Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Ramani ya Kiswahili
Ramani ya Kiswahili
Ramani ya Kiswahili
Ebook266 pages1 hour

Ramani ya Kiswahili

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Ramani ya Kiswahili ni kitabu ambacho kina uwezo wa kusaidia walimu na wanafunzi wakati wanafanya marudio yao. Kitabu chenyewe kimegawanyika katika sura kumi na moja. Baadhi ya sura hizo zinahusiana na lugha, ngeli za maneno, sauti, silabi, vitate, visawe, vitawe, aina za maneno, shamirisho, chagizo, kijalizo, uchanguzi wa sentensi, aina za sentensi, viambishi na viungo vingine vya sarufi. Baada ya kila sura, kuna maswali ya kukusaidia wakati wa kudurusu.

 

 

LanguageKiswahili
PublisherKelvin Munene
Release dateOct 25, 2022
ISBN9798215647455
Ramani ya Kiswahili

Related to Ramani ya Kiswahili

Related ebooks

Reviews for Ramani ya Kiswahili

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Ramani ya Kiswahili - Kelvin Munene

    SURA YA KWANZA:  SARUFI

    MAANA YA SARUFI

    Sarufi ya lugha ni mfumo wa kanuni zinazomwezesha mtu anayezungumza au kuandika lugha, kuunda sentensi sahihi zisizokadirika idadi, na ambazo zitaeleweka kwa watumiaji na wazawa wa lugha hiyo wanaposoma maandishi au kusikiliza mazungumzo.

    Kanuni zinazotumiwa kuangazia sarufi sanifu ya lugha ya kiswahili ni: hali ya matamshi ya herufi na vitamkwa vya lugha, maana ya lugha pamoja na matumizi ya lugha, miundo ya lugha, miundo ya lugha na maumbo ya lugha.

    TANZU ZA SARUFI

    1)  Sarufi maana/Semantiki – tanzu hii hujihusisha na maana mbalimbali za maneno na tungo za wazi. Aidha huelekeza namna ya kuchunguza tungo ili kupata maana, hasa iliyofichika.

    2)  Isimu jamii – tanzu hii hujishughulisha na kaida na adabu ya matumizi ya lugha. Hueleza aina ya lugha inayoruhusiwa kutumika na watu wa umri, vyeo, na hali mbalimbali katika muktadha na mazingira tofauti tofauti na kwa sababu maalumu.

    3)  Maumbo/Mofolojia – hushughulikia jinsi herufi zinavyounganishwa kujenga maneno na kazi kazi zake katika tungo.

    4)  Sarufi miundo/sintaksia – ni utanzu unaoshughulikia mpangilio au mfuatano wa maneno katika tungo ili yalete maana iliyokusudiwa.

    5)  Sarufi matamshi/Fonologia – hushughulikia matamshi ya vitamkwa kwa kuelekeza jinsi na mahali pa kutamkia katika kinywa cha msemaji.

    ––––––––

    UMUHIMU/DHIMA YA SARUFI

    a)  Kanuni huwawezesha watu kutenga vipengele vya lugha vya kufunza na kufanyia mazoezi.

    b)  Huwapa watumiaji ufahamu wake na uwezo wa kufafanua mfumo wa lugha.

    c)  Huhakikisha ulinganifu katika matumizi ya lugha ili kurahisisha matumizi.

    d)  Huwafunza watu istilahi za kutumia katika kuufafanua mfumo wa lugha.

    e)  Kuweka wazi kanuni ili watumiaji wazalishe tungo sahihi.

    SABABU ZA WATU KUCHUKIA SARUFI

    Watu huchukia kama jambo wanalolazimishiwa.

    Binadamu huchukulia sarufi kama njia ya kuwakosoa na kuwapunguzia uhuru wa kutumia lugha.

    Wengi husema sarufi huwa inachosha.

    Wengine nao huonelea kuwa hakuna haja ya sarufi baada ya mtu kuelewa jinsi ya kusoma na kuandika maneno ya kiswahili.

    SURA YA PILI: LUGHA

    Lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano. Tunaposema lugha ni mfumo wa sauti tunamaanisha kuwa sauti ambazo hutumika katika lugha yoyote huwa na utaratibu na mpangilio fulani wa maneno yake. Konsonanti na irabu huchukua mpangilio fulani wakati wa kuunda maneno. Aidha, tunaposema kuwa ni sauti za nasibu, huwa tunamaanisha kuwa kila lugha ina sauti zake miongoni mwa sauti nyingi ambazo zinaweza kutoka katika kinywa cha binadamu. Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu.

    Wanyama hawatumii lugha kama chombo cha mawasiliano, kwa kuwa lugha ni sauti zenye maana na kukubaliwa na jamii.

    Sifa za lugha

    Lugha pia hufa kwa msamiati wake kupotea.

