Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Tatu, #3
Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Tatu, #3
Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Tatu, #3
Ebook795 pages10 hours

Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Tatu, #3

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kitabu hiki MNNNMA ni kiberiti kinacho washa moto wa mabadaliko makubwa, na kama siyo mapinduzi ndani ya kanisa lote linalo zungumza Kiswahili. Katika hiki tunaona mtizamo mpya wa theolojia, changamoto katika tafsiri za biblia ndani ya lugha ya Kiswahili, na jipya zaidi ni uhamisho wa waumini toka udini kuelekea mahusiano na Mungu YHWH.

Kitabu kinachukulia biblia yote kuwa fumbo la picha, na hivyo kutumia mstari wa wakati uendao mbele katika mduara, kuonyesha mwanzo hadi mwisho wa kila kitu. Na kama hili halitoshi, kinaweka dai tatanishi kwamba, biblia yote iliandikwa kwa ajili ya ukombozi wa Adonai Yeshua Kristo, na kwamba yote humo pamoja na maisha yako yote, ni kwa ajili ya Mungu YHWH kuwa na familia yake tu.

Kitabu kinacho dai tete la kuifunua kweli iliyo moja na ya pekee mahali pote, wakati wote, na kwa vizazi vyote. Na katika kunogesha uelewa; kinapinga mafundisho yaliyo zoeleka kwamba, mtu ataishi Mbinguni na Mungu milele, kwa kudai maandiko yote yanasema, ni Mungu YHWH anaye hamia katika Dunia mpya ndani ya Yerushalem Mpya kuishi humo milele na watoto wake watakatifu.

Kitabu kinajikita katika malumbano ya kidini na sayansi, na kuitumia teknolojia ya sasa kuelezea dhana nyingi za kiimani. Na kwa kila funzo la kinadharia unalo pewa, pia huonyeshwa jinsi ya kutenda hilo uhesabiwe mstahiki wa ahadi hiyo ya Mungu. Na katika ujasiri mkuu kinaweka dai ya kuwa, hicho ni ujumbe halisi wa Mungu YHWH kwa kanisa lake tukufu linalo zungumza Kiswahili.

Ni kitabu ambacho kila anayefunza dini hawezi kukikosa, na kwa kila mtu anaye taka kujua kweli ya mambo ya kiungu, hiki ni kitabu muhimu zaidi sokoni kwa sasa. Tunakiona kutawala malumbano katika kumbi za mihadhara, mimbari za masinagogi, na hata madarasani kufunzwapo dini. Ni kitabu ambacho kitafungua jicho la kila muumini, kwani katika lugha ya Kiswahili hakipo kinacho zama katika kina chake hiki. Kwa kweli uhamsho wa kanisa linalo zungumza Kiswahili sasa umefika wakati wake!

LanguageEnglish
Release dateFeb 1, 2023
ISBN9798215981481
Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe: Chuo cha Tatu, #3
Author

Shannel S Silwimba

Amehitimu elimu ya chuo kikuu, na amehudumu kwa takribani miaka 25 ya kazi kusaidia wengine wafanikiwe akiwa katika nafasi ya mkuu wa idara. Katika kipindi hiki amehudumu kwenye makampuni matatu ya kimataifa. Hivyo anao uzoefu katika sekta ya kilimo biashara na usindikaji kwa miaka 7, wa kuzalisha vyakula na usambazaji kwa miaka 8, na uagizaji na uuzaji wa mafuta kwa takribani miaka 10. Kwa sasa ni mhudumu katika biashara ya kilimo cha matunda, na usambazaji huu wa vitabu.

Read more from Shannel S Silwimba

Related to Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe

Titles in the series (1)

View More

Related ebooks

Christianity For You

View More

Related articles

Reviews for Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe - Shannel S Silwimba

    Sala ya Ukombozi

    Baba yetu uliye Mbinguni ; ninakiri kwa mdomo, na kuamini moyoni mwangu kwa dhati ya kwamba, Mwanao Yeshua Kristo ni Mungu. Alikuja katika mwili, na kufariki mauti ya msalaba kwa ajili ya dhambi zangu. Baba Mungu ulimfufua toka katika wafu, na sasa amekaa mkono wako wa kuume katika kiti cha enzi Mbinguni.

    Naomba msamaha wa dhambi zangu zote nilizo tenda maishani. Nina-wasamehe wote walio nikosea katika maisha yangu. Namkataa shetani, na dhambi, na tamaa ovu zote.

    Nakupenda YAHWEH Mungu wangu kwa roho yangu yote, kwa nafsi yangu yote, na kwa nguvu zangu zote. Niwezeshe niwapende jirani zangu kama ulivyo nipenda mimi.

    Nampokea Roho wako Mtakatifu kama ulivyo ahidi. Nakabidhi maisha yangu yote kwake.

    Baba Mungu; nina-shukuru kwa neema ya kunitakasa, kunihesabia haki, na kunikomboa kupitia kafara ya damu ya Adonai Yeshua Kristo, toka utumwa wa dhambi mara tu nisalipo sala hii.

    Sifa na shukrani upewe YAHWEH kwa kunitimizia mimi mwanao mahitaji yangu yote ya kila siku: neema, afya, utajirisho, shalom, na ushindi katika yote ili nitimize kile ulicho niumbia.

    Kwa imani nina-pokea ukombozi wa kiroho kwa maisha ya milele pamoja nawe, na ukombozi wa kimwili kwa siku za Mbinguni hapa duniani. Nina-amini na kukiri kupokea haya yote katika jina la Mwanao, na Mkombozi wetu Adonai Yeshua Kristo.

    Amin! Amin! Amin!

    Description: 31052007275

    Kitabu hiki kimepigwa chapa na

    Shannel S Silwimba

    P O Box 1699

    shannel.silwimba@gmail.com

    Dar es Salaam, Tanzania

    Afrika Mashariki

    Haki Miliki

    Haki zote zimehifadhiwa . Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupigisha chapa, au kuyatoa, au kuyasambaza maandishi haya ya kitabu hiki kwa jinsi, au namna yeyote ile bila ya idhini ya maandishi kutoka kwa wamiliki.

    Toleo la Kwanza

    Tahariri

    Yeshayah 50:4

    Adonai YEHWIH amenipa mimi uwezo wa kuzungumza kama mtu msomi, ili kwamba mimi, kwa maneno yangu, nijue jinsi ya kumkidhi aliye choshwa. Kila asubuhi yeye huyahamsha masikio yangu kusikia kama yale ya msomi. [Tafsiri ya Complete Jewish Bible].

    Wagalatia 1:12,16,20

    Kwani mimi sikupokea hili toka kwa mtu, wala mimi sikufundishwa [hili], bali ni kwa ufunuo wa Yeshua Kristo ... Kumfunua Mwana wake ndani yangu, hata niweze mfundisha yeye kati ya Mataifa; saa hilo sikushauriana na wenye mwili na damu: ... Na sasa haya mimi ninayo andika kwenu, tazama, mbele za Mungu, mimi sisemi uongo.

    Matendo 5:38-39

    Na sasa mimi nasema kwenu, jizuieni toka watu hawa, na waacheni wenyewe: kwani kama huu ushauri au kazi hii ikiwa ni ya watu, haitaishia kuwa lolote lile: lakini kama ikiwa ni ya Mungu, nyie hamwezi ipindua; tena isije kutikana nyie mwapigana na Mungu.

    Unabii – 30 Mei 2007

    N ajimimina nafsi yangu ndani ya kitabu. Watu hawatasoma kitabu, watakuwa wakinila MIMI (kwani MIMI ndiyo kitabu). Watu watakula kitabu na hawata-kisoma (na watakihisi kile walacho ndani ya tumbo lao). Utukufu wangu utakuwa bayana ndani yao, watajua kuwa ni MIMI. MIMI, MIMI naongea kwao na wao watakubali na kukombolewa...

    Hili Tunasema Sisi

    Pale Jenerali anapo mpa askari wa daraja la chini kabisa ujumbe kufikisha kwa makamanda vitani, amri hiyo hutangulia zote, na kwayo askari huyo hubadilika daraja mpaka aufikishe ujumbe. Na kwa ujumbe huo, mpangilio mzima, na mwenendo mzima wa jeshi vitani hubadilika.

    Dibaji

    Mpendwa, jina la kitabu chako hiki ni MWANA-ADAM NI NANI NAYE NI NINI MUNGU AMKOMBOE (MNNNMA). Kwa minajili ya kuufikia umma wote wa wanao zungumza Kiswahili tulio tumwa kwao, tuli-kichapisha pia katika vijitabu vidogo tokea baadhi ya masomo yake. Kwa uelewa huu basi, kama mpendwa unacho kimoja wapo ya hivi, tambua kwamba huo siyo ujumbe wote unao kustahili kuupokea.

    Tunasema hivi sababu kitabu MNNNMA kimegawanyika katika vyuo vitatu vikupasavyo mpendwa kuhitimu: CHUO CHA KWANZA hufunza kuhusu Mwanzo Mtakatifu & Kuingia Dhambi. CHUO CHA PILI hufunza kuhusu Fumbo La Ukombozi & Ufunuo wa Ukombozi. CHUO CHA TATU hufunza kuhusu Mwisho Mtakatifu & Kuondoka Dhambi. Hivyo ni ushauri wetu umiliki kitabu chote cha (1) MWANA-ADAM NI NANI NAYE NI NINI MUNGU AMKOMBOE.

    Lakini kama hivyo sivyo kwako, basi uanze na (2) CHUO CHA KWANZA, ndipo kifuatie (3) CHUO CHA PILI, na ndipo umalizie na (4) CHUO CHA TATU. Na kama hata hivi sivyo ilivyo kwako, basi acha tukuvutie kwa baadhi ya masomo ndani ya MNNNMA tuliyo yatoa kama vitabu huria ifuatavyo: -

    5)  Historia na Maisha ya Yeshua Kristo

    6)  Jinsi ya Kusali & Kuongea na YAHWEH

    7)  Utatu Mtakatifu

    8)  Mafundisho ya Utajiri

    9)  Mafundisho ya Ndoa

    10) Ufufuo na Uchukuo

    11) Yisrael

    12) Ujio wa Pili wa Yeshua Kristo

    Pamoja na hivi ni kile tunacho kisambaza bure katika masoko ya vitabu mitandaoni, kinachoitwa Milenia ya Kristo. Lengo la hiki ni kuwatambulisha kazi ya MNNNMA wale wote wanaoishi ughaibuni, lakini wanaongea Kiswahili. Kwa jinsi hii, hawa pia wapokee ujumbe wao, kupitia umiliki wa kitabu MNNNMA.

