya Adonai na Agano Jipya [440-483]

    7.9.  Mafundisho ya Utajiri [483-571]

    7.10.  Mafundisho ya Ndoa [571-641]

    7.11.  Wito wa Kazi ya Adonai [641-654]

    7.12.  Mafundisho ya Kifo 654-701]

    Chuo cha Tatu

    Mwisho Mtakatifu & Kuondoka Dhambi

    8.  Ukamilifu wa Upendo & Ukombozi

    8.1.  Ukamilifu wa Ukombozi - Kiroho & Kimwili [706-714]

    8.2.  Ufufuo & Uchukuo [715-778]

    8.3.  Miaka 7 ya Kanisa Mbinguni [778-794

    8.4.  Miaka 7 ya Tabu & Tabu Kuu Duniani [794-833]

    8.5.  Yisrael [833-878]

    9.  Ujio wa Pili wa Yeshua Kristo

    9.1.  Hekalu la Tatu [883-942]

    9.2.  Vita vya Harmagedoni [942-967]

    9.3.  Wasifu wa satani lucifer & mpingaKristo [967-1003]

    9.4.  Hukumu ya Watakatifu [1003-1009]

    9.5.  Utawala wa Miaka Elfu [1009-1038]

    9.6.  Vita ya Pili ya Gog & Magog [1038-1042]

    9.7.  Hukumu ya Wasio Amini [1042-1053]

    10.  Maisha ya Milele

    10.1.  Dunia na Mbingu Mpya [1057-1059]

    10.2.  Yerushalem Mpya [1059-1066]

    10.3.  Karamu ya Mwanakondoo [1066-1069]

    10.4.  Watakatifu katika Maisha ya Milele [1069-1071]

    10.5.  Watu Wapya [1071-1076]

    10.6.  Watakao Ishi Mbinguni [1076-1078]

    10.7.  Nia ya Mungu –Tokea Milele Hata Milele [1078-1080]

    Chuo cha Pili

    Fumbo la Ukombozi & Ufunuo wa Ukombozi

    CHUO CHA PILI kinalenga ku-kuonyesha mpendwa lipi ndilo FUMBO LA UKOMBOZI wako, na upi ndiyo UFUNUO WA UKOMBOZI huo. Fumbo ni kwa yale yaliyo fichwa tokea kusimikwa kwa misingi ya ulimwengu, wakati ufunuo ni kwa yale yaliyo kuja tambulika baadaye, na tena kwisha ukamilifu wake kupita.

    Ilisemwa hivyo kwa Yokhana 12:16 ... Mambo haya wafuasi wake hawaku-yaelewa awali: lakini pale Yeshua alipo pokea utukufu {alipo tukuzwa}, ndipo wao walipo kumbuka kuwa mambo haya yali-andikwa kumhusu yeye, na mambo haya wao wame-mtendea yeye. ...

    FUMBO LA UKOMBOZI wako ni yale yaliyo hifadhiwa katika wingi wa maandiko tuyaitayo agano la awali (kale), na UFUNUO WA UKOMBOZI ndicho tulicho kiita agano jipya la mwisho. Kwalo hili, yale ya siri kuu za nyakati zote, yalianikwa hadharani kwa wote wenye miili kuyatanabahi[2]. Hivyo agano la awali (tanakh[3]) lili-fumbia, na hili jipya la mwisho (injili), likafumbua (Marko 4:11, Warumi 16:25, Waefeso 3:9, Wakolosai 1:26).

    Kitabu chako hiki chote kilikuja, ili kuishuhudia kweli hii moja. Na kweli hiyo ndiyo Mpango wa Ukombozi, ambao ndiyo utekelezaji wa ile fikra ya awali ya yote, kupitia njia zake hizi zote, hata mwishowe yeye awe na familia yake mwenyewe (Yeshayah 55:8-9, I Wakorintho 2:16).

    5. Toraha ya Yahweh na Ufunuo wa Dhambi

    ... Kwangu mimi, ambaye ni mdogo zaidi ya aliye mdogo kati ya watakatifu wote, ndiyo hii neema ili-kabidhiwa, kwamba nihubiri {nitangaze habari njema} kati ya Mataifa utajiri wa Kristo usio chunguzika {usio julikana mwanzo wa asili yake}, Na kupelekea wote kuona nini [ndiyo] ushirika wa siri ya ajabu, ambayo tokea mwanzo wa nyakati ilikuwa imefichwa ndani ya Mungu, yeye aliye umba kila kitu kupitia Yeshua Kristo:

    Ili kwamba iweze kupelekea sasa kujulikana kwao wakuu na mamlaka {Waefeso 6:12, I Petros 1:10-12} katika [maeneo] ya juu, kupitia eklesia {kusanyiko[4], usharika[5], sinagogi[6], kanisa[7]}, wingi mkuu wa hekima za Mungu, kwa kadri ya kusudio lake la milele alilo lifanya yeye katika Kristo Yeshua Adonai wetu: Katika yeye sisi tunayo hakika na kibali {ruhusa} katika utegemezi wa imani yake. ... [Waefeso 3:8-12].

    Shuruti sasa wote tunajua kuwa, ni kwa uwepo wa mishpati[8] (elekezo, injili) ya Mungu, ndiyo wema au uovu hutambulika, pasipo hilo yote huwa kawaida tu (common). Kwa jinsi hii toraha ilishushwa duniani ikiwa mwalimu mkuu, kuitofautisha dhambi (sin) toka haki (righteous), na usafi (clean) toka najisi (unclean), na utakatifu (holy) toka asiye au kisicho kitakatifu (unholy).

    Hakika yake haya ni Warumi 7:7 ... Sasa sisi tuseme nini? [Je] Toraha dhambi? Mungu apishilie[9] mbali. Lakini {pasipo hiyo}, mimi nisinge-ijua dhambi, ila kupitia Toraha: kwani mimi nisinge-jua kutamani, isipo kuwa Toraha ilisema, wewe shuruti usitamani {Kutoka 20:17, Torati 5:21}. ...

    Ndani ya maandishi ya agano la awali, tuliona agano la Abraham likianzisha kile kilicho ahidiwa bustanini Eyden, kuhusu ukombozi wako mtu. Hivyo agano la Adam lili-pelekea hili la Abraham, kama nalo lilivyo pelekea hili la Mosheh (Moses), lihusulo toraha atufunzayo hapa. Toraha aliyo pewa Mosheh ni maelekezo (mitzvoth) 613: -

    Kuhusu mahusiano ya mtu na Mungu (divinity), na mtu na mtu (civic/ moral),

    Kuhusu kafara (rituals) na sherehe (moedim), na

    Kuhusu ukuhani (priesthood).