    Lugha ina uwezo wa kukua. Kwa mfano: Kiswahili kimebuni msamiati teknolojia kama vile kipepesi, mdahilishi, rununu, runinga.

    Hakuna lugha iliyo bora kushinda nyingine. Kwa hivyo, lugha zote ni sawa.

    Kila lugha ina sauti zake zilizo tofauti na nyingine.

    Lugha lazima iwe inahusu binadamu.

    Sauti- sauti hufanywa na mwanadamu.

    Lugha hufuata misingi ya fonimu, yaani, a, b, ch, d, f, h, z  n.k.

    Lugha huwa na mpangilio maalamu wenye kubeba maana. Mpangilio huo huanza na fonimu———⇨ silabi—-⇨ neno.

    Lugha hujitambulisha ili kuzalisha maneno mengi.

    Lugha hubadilika ikitegemea mazingira, aina ya tukio, wakati na watumizi wa lugha hio.

    Lugha husharabu. Lugha husharabu kwa maana ya kwamba lugha huchukua maneno kutoka lugha nyingine ili kujiongezea msamiati wake.

    Tabia za lugha

    Lugha huathiriwa: jamii hurithi lugha kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

    Lugha zina ubora: lugha zote ni bora hakuna lugha bora kuliko nyingine zote.

    Lugha huathiriana: lugha yoyote inaweza kuathiriwa na lugha nyingine.

    Lugha hutohoa: lugha ina tabia ya kuchukua au kukopa maneno kutoka lugha nyingine.

    Lugha hufundishika: mtu yeyote anaweza kujifunza walau kiasi lugha yoyote hata kwa njia ya ufundishaji.

    Lugha huzaliwa: ni kutokana na lugha nyingine moja au Zaidi zilizotanguliwa kuwepo.

    Lugha hukua: lugha hukua ( kuongezeka kwa maneno, kuongezeka kwa idadi ya wazungumzaji, kuwa na mawanda mapana, kusanifiwa) kadiri inavyoendelea kutumiwa na jamii.

    Lugha lazima ijitosheleze: kila lugha inajitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii inayotumia lugha yenyewe.

    Lugha hufa: inapozidi mno kubadilika mwisho si yenyewe tena, lakini pia inapoachwa isitumike tena kwa kuwa wahusika wanapendelea lugha nyingine.

    DHIMA ZA LUGHA

    Lugha hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashiana habari.

    Lugha hutumika kutoa burudani.

    Lugha hutumika kujenga umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanajamii.

    Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa kabila / jamii au taifa fulani.

    Lugha hutumika kutunza, kukuza, na kuendeleza utamaduni wa jamii.

    Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali (ni nyenzo ya kufundishia).

    Lugha ni chombo ambacho hutusaidia kujieleza na kutoa mawazo yetu.

    Lugha ni kitambulisho cha taifa.

    Changamoto katika lugha ya kiswahili

    Dhana ya kunasibisha Kiswahili na dini ya Kiisalamu. Hili limechangia dini nyingine kama wakristu, wahindi kujiepusha katika matumizi ya kiswahili kwa sababu ya tofauti za kidini.

    Upinzani kutoka kwa lugha ambazo zimekwisha jitanua katika dunia. Kwa mfano: kiingereza, kifaransa, kireno na kiarabu. Watumizi au watu wenye asili na lugha hizo hukipiga vita kiswahili wakihofia kuwa wasipofanya hivyo kitazimeza lugha zao.

    Kudharauliwa kwa lugha ya kiswahili na kupigwa chapuo kwa lugha za kigeni kwamba ndio pekee zinafaa kutumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Kwa mfano: watumizi wengi kukitukuza Zaidi kiingereza na kutojua kuwa Kiingereza ni saw ana lugha nyingine tu.

    Kucheleweshwa kwa maamuzi ya sera ya kukipa hadhi Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika nyanja zote za elimu, na Kiingereza kuwa somo tu. Swala hili linarudisha nyuma maendeleo ya Kiswahili.

    Watumizi kuwa nyuma katika kufanya tafiti mbalimbali juu ya lugha ya Kiswahili. Utafiti husaidia watumizi kufunguka kiakili na kufahamu umuhimu wa kuwa na lugha ya kiswahili.

    Uchumi mdogo wa mataifa mengi, haswa ya mashariki Afrika, umekwamisha maendeleo ya haraka ya lugha ya Kiswahili duniani. Kwa kuwa nchi nyingi zimeshindwa kuzalisha wataalamu wengi wa lugha hii, aidha wameshindwa kutafsiri maandiko kutoka lugha nyingine kuwa katika lugha ya Kiswahili kwa sababu kumekuwa ghari mno.

    Ukosefu wa msaada kwa wasanii wanaotumia Kiswahili katika muziki na hata uandishi wa vitabu vya kiswahili.