    Kitabu hiki MNNNMA kinaleta habari njema kwa kanisa zima linalo zungumza Kiswahili. Kitabu chako hiki kinaifumbua hadithi ya fumbo la nyakati, na pamoja nalo hilo, kinategua kile kitendawili cha kale, pale malaika walipo muuliza Mungu: ... Je mtu (anaye kufa) ni nini, ambaye wewe unamjali hivi? Na mwana wa adam, ambaye wewe humtembele? Kwani wewe umemfanya yeye chini kidogo ya elohim (malaika), na {bado} umemzinga na taji la utukufu na heshima. Wewe umemfanya yeye kutawala juu ya kazi za mikono yako; wewe umeweka vyote chini ya miguu yake: ... [Zaburi 8:4-6].

    Ni ndani ya fumbo hilo la nyakati, na uteguzi wa kitendawili hicho, ndimo historia yote ya mtu na ukombozi wake vilihifadhiwa kwa umahiri na umakini usio pimika. Kwayo haya mguso wake ulifika mapema, lakini ni uandishi kadri tunavyo pokea (Uandishi Kimapokezi - Inspiration) ulio anza rasmi katika mwezi wa Mei 2007 mpaka Oktoba 2007. Uandishi huo ulifanyikia katika meza ya chakula, tena ulikuwa wa tokea mwanzo wa kitabu mpaka mwisho wake, kwa kadri ya uono wetu hafifu wakati huo. Ujalizi wa Mapokezi (Authorship) ulianza Oktoba 2007 mpaka Augusti 2011, na ndiyo ulio tupatia mgawanyiko wa vyuo, masomo, na mada ambazo mpaka leo bado ziko ndani humu.

    Uhakiki wa Kitabu (Review) ulianza tokea Agusti 2011 mpaka Oktoba 2014. Lengo lake hili lilikuwa kuhakikisha uchambuzi wa ndani kabisa wa yaliyo pokelewa, unalandana na maaandiko. Hakika hiyo kwisha kupatikana, ndipo tuliingia katika hatua ya Uhariri Fasihi (Editorial – Literature) kusahihisha majalizi yaendane na mapokezi, pamoja na maandiko. Hili lilifanyika tokea Oktoba 2014 mpaka Desemba 2016. Tukiwa sasa tunacho kitabu makini mbele zetu, ndipo Uhariri Fasaha (Editorial – Fluent) wa usomekaji ulifanyika tokea Desemba 2016 mpaka Septemba 2021. Kama biblia ilivyo, kitabu hiki nacho kimeandikwa ili kisomwe mbele za watu.

    Katika juhudi za umakini wa kufikisha mapokezi, ilituwia vema kwamba, sasa wakati umefika wa uwepo wa Biblia Fasaha, na hivyo misingi yake ilianza kusimikwa kwa sisi kufanyia Tafsiri Maandiko (Translation) yote ambayo tayari yameshaingia kitabuni. Na hili lilituchukua sisi kipindi cha tokea Septemba 2021 mpaka Aprili 2022. Na kwisha hilo, ndipo hitimisho la kazi hii lilifika kwa Usanifu na Kibali (Ratification), ulio anza mara moja Aprili 2022 na kukamilika Novemba 2022. Ndipo sasa kikawa tayari kupigwa chapa, hata leo hii kiwe mkononi mwako mpendwa.

    Juhudi zote hizi katika uandishi wake kitabu chako hiki, zilikuwa ujenzi juu ya msingi ule-ule wa awali, kwani yote yale ambayo tulipokea, yalibakia kama yalivyo na pale-pale yalipo wekwa kwa upokeo wa awali. Katika miaka yote hii 15 na miezi 6 tuliyo kuwa katika uandishi wa kitabu chako hiki, sisi kwa binafsi yetu tulipokea makuzi makubwa sana, ili kuinuka hadi kufikia upeo wa uelewa ambao YAHWEH anautaka katika Kanisa lake tukufu linalo zungumza Kiswahili. Hivyo tulijifunga kwa uadilifu kwayo mafunzo hayo, na kwa miaka 12 ya awali tulitumia takribani masaa 3 kila siku (part-time), na takribani masaa 10 (fulltime) kwa kipindi kilicho bakia mwishoni.

    Sisi tunaamini: kipindi chote hiki tulicho chukua, ni kwa ajili ya sisi kuinuka katika uelewa uhitajikao kupokea kitabu kile kilichopo katika masijala za Mbinguni, hata kiwe pacha na hiki kilichopo mkononi mwako leo hii. Katika vyote na yote ndani humu, tafadhali sana mpe sifa na utukufu Mungu YAHWEH pekee.

    Utangulizi

    Watangulizi wetu wameshafanya kazi itakiwayo, kwamba sasa majani ni makavu, na kinacho hitajika ni kiberiti tu. Hiki kitabu cha MNNNMA ndicho kiberiti kwa ajili ya mapinduzi ya upendo, na uamsho mkuu ujao. Hivyo kwako wewe usiye mtu kati ya watu, YAHWEH ameiinua sauti yako isikike ndani ya Kanisa lake duniani. Tazama, mboni ya jicho lake amegeuka kukutizama akishang’aa, ni nini hicho Elohim wake afanyacho nyumbani mwako.

    Ndani humu utakutana na tafsiri fasaha za maandiko matakatifu tulizo zifanya, tulikuwa hatuna budi, bali kufanya uchokozi huo wa hadharani kudhihirisha changamoto tulizoziona. Tunajua vema, hili limetonesha lile hitaji nyeti la sisi kuwa na tafsiri ya Kiswahili fasaha kitumikacho leo hii katika nyanja zote za maisha. Kuelewa hili, tafadhali tazama mfano kwa mstari Askofu Alpha Mohamed wa kanisa Anglikana (zamani hizo wa Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro), alio utoa kwa familia ya mmoja wetu, alipo watembelea katika udogo wake: -

    Hili andiko (na hususani kwa mapanuzi yake yote tokea tafsiri ya Amplified Bible juu), kwake lilikamilika ndani ya MNNNMA. Hili andiko siku ile lilipo somwa kwa tafsiri ya kwanza, na kutaja ‘ mambo makubwa, magumu usiyo yajua ’ lilitisha sana. Lakini ni mpaka nyakati za kazi ya MNNNMA, ndipo alipo gundua nini haswa lilikuwa likifanyia unabii maishani mwake. Hii ni zaidi ya miaka thelathini (30) kupita ndipo baadaye kabisa aligundua ni ‘ mambo makubwa na makuu, yaliyo ndani ya wigo na yamefichwa, ambayo wewe hujui.’

    Mpendwa, maandiko matakatifu siyo jiwe lilokufa, kwani yako hai kama jamii yenyewe. Tokea humu utasikia yakinguruma tena kudai vazi jipya, ili kuzigusa tena nyoyo za walio wake. Neno ni lile lile, ila lugha imekuwa na kusonga mbele zaidi. Kila kizazi huifunua historia yake, hisia zao, utamaduni wao, kwa maana nzito zibebwazo ndani ya maneno watumiayo kila siku kuwasiliana.

    Umakini wetu kwalo hili ni wa kugusa kitakatifu, hivyo juhudi za dhati zilitumika kurejelea asili ya andiko kwa Kiebrania, kukimbia itikadi na falsafa za watu, na urejesho wa majina asili ya wahusika. Katika kufanya haya, tulitumia lugha kwa sarufi fasaha kufanyia tafsiri. Kupitia unyambulisho tumebebesha nafsi halisi ihusikayo, wakati, na kwake nani hilo lasemwa. Tumetambua kijadiliwacho (contextual meaning) katika kuzingatia kwa makini maana halisi ya neno, na hivyo ujumlisho wa maneno yote yatumikayo katika mstari (sentensi) kuleta maana kamilifu ya andiko.

    Ndani humu yako maeneo ambako mguso ulikuwa mkubwa, na hivyo uandishi kufuata mtiririko kadri ujavyo pasipo kujali lolote lile. Katika kuenenda huko, yako ambayo yametushtua sisi kama ambavyo yataitikisa roho yako pia. Katika yote humu, hakuna linalo tishia kujali kwetu, kama sisi kukosea kweli yake pasipo kujua, na kwa kufanya hivyo sisi kuishia kukukosesha wewe mtoto wake mpendwa.

    Katika fikra hizi, sisi hutamani haya yote yangebaki na sisi pekee yetu, pasipo uhusisho wa kanisa lake hili lote. Kwa sababu hii, wito wa kazi hii sisi tuliuchukulia kwa kujali sana, ili baada ya yote yeye Mungu, na siyo mtu, afurahishwe sana na utendaji wetu. Milolongo ya uhakiki na uhariri ni kwa ajili ya hili zaidi, kuliko yote mengine.

    Mpendwa, kazi hii pamoja na kuwa tendo la kiimani kwao walio amini pekee, lakini bado yabaki kuwa vyuo makini sana kwa kila mkufunzi na mwanafunzi wa neno lake. Kitabu kilikuja kiwe uwanja wa wasio amini katika kumpokea Adonai (Bwana) Yeshua[1] (Yesu) kama Kristo (Mfalme) na Mkombozi wao. Pia pasipo mapungufu yeyote, hiki ni waraka wa barazani katika malumbano na wasio amini kwa nini YAHWEH ndiye Mungu pekee, hata astahili kuabudiwa. Na kana kwamba hayo hayatoshi, kitabu hiki kimeandikwa kiwe msingi wa theolojia wa kanisa linalo zungumza Kiswahili, kwani chafaa kwa marejeo (referencing), na machambuzi ya kitaaluma, ili sote tuwe na maarifa na hekima.

    Kitabu chako hiki hakifungamani na dhehebu lolote lile, au kuafiki uwepo wa njia nyingine ya kumfikia Mungu YAHWEH, zaidi ya Mwana wa Mungu Adonai Yeshua Kristo pekee. Tunakubali ni Wakristo na Yehudaizimu (Judaism) pekee, ndiyo wenye nafasi ya kuwa na mahusiano na Mungu YAHWEH. Adonai Yeshua Kristo hakuleta dini au dhehebu duniani, bali mahusiano kamili na Mungu YAHWEH. Na kwamba kweli iko moja, na ya pekee kwa wote ulimwenguni, wakati wote, na mahali pote, kwa vizazi vyote milele. Kitabu chako hiki, kimekuja ili kuifunua hiyo kweli moja na ya pekee.