    Toraha ilifuatia ukamilifu wa ukombozi wao Yisrael toka utumwa wa Misri, na kamwe toraha haikuleta ukombozi huo. Kupitia hayo 3 juu ya toraha, ukombozi hubaki ndani yako, na kustawi katika tumaini la maisha ya milele, na siku za Mbinguni leo hii hapa duniani. Kwa kusema hivi tunakiri toraha hulenga kuleta mahusiano toka kwa mtu kumwelekea Mungu wake, wakati imani katika Kristo Yeshua, hugeuza mwelekeo wa mahusiano hayo kupitia agano jipya, kwani sasa hutoka kwa Mungu akiku-fuatilia wewe popote pale ulipo.

    Hivyo kwako wewe ambaye siyo Myisrael, wala bado kusali Sala ya Ukombozi ili uwe sehemu ya Kanisa lake, kwako wewe haipo bugudha yeyote toka toraha hii ya Mungu. Wewe siyo wake, na hivyo mfumo wa maisha yake haukuhusu. Lakini pale wale walio wake walipo ipokea, ilijitokeza katika hali hizi 3: -

    Ilijitokeza kama inayo eleweka vema, nini inacho hitaji (logical),

    Pia ilijitokeza kama ikumbushayo (commemorative) ya yale atakayo mtu kutimiliza; mfano sherehe zake za ahadi (moedim),

    Na mwisho ilijitokeza kwao kama ifumbiayo yasiyo eleweka (concealed). Mfano Torati 6:8 tefilini ambazo huvaliwa mkononi na kichwani, na mengi mengine yaliyo chota toka desturi za kale zaidi kwao (Kutoka 23:19).

    Mungu YAHWEH aliwachagua (elected) Yisrael toka mataifa yote ya Dunia, na kisha kuwatenga (separated) toka Misri, na kwa hivyo kuwa walio-gawanywa (divided) toka watu wote kwa ajili yake pekee. Kwa jinsi hii Yisrael (am) alifanyika mfano, na kivuli kwa watu na mataifa yote (goy) duniani. Hii kanuni pia, ndiyo elekezi kwa uelewa wa mkondo wa mbegu (a seed) ya baraka kati yao.

    Hakuna wakati wowote katika historia ya mtu, uchaguzi wao huu ulikuwa jambo la kibaguzi (racism) kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, asili yao, au utaifa wao. Watu wote wengine (races) walio kuwa tayari kuacha (denounce) desturi na dini za mataifa yao, na kumfuata YAHWEH Mungu wa Yisrael na toraha yake, hukaribishwa wakati wote kujiunga nao.

    Hata katika utoko wao (exodus) kule Misri, watu wa mataifa takribani yote walijiunga nao. Hivyo katika kundi lile jangwani, Shem (semitic) alikuwa pamoja na nduguze Yaphet na Ham kati yake. Mstari wa taifa la Mungu huanza na Adam-Seth-Shem-Abraham-Yitzhakh-Yahkob (Yisrael); na hivyo wana hawa wote wa Yisrael. Ukaribisho wa watu wote ni bayana, lakini ukamilifu wake hilo upo katika Kristo Yeshua pekee.

    Kila mmoja kati yetu shuruti sasa anajua vipi toraha hufanya ufunuo wa dhambi kupitia mitzvoti zake 613, lakini swali toraha ni nini, hilo bado sisi kusimama, ili tujifunze pamoja kwalo. Pamoja na swali hilo, pia itakuwa vema kwako kutambua: hivi toraha ilitokea wapi? Nani alianzisha toraha? Ipi tofauti kati ya toraha na sheria? Kama ipo tofauti, nini basi itakuwa tofauti kati ya sheria na imani? Au iko tofauti kati ya sheria na neema katika mlinganisho?

    Pamoja nayo haya maswali, ni lipi lilikuwa lengo la toraha aliyo pewa Mosheh? Hii toraha ilimfikiaje Mosheh? Nani ali-iandika? Iliandikwa kwa lugha gani kule juu ya mlima Sinai? Vipi toraha huweza ifunua dhambi? Haya maswali ni mengi kiasi kutosha kitabu chake, lakini sisi tuta-bananisha hapa-hapa.

    Neno toraha kamwe halimaanishi sheria, bali humaanisha maelekezo (instructions), au mafundisho (teachings). Pia hurejelea vile vitabu 5 vya awali katika tanakh (biblia) ya Kiebrania iliyo na vitabu 25, yaani: Mwanzo (Bereishith), Kutoka (Shemoth), Walawi (Vayiqra), Hesabu (Bamidbar), na Torati (Dhavaarim).

    Kidesturi neno hili toraha hujumlisha pia mafundisho ya kimapokezi ya rabai wao (oral torah) hata kufanya uwepo utofautisho na toraha hii iliyo andikwa kwa tanakh hizi 25 (written torah). Kimapokezi hii toraha isiyo andikwa, yaani halakha, ilikabidhiwa kwa simulizi toka kizazi hadi kizazi, na leo hii hupatikana katika makusanyo ya vitabu vya Talmudi yaani Gemara na Midrashi. Ni kwayo hii halakha ndiyo Yehudaizimu (Judaisim) husimama, kwani ndiyo zaidi ifunzwayo katika kila sinagogi na marabai, wakati toraha iliagizwa kufunzwa na makuhani hekaluni, imedorora.

    Hii ya kimapokezi ilikuja ili kufunza iliyo andikwa, na hususani eneo lile lilofichika (concealed) kwa msomaji wa kawaida. Pia ndiyo hii Yeshua Kristo aliyo ipinga kama desturi za kimapokezi (halakha) zinazo potosha kweli ya ile iliyo andikwa. Tazama mfano wake hili kwa Matityahu 15:2-3 ... Kwa nini wafuasi wako wanazivunja desturi za wahenga[10] {halakha[11]}? Kwani hawaoshi mikono wanapo kula mkate. Lakini yeye aliwajibu na alisema kwao, kwa nini na nyie pia mnaivunja amri ya Mungu {Toraha} kwa halakha yenu? ...

    Lengo la Talmudi ni kuelezea maandiko yana maana gani, vipi yatafsiriwe toka kizazi hadi kizazi pasipo kujali mabadiliko ya kimazingira, fikra, desturi, na jinsi ya kuzitia taratibu zake kazini wakati wote na mahali popote. Wayehudah wenye msimamo mkali (orthodox), huona hili kuanza na Elohim ambaye alimfunza Mosheh toraha kwa jinsi hii. Na kwamba desturi hii iliendelea tokea Mosheh kwa simulizi za mdomo (oral) mpaka 200AD, pale mapokezi haya ya mdomo yalipo nukuliwa katika nyaraka zilizoitwa Mishnah[12].

    Kwa karne chache zilizo fuatia, maoni ya ziada kuelezea Mishnah yaliandikwa Yerushalem na Babyloni. Hizi nyongeza ndizo hujulikana kama Gemara, na hivyo kwa pamoja na hii Mishnah ilijulikana kama Talmud pale ilipo kamilka 500AD. Hivyo ziko Talmudi mbili, hii ya Yerushalem, na ile ya Babyloni iliyo kubwa zaidi hata pale mtu asemapo Talmudi bila kufafanua ipi, humaanisha hiyo.