    Waafrika kukosa moyo wa kuthamini na kujadili tamaduni zao. Kiswahili ni lugha inayotangaza utamaduni wao lakini waafrika wanathamini tamaduni za kimagharibi.

    Dhana ya kuwa Kiswahili ni lugha ya watu duni kitaaluma. Kwa mfano: watu walioishia darasa la pili ama waliokosa kwenda shule hivyo hufanya watu kutaka kujifunza kiingereza. Hata hivyo, kuna wasomi wengi waliobobea katika somo la kiswahili na pia kuna watu wanaoboronga kimatamshi na kimaandishi.

    Suluhisho zinazofaa kufanywa ili lugha ya kiswahili kuboreka

    Kuongeza kongamano na vituo mahususi za kufanya utafiti wa lugha ya kiswahili. Kongamano hizi zinafaa kuwa na wataalamu waliobobea na kuhitimu kwenye lugha ya Kiswahili ili kuwasaidia waandishi, wasomi na watumizi wa lugha hii Madhubuti ya Kiswahili.

    Kufanya Kiswahili lugha ya mafunzo kwenye shule za chekechea, upili,  sekondari na vyuo vikuu.

    Kuwazawidi wanaokitumia na kukiandika lugha ya Kiswahili kwa usanifu. Kwa mfano: serikali na idara za kibinafsi zinafaa kufanya tuzo zinazozingatia kuwatunuku weledi wa lugha ya Kiswahili, haswa waandishi wa magazeti, watangazaji wa redio na runinga, wanafunzi, wanasiasa na hata wananchi wa kawaida wanaokidhamini Kiswahili.

    Kutenga hela za kuwasaidia wanaokipigania kiswahili kwenye ramani ya dunia. Kwa mfano: kuwasaidia wakati wa kuchapisha vitabu vya Kiswahili.

    Kutumia Kiswahili katika matangazo ya biashara, katika vipindi vya mazungumzo na hata kwa vipindi vya kuigiza. Kupitia njia hizi, watu wataweza kupata lugha ya Kiswahili n ahata kusanifisha lugha yao.

    Kufanya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa. Kwa mfano: Lugha ya Kiswahili ni lugha ya taifa kwa mataifa ya Kenya na Tanzania.

    Kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii ili kupata wosia ama maoni ya watu kuhusu lugha ya Kiswahili. Jambo hili litachangia kuvumbua maneno mapya na hata kugundua udhaifu katika idara ya Kiswahili. Aidha, mtandao wa kijamii utasaidia watafiti wengine kupata majibu ya maswahili yao bila kubeba matopa ya vitabu.

    Kutengeneza mabango yanayoashiria hatua zinazoimarisha lugha ya Kiswahili. Jambo hili linasaidia kuwafahamisha watu ni vyema kuenzi lugha ya Kiswahili kwani kuna faida kabambe.

    Kutengeneza mashidano yanayohusiana na lugha ya kiswahili. Kwa mfano: kukariri mashairi, kutunga nyimbo na kuandika insha.

    Kuyapa maeneo majina ya Kiswahili. Kwa mfano: unaeza mahali ‘fanaka’ kumaanisha eneo hilo litakuwa na ufanisi.

    Kutumia lugha ya kiswahili kwenye vyumba na makao ya kiserikali. Kwa mfano: wabunge wanafaa kutumia lugha ya Kiswahili wakati wa kujadili miswanda mbungeni.  

    Kuchapisha Makala muhimu kwa lugha ya kiswahili. Kwa mfano: Katiba za nchi zinafaa kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili kwani ni lugha asili na inayoeleweka kwa haraka.

    Kutumia lugha ya Kiswahili kama Lugha ya Kwanza katika vyombo ya mawasiliano. Jambo hili linarahisisha ukuaji wa kiswahili.

    Kuvumbua shule za ufunzi wa Kiswahili katika mataifa ya kigeni. Kwa mfano; Kujenga shule za ufunzi wa Kiswahili uko bara ulaya ili kuchangia ushindani na lugha nyingine za kimataifa ili Kiswahili iwekwe kwenye ramani ya duniani.

    SURA YA PILI:  SAUTI

    MAANA YA SAUTI

    Sauti ni mlio unaotokana na kitu, mtu au mnyama. Kwa mfano, binadamu huzungumza ilhali wanyama hutoa milio.

    Ili sauti kusikika, mapafu husukuma hewa kupitia kooni kwenye nyuzi-sauti. Hatimaye hewa hiyo hutokea kinywani au puani na kuwa sauti.

    Sauti zimegawanywa katika makundi mawili; irabu(vokali) na konsonanti.

    Irabu za kiswahili huwa tano, nazo ni: a, e, i, o na u. konsonanti nazo ni; b, ch, d, f, g, h, j, k, L, m, n,p, r, s, t, v, w, y na z.

    TANBIHI: Konsonanti zisizotumika

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1