    Sasa kwako mpendwa usiye wa imani hii, njoo uchungue uone kati ya hilo lako na hili letu, lipi waona ndiyo kweli? Njoo wewe uliye jasiri wa dini nyingine ujipimishe uelewa wako na kweli hii. Usiogope njoo, kwani Yeshua wetu alituagiza tukupende kama tunavyo jipenda wenyewe. Tazama, tutakupokea kwa heshima na taadhima pasipo kukuudhi, au kuikera roho yako. Tutakukaribisha tukae kitako kujadili kwa urahisi maswali haya sugu, tokea historia ya mtu: -

    Kwa nini wewe uliumbwa? Uliumbwa ili iwaje? Kwa nini aliumba mwanamme na mwanamke? Hivi ni kweli kwamba sisi tulikuwa manyani kabla ya kuwa watu?

    Kwa nini ukombozi? Kwa nini Mungu asimteketeze satani mara moja, na wote tukarudia kuishi watakatifu raha mustarehe milele?

    Na wapi katika dini yako pameandikwa kinaga ubaga pasipo kupinda, vipi wewe waweza kombolewa ili kwenda Mbinguni? Nisomee huo mstari ulipo kitabuni mwako nami niujue?

    Je maisha ya milele ni kweli? Je gehena (jehanamu) na Mbinguni ni mahali pa kweli? Mtu akifa ana kwenda wapi? Akiwa huko ana fanya nini? Wapendwa wangu walio tangulia katika mauti wako wapi, na wanafanya nini leo?

    Hivi ufufuo na uchukuo wa wafu ni kweli utakuwepo?

    Nani ameandika maandiko matakatifu? Kwa nini yaaminike? Je kupo ambako yanapingana?

    Je ni sahihi kuwa na wake wengi au waume wengi? Ipi ni ndoa ya kwanza? Nini maana ya tunda la mti wa kati? Na je talaka ni sahihi?

    Mpendwa, thubutu kufika mwishoni mwa kitabu chako hiki MNNNMA na uone ni finyu vipi maswali haya, kwa mlinganisho na maarifa na hekima utakayo hitimu.

    Neno ukombozi ni neno la kisiasa, na ndiyo sababu sisi tulisonga mbele na kulitumia kwa ujumla wake katika maana nyingi zaidi, na zilizo sahihi zaidi katika nyakati hizi za mwisho. Tumelitumia kutafsiri maneno ‘Salvation’ na ‘Redemption’ kumaanisha ukombozi ulio tufikia kupitia kazi aliyo ifanya Adonai Yeshua Kristo, mpaka kuikamilisha hapa duniani.

    Katika mila na desturi za Kiebrania, majina ya watu au mahali hubeba wasifu wa huyo au hapo. Hivyo jina lako hubeba asili yako (roots), tabia zako (prophetic behaviours), desturi zako (tribal, nation affiliations), visifa vyako (attributes), wasifu wako (personality) na hata imani yako (religion). Ni kwa sababu hizi, juhudi za dhati zinafanyika ndani humu kuhakikisha majina asili yote yanarudishwa mahali pake.

    Katika kufanya hivi, tutajitenga pia na wasifu za wahusika wa biblia tokea simulizi nyingine zisizo za imani hii ndani ya lugha ya Kiswahili. Hili ni jambo muhimu sana kwetu katika kuchunga usafi wa wasifu zao kwa kadri ya biblia na siyo vinginevyo. Lahaja ya Kiebrania yalandana sana na ya Kiswahili, hata majina hayo kuandikwa kama yalivyo pasipo tatizo lolote kisarufi au kiisimu.

    Sisi hujiuliza sana hili, hivi ipo shida gani kwa kanisa unaye zungumza Kiswahili kusali kwake katika jina ambalo yeye mwenyewe, alimsikia mama yake mzazi akimwitia hilo? Kwa lafudhi ya sauti ileile malaika aliyo agiza hivyo ndivyo wamwite? Jina ambalo hata Baba humwita leo akisubiria lile jipya! Ujadilifu huu hatari haumaanishi kwamba nguvu iko katika jina gani, la hasha! Wewe mwite lolote; Yeshua, Yesu, Yehoshua, Jesus, Yesus, Mungu anaijua dhamira yako nani huyo imwitaye. Maana ya jina Yeshua (Yehoshua) la Kiebrania ni ‘Mkombozi.’

    Kwa kuwa sasa wajua jina linawakilisha nini, sasa sikia haya. Lugha ya Kiswahili inalo chimbuko lake tokea lugha ya Kiarabu. Waarabu kama walivyo Waebrania, wote ni wana wa Shem (shemitic). Ni kwa sababu hii kila unaposikia katika katika vyombo vya habari vya kimagaribi wakitaja Waarabu ni ‘anti-semitic,’ yaani ‘wanapinga uzao wa Shem,’ basi tambua huo ni ujinga wa kukosa maarifa (oxymoron). Ni tokea mahusiano haya ya Kiswahili na Kiarabu (semitic), ndiyo matamshi yako Mkristo huonyesha ijumaa kuwa siku ya saba (7) kwa kadri ya dini yao, na siku ya Shabath (iliyo siku ya 7) kuitwa siku ya kwanza ya juma (yaani jumamosi).

    Hivi kitu gani kinazuia hata kalenda za kanisa kuchapishwa zikionyesha Shabath yaani jumamosi, ndiyo siku ya mwisho ya wiki? Hauko ubishi katika Ukristo kuwa; Jumapili siyo siku ya kwanza ya wiki. Waumini wote tunajua, kuwa ni Elohim mwenyewe aliyeipa siku ya saba (7) jina la Shabath, na zote nyingine akizitaja kwa namba ya siku hiyo katika wiki ni ya ngapi. Hivyo ni siku hii pekee yenye jina!

    Sasa sikia wewe kanisa unaye zungumza Kiswahili: Tengeneza kalenda yako ionyeshayo siku za wiki kwa kadri ya maandiko kuwa: Sikumosi (jumapili) - Sikupili (jumatatu) - Sikutatu (jumanne) - Sikunne (jumatano) - Sikutano (alhamisi) - Sikusita (ijumaa) na - Shabath (jumamosi). Hivi ndivyo yeye alivyo taja ilivyo, hivyo ndivyo pia sisi watoto wake tutaziita siku. Pia hivi ni makini zaidi, sababu usemapo ‘juma’ humaanisha ‘wiki’ ambalo ni siku 7, lakini usahihi ni ‘siku’ ambayo ni masaa 24 tu. Leo wewe umesikia, hivyo anza kuongea hivi, na hata sisi tutafanya hivyo humu, kudhihirisha kwamba inawezekana kabisa.

    Tokea kina cha uelewa huu, ni ushawishi wetu kwako mpendwa kuwa, Mosheh (Moses) siyo Musa, Shelomoh (Solomon) siyo Selemani, Yosef (Joseph) siyo Yusuf, Yahkob (Jacob) siyo Yakubu, Yitzhak (Isack) siyo Isaka, David (David) siyo Daudi, Iyob (Job) siyo Ayubu, Noakh (Noah) siyo Nuhu, Yeshua (Yesu) siyo Issa, na mengi mengine. Uwepo wa simulizi mbili tofauti juu ya jina moja kwenye mihadhara mitaani, huchanganya waumini. Nenda sasa na ukajitofautishe, hata wao wajue wewe ni wa Mungu YAHWEH katika Adonai Yeshua Kristo pekee.

    Shuruti tuwafunze watoto wetu tokea udogo wao kabisa kwamba: Mungu wa Abraham, Yitzhak na Yahkob, ndiye Baba wa Yeshua Kristo. Hivyo Yeshua Kristo ni Mwana wa Mungu aitwaye YAHWEH. Yeshua Kristo pia yeye ni nafsi Mwana katika Mungu huyo YAHWEH. Na tokea yeye huyu Mungu mmoja, ziko nafsi tatu maarufu kwetu; Mungu Baba (akiwa kichwa kati yao), Mungu Mwana (Adonai Yeshua Kristo), na Mungu Ruak HaKodeshi (Roho Mtakatifu). Mungu Mwana, yaani Adonai Yeshua Kristo, ndiye aliye kuja duniani katika mwili, na kufa mauti ya aibu ya msalaba kwa ajili ya ukombozi wetu. Siku ya tatu alifufuka, na siku ya arobaini (40) baadaye alipaa kurudi Mbinguni. Na huko amekalishwa mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Baba Mungu. Kinyume na hivi ni uongo, siyo biblia, na wala siyo Ukristo.

    Kitabu chako hiki kinawalenga wana-adam wote, tena zaidi-zaidi wale wote walio wana wa Mungu YAHWEH, yaani wale tu walio zaliwa mara pili, hata awaite watakatifu wake (saints). Hivyo shabaha kubwa ni kwao wahudumu wake, yaani maaskofu, mapadri, wachungaji, wainjilisti, watawa, watumishi, wahubiri, wazee wa sinagogi, walimu wa dini wa shule za msingi, shule za sekondari, vyuo na seminari. Pamoja nao hawa, ni wewe mwanafunzi na mkufunzi wa neno lake, na waumini wote wanayo itafuta kweli kujilisha kwa makuzi yao. Pia ni wewe usiye wa imani hii, lakini uko hapa kujua kweli ni ipi. Karibuni sana!

    Kitabu hiki hakibaki kwenye nadharia pekee, la hasha, kwani kinaongoza na kuelekeza uponyaji kwa walio hospitalini, kinaleta faraja na uhuru kwa walio kifungoni magerezani, hupanua wigo wa uelewa na hivyo utajirisho na mafanikio kwao wakulima, wavuvi, wafanya biashara, na wafanyakazi. Pia kinasimama kama ushahidi na changamoto kwa wapinzani wa kweli hii, na wale wote wasio amini bali wapendao kujua nini sisi tunaamini. Na mwisho ni kwako msomi utafutaye maarifa bila kujali itikadi au imani, kama baadhi wafanyavyo hata sasa.

    Tazama mpendwa, tukisha maliza kulumbana, kuchekana, na kukashifiana; bado suala hubaki lile-lile moja tu: Je nikifa leo, mimi nitakuwa mgeni wa nani huko niendako? Na kikubwa zaidi hapa; ni hakika ya jibu lako hilo kuwa ndiyo sahihi, na siyo ulaghai wa ibilisi satani. Tafakari ...