    Talmudi siyo rahisi kusoma, ni kama kumbukumbu fulani ambazo wewe haukuwepo kwenye tukio hilo. Mara nyingi upo uwazi (vacuum) usio tolewa maelezo, sababu yafikirika tayari wajua wazungumzialo na dhana hutajwa kifupi na maandiko ya kibiblia hurejelewa kwa maneno machache kama mawili au matatu hivi tu.

    Talmudi uhifadhi mchanganyiko wa maoni takribani kwa kila kitu, na siyo kila wakati hutaja maoni yapi ndiyo yakubalikayo. Na Mishnah imegawanyika katika sehemu 6 ziitwazo sedarim. Kila sedarim ina-gawanyika mara moja au zaidi, ziitwazo masekhtot, na ziko masekhtot 63 kwenye Mishnah. Takribani nusu yake zime-elezewa katika Talmudi.

    Kimsingi neno hili toraha maana yake Kiebrania ni sawa na kutaja utamaduni wa jamii fulani ya watu. Yaani huelezea asili yao, historia yao, mababa zao, utaifa wao, dini yao, Mungu wao, kanuni na taratibu za maisha yao; yaani desturi zao, mila zao, sheria zao, ibada zao, mapokezi yao, na kwa ufupisho: toraha ni ujumlisho wa maisha yao yote, na kila kitu tuitacho Uebrania, au Yisrael, au Yehudaizimu. Hivyo basi, toraha ni mafundisho ambayo huonyesha njia ya maisha kwa yule aliyeisha kombolewa.

    Hii dhana ya kukombolewa katika Yehudaizimu iko tofauti kidogo na yako ya Kikristo mpendwa, Yisrael alikombolewa na Mungu YAHWEH toka utumwa wa Misrayim, na hapo hapo kupewa agano la toraha, ili ajue jinsi ya kuenenda mbele za Mungu YHWH. Tokea manabii wanajua Mashiah pale ajapo wata-kombolewa tena toka utawala wa Mataifa, na wao kuwa watawala wa Dunia nzima milele. Huyu ndiye Mashiah (ben David) wanaye msubiria, na sisi tunajua hili ni kuanzia milenia.

    Sasa tokea msingi huu, tazama jinsi wao waonavyo ukombozi kuwa jambo la kidunia kwa kurithi nchi itiririkayo asali na maziwa awali, na sasa huko mbele siku zijazo, kuwa maisha ya Mbinguni hapa hapa duniani (sisi tunajua hiyo ndiyo Yerushalem Mpya). Lakini tuko hapa mpendwa, ili uone sehemu ya toraha kwa mafundisho yao; kuwa ni jinsi ya kuenenda kwa usahihi mbele za YHWH, na kamwe siyo ukombozi, kwani hilo lilifuatia kwisha kukombolewa! Hivyo pale uangukapo (kulitoka agano la ukombozi wako), wewe hutolewa nje ya kambi, hadi uji-safishe na aku-takase, ndipo wewe hurejea kambini ukiwa mtakatifu (saint) wake.

    Sasa turejelee tafsiri yetu ile ya toraha ni nini, tuliyo ikatisha hapo juu. Pia toraha humaanisha mafundisho ya tanakh zote 25, ujumlisho wa mafundisho yote ya Kiebrania, utamaduni na maisha yote ya kila siku ya Muebrania anaye ifuata hiyo. Ndani yake haya ndimo uumbaji, uito wao kuwa watu wa YAHWEH, utii na majaribu yao, maagano yao na YAHWEH, ambayo kwayo zipo kanuni za mahusiano (morals), kanuni za kidini (rituals), na sheria za kijamii zijulikanazo kama halakha (civil laws). Kimsingi hapa ni kwamba, taifa la YAHWEH, halina utengo wa taifa na dini (separation of state and temple), au mambo ya kidini (moral duties) na maisha ya kawaida (civic duties).

    Uhalalisho wa uwepo wa Talmudi ni kitabu hicho chenyewe pale kisemapo kwamba, Mosheh kule juu ya mlima Sinai, alipokea toraha iliyo andikwa (written torah), na maelekezo yake kimafundisho kuelewa hicho kilicho andikwa (oral torah). Na kwamba ni maelekezo hayo, ndiyo kimapokezi toka kizazi hadi kizazi, yaliishia kunukuliwa ndani humu ya vitabu hivi viwili.

    Inatajwa kwamba, zamani zile za jangwani, na kisha Yisrael ya awali toka waamuzi hata wafalme, ili-katazwa kuiandika toraha hii ya kimapokezi, sababu isinge-wezekana tena kuwa kamilifu na inge-athirika na tafsiri binafsi na upotoshaji wa makusudi. Katazo hili lili-ondolewa katika zama za uhamisho (captivity) na utapanyo (diaspora), ili kuhifadhi kwa hofu ya muingiliano na tamaduni ngeni waliko tapanywa.

    Katika mwaka 200AD rabai Judah haNasi alimaliza kazi ya makusanyo kwenye Mishnah. Mapokezi mengi yaliyo achwa kwenye Mishnah ni Tosefta na Midrashim. Miaka ilivyo songa mbele, ndiyo maoni mengi yaliongezwa na Mishnah ikawa Gemara ambayo iliandikwa Kiarameiki (Aramaic). Ni Mishnah na Gemara kwa pamoja zijulikanazo kama Talmudi. Wayehudah huchukulia hizi kama njia pekee ya kuelewa toraha iliyo andikwa.

    Kwa Muebrania (hata walio kuwa wafuasi wa Yeshua na mitume), tanakh siyo agano la kale, sababu kwao agano ni lile lile moja lifanyiwalo ujazilisho, ili ukamilifu wake wote ufichuke. Maagano yote ni ujalizisho wa lile la Abraham. Hivyo utangulizi wa agano haulifanyi kuwa la kale, au upya wa agano haupelekei lile la kwanza kufutwa. Agano likisha simikwa huwa la milele, likiendelea kusimama mpaka vipengele vyake vyote vikamilike. Yisrael leo bado kuikubali kwa ujumla wake injili, hivyo tanakh inabaki kwao vitabu hivi 25 (biblia ya kanisa yakubalika zaidi kuwa na vitabu 66): -

    Watangulizi wetu walitafsiri dhana nzima ya toraha kuwa sheria kwa Kiswahili, wakiligeza neno la Kiingereza ‘law’ ambao nao walifanya hivyo toka Kilatini kwa neno ‘lex.’ Hawa waliligeza none la Kigiriki ‘nomos.’ Lakini neno nomos angalau lili-maanisha muunganisho wa mila na desturi za watu. Sisi huita urejesho wa neno ‘toraha’ kama lilivyo kwa ujumlisho wa yote dhana hiyo ibebayo.

    Pale Mungu alipo maliza kuoredhesha Maneno 10[13] mbele ya kadamnasi cha Yisrael wote, ndipo sasa alipo mwita Mosheh juu na kuanza kumpa Torah kwa mitzvoth zake zote 613. Na pale alipo fanya hivyo, hivi ndivyo alivyo ziiita hizo: ... Sasa hizi [ndizo] mishpat {nilicho hukumu[14], mfumo wa maamuzi ya haki[15]} ambazo wewe utaziweka mbele zao. ... [Kutoka 21:1].

    Neno mishpat limetafsiriwa na tafsiri mbalimbali za biblia kama hukumu (judgement), maamuzi (ruling), sheria (ordinance), kanuni (rules), mfumo wa haki (justice) nakdhalika. Sisi tumesha litafsiri neno hilo ndani humu kwa jinsi zao, lakini pako ambapo tulitafsiri binafsi kama neno la Mungu likomboalo[16]. Martin Luther King katika tafsiri yake ya biblia, ali-litafsiri neno hilo kama neno la Mungu. Je hii siyo pia tafsiri ya injili?

    Wako wengi wanao amini injili ni milki binafsi ya agano jipya la mwisho pekee, hivi hatusomi kwa mtume Paulos kuwa, injili ili-hubiriwa kwa Abraham katika Wagalatia 3:8, na hapa pia kwa Kutoka 21:1 hatuoni Mungu akiita toraha yake injili? Yaani habari njema ifichuayo dhambi, na kuelekeza jinsi ya mkombolewa kuenenda maishani, na katika mahusiano naye?

    Hebu tazama kile Mungu asemacho kwa mtizamo wa Martin Luther King na Tom Bradford, na kisha linganisha na wingi uliopo leo wa tafsiri za neno hilo, katika biblia takribani zote:

    Yeshayah 42:1-4 ... Mtizame mtumishi wangu, huyo Mimi namtunza {napelekea awepo, namsaidia, na mfuatilia kwa karibu}; chaguo langu, [katika yeye] nafsi yangu inafurahishwa; Mimi nimemweka Ruak wangu juu yake: yeye shuruti alete mbele mishpat {nilicho hukumu[17], mfumo wa maamuzi ya haki[18]} kwao Mataifa. Yeye hatapiga ukulele, wala kugombesha, wala kupelekea sauti yake isikike nje.

    Mmea ulio chubuka yeye hata-uvunja, na taa inayo fifia yeye hata-izima: yeye shuruti alete mbele mishpat {nilicho hukumu[19], mfumo wa maamuzi ya haki[20]} katika kweli {uaminiifu, hakika}. Yeye hata-kuwa dhaifu wala kuchubuliwa, mpaka atakapo maliza kusimika mishpat {nilicho hukumu[21], mfumo wa maamuzi ya haki[22]} katika nchi [kavu]: hata visiwani shuruti wataisubiria {wataitumainia} toraha yake. ...

    Sasa Badili Neno Mishpati kwa Injili

    Yeshayah 42:1-4 .. . Mtizame mtumishi wangu, huyo Mimi namtunza {napelekea awepo, namsaidia, na mfuatilia kwa karibu}; chaguo langu, [katika yeye] nafsi yangu inafurahishwa; Mimi nimemweka Ruak wangu juu yake: yeye shuruti alete mbele INJILI kwao Mataifa. Yeye hatapiga ukulele, wala kugombesha, wala kupelekea sauti yake isikike nje.

    Mmea ulio chubuka yeye hata-uvunja, na taa inayo fifia yeye hata-izima: yeye shuruti alete mbele INJILI katika kweli {uaminiifu, hakika}. Yeye hata-kuwa dhaifu wala kuchubuliwa, mpaka atakapo maliza kusimika INJILI katika nchi [kavu]: hata visiwani shuruti wataisubiria {wataitumainia} toraha yake. ... [Tumeweka herufi kubwa na wino mwingi uone tulipo-badili].

    Katika zama za kale kule Uingereza, wakati neno mishpati lina-tafsiriwa hukumu (judgement), neno hilo hukumu lilikuwa pasipo makali ya leo katika uhusisho na kile hakimu afanyacho mahakamani. Katika zama hizo neno hilo, lilikuwa sawa na jinsi tunavyo tumia neno ‘mtizamo’ leo hii.

    Kimsingi Mungu alishusha maelelekezo kwa mtizamo wake yeye Muumbaji wetu, wa jinsi ya kufanyia uamuzi mambo kadhaa maishani. Hivyo kwa maelekezo (mitzvoth) 613, alifanyia ufupisho kwa mifano-kanuni, vipi mahusiano yake na mtu yapasavyo kuwa, na jinsi mahusiano ya mtu na mtu, na hata mtu na vyote vilivyo umbwa yapasavyo kuwa. Toraha ni sawa na kitabu cha maelekezo ya mtengenezaji (manufacturer’s manual).

    Inafikirika na wanazuoni makini kuwa, ni matumizi haya ya neno hukumu kama mbadala wa neno mishpati upelekeao Wakristo kufikiri Mungu wa agano la kale ni mwingi wa hasira (wrath), na afanyaye hukumu (judgments) wakati wote, na hivyo kudai Mungu wa agano jipya la mwisho ni Mungu wa neema (kana kwamba hata hili ni jipya na maalumu kwa agano hili pekee).

    Sasa tazama, kama vile basi tanakh yote ilivyo toraha, ndivyo hivyo-hivyo navyo agano jipya lote la mwisho lilivyo toraha, kwani humo pia yamo mafundisho, maelekezo, na neno la Mungu. Hivyo pasipo kujali Yehudaizimu (Yisrael) au Umashiah (Ukristo), sote tunashiriki mwanzo huu mmoja, ulio chimbuko la jinsia yetu mpya, yaani sisi wawili tulio sasa ‘mtu mmoja mpya’ (Waefeso 2:15, 4:24, Wakolosai 3:10).

    Kimapokezi wenzetu wana simulizi nyingi sana kuhusu chimbuko na asili ya toraha kama tuionavyo leo. Kwa ajili ya upendo wa kanisa lizungumzalo Kiswahili, inatuwia wajibu kwamba, nawe ujue kile wakijuacho kimapokezi kaka na dada zako Yisrael:

    Toraha ilishushwa na Mungu YAHWEH duniani ikitokea Mbinguni, na kukabidhiwa kwetu kupitia mpatanishi Mosheh, kule juu ya mlima Sinai. Pia wao hudai toraha ilikuwepo Mbinguni hata kabla ya Dunia kuumbwa. Marabai hufunza kimapokeo kwamba, toraha ni mojawapo kati ya vitu 6 au 7 vilivyo umbwa kabla ya ulimwengu.