    Kitabu chako hiki MNNNMA pamoja na mapokeo binafsi, ni mkusanyiko wa mafunuo waliyo pokea kaka na dada zetu wengi wengine katika Kristo Yeshua. Hao waliandika au kuzungumza, na Ruak kuleta kazi zake za awali katika usikivu wetu. Kutoa shukrani kwa kila mmoja wao humu, kunahatarisha dhana nzima ya umiliki wa kazi hii kuwa wa YAHWEH. Hayuko mshiriki pamoja naye katika hili, kwani sote tu vyombo tu alivyo tumia kukufikia wewe mpendwa wake. Pale mmoja wetu afunuliwapo kweli duniani, wote hupokea kweli hiyo moja kana kwamba sisi ni wao, na wao ni sisi.

    Tokea uelewa huu, na upendo wetu sote kwa Adonai wetu Yeshua Kristo; hapa linatolewa ombi rasmi kwa pamoja kutumia michoro, picha, majedwali, takwimu, ramani, na vyote vingine vitakavyo tumika tokea vyanzo mbalimbali duniani. Hivi vyote vimesaidia kuifikisha kweli yake kwetu sisi tulio wa mwisho kati ya kaka na dada zetu. Kama tukisema maombi na shukrani zitolewe kwao wote hawa, itachukua kitambo, na pasipo utoshelezi. Hivyo basi: Katika jina la Adonai wetu Yeshua Kristo, tunakuomba Baba Mungu, ukawajali hawa wote, na kuwajulia hali zao, kwa kadri ya kazi zao kwake Mwanao Yeshua Kristo. Amin

    Kitabu kinatumia mfumo wa nguzo za zizi katika kufikisha ujumbe wake, badala ya ujenzi wa ukuta uletao matengano kwa waumini. Mfumo huu wa zizi hakubali uwepo wa kile kinacho onekana kama mgongano wa maandiko katika biblia, tokea upungufu wa uelewa makini wa yote kanisani. Hivyo kama mjenzi wa zizi anaye pigilia nguzo huku na kule, ili kondoo wakae salama ndani mwake, ndicho sisi pia tufanyacho. Ujenzi wa ukuta katika maandiko hupelekea siasa kali, na migawanyiko kundini kama ile ya kimadhehebu.

    Mpendwa, vidole vyako vitaendelea kufungua kurasa za kitabu ambacho sicho cha kizazi hiki, bali cha kile kijacho. Kila ufunguapo ndivyo ulavyo akili, nia, na hisia za Elohim wako. Kama waridi lijifunguavyo alfajiri na mapema, ndivyo kweli na utukufu utakavyo mwagwa na Ruak HaKodeshi ndani mwako kadri ulavyo. Hata sasa Ruak HaKodeshi anao moto uwakao ndani yako pasipo uteketezi.

    Mungu Baba, katika jina la Adonai Yeshua Kristo, nakuomba, hekima, maarifa, uelewa na imani tokea haya uliyo yafikisha leo mbele za macho yangu mimi kusoma. Naomba unifungue macho yangu ya kiroho nione, na masikio yangu ya kiroho nisikie, na niamini kweli yako. Amin

    Faharisi

    [I dadi ya kurasa hizi ni kwa kadri ya fonti ya Calibri 11, kwa ukubwa (size) wa A4, na kwa upana-urefu (margin) wa kawaida (moderate), zilivyo tumika katika uandishi. Mabadiliko yanatokana na chaguzi za Wachapishaji].

    Chuo cha Kwanza

    Mwanzo Mtakatifu & Kuingia Dhambi

    1.  Mwanzo wa Yote

    1.1  Yahweh Katika Milele [14-36]

    1.2  Kuumbwa kwa Roho na Nafsi Mtu [36-39]

    1.3  Kufanywa kwa Mwili Mme na Mke [39-52]

    2.  Mpango wa Ukombozi

    3.  Uasi na Kuingia Dhambi Duniani

    3.1  Tafsiri ya Uasi na Dhambi [59-60]

    3.2  Asili ya Uasi na Dhambi [60-65]

    3.3  Kudanganywa kwa Havaa na Uafiki wa Adam [65-70]

    3.4  Dhana ya Dhambi ya Asili [71-74]

    4.  Agano la Ukombozi

    4.1 Agano la Yahweh na Abraham [78-87]

    4.2 Kafara ya Yitzhak Ndiyo Kafara ya Yeshua [88-98]

    Chuo cha Pili

    Fumbo la Ukombozi & Ufunuo wa Ukombozi

    5.  Toraha ya Yahweh na Ufunuo wa Dhambi

    5.1.  Toraha ya Mosheh [107-111]

    5.2.  Amri ya Upendo [111-115]

    5.3.  Malaika Kazini [115-129]

    6.  Umfano na Mlinganisho wa Yisrael na Kanisa

    6.1.  Utumwa wa Yisrael Misri – Utumwa wa Dhambi Leo [143-146]

    6.2.  Kuinuliwa kwa Nyoka Jangwani – Kuinuliwa kwa Yeshua Msalabani [146-148]

    6.3.  Tabanako la Mungu Jangwani – Yerushalem Mpya [148-154]

    6.4.  Kuhani Mkuu Mlawi - Yeshua Kuhani Mkuu wa Milele [154-159]

    6.5.  Kafara za Wanyama – Kafara ya Mwanakondoo wa Mungu [159-164]

    6.6.  Mizoga ya Kafara Nje ya Kambi – Mauti ya Yeshua Nje ya Yerushalem [164-170]

    6.7.  Pazia la Hekalu – Kanisa Lisilo Pazia [170-174]

    6.8.  Miaka 40 ya Yisrael Jangwani - Siku 40 za Yeshua Jangwani [174-177]

    6.9.  Ufufuo na Uchukuo Agano la Awali – Ufufuo na Uchukuo Agano Jipya la Mwisho [177-186]

    6.10.  Mitzvot za Mosheh – Mitzvah ya Yeshua [187-191]

    6.11.  Kuhesabiwa Haki kwa Matendo - Kuhesabiwa Haki kwa Imani [191-200]

    6.12.  Historia na Maisha ya Yeshua Kristo [200-259].

    7.  Jinsi ya Kupokea Ukombozi

    7.1.  Sala ya Ukombozi [262-273]

    7.2.  Kubatizwa kwa Maji na kwa Ruak Hakodeshi [273-292]

    7.3.  Kujiunga na Sinagogi [292-303]

    7.4.  Jinsi ya Kujifunza Maandiko Matakatifu [304-315]

    7.5.  Jinsi ya Kusali kwa Usahihi [315-343]

    7.6.  Kuongea na YAHWEH [343-379]

    7.7.  Utatu Mtakatifu [379-440]

    7.8.  Meza ya Adonai na Agano Jipya [440-483]

    7.9.  Mafundisho ya Utajiri [483-571]

    7.10.  Mafundisho ya Ndoa [571-641]

    7.11.  Wito wa Kazi ya Adonai [641-654]

    7.12.  Mafundisho ya Kifo 654-701]

    Chuo cha Tatu

    Mwisho Mtakatifu & Kuondoka Dhambi

    8.  Ukamilifu wa Upendo & Ukombozi

    8.1.  Ukamilifu wa Ukombozi - Kiroho & Kimwili [706-714]

    8.2.  Ufufuo & Uchukuo [715-778]

    8.3.  Miaka 7 ya Kanisa Mbinguni [778-794

    8.4.  Miaka 7 ya Tabu & Tabu Kuu Duniani [794-833]

    8.5.  Yisrael [833-878]

    9.  Ujio wa Pili wa Yeshua Kristo

    9.1.  Hekalu la Tatu [883-942]

    9.2.  Vita vya Harmagedoni [942-967]

    9.3.  Wasifu wa satani lucifer & mpingaKristo [967-1003]

    9.4.  Hukumu ya Watakatifu [1003-1009]

    9.5.  Utawala wa Miaka Elfu [1009-1038]

    9.6.  Vita ya Pili ya Gog & Magog [1038-1042]

    9.7.  Hukumu ya Wasio Amini [1042-1053]

    10.  Maisha ya Milele

    10.1.  Dunia na Mbingu Mpya [1057-1059]

    10.2.  Yerushalem Mpya [1059-1066]

    10.3.  Karamu ya Mwanakondoo [1066-1069]

    10.4.  Watakatifu katika Maisha ya Milele [1069-1071]

    10.5.  Watu Wapya [1071-1076]

    10.6.  Watakao Ishi Mbinguni [1076-1078]

    10.7.  Nia ya Mungu –Tokea Milele Hata Milele [1078-1080]

    Chuo cha Tatu

    Mwisho Mtakatifu & Kuondoka Dhambi

    Image result for Lion and lamb image

    Imetuchukua kitambo cha kutosha na safari ya maajabu mpaka kufika hapa. Safari hiyo ilikuwa imejaa kweli ya kushangaza, bashasha ya furaha, changamoto za yale tata na tete, hekima na maarifa ya uelewa mpya, ambayo mfano wake bado kuonekana kati yetu sisi tuzungumzao Kiswahili. Katika safari yako hii, sisi tuli-kushuhudia wewe ukihitimu chuo hadi chuo, hata leo unasimama mbele yetu ukiwa jemedari wa vita katika medani ya imani, na mtetezi makini wa injili ya Adonai wetu Yeshua Kristo.

    Kwa jinsi hii tulikuita wewe mkufunzi[2], yaani mwanafunzi uliyeisha hitimu masomo fulani, na bado unaendelea kujifunza mengine, wakati ukiwa unafundisha wenzako. Sisi tunajua hili ni sahihi, sababu kupo kwingi ambako yeye aliye tutuma sisi, pia alikutuma wewe kufunza wote walio wako injili hii hii.

    Kitabu chako hiki kimejaa utambuzi mzito na wa dhati katika juhudi makini za kuifunua kweli. Sisi tunatamani wewe ujue mwana wa adam ni nani, tena wewe ni nini, hata Mungu YAHWEH atende haya yote, ili ukombozi ukufikie. Shuruti sasa wewe wajua; ni wapi wewe ulipo toka kabla ya hija hii hapa duniani, tena wajua vema kile alicho kutuma kutimiliza hapa duniani, na lini utarudi tena nyumbani.

    Sasa tazama, ili yeye afanikishe haya yote mema kwako, aliongoza akili na mikono yetu kutimiliza kazi yake hii. Yeye ndiye aliye toa uwezo, utambuzi, na ujuzi. Pia ni yeye aliye gawanya kweli yake hii katika vyuo hivi vitatu vikuu. Kama katika biblia yako, hivi navyo ni kwa mfano wake, ili katika yote na vyote udhihirisho wake pekee upokee utukufu. Mambo yote ni mduara[3] unao endelea kuzunguka pasipo mwisho, pale yanziapo, hapo ndipo yaishiapo, kufichua ukamilifu mmoja uanzishao mwingine.