    Kwa mafundisho ya Eliezer ben Yose Mgalilaya, anadai kwa vizazi 974 kabla ya kuumbwa ulimwengu, toraha ilikuwa kifuani mwa Mungu ikiungana na malaika katika nyimbo. Simeon ben Lakish alifundisha kwamba, toraha imeutangulia ulimwengu kwa miaka 2000, na kwamba iliandikwa kwa moto mweusi juu ya moto mweupe. Judah Barzillai wa Bercelona anaona kwa kufanya hivi, huja tatizo la mahali ilipo kuwepo kabla ya uumbaji, na usuluhishi wake ni kwamba; ndiyo toraha ilikuwepo kabla ya uumbaji, lakini katika umbo ndani ya nafsi ya Mungu.

    Naye Ibn Ezra huona kauli zao hizo zina tatizo la muda, na hivyo haiwezekani kuwepo miaka 2000 zaidi au hata  nukta moja kabla kwa sababu, muda (time) ni matokeo ya mwendo (acceleration/motion), na kwamba haukuwepo mwendo kabla Elohim hajaumba vilivyomo angani (celestial spheres), na hivyo mafunzo hayo ni ya kutamka tu pasipo ujuzi wa uasilia.

    Toraha yaonekana kufunza kwa kanuni kuu kuwa, njia ya kuendea maisha sahihi ni uelewa wa kweli kwamba, imani (faith) na matendo (deeds/ works) kamwe havitengani. Inatajwa maandikoni kwamba, kwa ukubalifu wake Abraham alionekana kumiamini YAHWEH, na yeye alimuhesabia haki kwa hilo (Warumi 4:6). Lakini imani yake hiyo ilijaribiwa na kuthibitika kwa tendo la kafara ya Yitzhakh.

    Lengo la toraha lilikuwa wewe kutimiliza nia ya Mungu kwa vitendo, na walio wake shuruti tumtegemee yeye pekee. Tazama nia ya injili iliyo mwondelezo wa toraha hii moja toka kinywa cha Adonai Yeshua kwa Matityahu 6:33 ... Lakini nyie utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na mambo yote haya {vitu vyote hivi} shuruti vitaongezwa {vitazidishwa} kwenu. ... Amin

    Ni katika jinsi hizi Waebrania wanaipenda sana toraha yao, wanaiamini, na mioyoni mwao hupenda kuifuata hiyo siku zote za maisha yao. Kwao hii ndiyo nia ya Hashem (Jina) kwao. Upendo wao kwayo siyo shuruti, bali ridhaa safi ya mioyo yao. Kwao hizi ndizo njia na fikra za Elohim wao. Nje yao hawa, na kwa jinsi hizi, jamii yeyote ya watu kufanya nukuu toka hili, ni kujulisha upepo tu.

    Pamoja na msimamo wetu kuhusu urudio wa asili ya neno toraha, bado sehemu ile ya neno sheria ndani ya toraha ipo. Siyo wanazuoni wetu pekee walio geuza toraha kuwa sheria, kwani hata ilipofika zama za Yeshua, tayari Yisrael walishafikia ufupisho huu kwa neno hili-hili kuhusu toraha waliyopewa. Kama hivi ndivyo, basi acha tuangalie nayo sheria maana yake nini.

    Sheria hutafsiriwa ndani ya  ‘Oxford Dictionary of Law, New Edition, 1997, Oxford University Press’ kama muunganiko wa maneno mbalimbali ya amri, au kanuni, au sharti, ambazo kwazo jamii fulani huwalazimu kuzitii kwa hiari, au shuruti, kwa jinsi ya zawadi, au adhabu, zitakanazo nayo. Hivyo sheria ni mjumlisho wa makubaliano ya jamii kupitia vyombo vistahilifu (bunge) kwa ajili ya kuthibiti amani, usalama, na hivyo maendeleo, ndani ya jamii husika. Huu ndiyo upande wa kwanza, na wa pili ni kuleta haki, ustaarabu, kuadhibu, na maelewano kati ya watu. Pia ni mhimili muhimu wa usuluhishi katika masuala tata, tete, na yenye ushindani.

    Toraha ni mkusanyiko wa maelekezo (mitzvah,) na mafundisho maalumu 613, yaliyo vipengele vya kanuni za mfumo wa haki, na mahusiano yote kati ya YAHWEH, mwana-adam, na uumbaji. Mambo haya yote 613 uhitaji utii, na utekelezaji wako wewe uliye kombolewa. Ukiukaji wa yeyote kati ya hizi kwa kukusudia, ilikuwa dhambi isiyo na kafara ya kitubio. Kwa jinsi hii toraha ilileta hukumu na kifo, ijapo kuwa yenyewe ikiwa takatifu, na makini kwa yote iliyojia.

    Kwa kubainisha haya yote, YAHWEH aliondoa funiko la siri ya dhambi, hata uchi wake kujulikana kadamnasini. Kila Myisrael alijua dhambi ni nini, na ipi tokea mitzvothi hizi 613 maalumu kwao. Hivyo kwa toraha ya Mosheh, alicho kitaka YAHWEH kwetu ni: -

    Wewe uzifahamu dhambi zote na kuziepuka,

    Utambue haki, usafi, utakatifu, na utakaso; uweze kumsogelea katika mahusiano,

    Kupitia kivuli cha kafara za kikuhani, aifunue kanuni ya damu ya mwenye haki, kuwa msingi wa msamaha na ondoleo la adhabu ya dhambi (kifo) hapa duniani.

    Sisi tunajua na kuafiki toka Matendo 7:53 kuwa, toraha ilishuka duniani toka juu Mbinguni kupitia malaika kadhaa, ili kukamilishi ukabidhi wazo kwa Mosheh. Tena maandiko yakiri ni hapa katika ushusho wake, ndiyo Mosheh alinukuu maneno hayo yote katika skroli[23]. Hivyo sheria hizo hapa duniani zilikuwa za kiroho (Warumi 7:14). Na wala siyo kwa wale wa matendo ya kimwili, bali kwako wewe wa matendo ya kiroho kwa imani, ndiyo toraha ilifumbiwa.

    Tazama ushahidi wetu kwa Warumi 8:4 ... Kwamba haki ya toraha iweze kamilika ndani mwetu, wale tutembeao siyo kwa yale ya mwili, bali kwa yale ya Ruak {HaKodeshi}. ... Hii ndiyo haki ile ambayo kwa agano hili jipya la mwisho, iliandikwa moyoni mwako (Yeshayah 59:20-21, Yeremiyah 31:31-35, Waebrania 10:1-18). Tafakari

    5.1 Toraha ya Mosheh

    Katika zama za tabanako linalo hama toka mahali mpaka mahali, ilishuhudiwa kuwa; Ruak HaKodeshi  hushuka mara kwa mara na kubaki humo. Na kwamba pale awapo humo, wale Walawi walinzi waliopiga kambi kulizunguka, husimulia kuhusu pumzi kuu kama ya mtu apumuaye, ambayo husikika kutoka patakatifu pa patakatifu.

    Leo wewe na sisi kanisa ndiyo tabanako lake, yaani nyumba ya hekalu lake litembealo. Toka kwetu ndiyo utukufu ule wa shekinah (Kutoka 29:42, 40:34-35) hutoka, hata kuwabadili (transforming) wale wote wanao kutana na sisi. Amin

    Toraha ya Mungu YAHWEH hujulikana zaidi kama Sheria ya Mosheh, iliandikwa mara moja tu, lakini Maneno 10  juu ya vibao viwili vya mawe, ndivyo Mosheh kwa hasira alivivunja (kuashiria uvunjikaji wa agano) hata ikabidi viandikwe vingine mara pili.

    Inasomeka hivi kwa Kutoka 32:15-16 ... Na Mosheh aligeuka, na kushuka chini toka mlimani, na vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} viwili vya agano mkononi mwake: vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} vili-andikwa pande zote mbili; upande mmoja na upande mwingine vili-andikwa. Na vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} [vilikuwa] kazi ya Elohim, na maandishi yalikuwa uandishi wa Elohim, yamechimbiwa[24] juu ya vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa}. ...

    Kwa mapokezi Wayisrael hata leo hufunza wana wao Maneno 10 tofauti na tufanyavyo Kanisa. Wao huwafunza na kuwaonyesha jinsi ambavyo amri ya 1-5 huelezwa na amri ya 6-10. Tunajua hii shuruti iwe dhana mpya kwako. Je ukichukua vipande hivi viwili na kuviweka pamoja ili uweze kusoma kama wafanyavyo Wayisrael, kile utakacho kiona mbele yako ni vipande viwili vya mawe vichoravyo msalaba.

    Kama hilo halitoshi, wanahistoria na wana-akiolojia leo hii, wanazo herufi ambazo zilitumika na Mosheh kuandika toraha. Je si jambo la kushangaza kwamba, herufi ‘A’ ya kwanza ilikuwa ni alama ya ‘mwanakondoo’ na herufi ‘Z’ ya mwisho ilikuwa ni alama kama msalaba! Kwamba ukombozi utaanza na kafara ya mwanakondoo wa Misri, na kuishia juu ya msalaba[25] wa kafara ya Yeshua Mwanakondoo wa Mungu.

    Vibao vya pili ni tofauti na vile vya kwanza, vile Elohim alivikata mwambani na kuandika kwa kushindilia juu yavyo, lakini hivi vya pili alivikata Mosheh na kuandika Elohim. Hivyo hivi ni kazi ya Mungu na mtu kama inukuliwavyo toka Kutoka 34:1,4 ... Na YAHWEH alisema kwa Mosheh, wewe chonga vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} katika mfano wa vile vya awali: na Mimi nitaandika juu ya vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} maneno ambayo yalikuwepo katika vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} awali, ambavyo wewe ulivivunja.

    ... Na yeye alichonga vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} viwili katika mfano wa vile vya awali; Na Mosheh aliamka asubuhi na mapema, na kukwea mlima Sinai, kama vile YAHWEH alivyo muamuru, na alichukua mkononi mwake vibao vya mawe {vilivyo katwa na kusawazishwa} viwili. ...

    Maandiko yashuhudia katika uandishi huu wa toraha, Mosheh alikaa juu mlimani kwa siku 40 akiipokea pasipo kula wala kunywa (mtu hataishi kwa mkate pekee, bali kwa kila neno litakalo kinywani mwa Mungu). Pia maandiko yashuhudia, aliongea na Mungu uso kwa uso[26] kama vile mtu aongeavyo na rafikie.

    Ni tokea ushahidi wa Yokhana Mbatizaji kwa Yokhana 1:18 ... Hakuna mtu aliye muona Mungu katika wakati wowote ule; Mwana wa kiume wa pekee wa Mungu, ambaye yuko kifuani mwa Baba, yeye ndiye aliye mtangaza. ... Sisi hufikiri kuwa, huyu aliye kuwa na Mosheh ni Mwana wa Mungu, Mungu Neno (Yokhana 8:58). Sababu tunajua kwa Kutoka 33:18-23, pale Mungu Baba alipo tokeza hapo, ilibidi amfiche Mosheh katika upenyo wa mwamba wa mlimani.

    Tokea uelewa huu, je wajisikiaje sasa mpendwa unapo tafakari injili na kumwona Adonai Yeshua kubishana na mafarisayo, waandishi wanasheria, marabai, na masudukayo kuhusu kitabu ambacho ni yeye aliye wapa babu zao awali kwa msaada wa uandishi wa malaika? Vipi ilikuwa pale walipo mtahini kuhusu sheria ipi ni kuu kuliko zote, wakati ndiye aliye zishusha hata kuwafikia? Na kama kuongea na watoto ni ajabu, vipi pale abishanapo nao kuhusu Mashiah wamsubiriye atakuwa mwana wa David, wakati David naye anamwita Adonai? Au vipi kwamba alikuwepo kabla ya Abraham, na hivyo Mosheh pia?

    Adonai Yeshua Mashiah (Kristo) alijua kinaga ubaga kuwa, toraha ilipewa kwao ili: -

    Kurudisha na kurasmisha mahusiano ya upendo kati ya mtu na Mungu wake, na yale ya mtu na mwenzi wake.

    Na tokea hiyo mfumo wa haki ulisimikwa ulimwenguni, na kwa kufanya hivi siyo tu dhambi ilifichuliwa, bali hata chaguzi za nafsini zilidhihirishwa kwa ajili ya utambuzi wa familia ya Mungu kupitia yeye.

    Na la mwish; ni kusimika daraja la ukuhani, taratibu za hekalu, na mfumo wa kafara za Kilawi, kwamba, msamaha na upatanisho shuruti uwe kwa damu isiyo hatia.

    Pamoja na mazuri haya yote, bado toraha ya Mosheh ilikuwa na mapungufu yake, iliweza kusamahe kwa upatanisho dhambi, makosa, na kushindwa kule kwa kutokusudia (un-intentional) pekee. Siyo sahihi na tena siyo haki, kumlinganisha tembo na kunguru, na kisha kumhukumu tembo kuwa hawezi kupaa angani, sababu haku-umbwa kutenda hilo. Hivi ndivyo Kanisa kwa karne nyingi tume-ihukumu toraha kushindwa kukomboa, pasipo umakini wa kiini cha kushushwa kwayo. Toraha kwa haya 3 ilitimilisha vilivyo kile ilicho shushwa kutimiliza, tena kwa umakini na ukamilifu mkuu pasipo kasoro au pungufu lolote lile.