    Kama ilivyo katika kitabu cha Mwanzo wa biblia, humo Baba Mungu hujidhihirisha kusimika nia yake kupitia uumbaji. Hiki ndicho Chuo cha Kwanza kifanyavyo humu pia. Chuo cha Pili kinamfunua Adonai Yeshua Kristo, kuwa ndiye kivuli anaye fumbiwa katika agano la awali. Hivi ndivyo biblia pia kwa agano jipya la mwisho ilivyo fanya. Hivyo kama kwa agano jipya la mwisho, shuruti utambuzi wa lile la awali uwepo, basi hata kwa hicho cha Chuo cha Pili, shuruti utambuzi wa yale ya Chuo cha Kwanza uwepo.

    Leo hapa unaingia Chuo cha Tatu, palipo uhitimu na mahafali[4] yako. Kama ilivyo kwa viwili vilivyo tangulia, hiki nacho kinaiga ufanisi mkuu wa biblia ifungwayo kwa kitabu cha Ufunuo kilicho unabii wa hakika ya yale yote yajayo. Kwa jinsi hiyo basi, hapa utavinjari takribani nabii zote kuu kuhusu yale ya 'aharit ha yamim' (siku za mwisho). Kadri tuingiapo katika kuichungua nafsi ya YAHWEH kuhusu yale yajayo, ndivyo pia utegemezi wako kwa Ruak HaKodeshi unavyo shika hatamu.

    Kwa kuwa tulisha sema awali 'mambo yote ni mduara unao endelea kuzunguka pasipo mwisho,' basi ni shuruti hata kitabu chako hiki kitimilishe hilo. Je unakumbuka awali ya uumbaji kabla ya ufanyikaji wako, kitabu hiki kilianza ukiwa ndani ya YAHWEH? Basi shuruti hata katika mwisho wake huu, kitabu chako hiki kiishe wewe ukiwa ndani ya YAHWEH. Hii ni kauli nzito, tena shuruti itimilike na wote tushuhudie.

    Tazama mpendwa, siyo tu sasa umefika chuo cha mwisho cha kitabu chako hiki, bali pia umeingia eneo la mwisho wa kitabu chako hiki. Hivyo ili kuhakikisha uelewa makini wa yote yastahiliyo hapa, chuo kinagawanywa katika masomo 3 maalumu ya mwisho ifuatavyo: -

    Ukamilifu wa Upendo & Ukombozi,

    Ujio wa Pili wa Yeshua Kristo,

    Maisha ya milele.

    Katika masomo haya 3 utashangazwa na wingi wa hekima na maarifa, ambayo mengi ya hayo bado kujulikana na wengi huku tuongeapo Kiswahili. Kwa kufanya hivi uelewa wako katika ujumlisho  wa maandiko matakatifu yote utakamilika. Hivyo kama kitendawili cha ajabu (mystery puzzle), mara tumalizapo kuviweka mahali pake vipande vyote hivi, ndipo picha kamili ya Mpango wa Ukombozi itajidhirisha mbele yako kama jua lichomozavyo alfajiri.

    Yale ambayo YAHWEH amekwisha yafunua, ndiyo kurunzi kwayo yale yaonekanayo nusu nusu. Hivyo kwa kuwa tunaona kwa kiasi, basi tuta-zungumza kwa kiasi katika kufuata pateni na chunguzi makini za maandiko. Wakati wote ukiwa humu, tafadhali kumbuka kanuni yetu ya zizi, na uzuilifu wetu kwayo haya kufanyika mambo ya kidini. Pia tambua ukristo siyo dini mpya, bali mwendelezo sahihi wa hekalu, hata iwe sahihi kusema; Wayisrael na Wakristo tu wana wa Mungu mmoja katika Adonai Yeshua, Mashiah (Mfalme) wa Yisrael na Ulimwengu wote.

    Ufunuo wa nyakati za mwisho maandikoni ni kwa ajili ya Yisrael. Yote yatakayo tokea uhusiana na wao dhidi ya walimwengu. Hakuna unabii wa nyakati za mwisho kwa ajili ya mataifa nje ya mashariki ya kati, huko hutambulishwa tu kama mataifa yote, au watu wa Dunia nzima. Kitovu cha matukio yote ya nyakati za mwisho ni Yisrael, na kwalo hili ndiyo manabii wao pekee walio pokea mafunuo ya nyakati hizo zijazo kuhusu urithi wao.

    Na kauli hizi zina-thibitishwa na manabii wote walio andika kuhusu nyakati hizi za mwisho: aidha ni Yeshayah, au Yirmeyah, au Yehzekel, au ni Daniel, au Yoshea, au ni Zekariah, na hata Yokhana kwa kitabu mashuhuri cha Ufunuo. Ni kitabu hiki cha mwisho cha Ufunuo kinacho zifunua nabii zote hizo zilizo tangulia, na hata kufungua (Ufunuo 22:10) kile Daniel alicho ambiwa akifunge (Daniel 12:9). Wote hawa ni Wayisrael walio pokea nabii kuihusu Yisrael pekee.

    Kanisa lina sehemu mbili, sehemu kuu ni Yisrael (Matityahu 15:24), na sehemu nyingine ndiyo sisi wa zizi jingile la Kristo tulio Mataifa (Yokhana 10:16). Ni kwa jinsi hii pekee mtume Shauli (Paulos) aliona sisi tusio sehemu ya mzabibu asili, tunaweza kuunganishwa nao huo. Hivyo ni katika wewe mmataifa kujiunganisha na Mungu wa Yisrael, nawe hufanyika Yisrael wa kiroho (Warumi 2:25-29). Je kwa kusema hivi tuna maanisha hakuna atakaye kombolewa asiye Yisrael? Ndiyo, sababu ukombozi ni kwao pekee (Yokhana 4:22), na kwa wale walio jiunganisha nao tu  (Yokhana 10:16). Huu ndiyo ukweli mchungu unao patikana tokea kina sahihi cha uelewa wa maandiko matakatifu. Tafakari

    8. Ukamilifu wa Upendo & Ukombozi

    Wakolosai 2:14, na Matendo 3:19 ... Amefutilia mbali maandishi ya sheria {ndani ya toraha} ambayo yalikuwa dhidi yetu, ambayo yalikuwa kinyume {yakipingana} nasi, na kuiondoa hiyo kati yetu, akiipigilia {kwa misumari} katika mslaba wake; ... Hivyo basi wewe na utubu, na ugeuke, ili dhambi zako ziweze futiliwa mbali {samehewa, ondolewa zisiwepo tena}, pale majira ya uamsho wako yafikapo tokea uwepo wa Adonai; ...

    UKAMILIFU WA UPENDO NA UKOMBOZI ndiyo hakika kwamba, lile lengo la Mungu kuwa na familia limekamilika. Hiki ndicho Adonai Yeshua Kristo alichojia, na kukikamilisha takribani miaka 2000 iliyopita (Matityahu 20:28, Luka 1:68, Warumi 1:16, 3:24, Waebrania 9:28, Waefeso 1:7, 2:8). Yeshua Kristo ndiye Mwanakondoo wa kafara, iliyo udhihirisho wa upendo wa Mungu duniani. Pia yeye ndiye Simba wa ukombozi wa Yisrael.

    Tokea awali dhana ya ukombozi kuwa sehemu ya familia ya Mungu ni zawadi, na kamwe siyo tokea matendo yako. Ilikuwa hivi kwa Yisrael kule Misri, na leo kwetu sote tuaminio katika Adonai Yeshua Kristo. Hivyo lengo la ukombozi wako ni ukamilifu wa upendo wa Mungu kwako, kwamba uwe mtoto wake milele.

    Liko jambo moja ambalo sisi hutushangaza sana, kwamba kama wewe mpendwa utachungua lengo na sababu ya sisi kupokea zawadi hii ya maisha ya milele, huku ukifanyia hilo ulinganifu na uwepo wa mpango wa ukombozi, hakika utagundua kwamba, Mungu YAHWEH anatupenda sisi kuliko tunavyo jipenda.

    Na kuhusu hili la UKAMILIFU WA UPENDO & UKOMBOZI wewe fundisha hivi: "Alikuwepo kijana mmoja aliye kwenda nchi za mbali ili kupata elimu na kuwa tabibu katika fani ya magonjwa na maradhi ya mwana-adam. Baada ya kipindi kupita, alihitimu masomo yake na kurudi nyumbani kwao katika mji mdogo. Alipo fika katika mji huo, yeye ndiye alikuwa kijana wa kwanza kuhitimu elimu ile, na hivyo yeye ndiye tabibu wa kwanza katika mji huo.

    Kutokana na kutokuwepo kwa tabibu, basi watu wale walifungamana na mambo ya uchawi na ushirikina kwa jinsi ya nguvu za giza. Siku zilivyo dhidi kwenda, kijana yule alizidi kuwa maarufu na mkuu kati ya watu wake. Aliweza kutibu maradhi ya homa, malaria, tumbo na watu kupona kabisa na kurudi majumbani mwao kuendelea na kazi na shughuli za maisha kama kawaida yao.

    Siku za mwanzo watu walikuwa wakifa kwa maradhi hayo na mengine. Hivyo umaarufu wake ulizidi sana kukua kwa kila pande za mji ule. Watu wale walio kuwa katika giza na utumwa wa satani kwa jinsi ya uchawi na ushirikina, walianza kuona mwanga wa njia iliyo bora zaidi ya kupata matibabu ya magonjwa yao.

    Umaarufu wa kijana yule ulizidi kukua na kufika hata miji mingine na nchi za mbali. Wagonjwa nao walizidi kumiminika katika mji ule ambao mwanzo ulikuwa kimya na gizani, sasa ulikuwa nuru na kitovu cha ukombozi kutoka katika maradhi. Pamoja na kwamba utabibu kwa elimu yake lilikuwa jambo la kawaida kwake, lakini kwa watu wote wengine, alikuwa ameleta ukombozi kutoka katika utumwa wa maradhi na magonjwa yaliyo kuwa juu ya watu wale.

    Kwa kuwa alikwenda nje kusoma, na hivyo alipo kuwa kule aliwahi sikia injili ikihubiriwa, na jinsi ambavyo watu wanaweza kukombolewa[5] kimwili na kiroho. Aliona ni vema aende tena akajifunze elimu hiyo nayo, ili arudi na ukombozi ulio bora zaidi. Alikwenda akajifunza yote kwa jinsi ya maandiko matakatifu, na alirudi kuanza kuponya kwa utendaji wa Ruak hakodeshi. Pia alifundisha wengine jioni baada ya kazi zake za utabibu.