    Itakuwa pasipo tija kama hatuta-kuonyesha angalau mitzvoti 12 kati ya zile 613, tena zilizo tofauti na yale Maneno 10, ili uweze kuona na kugusa toraha. Haya yatakuwa mapitio finyu sana ya kitabu cha Kutoka 34:1-35, ili ujionee mdahalo wetu kuwa, je hizi ni hukumu (kwa maana ya neno hilo leo), au sheria, au ni mafundisho na maelekezo ya neno la Mungu linalo tunza utakatifu: -

    Uzivunje altare zao na kuvunja vunja nguzo zake na mahali pao pa heshima. Nyie hamtaabudu mungu mwingine: kwani YAHWEH ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu.

    Usifanye agano na wakazi wa nchi, na ukenda fanya ukahaba na miungu yao, na kufanya kafara kwa miungu yao, na mmoja wao akakuita nawe ukala kafara zao.

    Usiwaoze mabinti zao kwa vijana wako, na mabinti zao wakafanya ukahaba kwa miungu yao, na kuwafanya vijana wako kufanya ukahaba na miungu yao.

    Usijifanyie miungu wa kuyeyusha mwenyewe.

    Lazima ufanye sherehe ya mikate isiyotiwa chachu. Kwa siku 7 ule mikate isiyotiwa chachu. Kama alivyo kuagiza, katika muda uliopangwa katika mwezi wa Abibu ambao ndiyo nyie mlitoka nchi ya Misri. Huu ni mwezi wa nafaka mpya wakati wa kiangazi.

    Wale wote walio wazaliwa wa kwanza ni wangu, na kila mfugo wako wa kiume wa uzao wa kwanza, aidha ng’ombe au kondoo.

    Na yeyote asije mbele yangu bila kitu.

    Nawe utafuatilia siku kuu za wiki, hata za mavuno ya tunda la kwanza ya ngano, na sherehe ya kukusanya katika mwisho wa mwaka.

    Mara tatu katika mwaka wanaume wote lazima waje mbele za Mungu YAHWEH, Mungu wa Yisrael.

    Anakataza kutoa damu ya kafara na mkate uliotiwa chachu; na wala kafara ya pesaka isibaki mpaka asubuhi.

    Uzao wa kwanza wa shamba lako utaupeleka katika nyumba ya Mungu wako YAHWEH.

    Usi-mchemshe mwana mbuzi katika maziwa ya mama yake.

    Sasa na tutizame toka umakini wa ufasaha wa vitabu vya Kutoka 20:1-17 na Torati 5:6-21, ambako ndimo Maneno 10 huthibitika kwa usahihi wa kile Mungu YAHWEH alicho kisema katika usikivu wa Yisrael. Mpendwa, mpinge kwa nguvu zako zote yeyote abadilishaye Maneno 10 haya kwa kuondoa neno la kwanza, na kisha kugawanya neno jingine, ili bado yabaki Maneno 10.

    Ndani ya Maneno 10 maandiko hutaja neno Misri na Shabath (Shabath), je kitabu chako cha sala au liturgia ya kimadhehebu hutaja pia? Kama hakitaji ni kwa nini? Je dhehebu lako linayo agenda ya kuificha historia ya Yisrael, na kwamba haya ni Maneno 10 waliyopewa wao pekee? Je kuondolewa kwa utajo wa Shabath, ni mbinu ya dhehebu lako kubadili nyakati za Mungu duniani?

    Mpendwa, linganisha maandiko tuliyo kupa, na huu ufupisho tukupao, na hayo ambayo ulifunzwa, au wana wako hufunzwa leo. Kama ni tofauti, waombe kwa kusii sana wazee wa kusanyiko (sinagogi) lenu kufanya marekebisho stahilifu, ili Maneno 10 yawe kama vile Mungu YAHWEH alivyo yatamka mbele ya halaiki ya Yisrael, na kurekodiwa hivyo maandikoni. Pinga kabisa, na tena hadharani katika utetezi wa usahihi wa maandiko, dhidi ya itikadi babaishi za kimadhehebu.

    Katika utangulizi wa mpasuko na mshindo wa radi kuu, mlima Sinai uwakao moto pasipo kuteketea mbele zao, ndipo ukaja ukimya mkuu kwa wana wa Yisrael, hata sindano idondokayo kusikika. Ndipo Mungu YAHWEH alisikika kwao wote, takribani nafsi milioni 3 akitamka haya Maneno 10 ifuatavyo: -

    Mimi ndiye Mungu wako YAHWEH, ambaye nilikutoa nchi ya Misri, toka nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu wengine zaidi yangu.

    Wala usijifanyie sanamu ya kuchonga kwa mfano wa chechote Mbinguni, au hapa duniani, au kilicho kwenye maji chini ya Dunia. Usiwasujudie wala kuwatumikia miungu wa uongo, kwa kuwa Mimi Mungu wako YAHWEH ni Eli[27] mwenye wivu.

    Usilitaje bure jina la Mungu wako YAHWEH; kwa kuwa YAHWEH hataacha kumhesabia hatia, yule alitajaye jina lake bure.

    Ikumbuke siku ya YAHWEH ya Shabath na uifanye takatifu, kama Mungu wako YAHWEH alivyo kuamuru. Ufanye kazi siku sita; na fanya kazi zote. Lakini siku ya saba ni Shabath ya Mungu wako YAHWEH. Siku hiyo hautafanya kazi yeyote, wala kijana wako, wala binti yako, wala mtumishi wako, wala maksai wako, wala punda wako, wala mgeni katika nyumba yako. Wewe na walio katika mji wako pumzikeni.

    Waheshimu baba na mama yako, ili siku zako za kuishi ziwe nyingi, na upate heri katika ardhi aliyokupa Mungu YAHWEH.

    Usiue.

    Usizini.

    Usiibe.

    Usitoe ushahidi wa uwongo dhidi ya jirani yako.

    Usimtamani mke wa jirani yako, wala nyumba ya jirani yako, shamba lake, au mtumishi wake, maksai wake, au punda wake, au chechote kile alicho nacho jirani yako.

    Tokea msingi huu, tuta-endelea kujenga juu yake katika masomo na mada nyingi zijazo mbele, kwani hivi ndivyo ilivyo kuwa, ilivyo sasa, na itakavyo kuwa mpaka yote ya kiagano yame-kamilika. Amin

    5.2 Amri ya Upendo

    ... Na mmoja wapo wa waandishi {wanasheria [28]} alikuja, na akiwa amesha wasikia wao wakijadili {kwa kubishana} pamoja, na kutambua kwamba yeye aliwajibu wao vema, akamwuliza, ipi ni amri inayo zitangulia zote? Na Yeshua alimjibu yeye, amri inayo zitangulia zote [ni], Sikia {na utii}, Oh Yisrael; YAHWEH Mungu wetu ni YAHWEH mmoja: Na wewe shuruti umpende YAHWEH Mungu wako kwa moyo {fikra, hisia} wako wote, na kwa nafsi {roho} yako yote, na kwa akili {mawazo, uelewa} zako zote, na kwa nguvu {uwezo} zako zote {Torati 6:4-5}: Hii [ndiyo] amri ya kwanza. Na ya pili, yafanana nayo, Wewe shuruti umpende jirani yako kama unavyo jipenda {Walawi 19:18}. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

    Na mwandishi {mwanasheria} alisema kwake, vizuri, Rabai, wewe ulisema ukweli: kwani yupo Mungu mmoja; na hayupo mwingine ila yeye: Na kumpenda yeye kwa moyo {fikra, hisia} wako wote, na kwa uelewa {akili} wako wote, na kwa nafsi {roho} yako yote, na kwa nguvu {uwezo} zako zote, na ampende jirani yake kama anavyo jipenda, ni zaidi ya olah na zebah yote. Na pale Yeshua alipo-ona kwamba amehitimisha kwa uangalifu na sahihi, alisema kwake, Wewe haupo mbali na Ufalme wa Mungu. Na tokea hapo hakuna mtu aliye thubutu {kuwa na ujasiri} kumuuliza {swali}. ...

    Mimi nakupa wewe mitzvah mpya, kwamba nyie mpendane mmoja na mwenzake; kama vile Mimi nilivyo kupenda wewe, kwamba nyie pia mpendane mmoja na mwenzake. ... Hakuna aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba mtu ana utoa {weka chini} uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. ... [Marko 12:28-34, Yokhana 13:34, 15:13 – msisitizo wa mistari ni wetu].

    Tayari wewe waujua upendo kama kiasili kimojawapo cha uumbaji, na sasa una-uona upendo kama ufupisho wa toraha nzima. Je upendo huu hufikaje ndani mwako? Upendo uko ndani mwako wewe mpendwa uliye amini, kupitia njia hizi tatu ifuatavyo: -

    Katika uumbaji wako ulipewa roho wa upendo: ... Kwani Mungu hakutupa sisi roho ya hofu {isiyo ujasiri, au hakika}; bali ya nguvu {uweza[29]}, na ya upendo {agape}, na ya akili timamu {nidhamu, kujizuia}. ... [II Timotheo 1:7].

    Kwa kuwa Adam wa kale hufa na mpya uzaliwa katika kupokea kwako ukombozi, basi katika siku hiyo Ruak HaKodeshi humwaga upendo tena ndani mwako: ... Na tumaini halikufanyi uaibike {uumbuke[30]}; sababu Ruak HaKodeshi tuliyo pewa sisi amejaza mioyoni {akilini} mwetu upendo {agape} wa Mungu. ... [Warumi 5:5].

    Pia kwako wewe uliye kombolewa, upendo ni tunda la uwepo wa Ruak HaKodeshi ndani mwako: ... Lakini tunda la Roho ni upendo {agape}, furaha {uchangamfu, ucheshi}, shalom {hakuna kinacho kosekana: amani, mafanikio, usalama, utulivu, ustawi n.k}, uvumilivu (katika subira}, staha[31] {hadhi, adabu}, wema {tabia nzuri, kusaidia wengine}, imani {kuafiki kuwa ni kweli/ hakika kidini}, upole {kuto-jikweza, unyenyekevu}, kujizuia {kuwa na kiasi}: dhidi yake haya hakuna toraha. ... [Wagalatia 5:22-23].

    Je bado wa ikumbuka ile njia watoto wa Kiebrania wafunzwavyo Maneno 10, kwamba ya ubao mmoja wa mawe hufafanua yale ya ubao wa pili? Tazama hiki mfarisayo msomi wake hiyo toraha afanyavyo kwa hili la upendo toka sura nzima ya I Wakorintho 13:1-13:

    Kwamba, hata kama wanena kwa lugha pasipo upendo wewe ni bure tu. Kwamba, hata kama wewe ni nabii, mjuzi wa siri za nyakati, na maarifa yote, na uliyejaa imani tele lakini pasipo upendo wewe ni bure tu. Kwamba, hata kama ukitoa kila ulicho nacho kuwalisha fukara, au kuufanya mwili wako kafara ya kuchomwa moto, pasipo upendo ndani yako, haya yote ni kazi bure tu. Sasa tazama ile kanuni ya vibao viwili katika jedwali chini, ili kutambua tulengacho shabaha.

    Hivyo basi, upendo huvumilia pasipo ukomo, na ni mpole, usio tamani kisicho chake, haujigambi, wala kujikweza. Upendo hautendi isivyo stahili, hautafuti yaliyo yake, hau-kasirishwi kirahisi, na haufikirii mabaya. Hau-furahishwi na udhalimu, kwani hufurahi katika kweli. Upendo huvumilia yote, huaminii  yote, hutumainia yote, na hustahimili yote. Upendo kamwe haushindwi!

    Hii ndiyo tafsiri itendekayo (operational definition) ya amri ya upendo, kama tulivyo pewa sisi majeshi yake Wakristo, na Amiri Jeshi wetu Mkuu, Adonai Yeshua Kristo. Hivyo mzunguko umekamilika, kwani hata sisi sasa tumelirudia lile la toraha moja, kama ilivyo kuwa kwa Adam na Havaa. Kumpenda Mungu YAHWEH, ndiko kumchagua yeye. Na kumchagua yeye, ndiko kuitii injili yake, kwani anaye itii injili yake, huyo ana tekeleza hayo yote juu ya wasifu za upendo. Katika lugha ya Mbinguni: upendo siyo jambo la kihisia tu, kwani limesheheni matendo halisi.

    Kama hivi ndivyo, na matendo hayo ndiyo uthibitisho wa uchaguzi wako kwake, basi kuivunja hii amri ya upendo ni dhambi (I Yokhana 3:4). Kwako Mkristo, kila unapo jikuta nje ya upendo, ni shuruti ujirudi kwa kufanya toba la dhambi hiyo mara moja. Tunajua kwamba, yeye ni muaminiiifu  na mwenye haki, hata akusamehe na kuifutilia mbali dhambi hiyo (I Yokhana 1:9). Kwa jinsi hii, upendo ufanya kazi kwa imani kupitia neema ya Kristo (Wagalatia 5:6).

    Hata hapa waona kuwa, kiini cha injili yote ni toraha ya upendo, ambayo hiyo hufupishwa na Maneno 10, yaliyo ufupisho wa mitzvot zote 613. Ni kwa jinsi hizi agano jipya la mwisho ni mwendelezo wa agano lile-lile la awali, kwa lengo la kufikisha ukamilifu wake. Sasa sikia haya matatu kuelewa ipasavyo hili: -

    Matityahu 5:17-18 ... Usifikiri kwamba Mimi nilikuja kuitangua[32] Toraha, au Manabii: Mimi sikuja kuitangua, bali kuikamilisha. Kwa hakika Mimi nasema kwako, mpaka mbingu na Dunia zimepita, siyo herufi[33] moja au alama moja ya mkato[34] kwa namna yeyote ile

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1