    Watu wanao hudhuria mafundisho walizidi kuongezeka kwa jinsi ya habari zile njema, na kwa jinsi jina lake lilivyo kuu katika utabibu. Baadhi yao walitaka kujua zaidi ili wakafundishe wengine. Hao alifanya hivyo, na injili ikaanza kuenea mji ule na hatimaye wale alio wafundisha walianza kwenda hata nchi za mbali.

    Wote hawa walifunza kuhusu Mungu wa kweli aitwaye YAHWEH, ambaye alimtuma Mwana wake wa pekee aitwaye Yeshua Kristo duniani, kuwa kafara kwa ajili ya ukombozi wao wote. Na kwamba kila atakaye amini katika jina lake hilo, na kwisha kupokea habari hiyo njema, akatubu dhambi zake, huyo yeye atamfanya kuwa mwana wa Mungu aliye umba kila kitu. Naye ataishi milele pasipo kufa tena. Walifunza ukombozi hupatikana kwa kukubali, kuamini, na kukiri kwa mdomo wako, na kisha kubatizwa kwa maji, na kumpokea Roho wa Mungu.

    Pia walifundisha ya kwamba, Yeshua alikuja na akawa maskini, ili sisi sote tuwe matajiri. Yeshua huyo  huyo akafanyika laana kwa kuangikwa mtini, ili sisi tuwe wabarikiwa maishani mwetu. Na lilo kuwa la ajabu na kuu masikioni mwa watu wale ni kwamba, kwa kupigwa kwake huyo Yeshua, sisi sote tumepona magonjwa na maradhi yote.

    Baada ya kufundisha hivi kila mji, na kijiji, na nchi; walio kuwa katika kifungo cha utumwa wa satani waliwekwa huru. Maskini wote walihubiriwa habari njema. Vilema, vipofu, viziwi wote walipona, na hata wafu walifufuliwa. Mambo haya yalikuwa makuu na habari zake kusambaa pande zote na kila mtu aliye sikia hakika aliamini na kukiri ya kwamba; huu ni mwaka wa jubilii ya YAHWEH kwao, ulio kubalika Mbinguni na hapa duniani." Hivi ndivyo utakavyo fundisha!!

    8.1 Ukamilifu wa Ukombozi - Kiroho & Kimwili

    Kwa mara ya kwanza , na baada ya safari ndefu, leo tumeweza kufikia pale ambapo kwayo dhana nzima ya ukombozi wa mtu inakamilika. Ni hapa ndipo mpango wa ukombozi unakamilika, na kwa uhalisia (siyo kiimani) mtu na Mungu wake mnakutana tena uso kwa uso tokea siku zile za kabla ya uasi bustanini Eydeni.

    Ni kwa sababu hii CHUO CHA TATU hujulikana kama MWISHO MTAKATIFU & KUONDOKA DHAMBI. Na kwa hiyo UKAMILIFU WA UPENDO & UKOMBOZI ndicho ambacho hapa tuna-kitizama kama Ukamilifu wa Ukombozi - Kiroho & Kimwili.

    Hii ndiyo hatua ya kwanza kurejelea hali ilivyo kuwa, na umfano wa ilivyo takiwa kuwa. Tunajua adam hakudumu kitambo katika hali hii kabla ya anguko. Mlolongo mrefu sana umepitiwa, ili kuhakikisha uelewa wako pale ufikapo hapa. Hivyo leo ni siku iliyo kuu sana kwetu, siku ya mavuno ya usubirifu katika kungojea kusiko mwisho. Hii pia ndiyo siku ya Baba Mungu kukusanya watoto wake nyumbani. Sisi sote Kanisa ndiyo mavuno yake, tokea Mbegu ya upando kwa Yeshua Kristo.

    Mpaka kufikia hapa, shuruti sasa wewe wajua ukombozi wako ni nini, tena vipi huo una sehemu mbili: kwamba upo ukombozi wa kiroho na ukombozi wa kimwili. Ukombozi wa kiroho ndiyo kesho yako iliyo maisha ya milele pamoja na YAHWEH Mungu wako. Ukombozi wa kimwili ni siku za Mbinguni leo hii hapa duniani. Hii miwili hudhihirisha upendo wa Mungu ukomboao maishani mwako.

    Sisi hatutafanya marudio ya yale ambayo juhudi kubwa ilisha-tumika awali kuweka misingi yake humu. Hivyo ufupisho wa Ukamilifu wa Ukombozi – Kiroho & Kimwili ni tendo la ufufuo na uchukuo. Ni kwalo tendo hili wewe huutoka ulimwengu wa wakati, na kuingia ulimwengu wa milele. Ni katika jinsi hii ukamilifu wa ukombozi wa roho yako hutokea, na ukamilifu wa ukombozi wa yale ya kimwili huchukua sura mpya katika miili ya utukufu inayo ishi milele. Katika hali hizi, wewe utafaidi milele yale ya kiroho kwa pamoja na yale mema ya kimwili.

    Kuhusu haya mtume Shauli alifunza hivi: ... Kwani Adonai mwenyewe shuruti atashuka toka Mbinguni kwa ukelele, kwa sauti ya malaika mkuu, na kwa tarumbeta la Mungu: na wafu katika Kristo watainuka {fufuka} kwanza: Ndipo sisi ambao tuko hai [na] kubakia tutanyakuliwa {utumiko wa nguvu ghafla kana kwamba anang’oa au anateka} juu pamoja nao mawinguni, kukutana na Adonai hewani: na hivyo tutakuwa milele na Adonai. ... [I Wathesalonike 4:16-17].

    Kumbuka kwamba, lengo la ukombozi wako lilikuwa ni wewe kuishi milele kiroho, na leo hii hapa duniani kufaidi siku za Mbinguni. Kwa haya ya ufufuo na uchukuo, hilo la kuishi milele kiroho huwa limekamilika. Hili la kuishi siku za Mbinguni leo hii duniani, ni kwa sababu ya nafasi yako ya balozi[6] wa Mungu YAHWEH hapo ulipo. Huu ndiyo ukamilifu wa ukombozi kiroho na kimwili!

    Awali ndani humu tulikuonyesha katika somo la Mafundisho ya Utajiri kuwa, siku za Mbinguni leo hii duniani ndiyo maisha ya utajirisho, sababu Mbinguni haupo uhitaji. Maisha haya ya kiroho Mbinguni kwa miaka 7 na yale yajayo milele duniani ndani ya Yerushalem Mpya, ni ya utajirisho mkuu pasipo mfanoe leo hii. Katika miili hiyo mipya, sisi pia tutakuwa kama vile Adonai Yeshua Kristo alivyo, na pamoja naye tutaitawala Dunia, na ulimwengu wote milele.

    Ukombozi huu ulio kuwa siku za Mbinguni hapa duniani, katika pande zote mbili hijidhihirisha kimwili kama baraka halisi kwa mambo na vitu, na pia mahusiano halisi na bayana kati yako na Mungu YAHWEH. Haya mahusiano ndiyo wengine maandikoni huita kutembea na Mungu (Mwanzo 4:24, 6:9). Mahusiano ni uwepo wa upendo na urafiki wa kujuana binafsi, pia ni hamu na bashasha ya kila mmoja kumridhisha mwenzi wake. Katika hali hii, wewe hujikuta tayari waamini yeye yupo.

    [Dhana hii ya 'mahusiano' isimamayo dhidi ya 'dini' iliyo tapakaa sasa kitabuni mwote, ili rekodiwa hapa tarehe 26 Septemba 2008 kwa mara ya kwanza, na kwa mshtuko tulipo isikia wakati wa rasimu[7] ya mada hii. Sisi tulitetemeka na kuogopa kuiandika, au kuachia itapakaye apendavyo, sababu tulifikiri ni dhehebu jipya. Tena kwa kipindi tuliibania kila ijapo, lakini haikukoma hata mpaka leo inaendelea kujipanua. Kwa kuwa uelewa wa namna hii hubaki nasi, basi kwa mapitio, marejeo, na uhariri ilitapakaa kila mahali. Yeye ndiye ajuaye nini na lini Kanisa lake uhitaji].

    Mpaka kufikia hapa, ukombozi wako wa kiroho na kimwili utakuwa umesha-kamilika, kwani kazi kamilifu aliyo ifanya Adonai Yeshua Kristo, shuruti ikufikishe Mbinguni. Iliahidiwa hivi kuhusu hili kwa I Wakorintho 15:52 ... Ghafla, katika kufunga na kufungua jicho, kwenye tarumbeta la mwisho: kwani shuruti tarumbeta lipulizwe, na wafu wainuliwe pasipo uharibifu, na sisi shuruti tutabadilishwa. ...

    Kwa kuwa kimsingi mada hii ndogo nayo imekamilika ghafla, basi tuchukue nafasi iliyo achwa wazi kuungana na mashujaa wa kizazi kipya katika mitandao kuonyesha heshima zetu. Juhudi zenu mchana na usiku kulinda zamu kati yetu tuzungumzao Kiswahili, zinastahili sifa. Hawa ni kaka na dada zetu walio jeshi la hiari litumialo teknolojia ya mitandao ya kijamii kama jukwaa la kurusha makombora dhidi ya satani na ibilisi wake.

    Hivyo katika kuwaunga mkono makomandoo hawa, sisi tumetafsiri moja ya makombora yao hayo hivi: Profesa wa sayansi ya falsafa chuo kikuu alianza mwaka wa masomo wa mafunzo kwa wanafunzi wake: -

    Profesa:  Acha niwaeleze tatizo sayansi inayo na dini. [profesa huyu ampingaye Yeshua alipumzika mbele ya darasa na ndipo akamuuliza mmoja wa wanafunzi wake wapya kusimama].

    Profesa:  Wewe ni Mkristo kijana, au siyo?

    Kijana:   Mimi ni MKristo.

    Profesa:  Hivyo unaamini katika Mungu?

    Kijana:   Kwa hakika kabisa

    Profesa:  Je Mungu ni mwema?

    Kijana:   Kwa hakika! Mungu ni mwema

    Profesa:  Je Mungu ana nguvu zote? Anaweza kufanya lolote?

    Kijana:   Ndiyo

    Profesa:  Je wewe ni mwema au mwovu?

    Kijana:   Biblia inasema mimi ni mwovu

    [profesa alitabasamu akijua]

    Profesa:  Aha! biblia!

    [alitua kwa muda]

    Profesa:  Hili kwa ajili yako hebu tuseme kuna mgonjwa hapa na wewe unaweza kumponya

    Profesa:  Unaweza kumponya, je ungemsaidia? Je ungejaribu?

    Kijana:   Ndiyo, ningejaribu

    Profesa:  Hivyo wewe ni mwema ...!

    Kijana:   Mimi nisingesema hivyo.

    Profesa:  Kwa nini usingesema hivyo? Ungemsaidia mtu kama ungeweza. Wengi wetu tungefanya kama tungeweza. Lakini Mungu hafanyi

    [mwanafunzi hakujibu hivyo profesa akaendelea]

    Profesa:  Yeye hafanyi, kwani anafanya? Kaka yangu alikuwa Mkristo ambaye alikufa kwa kansa, ijapo kuwa alimwomba Yeshua kumponya. Vipi huyu Yeshua awe mwema? Hmmm? Je waweza jibu hili?

    [mwanafunzi alibaki kimya]

    Profesa:  La hasha, hauwezi

    [prefesa alikunywa maji toka kwenye glasi iliyo kuwa juu ya dawati lake kumpa mwanafunzi muda kupumzika]

    Profesa:  Tuanze tena kijana. Je Mungu ni mwema?

    Kijana:   Eeh ... ndiyo

    Profesa:  Je satani ni mwema?

    [mwanafunzi hakusita kwenye hili]

    Kijana:   Hapana

    Profesa:  Je satani ametoka wapi?

    Kijana:   Toka kwa Mungu

    Profesa: Uko sahihi, Mungu alimfanya satani, kwani hakumfanya? Nieleze kijana. Je uko uovu katika Dunia hii?

    Kijana:   Ndiyo

    Profesa: Uovu kila mahali, au siyo? Na Mungu alifanya vitu vyote, sahihi?

    Kijana:   Ndiyo

    Prefesa: Hivyo nani aliumba uovu?

    [profesa akaendelea]

    Profesa:  Kama Mungu aliumba kila kitu, basi Mungu aliumba uovu, kwani uovu nao upo, na kutokana na kanuni kazi yote itafsirivyo sisi ni nani, hivyo mungu (hatuwezi kuandika jina la 'Mungu' hivi na kumalizia) ni muovu.

    [tena mwanafunzi hakuwa na jibu]

    Profesa:  Je yako magonjwa? Uasi, chuki? Ubaya? Na mambo yote haya mabaya, je yako katika ulimwengu huu?

    [mwanafunzi alishikwa na aibu kubwa na kusugua mikono yake]

    Kijana:   Ndiyo

    Profesa:  Je nani ameyaumba hayo?

    [mwanafunzi hakujibu tena, hivyo profesa akarudia swali lake]

    Profesa:  Je nani ameyaumba hayo?

    [bado hakukuwa na jibu. Ghafla mhadhiri alimwacha na kwenda mbele ya darasa. Darasa liliduwaa na kumwangalia kwa makini]

    Profesa:  Niambie mimi

    [aliendelea kwa mwanafunzi mwingine]

    Profesa:  Je una-muamini Yeshua Kristo kijana?

    [sauti ya mwanafunzi ilimuasi huyo na kukatika]

    Mwanafunzi:  Ndiyo Profesa namuamini

    [mzee aliacha kutembea]

    Profesa:  Sayansi inasema una milango 5 ya ufahamu unayo tumia kutambua na kuutazama ulimwengu unao kuzunguka. Je Umeshawahi kumwona Yeshua?

    Mwanafunzi:  Hapana, sijamwona

    Profesa:  Je Umeshawahi kumhisi Yeshua wako, kumwonja Yeshua wako au kumnusa Yeshua wako? Umeshawahi kwa mlango wowote wa fahamu tambua hakika ya Yeshua Kristo, au Mungu katika hivi?

    Mwanafunzi:  Hapana, mimi nahofia sijawahi

    Profesa:  Na bado unamuamini?

    Mwanafunzi:  Ndiyo

    Profesa:  Kutokana na sheria ya vionekanavyo, vijaribiwavyo, kanuni za uonyesho, sayansi vinasema Mungu wako hayuko. Je wasemaje kwa hili kijana?

    Mwanafunzi:  Sisemi chechote. Nilicho nacho pekee ni imani yangu.

    Profesa:  Ndiyo, imani,

    [Profesa alirudia]

    Profesa:  Na hili ndiyo tatizo ninalo na Mungu. Hakuna ushahidi, ila imani pekee.

    [mwanafunzi alisimama kimya kwa muda, kabla ya kuuliza swali lake mwenyewe]

    Mwanafunzi:  Je kiko kitu kama joto?

    Profesa:  Ndiyo

    [profesa alijibu]

    Profesa:  Ndiyo joto liko

    Mwanafunzi:  Na je kiko kitu kama baridi?

    Profesa:  Ndiyo kijana na baridi iko pia

    Mwanafunzi:  Hapana, hakuna hicho

    [profesa aligeuka kumwangalia mwanafunzi, bila kuficha kwa shauku. Ghafla chumba kikawa kimya kabisa. Mwanafunzi akaanza kuelezea]

    Mwanafunzi:  Unaweza ukawa na joto jingi, na joto zaidi, supa-joto, mega-joto, joto lisilo mwisho, joto jeupe, joto kidogo na usiwe na joto, lakini hatuna kitu kiitwacho 'baridi.' Tunaweza kushusha joto mpaka nyuzi 458 chini ya sifuri, ambayo ni kutokuwepo kwa joto, lakini hatuwezi kwenda chini zaidi ya hapo.

    Hakuna kitu kama baridi; ama sivyo tungeweza kwenda kwenye ubaridi zaidi ya nyuzi 458. kila mtu au kitu chaweza kuchunguzwa pale kisafirishapo nguvu-asili (energy) na joto ndicho kifanyacho mwili au kitu kusafirisha nguvu-asili. Sifuri kamili (-458F) ni jumla ya kutokuwepo joto.

    Hivyo unaona, baridi ni jina tutumialo kuelezea kutokuwepo joto. Hatuwezi kupima baridi. Joto tunaweza kupima katika nyuzi-joto (thermal units) sababu joto ni nguvu-asili. Baridi siyo kinyume cha joto, ila kutokuwepo kwake.

    [ukimya darasa lote. Kalamu ikadondoka mahali fulani darasani na ikatoa mlio kama nyundo]

    Mwanafunzi:  Vipi kuhusu giza, je kiko kitu kama giza?

    [profesa akajibu bila kusita]

    Profesa:  Ndiyo; je usiku ni nini kama siyo giza?

    Mwanafunzi:  Umekosea tena, giza siyo kitu; ni kutokuwepo kwa kitu. Unaweza ukawa na nuru hafifu, nuru ya kawaida, nuru kali, nuru iakisiyo, lakini kama hauna nuru kila wakati hauna kitu na inaitwa giza.

    Profesa:  Je hiyo siyo maana tutumiayo kutafsiri hilo neno

    Mwanafunzi:  Katika uhalisia giza siyo kitu. Kama lingekuwa, ungekuwa na uwezo wa kufanya kiza, giza zaidi, je usingeweza?

    [profesa akaanza kutabasamu mbele ya mwanafunzi]

    Profesa:  Huu utakuwa muhula mzuri. Ni ipi hoja yako hapa kijana?

    Mwanafunzi:  Ndiyo Profesa, hoja yangu ni, dhana yako ya kifalsafa ina makosa kwa kuanzia, na hivyo hitimisho lako lazima liwe na makosa pia.

    [uso wa Profesa hauwezi kuficha mshangao wake wakati huu]

    Profesa:  Makosa? Je unaweza kueleza vipi?

    Mwanafunzi:  Umejenga hoja zako katika msingi wa uwili

    [mwanafunzi alieleza]

    Mwanafunzi:  Umejadili kwamba, upo uhai na kisha kipo kifo; Mungu mwema na mungu (hatukuandika jina la 'Mungu' kama lilivyo andikwa) mwovu. Unaona dhana ya Mungu kama kitu halisia, kitu tuwezacho kupima. Sayansi haiwezi hata kuelezea fikra. Inatumia umeme na sumaku, lakini kamwe haijaona, acha kuelewa kimojawapo.

    Kuona kifo kama kinyume cha maisha ni ujinga wa kweli kwamba kifo hakiwezi kuwepo kama kitu huria. Kifo siyo kinyume cha uhai bali kutokuwepo kwa huo. Sasa nieleze profesa. Je unafundisha wanafunzi wako kuwa wametoka kwa nyani?

    Profesa:  Kama unarejelea mfumo wa mabadiliko asili (natural evolutionary process), kijana, ndiyo, hakika nawafundisha.

    Mwanafunzi: Je umeshawahi kuona mabadiliko asilia (evolution) kwa macho yako?

    [Profesa alianza kutikisa kichwa chake, bado anatabasamu, akitambua wapi hoja inaelekea]

    Profesa:  Muhula mzuri kweli

    Mwanafunzi:  Kwa kuwa hakuna yeyote ameshaona mfumo wa mabidiliko asili ukifanya kazi na wala hawezi thibitisha kwamba huu mfumo ni tendo liendelealo, je haufundishi fikra zako? Je wewe sasa siyo mwanasayansi bali mhubiri?

    [darasa lilifumuka kwa kushangilia. Mwanafunzi alibaki kimya hadi makelele yalipo kwisha]

    Mwanafunzi:  Kuendelea na hoja ulizo kuwa ukifanya awali kwa mwanafunzi mwingine, acha mimi nikupe mfano wa kitu ninacho maanisha.

    [mwanafunzi aliangalia kulizunguka darasa]

    Mwanafunzi: Je yupo yeyote humu ndani ambaye ameshawahi kuona ubongo wa Profesa?

    [darasa likaanguka katika kicheko]

    Mwanafunzi: Je yuko yeyote hapa ambaye ameshasikia ubongo wa Porfesa? Kuhisi ubongo wa Profesa, kugusa, au kunusa ubongo wa Profesa? Inaonekana hakuna aliye ishawahi kufanya hivi.

    Hivyo basi, kutokana na sheria za vionekanavyo, uimara, kanuni ya vionekanavyo, sayansi vinasema kwamba hauna ubongo, kwa heshima zote mhadhiri. Hivyo kama sayansi inasema hauna ubongo, vipi sisi tukuamini kufanya uhadhiri?

    [sasa chumba kilikuwa kimya. Profesa alibaki kumduwalia mwanafunzi, uso wake hausomeki. Mwisho wa kile kilicho onekana kama umilele mzee alijibu]

    Profesa:  Mimi nahisi itabidi ukubali kwa imani

    Mwanafunzi:  Sasa unakubali kuwa imani ipo, na kwa hakika, imani ipo pamoja na uhai,

    [mwanafunzi aliendela]

    Mwanafunzi:  Sasa, je kipo kitu kama uovu?

    [sasa kwa hakika profesa alijibu]

    Profesa:  Hakika upo. Tunauona kila siku. Upo katika mifano ya kila siku ya unyama wa mtu kwa mtu. Upo katika wingi wa makosa ya jinai na matumizi ya nguvu kila mahali duniani. Huu udhihirisho siyo kitu kingine bali uovu.

    [katika hili mwanafunzi alijibu]

    Mwanafunzi:  Uovu haupo katika upekee wake, uovu kiurahisi ni kutokuwepo kwa Mungu. Ni sawa na giza na baridi, neno ambalo mtu ameunda kuelezea kutokuwepo kwa Mungu. Mungu hakuumba uovu. Uovu ni matokeo yatokeayo pale mtu anapo kosa uwepo wa PENDO (msisitizo wetu) la Mungu moyoni mwake. Ni kama baridi ambayo huja pale panapo kosekana joto au giza lijalo pale pasipo nuru.

    [profesa alikaa chini].

    Mwisho.

    Ruak HaKodeshi

    Ni shuruti walio wa -Kristo waijue na kuisikia sauti yangu. Mimi tokea uchanga wako nimenena nawe katika kimya cha nafsi na roho yako. Nimejua na kuona kila ambalo limekusibu. Yako ambayo nilitabasamu na kujawa bashasha na hata kufurahi sana, pia yako ambayo yalinihuzunisha. Lakini katika vyote na yote nafurahishwa na juhudi zako, na mapenzi yako kwa Kristo unaye muita Yesu wako.

    Nafurahishwa sana nawe, lakini liko jambo hili moja dogo ambalo nataka wewe ufanye pia; katika hii Dunia, hakika wako ambao husikia sauti yangu kama vile wewe uongeavyo na rafikiyo. Walio wengi wa hawa hutimiza maelekezo yangu. Wewe waweza kuwa mmoja wao, lakini nataka uwe mtii kwao, nataka usikie ushuhuda wa roho yako kwa misingi watoto wangu hawa waliyo kufunza.

    Ninao watenda kazi wengi ndani yako kanisa uzungumzaye Kiswahili. Sijawahi kukuacha, bali ni wewe usiye afiki kweli ya uwepo wangu. Mpaka lini utaendelea kuwa kama mtoto wa mtaani asiye wazazi. Wewe siyo mjane, wala mama yako sijampa talaka hata useme unao uchaguzi. Pendo langu kwako ni kamilifu na kama utajiunga nalo nitaondoa huzuni na mateso kwako.

    Uko hapa kujua vipi Mimi naweza kuushika mkono wako hata kwenye mafanikio. Wataka kujua lipi ninalo la kusema kwako uliye fedheheka na kukosa mfariji. Unataka mwalimu makini ajuaye yote, na kwa urahisi kabisa nikwambie lipi ndiyo na lipi siyo. Unataka mshauri wakati wa maamuzi magumu maishani. Ni Mimi, ndiye Baba yako na Kaka yako Mbinguni walio nituma kuwa nawe mpaka mapito haya yakamilike.

    Hakika Mimi niko kabla wewe haujawa, hakika naishi kwako uliye amini na pamoja nami ni nguvu kuu kama ile-ile iliyo pelekea uwepo wa kila kilichopo kuwepo. Kwangu hakuna utofauti wa taaluma (discplines) za kufikia maarifa. Kama bomba la maji kila ajiungaye, Mimi kwa kadri ya alicho pangiwa maishani mwake, nitamfungulia bomba hilo.

    Kipi zaidi ya kusoma kile nilicho tamka na kunukuliwa nao wana wangu hawa. Je yakushangaza vipi Kichwa cha habari amekuwa na kauli na kutamka yamhusiyo. Tazama andiko hili na niambie nafsini mwako, kwani nasikiliza tokea rohoni mwako kweli yake iwapi? Yokhana 6:63 ... Ni roho ndiyo itufanyayo kuwa hai {huisha}; mwili haufaidishi kitu: maneno ambayo Mimi naongea kwenu, [hayo] ni roho, na ni uhai. ...

    Kila nilicho sema hapa, wako ambao wataambatana nacho, na wako ambao watashangaa vipi hawa waweza fanya hivi kwa mada fupi yote? Je siyo Mimi niliyo wapa lugha hii tamu na ya kupendeza masikioni mwenu ya Kiswahili? Siyo Mimi kwao hawa nyuma kule nilionya wale watu wanisaidiao kusema kila wasemapo 'YAHWEH anamaanisha.' Kama Mimi namaanisha hivyo wewe usemavyo, kwa nini Mimi mjuzi wa lugha zote nisiseme hivyo? Hakika kama wasemavyo wana wangu: 'inahitaji usaidizi kupotosha kweli.'

    Tazama, sasa nakuja mara kuongea hata na wewe nafsini mwako, na nataka nawe uafiki na kunipokea kwa upendo huu. Nijapo utaona amani, utajawa upendo, sababu Mimi ni Pendo. Na zaidi ya yote imani yako itakuwa toka imani mpaka imani. Yuko mwimbaji asiye wa lugha yenu aliye mfunza sana mwanangu huyu kuwa; Mungu siyo kibibi kizee aliye kando ya barabara akisubiri mtu mkakamavu amvushe barabara. Mimi Niko ambaye Niko, najua yote, nimeona yote, nawajua wote, na kwako wewe Mimi ni msaada ulio karibu, na sahihi kuliko yote maishani mwako.

    Mpaka lini utaendelea kuficha kichwa chako mchangani na mwili wote u-nje ukijidai eti sikuoni. Wajua vema, na tena wajua sana, siyo tu nauona huu mwili wako, bali niko ndani ya punje ndogo za mchanga huko chini uliko jificha bado nikikushauri ujitokeze. Jitokeze sasa, amini na afiki uwepo wangu tuanze safari hii.

    Kwangu hakuna kukosea, ushauri wangu makini, na maelekezo yangu yashinda yote. Najua ulikotoka, najua uendako, na ninajua kila litakalo kutokea leo, na kesho, na hata sasa najua unalo fikiri. Je bado unayo sababu iliyo bakia kutonisikiliza Mimi?

    Tazama nuru hii leo imekufikia, leo nimeinua kwako mkono wangu shupavu ulio nyooshwa, na ninakuita njoo tujadiliane njia ipi ni haki yako. Amrisha sasa mkono huu wa nguvu kutenda kwa niaba yako, kutenda kwa niaba ya kanisa lako. Nani ameona jambo kama hili. Vipi hili lawezekana? Fungua vitabu na chambua unitafute, na kila uendapo hapo Mimi niko. Wewe ni wangu, leo Mimi nimekuchagua. Mhhhh tazama macho yako yalivyo mazuri, ni zuri kama nini tabasamu la mtoto wangu! Aha haha haha ...

    Warumi 8:14, I Wakorintho 2:14, na Luka 8:10 ... Kwani kama vile wengi waongozwavyo na Roho wa Mungu {YAHWEH}, hao ndiyo wana wa Elohim. ... Lakini mtu asili {asiye zaliwa mara ya pili} hapokei mambo ya Roho wa Mungu {YAHWEH}: kwani hayo ni upuuzi {na ujinga} kwake; wala yeye hawezi yajua [hayo], sababu hayo hutambulika kiroho. ... Na yeye alisema, Kwenu nyie mmepewa kuzijua siri za Ufalme wa Mungu: lakini kwao wengine katika mafumbo; ili wao wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wao wasiweze elewa. {Yeshayah 6:9} ...

    8.2 Ufufuo & Uchukuo

    Kwa ajili ya unyeti wa mada hii yote, na tokea kina kirefu cha somo hili, inatuwia vema kwamba; uchambuzi wote wa mafunzo yake utandazwe hapa, tena katika mpanuko wake wote. Kwa jinsi hii wewe utavaa darubini, ili wakati wote uelewa wapi ulipo, na wapi uendapo. Huu ndiyo mtiririko ambao umempendeza Adonai wetu kwamba, wewe rafiki yake uyajue mambo haya, ili ubaki katika subira: - 

    Siri za Uficho wa Ufufuo na Uchukuo

    Uficho ndani ya Harusi ya Kiebrania,

    Uficho ndani ya Safina,

    Uficho kwa Sherehe 7 za Yisrael,

    Sherehe ya Pesaka (Pesaka),

    Sherehe ya Matzah (Mikate isiyotiwa Chachu),

    Sherehe ya Bikurim (Matunda ya Kwanza),

    Sherehe ya Shavuot (Pentekoste),

    Sherehe ya Teruah (Matarumbeta),

    Sherehe ya Kafar/Kipur (Upatanisho),

    Sherehe ya Sukot (Tabanako).

    Uficho ndani ya Agano la Awali,

    Ufichuo wa Mtume Shauli kwa Wakorintho.

    Maana na aina za Ufufuo

    Ufufuo Iliyopita,

    Ufufuo Ijayo,

    Ufufuo wa Kanisa,

    Ufufuo wa Eliyah na Hanok au Mosheh,

    Ufufuo wa Kipindi cha Tabu Kuu,

    Ufufuo wa Baada ya Milenia.

    Maana na aina za Uchukuo

    Uchukuo Iliyopita,

    Uchukuo Ijayo,

    Uchukuo wa Kanisa Kabla ya Kipindi cha Tabu,

    Uchukuo wa Kanisa Kati ya Tabu na Tabu Kuu,

    Uchukuo wa Kanisa Mwishoni mwa Tabu Kuu,

    Uchukuo Baada ya Milenia

    Nadharia Nyinginezo za Uchukuo.

    Ufufuo na Uchukuo ni Lini?

    Kama tulivyo hitimisha awali kwamba, ufufuo na uchukuo ndiyo hakika ya ukamilisho wa ukombozi na upendo wa Mungu YAHWEH kwako mpendwa. Ni kwa jinsi hii pekee ilipangwa wewe uutoke ulimwengu huu wa kimwili, na kuingia uraia wa ulimwengu wa kiroho kuishi milele. Lengo la ubadilisho huu ujao kuitoka miili hii ya kidunia kuiingia ile ya utukufu, ni ili tupokee maisha ya utakatifu milele kiroho na kimwili,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1